Kila January huwa napata ajali

Kila January huwa napata ajali

Raia Fulani

JF-Expert Member
Joined
Mar 12, 2009
Posts
11,866
Reaction score
4,252
Hii imenishangaza sana. Ni miaka minne mfukulizo. Pengine inaweza kuwa zaidi kwa kuwa sikufuatilia kabla. Natumia usafiri wa pikipiki. Sasa nikishapata ajali au kuanguka na pikipiki, basi sipati tena ajali mwaka wote. Au kuanguka.

Sasa mwaka ulivyoanza hii hali au kumbukumbu ikanijia. Na mara nyingi huwa ni kati ya tar 1 hadi 10. Sasa nikiwa njiani nakumbuka na najitahidi sana kuwa makini, ila ikipangwa imepangwa tu.

Leo imetokea. Bajaj aliyekuwa anatoka kwenye foleni bila umakini aliiingiza njia ya upande wa kulia nikajikuta namparamia. Nilidondoka vibaya nikaumia sehemu kadhaa. Ajali hiyo ilisababisha pkpk nyingine iliyokuwa inakuja mbele yangu kuharibika taa ya mbele.

Wakati naanguka nikawa nacheka tu nikijua tayari January imejibu. Pamija na kwamba niliumia, sikutaka kuhangaishana na bajaj. Nilichukua chombo changu na kuondoka nikimuacha kabananishwa na aliyeharibiwa taa. Nilijua ya January yametimia hivyo sikuwa na sababu ya kulumbana.
Hofu yangu ni kuwa hii trend itanijenge hofu ya January
 
Inaonekana mkuu hata kufa utakuja kufa mwezi january ya mwaka wowote!, hapo cha msingi badili ratiba zako january yote uwe unajifungia ndani uanze kusafiri mwezi february.
Suala la kufa bado sana kwa sasa, ila kama ni mwezi huo sina kipingamizi. Muhimu ni kuhakikisha January sipakizi mtu ili ikitokea niwe peke yangu
 
Back
Top Bottom