SoC02 Kilimo cha mazao ya muda mfupi

Stories of Change - 2022 Competition

imem2022

New Member
Aug 17, 2022
2
1
Kilimo ni uzalishaji wa mazao mashambani na ufugaji wa mifugo kama ng'ombe, mbuzi, kuku, Bata, nguruwe na kondoo. Kwa nchi nyingi za Afrika ikiwemo Tanzania kilimo ndiyo sekta muhimu kwani ndio uti wa mgongo kwa uchumi wetu, kwani ni miongoni mwa sekta ambazo zinachangia pato la taifa na ni sekta ambayo inahakikisha uwepo wa chakula hivyo basi kusaidia kukabiliana na baa la njaa.

Mazao ya muda mfupi ni mazao ambayo yanalimwa na kuvunwa chini ya miezi kumi na mbili kati ya miezi mitatu na miezi sita pia huitwa mazao ya mzunguko mfupi au mazao ya kila mwaka, mfano nafaka( mpunga,mahindi na maharage), mbegu za mafuta(pamba na ufuta), vyakula vya mizizi (viazi vitamu,viazi mviringo na magimbi na mihogo),mboga,(vitunguu,nyanya na mchicha) matunda(nanasi,embe,machungwa,parchichi,tikiti maji na ndizi).kama ilivyo jembe halimtupii mkulima ni maneno ambayo huwatia moyo wakulima wengi ambao wanafuata ushauri wa wataalamu wa kilimo huwasaidia kupata mazao mengi na kuwafanya wafurahie shughuli za kilimo .

Hali ya sasa ya kilimo cha muda mfupi
Kwa ujumla jamii iweze kujikwamua kiuchumi kilimo cha mazao ya muda mfupi kinatakiwa kipewe kipaumbele kwani kina faida nyingi kwa jamii ambayo inakifanya kwa mfano jamii kubwa ya nyanda za juu kusini kwenye mkoa kama Iringa, Njombe na Mbeya wamejikita kwenye kilimo cha mazao mfupi kama viazi na parachichi ambapo wanapata faida nyingi kama vile chanzo cha ajira, watu wengi wameajiriwa na kujiajiri katika kilimo hiki ambacho kinawasaidia kupata kipato ili kuendesha shughuli mbalimbali kama kuwapeleka watoto shule na shughuli nyingine ambazo zinahitaji pesa ili kuziendesha pato kwa taifa, serikali inapata pato kutoka kwa wakulima kwa kulipa ushuru ambao unatumika katika shughuli mbalimbali za kujenga taifa kama vile kujenga miundo mbinu kama barabara, shule na pia katika kupunguza umaskini wa nchi. Pia pato linaongezeka kupitia uwekezaji ambapo nchi mbalimbali za nje huwekeza katika kilimo cha muda mfupi kwa mikataba na nchi husika.

Virutubisho kama vile vitamini na protini ambavyo ni muhimu kwa ajili ya ukuaji. Virutubisho hivyo vinapatikana kutoka kwenye mazao ya kilimo kama vile maharage na mbogamboga. Japo kuwa kilimo cha mazao ya muda mfupi kina faida lakini jamii haijakitilia mkazo kutokana na changamoto mbalimbali kama vile ukosefu wa masoko ya uhakika, ukosefu wa elimu ya kutosha kuhusu kilimo hiki cha mazao ya mfupi kama vile faida zake.

Chanzo cha pesa za kigeni; kutokana na wakulima kuuza mazao yao nje ya nchi kunasababisha kuwepo kwa pesa za kigeni ambazo zinaongeza thamani ya shilingi yetu.


Maono
Kuinua kipato cha mtu mmoja mmoja kutokana na ajira za muda mrefu na muda mfupi zinazotokana na kilimo hicho.

