KILICHOJIRI MAHAKAMANI LEO TAREHE 18.9.2026.

Manyanza

Platinum Member
Joined
Nov 4, 2010
Posts
21,074
Reaction score
54,160
Mwenendo wote kesi ya Lissu leo

Ijumaa, Septemba 18, 2026

KARANI:* Anajiandaa kusoma kesi ya Criminal Session, Kesi Namba 19605 ya Mwaka 2025.

JAMHURI DHIDI YA TUNDU ANTIPAS LISSU

WAKILI AJUAYE ZEGELI:* Iwapendeze Waheshimiwa Majaji wa Mahakama Kuu, naitwa Ajuaye Zegeli, nikisaidiana na:

1. NASSORO KATUGA: Wakili wa Serikali Mkuu.

2. TAWABU ISSA: Wakili wa Serikali Mwandamizi.

3. JOB MREMA: Wakili wa Serikali Mkuu.

4. CUTHBERT MBILINYI: Wakili wa Serikali.

5. WINNIWA KASARA: Wakili wa Serikali.

Waheshimiwa Majaji, tunaiwakilisha Jamhuri katika shauri hili. Mshtakiwa Tundu Antipas Lissu yupo kizimbani.

Shauri linakuja kwa ajili ya utetezi. Tupo tayari kuendelea.

JAJI NDUNGURU: Mshtakiwa.

LISSU: Nipo tayari, Mheshimiwa.

JAJI NDUNGURU: Tunaimba benchi la kwanza na la pili liw…

LISSU: Ambaye nilikuwa nimempendekeza awe shahidi wangu wa leo, nimekutana naye Mahakamani, kwenye chumba hiki hiki.

Naweza kuthibitisha kwamba ameheshimu wito wa Mahakama, amekuja.

Na nimezungumza naye kuhusu suala la yeye kuwa shahidi wa upande wa utetezi. Nimezungumza naye kwa kiasi kirefu na kwa kutosha.

Baada ya kuzungumza naye na kumweleza maeneo ambayo ningependa ayatolee ushahidi, Kamishna wa Polisi Kingai akaniambia kwamba yeye hawezi na hayupo tayari kutoa ushahidi kwa upande wangu.

Kwa maneno yake mwenyewe, amesema yeye yupo upande wa wale wanaoomba na watakaoshangilia nikipatikana na hatia.

Kwa hiyo, amesema hayupo tayari kuja kutoa ushahidi kwa niaba yangu.

Na nimemwelewa, Waheshimiwa Majaji. Kama hayupo tayari, siwezi kumlazimisha atoe ushahidi ambao hataki kuutoa.

LISSU: Waheshimiwa Majaji, Kamishna wa Polisi Kingai ameniambia kitu kingine kuhusu mashahidi wengine wawili ambao nao Mahakama hii iliamuru wapelekewe wito.

Yaani, Jenerali Jacob Mkunda na Inspekta Jenerali wa Polisi Camilius Wambura.

Kuhusu hao, Kamishna wa Polisi Kingai amesema vilevile kwamba hata wao watakaporejea nchini na kupata wito wa Mahakama, msimamo wao utakuwa huohuo.

Kwamba na wao hawatakuwa tayari kutoa ushahidi wa upande wa utetezi.

Sababu ileile kwamba wapo upande wa wanaoomba na watakaoshangilia nikipatikana na hatia.

Katika mazingira hayo, Waheshimiwa Majaji, maana yake ni kwamba sina mashahidi zaidi.

Na kwa hiyo, naomba kufunga ushahidi wa upande wa utetezi.

Ni hayo tu, Waheshimiwa Majaji.

\(LISSU anakaa.\)

\(MAJAJI WANATETA.\)

JAJI NDUNGURU: Nimesikia hoja ya Mshtakiwa. Kwa hiyo, shauri kwa upande wa utetezi limefungwa.

Upande wa mashtaka?

LISSU: Waheshimiwa Majaji, kwa vile kesi ya pande zote mbili imefungwa, tunaomba Mahakama ituangalie siku ya kuja kuwasilisha hoja za pande zote (final submission).

Waheshimiwa Majaji, sijawasiliana na upande wa mashtaka ili tukubaliane. Tunaweza kuleta hoja za mwisho.

Kwa hiyo, ninaweza kupendekeza kwa upande wangu, na wao wataona kama ipo sawa.

Waheshimiwa Majaji, naelewa kwamba session inaisha tarehe 25 Septemba, wiki inayo…

LISSU: Ni wiki moja tu ndiyo imebaki.

Nina kurasa zaidi ya 1,000 za final submission.

