Kile kipindi ambacho nilipotea

Kile kipindi ambacho nilipotea

Nyamisati... dah umenikumbusha hapo sehemu tushapanda sana dau kwenda Mafia.. Maisha haya...
 
Nimetamani kusimulia hiki kisa muda sasa lakini waungwana walikuwa hawajatoa ruhusa bado
Nilipotea kwa vipindi viwili vyenye jumla ya siku 23, kati ya siku hizo ni siku chache sana nilikuwa nje ya Tanzania, nyingine zote nilikuwa hapa hapa ila kwenye dunia isiyoaminika na wengi, dunia ya ushirikina na uchawi katika uhalisia wake
Nitangulie kuomba radhi sitaandika kila kitu bali yale ya muhimu tu nitakayoona ni muhimu kuandika
Nilitoka Dar kwa dharura kuelekea sehemu ambako nitapata kile kinachonipeleka huko, safari yangu ikanipeleka mpaka Nyamisati, nikalala pale...
Siku ya pili asubuhi nikadamkia bandari bubu iitwayo gezani.... vituko vilianzia hapo
Nikiwa pale bandari bubu upande wa pili wa bahari nikamwona mtu mrefu sana akiwa kavaa kanzu nyeupe na kitambaa kichwani Chenye rangi nyeusi na nyeupe hiki kitambaa kilimfunika uso wote kasoro macho
Huyu mtu mrefu sana alikuwa anatembea kwenye tope kuja tulipo (kumbuka ilikuwa maji kupwa )mshangao wangu ulikuwa ni yule jamaa kutembea juu ya tope bichi bila kuzama na kanzu yake nyeupe
Ilibidi niwaambie wenyeji wangu wale vijana wala majani wakanicheka sana wakasema hakuna kitu kama hicho hayo ni maruerue tu ya 'bichi'
Sikutaka kuendeleza ubishani kwakuwa najua ila yule mtu mrefu alikuja na kutupita karibu kabisa...mimi nilimuona wengine hawakumuona
 
Back
Top Bottom