Kili Marathoni Vs NBC Dodoma Marathoni Vs CRDB Marathoni

Kili Marathoni Vs NBC Dodoma Marathoni Vs CRDB Marathoni

Ipi ni Marathoni bora na yenye tija zaidi kwa Tanzania?

  • Kili Marathoni

  • NBC Dodoma Marathoni

  • CRDB Marathoni

  • Zote ni bora.


Results are only viewable after voting.

uran

JF-Expert Member
Joined
Nov 11, 2013
Posts
18,416
Reaction score
30,738
Je, ipi ni Marathon kubwa zaidi Tanzania? Kilimanjaro Marathon au NBC Dodoma Marathon au CRDB Marathon?

Kwa miaka kadhaa sasa, Tanzania imekuwa na mbio za marathon zinazovutia maelfu ya washiriki kutoka ndani na nje ya nchi. Miongoni mwa marathon zinazozungumzwa zaidi ni Kilimanjaro Marathon, NBC Dodoma Marathon na CRDB Dar Marathon

Kilimanjaro Marathon

Hufanyika jijini Moshi, mkoani Kilimanjaro, ikiwa na historia ndefu na ushiriki wa wakimbiaji wa kimataifa. Mbio hizi zimechangia kuitangaza Tanzania kupitia utalii, hasa kwa kuhusishwa na Mlima Kilimanjaro, na huwavutia washiriki kutoka mataifa mbalimbali. Pia huleta mchango mkubwa katika uchumi wa eneo kupitia hoteli, usafiri na biashara nyingine zinazohudumia wageni.

NBC Dodoma Marathon
Hufanyika jijini Dodoma na imekua kwa kasi katika miaka ya karibuni. Mbali na mashindano ya riadha, marathon hii imejikita kwenye shughuli za kijamii kwa kukusanya fedha kwa ajili ya kusaidia sekta ya afya, ikiwemo huduma za afya ya mama na mtoto pamoja na magonjwa mbalimbali kupitia ushirikiano na taasisi za afya. Pia imekuwa ikivutia maelfu ya washiriki kila mwaka.

CRDB Bank Marathon (Dar es Salaam)
Hufanyika jijini Dar es Salaam na ni moja ya marathon zinazokuwa kwa kasi nchini. Mbio hizi zimejikita katika kuhamasisha afya na mazoezi, huku zikiwa na lengo la kuchangisha fedha kwa ajili ya kusaidia huduma za afya kupitia CRDB Bank Foundation.

Kwa mtazamo wako, ipi ni marathon kubwa zaidi kati ya hizi tatu?

Je, ipi iwe Mfalme wa Marathon zote Tanzania?
 
Hakuna sehemu yoyote niliyosema sipendi marathon, ila kuna mtu kasema kuna ma-ujinga na mimi nikauliza ma-ujinga gani?
Wakimbiaji wale wa ushindani ni wachache.
Zawadi mshind wa kwanza nadhani ni 15 Mill.

Sasa hawa wengne wanaenda kula bata.
Na baadhi ya Ofisi zinatoa ruhusa na posho kuhimiza wafanyakaz wao washiriki. Ila ni kama wasindikizaji.

Baada ya kusindikiza Wakimbiaji.
kinabakia ni Pombe, nyama choma na kunyanduana.

Ni kama Kijoint together flan hivi.

Na kama demu mnafanya nae ofisi moja . Mkifika kule mnachukua room moja. Kunachobaki ni Humu tu humu tu😊😊😊😊.

Niliwah kushiriki mara moja.
Nilipelekwa na ofisi.
 
Hua nashindwa kuamini unatoka mkoa wako unaenda mkoa mwingine kwa ajili ya kukimbia tuu, lazima kuwe na sababu nyingine nyuma yake.

Kwamba unatoka Dar unaenda Dom ili ukimbie tuu kisha urudi Dar
Makampuni mengi yakibiashara hutumia hizi nafasi kujibrand kuna watu wanalipwa kabisa Night na tickets kwenda kwenye hizi marathon
 
Back
Top Bottom