Hoteli ya nyota Tatu inajengwa Chato, Wana-CCM mnafurahishwa na kitendo cha kupeleka kila mradi wa ujenzi Chato?

Bujibuji

JF-Expert Member
Feb 4, 2009
57,975
2,000
Chato.JPG

Maelezo ya Picha: Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mary Masanja(Kulia) akikagua hoteli ya nyota tatu inayojengwa na Hifadhi za Taifa Tanzania inayojengwa Wilayani Chato mkoani Geita.
Mwalimu Nyerere akijua kabisa kuwa kuku wa taifa lazima aliwe na wote, aliamua almasi inayochimbwa Shinyanga Mwadui ikakatwe Iringa, ili Wanyalu nao wafaidike na madini hayo.

Hakupeleka kiwanda Cha Tancut Almasi Mara wala Butiama.
Magufuli amekuwa ni mtu wa kupendelea kwao tu utadhani Tanzania ni Chato tu.

1. Uwanja wa ndege mkubwa umejengwa Chato
2. Wanyama wamesombwa huko Serengeti, wamepelekwa Chato.
3. Uwanja mkubwa wa michezo kujengwa Chato.
4. Hospitali ya Kanda ya Ziwa imejengwa Chato.
Je, wanaccm mmeshindwa kukemea upendeleo huu?

Mjulisheni Mwenyekiti wenu kuwa anachokifanya sio uzalendo, ila ni ubaguzi. Anawabagua watu wasio wa Chato.

Kuku wa Taifa lazima aliwe na wote, hata watu wa Ileje na Tandahimba wanahitaji kwao kujengwe, sio kila kitu Chato tu

===

Naibu Waziri wa Utalii Mary Masanja akagua miradi ya utalii Geita​

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja amefanya ziara katika Mkoa wa Geita ambapo pamoja na mambo mengine amekagua miradi mbalimbali ya kiutalii inayotekelezwa na taasisi za Wizara ya Maliasili na Utalii mkoani humo, anaripoti John Bera (WMU) Geita.


Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja (katikati) akiwasili kukagua hoteli ya Nyota 3 ya Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania ( TANAPA) inayojengwa wilayani Chato mkoani Geita wakati wa Ziara yake ya kikazi ya kukagua miradi mbalimbali ya Wizara ya Maliasili na Utalii ya mkoani Geita. Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Chato, Eng. Charles Kabeho na kulia ni Kamishna Mwandamizi wa Uhifadhi Kanda ya Magharibi, Martin Loibooki.

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja (kushoto) akizungumza na Mkuu wa Mkoa wa Geita, Mhe. Robert Gabriel kuhusu mpango wa Wizara ya Maliasili na Utalii wa kutaka kuanzisha Utalii wa Madini katika mkoa huo wakati wa Ziara yake ya Kikazi mkoani humo.

Akiwa katika ziara hiyo amefanya mazungumzo na viongozi wa Serikali wa mkoa na wale wa taasisi zilizo chini ya wizara kuhusu namna bora ya kutangaza vivutio vya utalii vinavyopatikana katika mkoa huo.

Aidha, Mhe. Masanja ametembelea Mradi wa Ujenzi wa hoteli ya Kitalii ya Nyota 3 inayojengwa wilayani Chato mkoani Geita na kuagiza ujenzi wa hoteli hiyo ukamilike haraka ili watalii waanze kupata fursa ya kutumia huduma za malazi katika hoteli hiyo na kutembelea hifadhi mbalimbali zilizopo Kanda ya Ziwa.


Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja (kulia) akiwa anashuka kwenye hoteli ya Nyota 3 ya Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania ( TANAPA) inayojengwa wilayani Chato mkoani Geita wakati wa Ziara yake ya kikazi ya kukagua miradi mbalimbali ya Wizara ya Maliasili na Utalii ya mkoani Geita. Katikati ni Mkuu wa Wilaya ya Chato, Eng. Charles Kabeho.

Amesema, Wizara ya Maliasili na Utalii itaendelea kushirikiana na uongozi wa Mkoa wa Geita kuhakikisha shughuli za utalii zinasonga mbele huku akitoa rai kwa viongozi hao kuweka mkazo katika zao la asali ambalo amesema likisimamiwa vizuri litaongeza mapato.

