Umeeleza vizuri mkuu,binafsi ni mweupe kwenye mambo ya sheria na mahakama kwa ujumla.Shahidi ameitwa mahakamani, ametii wito. Lakini hajaridhia kuwa shahidi.
Upande wa Utetezi umekubali kwa ridhaa (Consented) kutoendelea nae kwa kauli yake tuu. Na Lissu ameridhia hilo na umeitaarifu mahakama kuhusu ridhaa hiyo (Hilo ni kosa upande wa Lissu).
Maana yake upande wa utetezi umeridhia na umeitaarifu mahakama kwamba haina nia ya kuendelea na shahidi.
Utamaduni wa mahakama ni kwamba: Mahakamani, kama usipodai haki yako, mahakama inakaa kimya kuhusu haki hiyo. Kukaa kimya kwa mahakama juu ya hilo ni hasara kwa upande wa utetezi. Angeweza kuweka pingamizi na kuisukuma mahakama kuamua juu ya hilo. Hapa Lissu hajashauriwa vizuri, amepoteza haki yake muhimu sana ambayo ingeweza kuamuliwa na mahakama kama uamuzi mdogo.
Kama Lissu angeiambia Mahakama kwamba bado anahotaji ushahidi (wa DCI) wa shahidi ni muhimu kwake. Angeilazimisha mahakama iamue na ingeweza kutoa amri hata kama (DCI) hataki (not consent).
Maoni yangu; Binafsi nimeshangaa Lissu kukubali na kuridhia (DCI) kutokuw tayari na ushahidi wake. Angeweza kuiachia mahakama iamue juu ya hilo.
Hii kwa upande wa Lissu ni pigo maana anakosa sababu za rufaa (Kama akipatikana na hatia). Alitakiwa kuiachia mahakama itafsiri sheria na iamue juu ya DCI.
Kwa hali hii, itakuja kujitokeza shahidi muhimu akasema hataki kuwa shahidi na hakutakuwa na rejea za uamuzi wowote wa Mahakama.
Lissu angeiachia mahakama iamue juu ya hilo kuweka msingi mzuri kisheria huko mbele. Kilichotokea ni kumpa ushindi wa mezani DCI, bila ufafanuzi wa mahakama.
Je inawezekana shahidi angepanda kisha kutoa ushahidi wa kumfunga mtuhumiwa?
If yes hapa Lissu atakuja na comeback kuwa hata wakuu hawakutishika na kauli zake.Wacha tuone.