Kwa siku zilizobaki, ili Mahakama iweze kuamua, itabidi Mahakama ifanye kazi kubwa sana.

Kwa upande wangu, naweza kusema naweza kuwa tayari kufanya submission kuanzia siku ya Jumatano.

Inamaanisha ni siku tano from today.

Ni siku chache, lakini nikijifungia katika kachumba kangu kale, naweza kukamilisha.

Kwa hiyo, mapendekezo yangu tuje Jumatano, siku ya tarehe 25, tuweze kufanya final submission.

Itabidi tukatafakari kusubiri session nyingine.

KATUGA: Waheshimiwa Majaji, kwa upande wetu tunaungana naye.

KATUGA: Lakini hakusema kama ni oral au written.

LISSU: Ni oral submission ili wananchi waweze kusikia, kwa kuwa mimi nipo gerezani, sina hiyo luxury kama wao ya vitendea kazi.

KATUGA: Waheshimiwa Majaji, kwa hiyo tunakubaliana naye.

Tutajitahidi.

Kwa kuwa ni off record, Waheshimiwa Majaji, na sisi tulikuwa na hamu ya cross-examination, Waheshimiwa, ya mashahidi watatu wa Mshtakiwa.

[MAHAKAMA KICHEKO.]

JAJI NDUNGURU: Kwa kuwa ni off record, hiyo hamu endelea nayo.

Maana hamu huwa inakuja na kuisha.

[MAHAKAMA KICHEKO.]

JAJI NDUNGURU: Baada ya kusikiliza hoja za pande zote mbili za hitimisho na final submission, tunakubaliana kwamba mawasilisho hayo yatafanywa kwa mdomo siku ya Jumatano, tarehe 25 Septemba, saa 3:00 asubuhi.

[Majaji wananyanyuka na kuondoka.]
 
Mwenendo wote kesi ya Lissu leo

Ijumaa, Septemba 18, 2026

KARANI:* Anajiandaa kusoma kesi ya Criminal Session, Kesi Namba 19605 ya Mwaka 2025.

JAMHURI DHIDI YA TUNDU ANTIPAS LISSU

WAKILI AJUAYE ZEGELI:* Iwapendeze Waheshimiwa Majaji wa Mahakama Kuu, naitwa Ajuaye Zegeli, nikisaidiana na:

1. NASSORO KATUGA: Wakili wa Serikali Mkuu.

2. TAWABU ISSA: Wakili wa Serikali Mwandamizi.

3. JOB MREMA: Wakili wa Serikali Mkuu.

4. CUTHBERT MBILINYI: Wakili wa Serikali.

5. WINNIWA KASARA: Wakili wa Serikali.

Waheshimiwa Majaji, tunaiwakilisha Jamhuri katika shauri hili. Mshtakiwa Tundu Antipas Lissu yupo kizimbani.

Shauri linakuja kwa ajili ya utetezi. Tupo tayari kuendelea.

JAJI NDUNGURU: Mshtakiwa.

LISSU: Nipo tayari, Mheshimiwa.

JAJI NDUNGURU: Tunaimba benchi la kwanza na la pili liw…

LISSU: Ambaye nilikuwa nimempendekeza awe shahidi wangu wa leo, nimekutana naye Mahakamani, kwenye chumba hiki hiki.

Naweza kuthibitisha kwamba ameheshimu wito wa Mahakama, amekuja.

Na nimezungumza naye kuhusu suala la yeye kuwa shahidi wa upande wa utetezi. Nimezungumza naye kwa kiasi kirefu na kwa kutosha.

Baada ya kuzungumza naye na kumweleza maeneo ambayo ningependa ayatolee ushahidi, Kamishna wa Polisi Kingai akaniambia kwamba yeye hawezi na hayupo tayari kutoa ushahidi kwa upande wangu.

Kwa maneno yake mwenyewe, amesema yeye yupo upande wa wale wanaoomba na watakaoshangilia nikipatikana na hatia.

Kwa hiyo, amesema hayupo tayari kuja kutoa ushahidi kwa niaba yangu.

Na nimemwelewa, Waheshimiwa Majaji. Kama hayupo tayari, siwezi kumlazimisha atoe ushahidi ambao hataki kuutoa.

LISSU: Waheshimiwa Majaji, Kamishna wa Polisi Kingai ameniambia kitu kingine kuhusu mashahidi wengine wawili ambao nao Mahakama hii iliamuru wapelekewe wito.

Yaani, Jenerali Jacob Mkunda na Inspekta Jenerali wa Polisi Camilius Wambura.

Kuhusu hao, Kamishna wa Polisi Kingai amesema vilevile kwamba hata wao watakaporejea nchini na kupata wito wa Mahakama, msimamo wao utakuwa huohuo.

