Kila mradi wa ujenzi wa Serikali kuwe na separation of duties usifanywe na taasisi moja, ni rahisi kuibiwa na kuwa na jengo substandard

YEHODAYA

JF-Expert Member
Aug 9, 2015
36,908
51,904
Unakuta mradi wa Serikali Mfano bango linaonyesha

Contactor ni NHC
Architect ni NHC
Quantity Surveyor ni NHC
Subcontractor ni NHC

Hakuna segregation of duties

Inatakiwa mfano Architect awe mwingine siyo NHC aweza kuwa Private sector au quantity surveyor akawa Private sector na subcontractor akawa private sector kuwe na mchanganyiko

Hii itadhibiti ubadhirifu,wizi na ujenzi wa majengo kuwa substandard sababu mtu hatakiwi afanye kila kitu kuanzia mwanzo hadi mwisho taasisi moja hiyo hiyo chini ya serikali hiyo hiyo kuwe mchanganyiko wa public na private kwenye miradi ya ujenzi yote
 
Lakini tenda za ujenzi zilikua zinatangazwa kwani?

Si ilikua Rais anapoint tu Wakala wa Majengo achukue tenda au atawapa JKT au Mayanga Construction.
 
Kwa maelezo yako

Chanjo hujachanjwa
Nyungu hujapiga
Hujajifungia unaenda kazini kila siku

Mbona hujafa na corona sasa?
 
Labda ianze sahivi, hapo nyuma ilikua mchora ramani yeye, mjenzi yeye, mlipa hela yeye, mkaguzi yeye... kisha anarudi kwa wanyonge na bla bla
 
Waliokuwa wakiyasema hayo mliwatukana na wengine hata kuwapiga risasi.
 
Waliokuwa wakiyasema hayo mliwatukana na wengine hata kuwapiga risasi.
Hivi wewe unaenda kumshauri bosi wako unaanza na neno Bwege atakusikiliza hata kama una hoja? Eti wewe bwege ngoja nikupa ushauri si atakukimbiza na marungu hata kabls hujaongea .

Eti unaanza ushauri unaannza na kusema wewe Jiwe au wewe Mataga unategemea nini? Usikilizwe ?presentation ya ushauri how you begin matters a lot.Ndio vyu.hukesha kufundisha prrsentation skills kwa theory na Practice tatizo wengi hawa pay attention akishamaliza chuo anatupilia mbali notes na kusema yale yalikuwa mambo ya darasani tu huku mimi nitamwita mtu
mataga au Jiwe tu sijali.
Ulimikiungo kidogo lakini matatizo yake makubwa usipoudhibiti
 
Back
Top Bottom