Kilichomponza Tido Mhando ni uzalendo wake

Kilichomponza Tido Mhando ni uzalendo wake

Televisheni ya Taifa, jina zuri kabisa siyo kama huu ushenzi alioleta Tido Mhando wa tbc!
ok asante sana. sasa tofauti ya hayo majina yaani tvt na tbc ni nini hasa? muundo wa tvt na tbc uko tofauti kiutendaji.
 
Usikute the issue sio Tido bali ni Azam!, haiwezekani Tido alipokuwa TBC, TBC ilingara, sasa yuko Azam, Azam inangara!, hivyo ikatafutwa namna yya kumcontain ili aondolewe Azam!, hata akiondolewa, jee ...itangara?.

Pole Tido, tuko nyuma yako!.

Paskali
hahahahahhahahaha dah
 
Duuuh issue ya kufukua makaburi hiii tokea 2008 kweli walikuwa wapi?
But issue ya kuisababishia hasara chombo hicho sio kama amechukua hizo pesa hapana bali actions zake za kiutendaji zimepeleka kuikosesha TBC pesa hizo.
Ukute hii ni ile vita inaendelea sasa hakipigwi chombo anapigwa mtu [emoji849]
 
Mtu akiwa na cv nzur ndo hashtakiwi....naona kujibu kwa hisia tu bila hoja....kama kafanya mazur mengi na ndan ya hayo mazur katupiga ashtakiwe tuu
 
Quinine Nimesikitika sana kwa malipo haya. Naomba nimwambie Tido kwamba amshukuru tu Mungu kwa kila jambo kama maandiko yasemavyo. Vita anayopigana nayo ni ya "forces of darkness" kutokana na mazuri anayofanya.
 
TIDO MHANDO!

Aliombwa na Rais JK kuja kuifufua na kuiokoa TBC, Tido akaifanya kazi hiyo kufa na kupona na TBC ikaimarika, ikawa Shirika halisi la Utangazaji la Taifa. Tangu Tido aondoke TBC shirika hilo limegeuka kuwa tawi la CCM na Serikali na si chombo cha wananchi.

Malipo anayopewa Tido ni hili la kuisababishia hasara serikali ya Shilingi Milioni 800. Sawa, sote tunajua kuwa mahakama itaamua, tuiwache iamue na ukweli utajulikana mbeleni.

Lakini wakati Tido akipandishwa kizimbani kwa kutuhumiwa kufanya ubadhirifu wa Shs. Milioni 800, wako magwiji wazito wa rushwa na ufisadi wenye ushahidi wa wazi ambao hawaguswi.

Mmoja wa magwiji hao ni Andrew Chenge, Chenge wakati akiwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG) alihusika kwenye mikataba mibovu ya ununuzi wa rada, kisha akapewa mgao (rushwa) ya zaidi ya Shilingi Bilioni 1 za Kitanzania. Ufisadi mkubwa!

Benki iliyowekewa fedha hizo ilihakikisha kupokea fedha hizo. Chenge mwenyewe alikiri kuwa amewekewa fedha hizo, tena akiziita vijisenti - hadi leo Chenge yuko huru, tena CCM na Bunge wamemchagua kuwa Mwenyekiti mmojawapo wa bunge letu tukufu.

Chenge, aliyekiri mwenyewe kuhongwa fedha za rada na kuliletea taifa hasara za mabilioni ya fedha leo anapandishwa vyeo na yuko huru. Tido ambaye aliinua TBC kitaifa na kimataifa yuko kizimbani kwa tuhuma nzito.

By the way, tangu Azam TV warushe mahojiano ya Tundulissu kwa kirefu na kwa uwazi, nilijua Tido na wenzake wanapaswa kujichunga. Serikali za Ki-Afrika huongoza kwa kutumia madaraka yake vibaya, zikiona mtu fulani anazivua nguo kwa mabaya yake, humwandama mtu huyo hadi anyooshe mikono.

Ni visasi juu ya visasi, ni kuwaumiza watu wasio na hatia kwa sababu ya misimamo yao. Tuliyaona kwa Yusuph Manji (japo yanatofautiana kidogo) lakini ajenda za maovu hayo ya dola dhidi ya watu wenye misimamo fulani, hufanana! Tumeona maaskofu wenye misimamo ya kuionya serikali wakihojiwa juu ya uraia wao, bila sababu - tumeona wabunge wanaoikosoa serikali kwa nguvu wakifunguliwa mashtaka kila uchwao. Ni uhuni juu ya uhuni!

Inatia hasira sana pale unapoona mafisadi wakuu wa ESCROW, EPA, RADA, NDEGE YA RAIS n.k. wakiwa mitaani wanakula raha, halafu watuhumiwa wa makosa ya kutengenezwa wanafikishwa mahakamani.

Tanzania yetu inaendeshwa kwa Double Standard za hali ya juu. Wapo wala rushwa na watoa rushwa wakubwa, wengine hadi wamerekodiwa wakishiriki vitendo vya rushwa, matokeo yake wanapandishwa vyeo.

Safari ya Taifa letu na wanataifa wake ni ndefu.

[HASHTAG]#Mtatiro[/HASHTAG] J
 
Back
Top Bottom