KWELI Rais Samuel Doe aliua Mawaziri, Jaji Mkuu, Rais wa Bunge na viongozi wengine waandamizi wa mtangulizi wake nchini Liberia

Taarifa hii imethibitika kuwa ya kweli baada ya kufanya tathmini ya kina
Kijana wa miaka 29 aliushangaza ulimwengu kwa kitendo cha kikatili kisichokuwa na chembe ya utu. Inadaiwa baada ya kumpindua na kumuua Rais aliyekuwa madarakani William Tolbert, Samuel Doe alihakikisha anamaliza mizizi ya mtangulizi wake kwa kuua viongozi wote waandamizi.

Inadaiwa Aprili 22, 1980 viongozi 13 walifikishwa ufukweni mwa bahari ya Atlantic nchini humo, wanaume hao 13 walikuwa nusu uchi ambapo walifyatuliwa risasi na vikosi vya Rais Samuel Doe.

Kati ya waliouawa ni pamoja na Frank E. Tolbert ambaye alikuwa Kaka yake na rais Tolbert, na Rais wa Bunge la seneti.

Doe.png

Picha: hali ilivyokuwa siku ya mauaji​

Muosha huoshwa, Rais Samuel Doe naye alikuja kupinduliwa na kuuawa kikatili sana na waasi.
 
Tunachokijua
Mtu wa kabila la Krahn, Samuel Kanyon Doe alizaliwa mnamo Mei 6, 1951 huko Tuzon, Kaunti ya Grand Gedeh, kusini mashariki mwa nchi Liberia.

Akiwa ametoka katika familia yenye asili ya hali ya chini, akiwa na umri wa miaka 18, alijiunga na jeshi la Liberia, akimaliza mafunzo yake ya kijeshi katika Shule ya Mawasiliano katika Wizara ya Ulinzi ya Monrovia mwaka wa 1971.

og-samuel-doe-9658.jpg

Samuel Kanyon Doe
Baada ya kuonesha uwezo mkubwa katika kuongoza, mwaka 1979 Doe alichaguliwa kupata mafunzo maalumu kwenye vikosi vya Marekani nchini Liberia, na ndani ya mwaka mmoja alipandishwa cheo na kuwa Sajenti.

Namna alivyoupata Urais wa Liberia
Mnamo Aprili 12, 1980, Doe akiwa na askari wengine 18 alitwaa madaraka na kufanya udhibiti mkubwa wa Liberia katika mapinduzi ya kijeshi.

Wakati wa mapinduzi hayo yaliyomwaga damu za watu wa Liberia, Mwanajeshi binafsi wa Doe anayefahamika kwa jina la Harrison Pennoh alimuua Rais wa Liberia William R. Tolbert mwenye umri wa miaka 66 akiwa katika jumba lake la kifahari. Mwanajeshi huyu baadae aligundulika kuwa na changamoto ya afya ya akili.

Baada ya kutwaa madaraka, Doe aliunda Baraza la Ukombozi wa Watu (PRC) likimjumuisha yeye na maafisa wengine 18, alijipandisha cheo mara moja na kuwa Kamanda Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi ya Liberia huku akisimamisha katiba ya nchi hiyo kwa miaka 4 hadi mwaka 1985 alipotwaa tena Urais wa nchi hiyo kwenye uchaguzi uliotajwa na waangalizi kama "uchaguzi wa udanganyifu usio huru na haki."

Madai ya Doe kuua viongozi wa Mtangulizi wake
Ili kujihakikishia usalama wake, kuongeza hofu kwa wapinzani pamoja na kuufuta kabisa utawala wa Rais mtangulizi, mwezi huohuo baada ya kufanya mapinduzi, Doe aliamuru mawaziri wote washitakiwe na kupewa hukumu ya kifo huku wakinyimwa haki ya kukata rufaa pamoja na kutetewa na Mawakili.

1980ExecutionSouthBeachMonrovia.JPG

Chanzo: Larry C. Price / Fort Worth Star-Telegram, 1980, kwenye The New York Times
Awali, ilidaiwa kuwa Mawaziri wote waliuawa, lakini Tawasifu ya Ellen Johnson Sirleaf, Rais wa 24 wa Liberia aliyetawala kati ya mwaka 2006-2018 yenye kichwa cha habari "Johnson Sirleaf, 'This Child will be Great. Memoirs of a Remarkable Life by Africa's First Woman President', ukurasa wa 102, inataja majina ya maafisa 13 pekee waliouawa hadharani kwa amri ya Rais Doe.

Majina ya wahusika hao ni;
  1. Frank E. Tolbert, Rais wa Bunge la Seneti na Kaka wa Rais William Tolbert
  2. Richard A. Henries, Spika wa Bunge
  3. E. Reginald Townsend, Mwenyekiti wa Chama cha True Whig
  4. Clarence Parker, Mweka hazina mkuu wa chama cha True Whig
  5. James A. Pierre, Jaji Mkuu
  6. Joseph J. Chesson, Waziri wa haki
  7. Cecil Dennis, Waziri wa Mambo ya nje
  8. Frank J. Stewart, Mkurugenzi wa Bajeti
  9. James T. Phillips, Waziri wa zamani wa wizara za kilimo, uchumi
  10. Cyril Bright, Waziri wa uchumi na mipango
  11. David F. Neal, Waziri wa zamani wa uchumi na mipango
  12. John W. Sherman, Waziri wa Biashara
  13. Charles T.O. King, Mwanachama wa Congress
Kwa mujibu wa Rais Ellen, tukio hili lilitokea asubuhi ya Aprili 22, siku 10 baada ya kufanyika kwa mapinduzi ya kijeshi.

