Kilimo cha zao la Ufuta: Masoko, Mbinu na Ushauri Toka kwa Wadau

Habari wa JF!
Naombeni ushauri au uzoefu wenu kuhusu madawa yanayoweza kutumika kufanya palizi kwenye shamba la ufuta.

Nafahamu yapo madawa ya kufanya palizi kwenye mpunga na hata mahindi na kwa kiasi kikubwa yanasaidia kupunguza gharama za kilimo kwa wanaolima mashamba makubwa.

Nimejaribu kutafuta madawa ya palizi ya ufuta lakini bado sijafanikiwa. Naomba ambaye anafahamu hayo madawa kama yapo anielekeze tafadhali.
 
1900 kilo ushirika, mtaani 1800 kg
Mkuu kwa bei izo ni zakawiada kwenye ufuta huwa inaanzia 1,500 to 3,000,bei itacheza kwenye izo namba kwaiyo wakulima wamezoea na bado inawalipa kwa sababu wengi wanalima eneo kubwa.

Pia COVID19 imechangia kushuka kwa bei nadhani msimu wa mwakani itapanda sana na ninampango wa kwenda kuwekeza uko.
 
Mkuu kwa bei izo ni zakawiada kwenye ufuta huwa inaanzia 1,500 to 3,000,bei itacheza kwenye izo namba kwaiyo wakulima wamezoea na bado inawalipa kwa sababu wengi wanalima eneo kubwa.,
Pia COVID19 imechangia kushuka kwa bei nadhani msimu wa mwakani itapanda sana na ninampango wa kwenda kuwekeza uko.
Mkuu hailipi kwa bei hiyo, coz ekari moja ya ufuta huwa inatoa gunia 3 kiwango cha juu, kwahiyo 1900×3= 570000. Ambapo mahindi ekari moja inaweza kutoa hadi gunia 10×60000= 600000 kiwango cha juu.

Hapo ilitakiwa bei ianzie walau 2500kg
 
Back
Top Bottom