Kila mfanyakazi anayo haki ya kugoma. Hata hivyo, sio kila mgomo unatambuliwa na Sheria

Sildenafil Citrate

JF-Expert Member
Jan 29, 2021
573
2,553
Mgomo ni usimamishaji wa kazi, unaofanywa na Wafanyakazi kwa lengo la kumlazimisha au kumshurutisha Mwajiri wao au Mwajiri mwingine au Jumuiya ya Waajiri ambayo Mwajiri wao ni mwanachama, kukubali madai ya Wafanyakazi, au Mwajiri kubadili au kuacha madai yake dhidi ya Wafanyakazi, madai ambayo yanahusiana na mgogoro wa maslahi.

Haki ya kugoma
Kila mfanyakazi anayo haki ya kugoma. Hata hivyo haki hii ya kugoma ni kwa migogoro ya maslahi peke yake. Kwa msingi huo chini ya Sheria ya Ajira na Uhusiano Kazini, Wafanyakazi hawaruhusiwi kugoma iwapo mgogoro wao ni lalamiko au mgogoro wa kudai haki.

Kuzuizi cha kugoma
Pamoja na haki ya kugoma kutolewa kwa kila mfanyakazi, wapo baadhi ya Wafanyakazi ambao wamenyimwa haki hiyo. Wafanyakazi hao ni hawa wafuatao:-
  • Wafanyakazi katika huduma muhimu
  • Wafanyakazi ambao wanapaswa kuendelea na kazi wakati wa mgomo kwa makubaliano ya pamoja ya utoaji huduma kwa kiwango cha chini.
  • Wafanyakazi ambao wanabanwa na makubaliano ya kupeleka mgogoro huo kwenye uamuzi
  • Wafanyakazi ambao wanabanwa na makubaliano ya pamoja au TUZO ya mwamuzi inayosimamia suala la mgogoro.
  • Mahakimu, Waendesha Mashitaka au Watumishi wengine wa Mahakama.
  • Wafanyakazi wanaobanwa na Tangazo la Kima cha Chini cha Mshahara na Masharti ya kazi yanayosimamia suala la mgogoro katika mwaka wa kwanza wa kutumika Tangazo hilo.
Utaratibu wa mgomo
Ili mgomo uwe halali ni lazima wafanyakazi wafuate hatua zifuatazo:-
  • Mgogoro uwe mgogoro wa maslahi
  • Mgogoro uwasilishwe Tume ya Usuluhishi na Uamuzi kwa ajili ya usuluhishi kwa kutumia fomu maalum (Fomu CMA 1)
  • Mgogoro uwe umeshindikana kusuluhishwa ndani ya siku 30 au zaidi kadri pande husika zitakavyokubaliana.
  • Kura za kuunga mkono mgomo zipigwe na wafanyakazi husika kwa mujibu wa Katiba ya Chama cha Wafanyakazi.
  • Notisi ya saa 48 ya kuanza mgomo itolewe kwa Mwajiri. Saa 48 zitakazohesabiwa ni saa za kawaida za kazi na notisi ni lazima ieleze mgomo utakuwa wa siku ngapi.
Hata hivyo wafanyakazi wanaweza kugoma bila kufuata utaratibu huo hapo juu, endapo itatokea Mwajiri akabadilisha masharti ya kazi bila kushauriana nao.

Endapo itatokea hali hiyo, wafanyakazi wanachotakiwa kufanya ni kuwasillisha mgogoro kwenye Tume kwa fomu maalum (Fomu CMA 1) wakimtaka Mwajiri kutotekeleza mabadiliko hayo au kama ameshaanza kutekeleza, kuyarejesha masharti ya awali kabla ya mabadiliko.

Endapo Mwajiri hatatekeleza madai yaliyoelezwa na Wafanyakazi ndani ya saa 48 kuanzia saa aliyopokea nakala ya fomu ya mgogoro, wafanyakazi wanaweza kugoma.

Vitendo vinavyokatazwa wakati wa mgomo
  • Piketi, kuunga mkono mgomo
  • Kutoajiri na kutumia wafanyakazi wapya mbadala wakati wa mgomo
  • Kuwafungia Waajiri ndani ya eneo la kazi
  • Kuwazuia Waajiri kuingia katika eneo la kazi
 
Back
Top Bottom