Taarifa zinazohusu mauaji haya zinapatikana pia kwenye Makavazi ya Britannica, Black Past, BBC na Liberia Past and Present.

Hatma ya uongozi wake pamoja na kifo
Katika kipindi chote cha uongozi wake Doe aliwapandisha vyeo watu wa kabila lake la Krahn, akiweka pembeni makabila mengine yote kwa kuhofia uwezekano wa kupinduliwa.

Akiwa amevidhibiti vyombo vyote vya habari vilivyoikosoa serikali yake, Doe aliwahoji mara kwa mara, kuwafunga, na kuwaua waandishi wa habari waliofichua mbinu zake nzito.

Aliunga mkono waziwazi sera za Vita Baridi vya Marekani barani Afrika na kukata uhusiano wote wa kidiplomasia na Muungano wa Jamhuri za Kisoshalisti za Kisovieti (USSR) ambao ulimletea ongezeko kubwa la misaada kutoka kwa Marekani chini ya utawala wa Ronald Reagan, Rais wa 40 wa Marekani (1981-1989)

Baada ya uchaguzi wa udanganyifu mwaka 1985 kumweka Doe madarakani, vuguvugu la upinzani lilianza kubadilika. Kufikia mwishoni mwa 1989 vikundi vingi vya wapinzani vilijaribu kumwondoa madarakani katika shindano ambalo lilikaribia kumalizika kwa vita vya wenyewe kwa wenyewe.

Moja ya makundi ni National Patriotic Front lililoongozwa na Charles Taylor aliyekuja kuwa Rais wa Liberia. Taylor na wafuasi wake walikuwa wa kikabila wa Gio, vita vidogo vya kikabila vilitokea kati ya wafuasi wa kiraia wa Doe na Taylor mwishoni mwa 1989. Sambamba na matukio haya, makumi ya maelfu ya raia wa Krahn na Gio walikimbilia nchi jirani ya Ivory Coast kuepuka vurugu.

Kuelekea mwisho wa utawala wake wa miaka kumi, Doe alionekana bila shaka kama dikteta kwa Waliberia na jumuiya ya kimataifa. Misaada kutoka Marekan ilipositishwa, Doe alikosa rasilimali za kuendelea na mapigano, akijaribu kuikimbia nchi.

Mnamo Septemba 9, 1990 kundi la watu sitini la Doe lilinaswa na kundi mashuhuri la upinzani chini ya uongozi wa Yormie Johnson. Siku iliyofuata, Septemba 10, 1990, Samuel Doe aliuawa.
Kundi la waamerika weusi waliorudi liberia walijikuta wao ndio wajuaji zaidi ya wenyeji,walijipatia madaraka makubwa na uonevu dhidi ya weusi wenzao,hii ilijenga chuki baina yao na kuanza kuwindana.

Samwel Doe naye alikufa kinyama
 
Tatizo hao viongozi walikuwa ni mabambadi(wazungu pori) huku wakijifanya wao bora zaidi na kuwadharau wa Liberia weusi,
Wa- Liberia wengi wao ni weusi ni majina tu yana sound whitesh. Yako hivyo sababu ni wajukuu na vitukuu vya watumwa waliorudishwa toka America na kuanzisha taifa huru la Liberia Jan 1822. Hata kama wapo White Liberian ni kama hapa kwetu Tanzania tulivyo wapo wazungu, wahindi, Half cast nk. But majority ya Liberian ni weusi
 
Na wakati wanamuua siyo kwamba walikua wanamtesa ili kulipiza aliyoyafanya ila walikua wanamtesa aseme hela alizoiba zote ameficha wapi ili wabaki nazo wao
 
Kijana wa miaka 29 aliushangaza ulimwengu kwa kitendo cha kikatili kisichokuwa na chembe ya utu. Inadaiwa baada ya kumpindua na kumuua Rais aliyekuwa madarakani William Tolbert, Samuel Doe alihakikisha anamaliza mizizi ya mtangulizi wake kwa kuua viongozi wote waandamizi.

Inadaiwa Aprili 22, 1980 viongozi 13 walifikishwa ufukweni mwa bahari ya Atlantic nchini humo, wanaume hao 13 walikuwa nusu uchi ambapo walifyatuliwa risasi na vikosi vya Rais Samuel Doe.

Kati ya waliouawa ni pamoja na Frank E. Tolbert ambaye alikuwa Kaka yake na rais Tolbert, na Rais wa Bunge la seneti.

View attachment 2732206
Picha: hali ilivyokuwa siku ya mauaji​

Muosha huoshwa, Rais Samuel Doe naye alikuja kupinduliwa na kuuawa kikatili sana na waasi.
Hiin inatufundisha nini tulipopita na tulipo?
 
4 Reactions
Reply
Back
Top Bottom