Kwamba na wao hawatakuwa tayari kutoa ushahidi wa upande wa utetezi.

Sababu ileile kwamba wapo upande wa wanaoomba na watakaoshangilia nikipatikana na hatia.

Katika mazingira hayo, Waheshimiwa Majaji, maana yake ni kwamba sina mashahidi zaidi.

Na kwa hiyo, naomba kufunga ushahidi wa upande wa utetezi.

Ni hayo tu, Waheshimiwa Majaji.

\(LISSU anakaa.\)

\(MAJAJI WANATETA.\)

JAJI NDUNGURU:
Nimesikia hoja ya Mshtakiwa. Kwa hiyo, shauri kwa upande wa utetezi limefungwa.

Upande wa mashtaka?

LISSU: Waheshimiwa Majaji, kwa vile kesi ya pande zote mbili imefungwa, tunaomba Mahakama ituangalie siku ya kuja kuwasilisha hoja za pande zote (final submission).

Waheshimiwa Majaji, sijawasiliana na upande wa mashtaka ili tukubaliane. Tunaweza kuleta hoja za mwisho.

Kwa hiyo, ninaweza kupendekeza kwa upande wangu, na wao wataona kama ipo sawa.

Waheshimiwa Majaji, naelewa kwamba session inaisha tarehe 25 Septemba, wiki inayo…

LISSU: Ni wiki moja tu ndiyo imebaki.

Nina kurasa zaidi ya 1,000 za final submission.

Kwa siku zilizobaki, ili Mahakama iweze kuamua, itabidi Mahakama ifanye kazi kubwa sana.

Kwa upande wangu, naweza kusema naweza kuwa tayari kufanya submission kuanzia siku ya Jumatano.

Inamaanisha ni siku tano from today.

Ni siku chache, lakini nikijifungia katika kachumba kangu kale, naweza kukamilisha.

Kwa hiyo, mapendekezo yangu tuje Jumatano, siku ya tarehe 25, tuweze kufanya final submission.

Itabidi tukatafakari kusubiri session nyingine.

KATUGA: Waheshimiwa Majaji, kwa upande wetu tunaungana naye.

KATUGA: Lakini hakusema kama ni oral au written.

LISSU: Ni oral submission ili wananchi waweze kusikia, kwa kuwa mimi nipo gerezani, sina hiyo luxury kama wao ya vitendea kazi.

KATUGA: Waheshimiwa Majaji, kwa hiyo tunakubaliana naye.

Tutajitahidi.

Kwa kuwa ni off record, Waheshimiwa Majaji, na sisi tulikuwa na hamu ya cross-examination, Waheshimiwa, ya mashahidi watatu wa Mshtakiwa.

[MAHAKAMA KICHEKO.]

JAJI NDUNGURU:
Kwa kuwa ni off record, hiyo hamu endelea nayo.

Maana hamu huwa inakuja na kuisha.

[MAHAKAMA KICHEKO.]

JAJI NDUNGURU:
Baada ya kusikiliza hoja za pande zote mbili za hitimisho na final submission, tunakubaliana kwamba mawasilisho hayo yatafanywa kwa mdomo siku ya Jumatano, tarehe 25 Septemba, saa 3:00 asubuhi.

[Majaji wananyanyuka na kuondoka.]
ok.🐒
 
Eye witness labda ni shahidi huyo tu ndio mwenye uzito lakini shida hati ya mashtaka inasema kuchapisha,kukinukisha na kuzuia uchaguzi.
 
Mh Lissu upenda sifa zisizo mfaa

Tena yumkin yeye Lissu ndio mwisho kamkataa Shahidi yake ndugu R. Kingai 🤣❗️
kuwa angemchoma vibaya mbele ya Majaji pale mahakamani

Leo mh Lissu Kinyovyote tulitegemea angefunga ushahidi wake😂✍️
 
Watalaamu wa sheria njoni mtufafanulie kwa kina Chivundu

Shahidi ameitwa mahakamani, ametii wito. Lakini hajaridhia kuwa shahidi.
Upande wa Utetezi umekubali kwa ridhaa (Consented) kutoendelea nae kwa kauli yake tuu. Na Lissu ameridhia hilo na umeitaarifu mahakama kuhusu ridhaa hiyo (Hilo ni kosa upande wa Lissu).

Maana yake upande wa utetezi umeridhia na umeitaarifu mahakama kwamba haina nia ya kuendelea na shahidi.