"Tuhamasishe zao la asali linalotokana na nyuki, sasa hivi kuna mnyororo mkubwa wa thamani ambao Serikali inaendelea kuupigania kwenye mazao ya misitu, hii itasaidia wananchi kuongeza kipato pia pato la Taifa,"amesema Mhe. Mary.

Aidha, ameongeza kuwa Wizara ya Maliasili na Utalii iko katika mpango wa kuanzisha Utalii wa Madini ambao kwa Kanda ya Ziwa utasaidia kuongeza idadi ya watalii na mapato.
 

Cvez

JF-Expert Member
May 19, 2018
1,636
2,000
Akili Utopolo ndio hizi Serengeti na Tarangire hifadhi zinazoingizia TANAPA mapato ya kutosha kwa miaka kadhaa wadau wamekua wakiiomba TANAPA ijenge hotels ili kuwezesha Mtanzania wa kawaida aweze pata huduma za malazi yaliyobora.

Ila hakukua na kitu kama hicho zaidi ya public campsites ambazo usalama ni zero ila leo wanaenda kufanya uwekezaji sehemu ambayo hata kujiendesha kwa faida haijaanza. Huu ni zaidi ya Utopolo.
 

Bujibuji

JF-Expert Member
Feb 4, 2009
57,975
2,000
Akili Utopolo ndio hizi Serengeti na Tarangire hifadhi zinazoingizia TANAPA mapato ya kutosha kwa miaka kadhaa wadau wamekua wakiiomba TANAPA ijenge hotels ili kuwezesha Mtanzania wa kawaida aweze pata huduma za malazi yaliyobora. Ila hakukua na kitu kama hicho zaidi ya public campsites ambazo usalama ni zero ila leo wanaenda kufanya uwekezaji sehemu ambayo hata kujiendesha kwa faida haijaanza. Huu ni zaidi ya Utopolo.
Kuna haja ya ku practice uzalendo kwa vitendo
 

Nyendo

JF-Expert Member
Jun 4, 2017
565
1,000
Chato.JPG

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mary Masanja( kulia) akiwa anashuka kwenye hoteli ya nyota 3 ya shirika la Hifadhi za Taifa inayojengwa wilayani Chato mkoani Geita.

Akiwa katika ziara yake ya kikazi kukagua miradi mbalimbali inayojengwa na Wizara ya Maliasili na Utalii Mkoani Geita.

Katikati ni mkuu wa wilaya ya Geita Mhandisi Charles Kabeho.
 

Bujibuji

JF-Expert Member
Feb 4, 2009
57,975
2,000
Muulize mbunge atakuambia!
Mbunge ndio financer? Niko hapa Isoko, na ninatembea almost kila Kijiji kwa ajili ya biashara zangu za minadani, usafiri ni wa hovyo, maji hamna, huduma za afya ni za hovyo, watu wanatolewa hospital wanapelekwa kwa waganga na kwenye maombezi.

Hiyo miradi iko wapi? Sisi watu was pande hii tumeikosea nini serikali?

Mnasema wapinzani wametuchelewesha Sana. Mbona hili Jimbo halijawahi kuwa chini ya upinzani?
 

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
42,113
2,000
Mbunge ndio financer? Niko hapa Isoko, na ninatembea almost kila Kijiji kwa ajili ya biashara zangu za minadani, usafiri ni wa hovyo, maji hamna, huduma za afya ni za hovyo, watu wanatolewa hospital wanapelekwa kwa waganga na kwenye maombezi...
Labda mbunge ni mbwiga hujawaona wenzake Taletale wa Morogoro na Mtemvu wa Kibamba walivyochangamka!
 

macho_mdiliko

JF-Expert Member
Mar 10, 2008
13,408
2,000
Kuna haja ya ku practice uzalendo kwa vitendo
Wabunge wote wako pale kwa hisani yake. Watathubutu kusema chochote? Jamaa aliona mbali. Alijua akiwaweka kwenye nafasi hizo hawawezi kufungua mdomo kwani mtu hawezi kukata mkono unaomlisha. Na hii miradi inaashiria kitu kimoja: Bado yupo sana kuhakikisha ameikamilisha na kuisimamia. Yupo beyond 5 years to come. Labda watanzania wawe wakali kweli kweli tena kweli ashindwe kujiongezea muda. Ila bado ataweka kikaragosi chake atakachokiendesha remotely.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom