Kilimanjaro: Wananchi Same wamkataa mbunge David Mathayo, wasema haonekani jimboni na bungeni

mwanamwana

JF-Expert Member
Aug 1, 2011
1,076
4,113
Katika ziara ya Mwenezi wa CCM, Paul Makonda Wananchi jimbo la Same wameonesha kutokuwa na imani na mbunge wao, ambapo wamedai kuwa mbunge huyo amekuwa akirudisha nyuma maendeleo ya jimbo hilo hasa kwa kuwagawa vijana na watu. Wamemnukuu Hayati Nyerere kuwa ili maendeleo yawepo lazima kuwepo na SIASA SAFI, lakini mbunge huyo amekuwa chanzo cha kukwamisha maendeleo.

Raphael Mruta amesema...

"Nyerere alishawahi kusema ili maendeleo lazima tuwe na siasa safi tupo na mbunge ambaye anagawanya vijana, anagawanya watu hata lile soko kufeli ni kwa sababu ya sumu ya wakazi wa Same hilo lipo wazi kuwa hatuna mbunge,"

"Wanaokwamisha maendeleo ya Same ni kutokuwa na siasa safi tuna mbunge ambaye haonekani jimboni wala bungeni," amesema huku akishangiliwa na wananchi.''

Wananchi hao wameendelea kudai kuwa mbunge wao huyo amekuwa haonekani bungeni jambo ambalo linawapa wasiwasi wananchi hao. ''Hapa tuna Mkuu wa wilaya na Mkurugenzi hatuna Mbunge, Jimboni hayupo na Bungeni Hayupo anawagawa wananchi"

Wananchi jimbo la Same wameonesha kutokuwa na imani na mbunge wao, ambapo wamedai kuwa mbunge huyo amekuwa akirudisha nyuma maendeleo ya jimbo hilo hasa kwa kuwagawa vijana na hata kukwamisha mradi wa soko.

Wananchi hao wameendelea kudai kuwa mbunge wao huyo amekuwa haonekani bungeni jambo ambalo linawapa wasiwasi wananchi hao. ''Hapa tuna Mkuu wa wilaya na Mkurugenzi hatuna Mbunge, Jimboni hayupo na Bungeni Hayupo anawagawa wananchi"

View attachment 2879588
Haya ni mazingaombwe. Mwendesha mazingaombwe mwenyewe, Makonda, ni tatizo kuliko hayo matatizo anayotaka kushughulikia.
 
Katika ziara ya Mwenezi wa CCM, Paul Makonda Wananchi jimbo la Same wameonesha kutokuwa na imani na mbunge wao, ambapo wamedai kuwa mbunge huyo amekuwa akirudisha nyuma maendeleo ya jimbo hilo hasa kwa kuwagawa vijana na watu. Wamemnukuu Hayati Nyerere kuwa ili maendeleo yawepo lazima kuwepo na SIASA SAFI, lakini mbunge huyo amekuwa chanzo cha kukwamisha maendeleo.

Wananchi hao wameendelea kudai kuwa mbunge wao huyo amekuwa haonekani bungeni jambo ambalo linawapa wasiwasi wananchi hao. ''Hapa tuna Mkuu wa wilaya na Mkurugenzi hatuna Mbunge, Jimboni hayupo na Bungeni Hayupo anawagawa wananchi"

View attachment 2879588
Mbunge Dr Mathayo David, wa Same ,Yuko CHUNYA, eneo la makongorosi, anachimba Dhahabu( Ramani Investment ( na mbunge mwezake wa Hai.
 
Mojaa Kati ya watu ambao Wana ukwasi wa kuitoshaa n hyu mtu!kwenye madin no habar nyngne kbs...@anyway wananchi wameamua
 
Saaafi, Kaskazini angalau wanajielewa nchi hii.
Pole pole wananchi wanaelimika.Wimbi la vijana wanaoelimika ni kubwa sana na itafika siku hao wazee walionufaika na udumavu wa wanachi kwa miaka mingi watazikimbia wenyewe ofisi.
 
Mojaa Kati ya watu ambao Wana ukwasi wa kuitoshaa n hyu mtu!kwenye madin no habar nyngne kbs...@anyway wananchi wameamua
Iko hivyo.hawa wanasiasa wachama chakavu kwa miaka mingi wamekua wakitumia mgongo wa chama kwenye nafasi za kisiasa ili kulinda maslahi yao binafsi sio kwaajili ya kusimamia maendeleo ya wananchi.na imekua hivyo kwasababu wote ni wale we hakuna wakumwajibisha mwenzake.
 
Back
Top Bottom