Kila mchezaji wa Taifa Stars kupata Tsh milioni 10 iwapo timu itafuzu kucheza AFCON

mwanamwana

JF-Expert Member
Aug 1, 2011
1,060
4,042
Mwenyekiti wa Kamati ya Saidia Taifa Stars Ishinde RC Paul Makonda amesema kamati yake itatoa Sh10m kwa kila mchezaji iwapo timu itafuzu kucheza AFCON
 
Hawa ni watumishi wa umma katika awamu ya tano. Mkuu wa Mkoa mshahara wake milioni nne kwa mwezi na hajawahi onyesha biashara zake anatoa wapi haya mamilioni?

Tusitumie Timu ya Taifa kutakatisha fedha wala tusitumie timu yetu kuwalisha vitu haramu. Tujue chanzo cha haya mabilioni anayotoa Mkuu wa Mkoa tena mbele ya Waziri Mkuu wa nchi.

Naamini Majaliwa mwenyewe hana huu utajiri

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tunawatakia ushindi ingawa kwa watumishi wa umma nadhani tutakua tumejifunza kitu. Tumekuwa tukiwalazimisha watoto wetu wasome ili baadaye waajiriwe na mwisho wa siku wanaishia kupata mshahara kiduchu mwisho wa mwezi.

Ona sasa kwa hao wachezaji ambao wengi wao hawajosoma kivile, lakini kupitia vipaji vyao vya kucheza mpira, wanalamba mamilioni ambayo kwa watumishi wa umma wanapokopeshwa hela kama milioni 10, watailipia kwa miaka 5 na kutozwa riba mara dufu. Nb: tuheshimu vipaji vya watoto wetu.
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom