Kile kipindi ambacho nilipotea

Kile kipindi ambacho nilipotea

Nimetamani kusimulia hiki kisa muda sasa lakini waungwana walikuwa hawajatoa ruhusa bado.

Nilipotea kwa vipindi viwili vyenye jumla ya siku 23, kati ya siku hizo ni siku chache sana nilikuwa nje ya Tanzania, nyingine zote nilikuwa hapa hapa ila kwenye dunia isiyoaminika na wengi, dunia ya ushirikina na uchawi katika uhalisia wake.

Nitangulie kuomba radhi sitaandika kila kitu bali yale ya muhimu tu nitakayoona ni muhimu kuandika.

Nilitoka Dar kwa dharura kuelekea sehemu ambako nitapata kile kinachonipeleka huko, safari yangu ikanipeleka mpaka Nyamisati, nikalala pale.

Siku ya pili asubuhi nikadamkia bandari bubu iitwayo gezani.... vituko vilianzia hapo.
Nyamisati...kaka wale wenzako wenye tunguli za kuvutia samaki uliwakuta...pale hawavui kwa kujichosha...
Samaki huvutwa kuja nch kavu kwa tunguli
 
hivi haujapata hata dawa tumroge yule jamaa wamagogonia kabla hajaamia dodoma,kama vipi nipe msaada wakwenda kuzimu nikatete na wale jamaa wakule tumalize kazi
Umechelewa...alipoapishwa tu...akapewa na walinzi wa Papa...hautoelewa wewe bado ukakuwa
 
Nyamisati...kaka wale wenzako wenye tunguli za kuvutia samaki uliwakuta...pale hawavui kwa kujichosha...
Samaki huvutwa kuja nch kavu kwa tunguli
Wapo kina mzee wa Kina.. Achana kabisa na ile number
 
Endeleza story...walinzi sisi lazima...tujifunze somo ra maarifa na hali za kichawi machale....nilifika hapo 2009
 
Rasta nyoka Huyu nahodha wetu ndio yule jamaa mrefu , alitusimulia mengi kwa sharti la kutoyasema popote nami sitayasema hapa...nitaandika yale aliyokubali tu kusemwa, Huyu jamaa husafiri bure popote kama akiamua hula chochote popote bila kulipa, mambo anayofanya si kwa utashi wake bali kuna roho ndio zinamuongoza
Rasta zake si nywele kama nywele za kawaida, gesti tuliyolala anasema ni kituo na mapito, muda mwingi huishi huko visiwani kwenye mapori ya mikoko
Husaidia majahazi ya Zanzibar na Pemba kupeleka mbao za mikoko bila kukamatwa na maliasili, pesa anayolipwa hatumii yeye
Hana wazazi hana familia, amekulia visiwa vya nyamisati, mengine hayasemi mengine sitayasema
Tulifanya ziara ya woga kwenye visiwa vine tu hatukuwa tayari kulala kisiwa chochote na nahodha wetu
Tulimaliza na kisiwa cha Simbaulanga, kisiwa mdomo wa kuingia baharini au kuingia njia ya Nyamisati
Ukimaliza nipatie contacts za huyo rasta..
 
Tulirejea nyamisati jioni tukalala pale, rasta nyoka hakuwepo tena hatukupeana namba sikumuona na somu hakupenda tupige picha hata moja
Kuna mengi sikuyasimulia hapa nimetii agizo , ila hapo Nyamisati Gezani , kilwani na visiwa vinginevyo Kuna siri kubwa kuhusiana na rasta nyoka...ukibahatika kwenda huko jaribu kumuulizia
Dah
 
Back
Top Bottom