Kuondoa tatizo la njaa kwa kuhakikisha kuna chakula cha kutosha; kutokana na mabadiliko ya tabia ya nchi kama ukame kumesababisha tatizo la njaa,hivyo kilimo cha mazao ya muda mfupi kinaweza kikatoa suluhisho la tatizo la njaa kwa kuhakikisha kunakuwepo na chakula cha kutosha.

Kutengeneza nafasi za ajira kwa watu wasiokua na ajira hasa vijana; ukizingatia kwamba kuna vijana wengi ambao hawana ajira hivyo basi kilimo hiki kinaweza kikaajili watu hivyo kupunguza wimbi la ukosefu wa ajira.

Kuwa na jamii yenye afya bora kwa kuzingatia mlo kamili; jamii kubwa ya watanzania hususani nyanda za juu kusini kwenye mkoa kama Njombe japokuwa wanalima mazao mengi ya chakula lakini wanakabiliwa na matatizo ya utapiamlo hivyo basi kilimo hiki cha mazao ya muda mfupi ni chanzo cha madini mbalimbali kwa ajili ya kuboresha afya ya watumiaji badala ya kutumia vyakula vinavyotengenezwa viwandani.


Mikakati
Kuhakikisha upatikanaji wa mikopo kwa wakulima

Kuna wananchi wanatamani kuanza kilimo lakini hawana fedha za kuanzia hivyo vikundi binafsi viweze kuundwa ili kuweza kukopa mikopo katika taasisi kama vile mabenki ambapo watatumia mkopo hiyo kama mitaji kwa ajili ya kununua pembejeo mbalimbali za kilimo.

Jamii ipewe elimu kuhusu kilimo cha mazao ya muda mfupi, elimu itolewe na waatalamuu kutokana na jiografia ya eneo husika ili kujua mahitajii ya mkulima kama mbolea, dawa na mbegu bora ambazo zinastahimili ukame na wadudu kama vile viwavi jeshi kwenye mahindi.

Kuhakikisha uwepo wa masoko ya uhakika ambayo yatawarahisisha wakulima kuuza mazao yao kwa mfano masoko ya ndani na nje ya nchi hivyo kuondoa hofu ya mazao yao kudolola.na pia kutengeneza vyama vya ushirika ambavyo vitarahisisha upatikanaji wa masoko.

Kupunguza kutegemea mvua kwa ajili ya kilimo kwakuhakikisha uwepo wa maji ya kutosha kwa ajili ya umwagiliajii kwa maeneo yasiokua na mvua za kutosha kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa, mvua zimekuwa zikipungua msimu kwa msimu hivyo jamii inaweza kutumia kilimo cha umwagiliaji ili kukidhi kiasi cha maji yanayohitajika kwa ajili ya kilimo.


Hitimisho
Jamii ipewe elimu zaidi kuhusu utunzaji wa mazingira ili kukabiliana na changamoto ya mabadiliko ya hali ya hewa na tabia ya nchi ili kuwezesha ukuaji wa mazao kama kutumia samadi badala ya mbolea za viwandani kwani kilimo ndio chanzo kikubwa cha ajira kwa watu. Mazingira yasipotunzwa hali ya ardhi itakuwa mbaya ambapo itachangia kupunguza uzalishaji wa mazao kwa ajili ya kujilisha kwa mzalishaji lakini zaidi sana kuyauza na kuweza kujipatia kipato ili kupunguza umaskini katika jamii zetu za kitanzania na kupunguza umaskini kwa mtu mmoja mmoja na kupunguza umaskini kwa jamii na kwa nchi nzima kiujumla. Lakini pia wataalamu wawape wakulima ushauri mapema kabla ya wao kuingia katika shughuli rasmi ili nguvu inayoelekezwa katika shamba iweze kuleta matokeo chanya kwa wakulima hao katika kujipatia kipato kutoka katika kilimo kwani binadamu hataacha kula au kutumia chakula kwahiyo kile kinachozalishwa (mazao) yana umuhimu mkubwa sana kama sio leo basi ni kesho.​
 
Back
Top Bottom