Tango73
JF-Expert Member
- Dec 14, 2008
- 2,128
- 1,225
Pamoja na ngeke la kufuzu Afcon lakini ukweli lazima usemwe kuhusu maufa ufa yaliyojaa katika timu ya Taifa stars. kwa ukweli kabisaa taifa stars haina ubora wa soka la kitabuni ambalo Yanga na Simba wanalionesha kwa mashabiki wao kila kukicha. tatizo kubwa likiwa ni kocha mtaalamu ambaye anafundisha soka la kisasa lenye ubora wa kulinda na kushambulia kama ilivyo Senegal,Cameroon, Ghana na Nigeria.
Kwa mantiki hii ya uzaifu wa taifa stars tusitarajie kuuza mchezaji mzalendo katika timu kubwa ulaya, uarabuni na latina america.
Ukiondoa 1982 afcon ya Nigeria, kila mara taifa stars hufanikiwa afcon kwa kubebwa na timu ya mwisho iliyojihakikishia kushinda. Misri afcon tulibebwa na Uganda mechi ya mwisho na leo watoto wa Ahmed ben bella wametubeba katika mechi ya mwisho.
Matokeo yake tunapocheza mechi za fainali za afcon kutafutwa bingwa timu yetu huonesha mchezo mbovu sana halafu huwa tunaonewa na kila mpinzani wetu. hivyo wachezaji wote huonekana hawana jipya la kupata soko huko kwenye ligi tajiri la kuwapa utajiri nje ya bahari.iweje TFF haiiigi kutoka kwa Yanga jinsi ya kuboresha timu? mbona yanga ilitoka katika udhaifu na kupambana kisayansi mpaka leo kuwa timu bora lenye kutisha Afrika?