KILICHOJIRI MAHAKAMANI LEO TAREHE 18.9.2026.

KILICHOJIRI MAHAKAMANI LEO TAREHE 18.9.2026.

Kwa hiyo DCI are kuipinga kazi yake?

Kuongozwa kutoa ushahidi upande wa utetezi sio kuipinga kazi yake; ni kuibua na ku prove facts.
Kitu msichojua ni kwamba; Mahakama ingeweza kutoa amri ya DCI kuongozwa na upande wa utetezi, atake au asitake.

Someni sheria ya ushahidi, mbona ipo wazi tuu. Ushahidi sio ridhaa, mahakama inaweza kukulazimisha kutoa ushahidi/kuongozwa kuutoa hata kama hutaki au humpendi mshitakiwa.
Mahakama ina nguvu hiyo, ikihitaji ushahidi wako na unakuwa chini ya kiapo.
 
lete vifungu kurahisisha mambo.
 
Mkuu narudisha heshina yako. Hii kesi hawa watu wamekusudia kumkuta na hatia. Kusema Lissu yupo karibu kutoka gerezani ni tunajilosha upepo. Kesi inakwenda kwenye submission, ni siku moja baada ya hapo tunasubiri hukumu.

Mimi naona wazi kulikuwa na umuhimu mkubwa, DCI kupanda kizimbani atake au asitake. Ni muhimu.
Kakataa Sasa!
 
Shahidi ameitwa mahakamani, ametii wito. Lakini hajaridhia kuwa shahidi.
Upande wa Utetezi umekubali kwa ridhaa (Consented) kutoendelea nae kwa kauli yake tuu. Na Lissu ameridhia hilo na umeitaarifu mahakama kuhusu ridhaa hiyo (Hilo ni kosa upande wa Lissu).

Maana yake upande wa utetezi umeridhia na umeitaarifu mahakama kwamba haina nia ya kuendelea na shahidi.

Utamaduni wa mahakama ni kwamba: Mahakamani, kama usipodai haki yako, mahakama inakaa kimya kuhusu haki hiyo. Kukaa kimya kwa mahakama juu ya hilo ni hasara kwa upande wa utetezi. Angeweza kuweka pingamizi na kuisukuma mahakama kuamua juu ya hilo. Hapa Lissu hajashauriwa vizuri, amepoteza haki yake muhimu sana ambayo ingeweza kuamuliwa na mahakama kama uamuzi mdogo.

Kama Lissu angeiambia Mahakama kwamba bado anahotaji ushahidi (wa DCI) wa shahidi ni muhimu kwake. Angeilazimisha mahakama iamue na ingeweza kutoa amri hata kama (DCI) hataki (not consent).

Maoni yangu; Binafsi nimeshangaa Lissu kukubali na kuridhia (DCI) kutokuw tayari na ushahidi wake. Angeweza kuiachia mahakama iamue juu ya hilo.

Hii kwa upande wa Lissu ni pigo maana anakosa sababu za rufaa (Kama akipatikana na hatia). Alitakiwa kuiachia mahakama itafsiri sheria na iamue juu ya DCI.

Kwa hali hii, itakuja kujitokeza shahidi muhimu akasema hataki kuwa shahidi na hakutakuwa na rejea za uamuzi wowote wa Mahakama.
Lissu angeiachia mahakama iamue juu ya hilo kuweka msingi mzuri kisheria huko mbele. Kilichotokea ni kumpa ushindi wa mezani DCI, bila ufafanuzi wa mahakama.
Duuh mbombo ngafu
 
Vyovyote iwavyo. Bado wasingekuwa upande wa Tundu Lisu.
Zaidi wangeonyesha namna Lisu alivyomhalifu
Na kwa sababu tayari wameshachagua upande wameogopa wasije wakapanda kisha wakajichanganya kwenye maelezo na kujikuta wanampa ushindi Lissu. Mtu ambae anajua ataongea ukweli hawezi kuogopa kuwa shahidi maana pale sio kwamba anaenda kumtetea mshitakiwa
 
Ndio kitu nawaeleza watu hapa, wenye hofu kwamba DCI angekwenda mmaliza Lissu. Shahidi anaongozwa kwenye facts, na ndio maana kukawa na wakili/mshitakiwa kuongoza shahidi.
Hii kesi alieichora ni DCI ( Huyo huyo Kingai), yeye kubanwa kwa facts za ushaidi uliotolewa linakuwaje jambo baya tena kwa utetezi.

DCI kubanwa na utetezi ilikuwa ni muhimu sana. Ushahidi upande wa mashitaka ushawasilishwa, hakuna facts mpya.
 
Back
Top Bottom