Kili Music Awards 2011

MSANII wa muziki wa kizazi kipya, 20 Percent jina lake halisi Abbas Kinzasa juzi alifanikiwa kutwaa tuzo tano kati ya sita kwenye kinyang'anyiro cha tuzo za muziki Tanzania za Kili 2011.

Katika hafla ya utoaji wa tuzo hizo iliyofana kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee, jijini Dar es Salaam, msanii huyo alinyakua tuzo tano huku akiwafunika nyota wengine kama Diamond na Ali Kiba ambao walikuwa wanapewa nafasi kubwa ya kutwaa tuzo mwaka huu.

Msanii huyo ambaye mashabiki walikuwa wakimshangilia kila alipotajwa ingawa aliwakilishwa na prodyuza wake, Man Walter ukumbini hapo, alishinda tuzo ya msanii bora wa kiume, mtunzi bora wa nyimbo, mwimbaji bora wa kiume.

Wimbo wake wa ‘Tamaa Mbaya’ ulitwaa tuzo ya wimbo bora wa mwaka na wimbo bora wa Afro Pop huku Banana Zorro akisema; “Nilijua 20 angewafunika, nyimbo zake zinagusa maisha halisi ya Mtanzania wa kawaida na hata mwaka usishangae akaendelea kutawala.”

Wasanii wengine waliofuatia kwa kujikusanyia tuzo mbili kila mmoja ni Linah, JCB na CPwaa. Linah alitwaa tuzo ya msanii mpya anayechipukia na mwimbaji bora wa kike wakati CPwaa na singo yake ya ‘Action’ alinyakua tuzo ya wimbo bora wa Ragga na video bora ya mwaka.

Wimbo wa ‘Ukisikia Paah’ wa JCB ambao amewashirikisha Fid Q, Chid Benz na Jaymoe uliwapa tuzo ya wimbo bora wa hip hop pamoja na wimbo bora wa kushirikishwa.

Wasanii wengine waliotwaa tuzo ni Lady Jaydee, ambaye aliibuka msanii bora wa kike, ‘My Valentine’ wa Jahazi ndio wimbo bora wa Taarab, wimbo bora wa Kiswahili wa bendi ni ‘Shika Ushikapo’ wa Mapacha Watatu huku ‘Nikikupata’ wa Belle 9 ukitajwa wimbo bora wa R&B.

‘Ujio Mpya’ wa Hardmad akimshirikisha Enika ndio wimbo bora wa Reggae, rapa bora wa bendi kwa mwaka ni Khalid Chuma 'Chokoraa', msanii bora wa Hiphop ni Joh Makini huku ‘Nitafanya’ ya Kidumu na Jaydee ikibuka nyimbo bora ya Afrika Mashariki na Lamar prodyuza bora.

Wimbo bora wa asili wa Tanzania ni ‘Shangazi’ wa Mpoki aliofanya na Cassim wakati ‘Nabembelezwa’ ya Barnaba ndio wimbo bora wa Zouk.

Mashabiki walionekana kufurahia maandalizi pamoja na programu ya shoo hiyo ingawa waliguna kwa nguvu alipotangazwa mshindi wa prodyuza bora wa mwaka ambaye ni Lamar na mshindi wa wimbo bora wa asili, Sylvery Mujuni au Mpoki, mchekeshaji wa Orijino Komedi.

Wengi wao waliwataja msanii Mrisho Mpoto au Mjomba na prodyuza Man Walter kuwa walistahili kwenye badala yao.

Msanii Diamond ambaye aliambulia patupu katika tuzo hizo licha ya kupewa nafasi kubwa alisema, “Nimeridhika na mchuano ulikuwa mkali walioshinda walistahili.”
20zawadi.jpg
 
Miezi michahe iliopita nilipata kusikia baadhi ya wanasiasa wakiulizana eti ni kitu gani hasa kimetufanya vijana TUKICHUKIE CCM kiasi hiki.

