Kilichomkumba aliyekuwa raisi wa Liberia hayati Samuel Kanyon Doe.... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kilichomkumba aliyekuwa raisi wa Liberia hayati Samuel Kanyon Doe....

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Leornado, Nov 14, 2010.

 1. L

  Leornado JF-Expert Member

  #1
  Nov 14, 2010
  Joined: Nov 12, 2010
  Messages: 1,534
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  [​IMG]

  Nadhani hii ni baada ya wananchi na waasi wa hii nchi kuchoshwa na manyanyaso ya raisi wao wakamtenda hivi baada ya kumpindua miaka ya 1990s, African presidents take care kwani uvumilivu wa wananchi wenu una kikomo yasijekukuta haya ndugu yangu...
   
 2. PayGod

  PayGod JF-Expert Member

  #2
  Nov 14, 2010
  Joined: Mar 4, 2008
  Messages: 1,255
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  mh mungu apushie mbali
   
 3. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #3
  Nov 14, 2010
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,474
  Likes Received: 4,134
  Trophy Points: 280
  Aiseee hii ni hatari, lakini hawa wengine hata hawajifunzi.
   
 4. Mtende

  Mtende JF-Expert Member

  #4
  Nov 14, 2010
  Joined: Sep 27, 2010
  Messages: 4,072
  Likes Received: 338
  Trophy Points: 180
  hawa wengine kina nani? fafanua plz
   
 5. K

  Kithuku JF-Expert Member

  #5
  Nov 14, 2010
  Joined: Nov 19, 2006
  Messages: 1,395
  Likes Received: 96
  Trophy Points: 145
  Hii habari ni kweli kabisa. Attempt yangu ya kwanza ya PhD ilikuwa political anthropology nikitazama patriotism from the perspective of tribal loyalty, bahati mbaya ile project niliiachia hatua za awali baada ya funding kukatika ghafla. Lakini nilikuwa nimeshajifunza mambo mengi, mojawapo ni hili. Supervisor wangu aliniunganisha na mtu wa Liberia anaitwa James Youboty tukawa marafiki na akawa ananitumia data nyingi. Ali-scan vitu vingi sana akanitumia, ikiwemo hata hotuba za mwisho za Samuel Doe alipokuwa anajitahidi kuungana na Prince Johnson ili kwa pamoja wamshinde Charles Taylor. Kulikuwa na details za jinsi Doe alivyotumia machifu wa kabila lake la Krahn kutoka eneo la Grand Gedeh, minutes za vikao nk. Jinsi askari wa kabila la Krahn walivyosimama kidete nyuma ya Doe hadi siku yake ya mwisho. Kikubwa kuliko vyote ambavyo James aliniruhusu kuona ni maktaba yake ya kanda za VHS zenye detail za mateso yote ambayo Prince Johnson alimfanyia Doe, ni ukatili wa ajabu mno na niliamini kuwa wale askari wake na yeye mwenyewe walikuwa wavuta bangi, huwezi kumtenda binadamu mwenzio hivyo! Kabla ya kifo chake ambacho kilitokana na kuvuja damu nyingi, Samwel Doe alikatwa masikio yote mawili na uume wake ulikatwa kwa singe lakini haukumalizikia, ndiyo unapoona hapo kwenye picha uume ulikuwa umevilia damu.

  Jambo moja pia ni kuwa James alikuwa kabila moja na Doe kwa hiyo alitoa sana story ya upande mmoja. Na pia kuweza kuwa na details zote za mateso ya Doe ilinipa picha kuwa alihusika na intelligence system yao pia (ingawa alidai ni mwandishi wa habari, lakini kuna kila ushahidi kuwa ni zaidi ya hapo). Kule US, wale mashushushu wa enzi ya Doe na familia zao wana umoja wao una nguvu sana. James pia ameandika kitabu kinaitwa 'A Nation in Terror', ambacho pia alinipa a signed copy. Kina fine details za mateso na kifo cha Samuel Doe ambaye huyu James anamsifu kupita kiasi kama shujaa wa Liberia
   
 6. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #6
  Nov 14, 2010
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,326
  Likes Received: 1,793
  Trophy Points: 280
  Kithuku Thanks Kithuku. Naona tunakuwa wazito kusoma mambo ya historia. Tunarudia makosa yale yale
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 7. Utingo

  Utingo JF-Expert Member

  #7
  Nov 15, 2010
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 7,121
  Likes Received: 184
  Trophy Points: 160
  and where is Prince Johnson now?
   
 8. Safari_ni_Safari

  Safari_ni_Safari JF-Expert Member

  #8
  Nov 15, 2010
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 22,469
  Likes Received: 5,847
  Trophy Points: 280
  Masikio Chwap....mimi ninahuruma kidogo...ntamnyoa mtu mamvi yake asiyotaka kuyanyoa...abaki kipara

  [​IMG]
   
 9. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #9
  Nov 15, 2010
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,296
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Ikifika Tz naona watu ndo wataelewa maana ya peoples power huwezi endesha watu kama watoto wako au familia yako
  Mbaya zaidi kwa kwenda kinyume na matakwa yao
  Munge aipushie karibu ilo janga
   
 10. Safari_ni_Safari

  Safari_ni_Safari JF-Expert Member

  #10
  Nov 15, 2010
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 22,469
  Likes Received: 5,847
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
   
 11. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #11
  Nov 15, 2010
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,296
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Ningekuwa na gazeti langu kesho ndo ingekuwa mada front page!
   
 12. Sajenti

  Sajenti JF-Expert Member

  #12
  Nov 15, 2010
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 3,673
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  ..Na hawana haja ya kujifunza kwani wanajua kabisa hakuna mwenye guts za kufanya hayo waliofanya watu wa Liberia so usijiumize roho bure.. Kama juzi tu FFU walipoanza kurusha mabomu ya machozi mkalainika na kukubali kuchakachuliwa matokeo ndio mtaweza kufanya hayo aliyofanyiwa Doe??? Never never ever:nono::nono::nono:
   
 13. K

  Kifimbocheza JF-Expert Member

  #13
  Nov 15, 2010
  Joined: Aug 7, 2008
  Messages: 496
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 45
  Jamani

  mimi hiyo Picha siiioni PleaSE PLEASE NAOMBA MUITUME TENA NIWEZE KUONA
   
 14. Mzee wa ngano

  Mzee wa ngano Senior Member

  #14
  Jul 13, 2013
  Joined: May 3, 2012
  Messages: 179
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Kama hukuiona awali utaionaje sasa? badili kioneo ndiyo dawa.
   
 15. K

  Kithuku JF-Expert Member

  #15
  Jan 29, 2014
  Joined: Nov 19, 2006
  Messages: 1,395
  Likes Received: 96
  Trophy Points: 145
  Tatizo la ukabila ambapo watu wanaelekeza loyalty yao kwa kabila kwanza kabla ya nchi linafufuka barani Afrika, lakini limechukua sura pia ya udini. Tumeona kinachotokea Sudani Kusini (ukabila Dinka dhidi ya Nuer) na Afrika ya Kati (udini). Cheche za yote mawili zipo Tanzania pia: udini (hasa mijini ambako kabila ni vigumu kujikusanya) na ukabila (tumeona kwenye mapigano ya Kiteto, na tunasikia sana tuhuma kwenye baadhi ya vyama vya siasa). Vyombo vya usalama vinapaswa kutambua na kuzima cheche hizi kukingali mapema.
   
Loading...