Hivi hii Kili music awards ina EVENT ORGANIZER? Ni kinyaa kitupu kwenye stage jamani. Watu hawawezi kujieleza, wanashukuru ukoo mzima, marafiki, maproduzer puh! Wengine wanagombea kupokea tuzo. Hao watoaji tuzo wenyewe wana maneno mengi, wewe umepewa kazi ya kumpa mwanamuziki tuzo unaleta story za nini? Mwishowe wanajiumauma na kuchemka kama Nsajigwa katia aibu alipokuwa anamtangaza mshindi.
Napendekeza kuwe na REHESAL kwa wanaowania tuzo wote, wagawa tuzo, na ma MC. Ikiwezekana umeze kabisa utakachosema ukifika pale stejini, na jinsi ya kuipoke tuzo yako. Loh! Halafu nani kasema huyo Milard Ayo anafaa ushereheshaji? Huyo ni presenter mzuri sana kwenye TV na radio but si MSHEREHESHAJI jamani! Anachemka kinoma. Mpoki amejitahidi, hajaongea utumbo, Mzee small na Bi Chau wamefurahisha, C Pwaa yuko presentable hata kwenye kupokea tuzo amejitahidi. Watu hawako serious, hawako presentable ni kichefuchefu.
Huyo Lina nae sijui kavaa nini, wacheza shoo wake wadada wamependeza kama nini na vigauni vyao vya silver , yeye hata sijuui kavaa nini. Duh! Bado tuko nyuma sana. Naona hata aibu jamani. Hivi huwa hawatizami Grammy, Emmy na tuzo zingine?