Utamaduni wa mahakama ni kwamba: Mahakamani, kama usipodai haki yako, mahakama inakaa kimya kuhusu haki hiyo. Kukaa kimya kwa mahakama juu ya hilo ni hasara kwa upande wa utetezi. Angeweza kuweka pingamizi na kuisukuma mahakama kuamua juu ya hilo. Hapa Lissu hajashauriwa vizuri, amepoteza haki yake muhimu sana ambayo ingeweza kuamuliwa na mahakama kama uamuzi mdogo.

Kama Lissu angeiambia Mahakama kwamba bado anahotaji ushahidi (wa DCI) wa shahidi ni muhimu kwake. Angeilazimisha mahakama iamue na ingeweza kutoa amri hata kama (DCI) hataki (not consent).

Maoni yangu; Binafsi nimeshangaa Lissu kukubali na kuridhia (DCI) kutokuw tayari na ushahidi wake. Angeweza kuiachia mahakama iamue juu ya hilo.

Hii kwa upande wa Lissu ni pigo maana anakosa sababu za rufaa (Kama akipatikana na hatia). Alitakiwa kuiachia mahakama itafsiri sheria na iamue juu ya DCI.

Kwa hali hii, itakuja kujitokeza shahidi muhimu akasema hataki kuwa shahidi na hakutakuwa na rejea za uamuzi wowote wa Mahakama.
Lissu angeiachia mahakama iamue juu ya hilo kuweka msingi mzuri kisheria huko mbele. Kilichotokea ni kumpa ushindi wa mezani DCI, bila ufafanuzi wa mahakama.
 
Mh Lissu upenda sifa zisizo mfaa

Tena yumkin yeye Lissu ndio mwisho kamkataa Shahidi yake ndugu R. Kingai 🤣❗️
kuwa angemchoma vibaya mbele ya Majaji pale mahakamani

Leo mh Lissu Kinyovyote tulitegemea angefunga ushahidi wake😂✍️
Sasa mbona kakataa kupanda Ili ampasue lisu
Haihitaji hata D Moja kujua lengo la lisu
 
Shahidi ameitwa mahakamani, ametii wito. Lakini hajaridhia kuwa shahidi.
Upande wa Utetezi umekubali kwa ridhaa kutoendelea nae na umeotaarifu mahakama kuhusu ridhaa hiyo (Hilo ni kosa upande wa Lissu).

Maana yake upande wa utetezi umeridhia na umeitaarifu mahakama kwamba haina nia ya kuendelea na shahidi. Mahakamani, kama usipodai haki yako, mahakama inakaa kimya. Kukaa kimya kwa mahakama ni hasara kwenye shauri, ambalo lingeweza isukuma mahakama kuamua. Hapa Lissu hajashauriwa vizuri, amepoteza haki yake muhimu sana ambayo ingeweza kuamuliwa na mahakama kama uamuzi mdogo.

Kama Lissu angeiambia Mahakama kwamba bado anahotaji ushahidi (wa DCI) wa shahidi ni muhimu kwake. Angeilazimisha mahakama iamue na ingeweza kutoa amri hata kama (DCI) hataki (not consent).

Maoni yangu; Binafsi nimeshangaa Lissu kukubali na kuridhia (DCI) kutokuw tayari na ushahidi wake. Angeweza kuiachia mahakama iamue juu ya hilo.

Hii kwa upande wa Lissu ni pigo maana anakosa sababu za rufaa (Kama akipatikana na hatia). Alitakiwa kuiachia mahakama itafsiri sheria na iamue juu ya DCI.

Kwa hali hii, itakuja kujitokeza shahidi muhimu akasema hataki kuwa shahidi na hakutakuwa na rejea za uamuzi wowote wa Mahakama.
Lissu angeiachia mahakama iamue juu ya hilo kuweka msingi mzuri kisheria huko mbele. Kilichotokea ni kumpa ushindi wa mezani DCI, bila ufafanuzi wa mahakama.
Maelezo marefu ila yamejaa ujinga

Kama hii kesi ingekuwa na mashiko Kingai angempanda jukwaani athibitishe uhaini wa Lisu

Kitendo Cha kukataa ni USHINDI Kwa Lisu maana adui wake amekimbia pambano
 
Lengo lilikuwa ni Hilo Hilo akatae kupanda jukwaani Ili USHINDI utangazwe Kwa aliyebaki jukwaani
Nilijua Lissu ange turn hii issue the other side ili kuonesha nia ovu waliyokuwa nayo uoande wa jamhuri ambayo kimsingi imethibitika kwa kauli ya Kingai kwa Lissu, kwamba watafurahi kama Lissu akikutwa na hatia.

Kundi la watu wa aina hii haitakiwi kuwaacha kirahisi namna hiyo kama Lissu alivyofanya.
 
Back
Top Bottom