Binafsi wauliza suali walinishangaza kweli na nikabaki nimeduwaa sana kwa hasira na simanzi moyoni. Hakika nilijihisi kwamba kumbe sisi vijana na baadhi ya viongozi wetu wala hatuishi katika sayari moja kamwe kiasi cha wao wala kutoguswa na matatizo yetu licha ya wala kutokuzifahamu.

Sasa kwa urahisi zaid kwenu ambao hamkawii kutumia mabilioni kwenye kuendesha utafiti kwenye kutafuta majibu ambayo yako wazi kabisa huku uswahilini tunamoishi, na wakati mwingine kuwatumia tu wasanii kama lichambo la kuwasaidieni kufikia malengo yenu kisiasa na baadaye wao kutelekezwa kama kamasi pindi itokapo puani, nawaombeni sana mkamsikilize uzuri na kwa makini sana nyimbo zake huyu kijana mwenzetu - hakuna asichowahi kukiimba juu ya mashaibu yetu kitaa huyu bwana.

Na kama muda bado utakua unaruhusu na basi mkapitilize zaidi kwa Bana Zoro na vibao vyake, Mr II, Mjomba, Afande Sele, na wengine wengi tu. Baada ya kujipatia hali halisi juu ya maisha tunayoishi ya kuunga unga huku mitaani na basi fedha ambazo mgetumia kufanyia utafiti mkapeleke kutusaidi huko kwenye mizahanati na utawala kuwa salama zaidi kwetu.

Big up sana Mheshimiwa 20 Percent, wewe ni zaidi ya baadhi ya hawa viongozi wengi mafisadi na wanafiki wanaofanya maisha yetu kuwa ni ya hati hati kila kukicha na watu tukaendelea kuonekana kama sanamu tu mbele ya hao hao 'waungwana' wa kuchonga.

Mungu akujalie sana maisha marefu uendelee kutufariji tukafarijiana na zaidi katika jehanamu tuliyalazimishwa kutinga hata kabla safari yetu ahera haijawadia.
 
Nyimbo zenu vijana wa sasa hazidumu sana ingawa mnatajirika haraka sana. Akina Juma Nature, Profesa J, Selemani Msindi, AY, Crazy GK, FA, TID, wako wapi?

Hivi kuna tafriri mpya ya neno tajiri hapa Tanzania? kumiliki Toyota starlet siku hizi ni utajili?
 
Mkuu mapungufu yalikuwepo lakini si kwa kiwango tunacho lalamikia, tatizo lingine ni kuwa watu wanataka liwe sawa na award za usa.
Mimi binafsi sikupendezwa na jinsi ITV walivyoshindwa kulionyesha vizuri.
Kilimnjaro wamejitahidi kutafuta client ambao ni best hapa bongo kutengeneza jukwaa nk na kwa bongo pale ndio mwisho. kuhusu pongezi walizotoa wasanii sijui umelinganisha na zipi maana hizo za wenzetu watu wanaongeaga utumbo hadi wananyanganywa mic, mavazi ndio usiseme watu wanavuaga hadi nguo jukwaani.
Kama ni muhudhuriaji mzuri wa show za hawa bongo fleva wala huwezi kushangaa maana ndio vile wanavyofanya jukwaani siku zote na usifananishe na wanavyoimba ktk videos zao, kilichoongezeka ni kuwa walikuwa wanapigiwa live band.
Jmani uandaaji wa tuzo za america music award bajeti yake ni karibu nusu ya bajeti ya tanzania usikae ukaanza kulinganisha sana, mwisho tutaishia kulalama tu bila kuzingatia factor kibao
Usizuge,wenzetu huwa wanajipanga wanapoongea,mbona mnatetea uchafu.kama wanavyofanya siku zote hata kama ni utumbo uuache tu!!!kuongea vizuri nako kunahitaji pesa??kila kitu ni ovyo pale
 
Back
Top Bottom