Kila mchezaji wa Taifa Stars kupata Tsh milioni 10 iwapo timu itafuzu kucheza AFCON

Tunawatakia ushindi ingawa kwa watumishi wa umma nadhani tutakua tumejifunza kitu. Tumekuwa tukiwalazimisha watoto wetu wasome ili baadaye waajiriwe na mwisho wa siku wanaishia kupata mshahara kiduchu mwisho wa mwezi.

Ona sasa kwa hao wachezaji ambao wengi wao hawajosoma kivile, lakini kupitia vipaji vyao vya kucheza mpira, wanalamba mamilioni ambayo kwa watumishi wa umma wanapokopeshwa hela kama milioni 10, watailipia kwa miaka 5 na kutozwa riba mara dufu. Nb: tuheshimu vipaji vya watoto wetu.
Sasa vijana wote wakicheza mpira bongo hii itakalika??
 
Mnamuonea. Hivi nikiwaambia amemuomba "baba" yake wa Magogoni na amempatia,mtabisha?Yeye na baba hufanya kazi zao kwa networking, ja!?
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Hivi mtu waanzaje shangia taifa staa ? Washangilia huku unangojea lesotho atakavyo score?
hata iwe
MSALABA 159 UGANDA 0
alafu Kap vedE 0 LEsotho 1 ni kazi bure.
 
Sasa hao wachezaji wanapewa hizo ela kwa kazi gani waliyoifanya maana hii mechi kuna wepesi wanafanyiwa na Uganda yani team imeshindwa kuifunga Lesotho mechi hata moja alafu leo uwapr pesa kirahisi

Kuna wanamichezo wengi tu tanzania wamefanya vuzuri lakini sikumbuki kama walitunzwa vizuri.

Hizo fedha si zinaweza kuboresha moja ya vieanja hapa Tanzania bora ziende huko
 
Sasa vijana wote wakicheza mpira bongo hii itakalika??

Vipaji vipo vingi na kucheza mpira ni sehemu tu! Nimetoa tu rai kwa jamii kubadili mtazamo wa kuwaaminisha watoto ya kuwa kusoma na kuajiriwa ndiyo njia pekee ya kutoka kimaisha.
 
Ninachokijua Ni Kuwa Hazina na TRA waliufyata kwa Governor wetu wa Jimbo kuu la Dar Es salaam

Ushaskia Tena Cha Mnada
Maana yake utaratibu wa kukusanya mapato wa TRA ulikiukwa halafu tutegemee kuacha kuwa omba omba.
 
Mwenyekiti wa Kamati ya Saidia Taifa Stars Ishinde RC Paul Makonda amesema kamati yake itatoa Sh10m kwa kila mchezaji iwapo timu itafuzu kucheza AFCON
Timu itafuzuje wakati ipo nafasi ya tatu! Hau wataifunga Uganda alafu wanakimbia kwenda kuisaidia cape Verde kuifunga Lesotho!!!?

Makonda hawe anatoa ahadi inayotekelezeka, bora angesema stars wakishinda mechi ya Uganda siyo wakifuzu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hawa ni watumishi wa umma katika awamu ya tano. Mkuu wa Mkoa mshahara wake milioni nne kwa mwezi na hajawahi onyesha biashara zake anatoa wapi haya mamilioni?

Tusitumie Timu ya Taifa kutakatisha fedha wala tusitumie timu yetu kuwalisha vitu haramu. Tujue chanzo cha haya mabilioni anayotoa Mkuu wa Mkoa tena mbele ya Waziri Mkuu wa nchi.

Naamini Majaliwa mwenyewe hana huu utajiri

Sent using Jamii Forums mobile app
Nyie mlizaliwa kwenye zizi la ng'ombe????hujui main sponsor wa Taifa stars ni Serengeti Breweries... Sasa 300 m kampuni kubwa kama ile inashindwaje kutoa..Uganda mwaka juzi walipewa 40 m
 
Back
Top Bottom