Kili Marathoni Vs NBC Dodoma Marathoni Vs CRDB Marathoni

Kili Marathoni Vs NBC Dodoma Marathoni Vs CRDB Marathoni

Ipi ni Marathoni bora na yenye tija zaidi kwa Tanzania?

  • Kili Marathoni

  • NBC Dodoma Marathoni

  • CRDB Marathoni

  • Zote ni bora.


Results are only viewable after voting.
Kuna zile ndogo ndogo.
Sijui Betika Marathon n.k

Nafikiri hizi 3 ndio maarufu zaidi kwa Tz
 
Kwa wapiga kura wachache waliojitokeza bado Kili inaongoza...

Tupate Marathon babalao
 
Makampuni mengi yakibiashara hutumia hizi nafasi kujibrand kuna watu wanalipwa kabisa Night na tickets kwenda kwenye hizi marathon
Kwa makampuni na wanaolipwa hao sina shida nao, kuna wale wao ndo wanalipa ili kwenda kukimbia.
 
Je, ipi ni Marathon kubwa zaidi Tanzania? Kilimanjaro Marathon au NBC Dodoma Marathon au CRDB Marathon?

Kwa miaka kadhaa sasa, Tanzania imekuwa na mbio za marathon zinazovutia maelfu ya washiriki kutoka ndani na nje ya nchi. Miongoni mwa marathon zinazozungumzwa zaidi ni Kilimanjaro Marathon, NBC Dodoma Marathon na CRDB Dar Marathon

Kilimanjaro Marathon

Hufanyika jijini Moshi, mkoani Kilimanjaro, ikiwa na historia ndefu na ushiriki wa wakimbiaji wa kimataifa. Mbio hizi zimechangia kuitangaza Tanzania kupitia utalii, hasa kwa kuhusishwa na Mlima Kilimanjaro, na huwavutia washiriki kutoka mataifa mbalimbali. Pia huleta mchango mkubwa katika uchumi wa eneo kupitia hoteli, usafiri na biashara nyingine zinazohudumia wageni.

NBC Dodoma Marathon
Hufanyika jijini Dodoma na imekua kwa kasi katika miaka ya karibuni. Mbali na mashindano ya riadha, marathon hii imejikita kwenye shughuli za kijamii kwa kukusanya fedha kwa ajili ya kusaidia sekta ya afya, ikiwemo huduma za afya ya mama na mtoto pamoja na magonjwa mbalimbali kupitia ushirikiano na taasisi za afya. Pia imekuwa ikivutia maelfu ya washiriki kila mwaka.

CRDB Bank Marathon (Dar es Salaam)
Hufanyika jijini Dar es Salaam na ni moja ya marathon zinazokuwa kwa kasi nchini. Mbio hizi zimejikita katika kuhamasisha afya na mazoezi, huku zikiwa na lengo la kuchangisha fedha kwa ajili ya kusaidia huduma za afya kupitia CRDB Bank Foundation.

Kwa mtazamo wako, ipi ni marathon kubwa zaidi kati ya hizi tatu?

Je, ipi iwe Mfalme wa Marathon zote Tanzania?

Nilichojifunza kwenye Kili Marathon na NBC Dodoma Marathon

Kwanza, Hawa wote wawili huwa wanatumia barua ( Official Letter) kwa Taasisi na Idara zote za Serikali ya JMT pamoja na Makampuni Binafsi Makubwa kuomba Wafanyakazi wao waweze kushiriki ukiwa pamoja na kuwalipia ada za ushiriki na posho za safari.

Ikumbukwe kuwa Taasisi za Serikali na Makampuni Wana Sera za Corporate Social Responsibility ( CSR) Kwahiyo kupitia fungu hilo la bajeti husaidia kuwawezesha watumishi wa Serikali na Makampuni Binafsi kushiriki.

Kili Marathon huwa anaonekana kinara kutokana Hana MPINZANI au mshindani wa biashara yupo Neutral lakini ukija kwa haya Mabenki kama imeandaliwa na NBC usitegemee Wafanyakazi wa Benki zingine kushiriki kwa maana hao wanaonekana ni washindani wao

Sasa kwa Upande wa NBC pia hamasa imetokana na ushiriki wao wa kufadhili ligi kuu ya Tanzania, ambao mashabiki wengi wa Moira wa miguu wamejitokeza na walioteka sehemu mbalimbali kwa sababu Dodoma ipo katikati ya nchi kwahiyo ni rahisi mashabiki wa Mpira wa timu mbalimbali kujichanganya na kukodi Coaster kutoka Tabora, Singida, Morogoro, Iringa, Tanga, Mbeya, Manyara, Arusha, nakadhalika kuweza kusafiri na kushiriki hiyo Marathon
 
Back
Top Bottom