Mbunge Igalula, Venant Daud aendelea na ziara jimboni, achangia madawati 300

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,895
940

MBUNGE IGALULA, MHE. VENANT DAUD AENDELEA NA ZIARA JIMBONI, ACHANGIA MADAWATI 300

Mbunge wa Jimbo la Igalula Mkoa wa Tabora Mhe. Venant Protas Daud amefanya ziara ya siku tano kuanzia tarehe 27 Februari 2023 mpaka tarehe 03 Machi 2023 katika Kata Nne zilizomo Igalula ambazo ni Kata ya KIGWA, GOWEKO, NSOLOLO, & IGALULA kwa ajili ya kukagua miradi ya maendeleo, kusikiliza kero za wananchi ili kuzitafutia ufumbuzi.

Akiendelea na ziara yake tarehe 01 Machi, 2023 Mbunge Wa Jimbo la Igalula Mhe. Venant Daud Protas (255782421122) katika Kata ya Goweko Kwa lengo la kusikiliza kero za Wananchi na kukagua miradi ya Maendeleo Kwa upande mwingine Mbunge Venant ametoa Madawati 300 Kwa shule za Msingi.

Katika ziara yake ya tarehe 02 Machi, 2023 Mbunge Wa Jimbo la Igalula Mhe. Venant Daud ameendelea na ziara yake katika Kata ya Nsololo. Mapema alishiriki na Wananchi wa Kata ya Goweko kwenye matoleo ya Ujenzi wa Kituo cha Afya Goweko. Ziara iliendelea Kwa kutembelea miradi ya maendeleo katika Kata ya Nsololo ambapo ujenzi wa bweni Nsololo wamepokea Shilingi Milioni 110 kutoka Serikalini na Ujenzi wa Zahananti ya Nsololo ilipokea Shilingi Milioni 50 na kufanya Mikutano ya hadhara katika vijiji vya Kimungi na Ntarasha.

Awali, tarehe 28 Februari, 2023 Mhe. Venant Daudi alishiriki kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM Mkoa wa Tabora ambacho kilihudhuriwa na viongozi mbali wa CCM na kuongozwa na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Tabora na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa Ndugu Hassan Wakasuvi.

Ziara hiyo ilijumuisha viongozi mbalimbali wa Chama Cha Mapinduzi na Serikali akiwemo Mkuu wa Wilaya ya UYUI, Mhe. Zakaria Mwansasu, Wenyeviti wa CCM Wilaya, Makatibu wa CCM Wilaya, Viongozi wa Wilaya na Mkoa wa UVCCM, Madiwani pamoja na wajumbe wa Kamati ya Utekelezaji wa Mkoa na Wilaya.

Miradi inayotekelezwa katika jimbo la Igalula ni pamoja na Mradi wa Bwawa la Goweko linagharimu Shilingi Bilioni 6 ambapo tayari zimeshafika Shilingi Milioni 900. Mradi huu utawanufaisha Wakazi wa Vijiji vya Goweko, Mwitikila utakapo kamilika na utaweza kumwagilia zaidi ya hekta 400.

WhatsApp Image 2023-03-03 at 09.56.30(2).jpeg
WhatsApp Image 2023-03-03 at 09.56.32.jpeg
FqGvzztWIAAcmK7.jpg
WhatsApp Image 2023-03-03 at 09.56.27.jpeg
WhatsApp Image 2023-03-03 at 09.56.30.jpeg
 
Protas kura 323
Mussa Ntimizi kura 299
Hawa walitofautiana kura 24 tu mwaka 2020 tena Protas ukiungwa mkono na Rais Magufuli.

Ntimizi ilimuondoa uhaba wa MAJI Igalula na wewe hujafanya lolote kutatua kero hii na sioni ukishinda kura za maoni 2025!

Igalula wanataka maji sio hiyo mikutano yako na mzee Wakasuvi

Heri kiinua mgongo chako fanyia mengine,huwezi shinda kura za maoni CCM Igalula 2025
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom