Kikwete yuko Vietnam

Kikwete yuko Vietnam

Unajua mlivyowajinga mnajitahidi kupotosha na kuhangaika na jk wakati wenzenu ccm wanaandaa vema mgombea ajaye nyie ukawa midomo mirefu kama chupa kazi umbea tu.

Kwa hiyo huyo mgombea ndio ameenda kutafutwa huko China na Vietnum?
 
Kwa hivyo Great Thinker unashauri Rais awe anabaki humu humu nchini ?? Halafu Marais wa hizo nchi za Ulaya, Marekani na Asia ndiyo waje wamtembeleee ? Wafanyabiashara na Wawekezaji waje kumtembelea ? Hiyo nayo SHULE !

Acha kuwa na akili fupi,hivi ni wafanyabiashara gani na wawekezaji wanaokuja hapa tanzania embu tupe data,hicho anochokifuata huko nje hata watanzania wana uwezo wa kukifanya sasa unaleta wawekezaji wakuja kuuza plastic na kununua machupa ya maji ya plastic kweli unawaita wawekezaji?
 
Mkuu Ritz hawa misukule wa UKAWA hawana jema, ndio maana tunawapuuza, wanamfananisha Rais wa nchi na Mzee Slaa ...

Ubarikiwe kwa kwa kuendelea kuwa na msimamo wa kuutetea ukweli pamoja na vikwazo mbali mbali kama MATUSI, VITISHO, KEJELI, na kila aina ya dhihaka kutoka kwa wafuasi wa CHADEMA.

Ni aibu kubwa kutetea ufisadi rushwa elimu kuanguka dawa hakuna
 
Last edited by a moderator:
Mnahangaika sana. JK ni mchapakazi hodari na akitoka ziara za nje kama kawa anafanya ziara za ndani

Mkuu hawa misukule hawajui hilo, JK ni Rais bora zaidi kusini mwa jangwa la sahara.

Wanapokosea ni kumlinganisha Prof.Jakaya na Padri BABU.
 
Kikwete ameingia Vietnam kwa ziara na msusururu wa Mtu kama miaa hivi, kudadeki... halafu kama hiyo haitoshi Pinda naye yuko Ulaya naye kabeba mtu kama 100 hivi na hiyo ni kwa wiki mbili sasa, huku nako Mwandosya yuko Zambia, achilia hao wengine ambao wala Ziara zao hazitangazwi kudadeki... hivi hakuna Mtu wa kumpindua huyu Jamaa arghhhhhhhhhh!

Na bado ana muda kibao kuendelea kuwatawala Watanzania ,halafu utawasikia ccm kwenye majukwaa ya kisiasa "nchi hii ni masikini".

Umasikini upo wapi wakati mna pesa za kumlipia raisi atekeleze majukumu yake angani!!!!.
 
Kwa hivyo Great Thinker unashauri Rais awe anabaki humu humu nchini ?? Halafu Marais wa hizo nchi za Ulaya, Marekani na Asia ndiyo waje wamtembeleee ? Wafanyabiashara na Wawekezaji waje kumtembelea ? Hiyo nayo SHULE !

We kweli matango aisee
 
Mbowe alikuwa South Africa akaunganisha Oman kisha akarudi Dar es Salaa, leo kaenda Hai.

Alikuwa na msafara wa watu wangapi? ziara zake zinatumia pesa za walipa kodi? Kutwa kuzurura halafu analazimisha kukata watu mishahara kwa kisingizio cha maabara, shule zijengwe maabara zishindikane? Amezidi sasa.
 
Viongozi wa Tanzania wana 100% attendance ya mialiko ya nje ya nchi... Kuanzia wafanyakazi, waBunge... Wote wa vyama vyetu na wakiongozwa na Mkuu wa NCHI....
 
Hivi wale waliosema kuwa nchi haitatawalika wapo hai au wamekufa?

Kwani sasa inatawalika? Kila mtu anaropoka lake necta wanataka daftari la wapiga kura, nape hataki, katiba isipitishwe kabla ya daftari la wapiga kura, mara president kapanga april, hakuna kutangaza nia ya kugombea urais, atakae tangaza atafukuzwa uanachama, watu wanaendelea kutangaza nia mpaka BBC. Nchi haitawaliki imekuwa mnara wa babeli, na makundi yatawanya waanze wao kupigana.
 
JK halaumiki ameenda kutafuta soko la kuuza mananasi, alisema akiacha urais ataenda kulima mananasi

Na kufuga mbuzi, naona ananza tabia ya mbuzi maana wanyama wafugwao mbuzi anaongoza kwa uzururaji, jamaa yuko field aweze kwenda sambamba na mbuzi
 
Ahhha Tafadhali bhana! Yaani Kikwete aajiriwe na NASA? Niijuavyo NASA hakuna hata kitengo kimoja ambacho Kikwete anaweza kushiriki ndani ya NASA hata kama NASA wanatafuta mtu tu wa kubonyeza kitufe kila atakapoona ishara fulani tu kwenye Kompyuta, huyu jamaa hawezi kupita huo Usaili!

Dr. Slaa akipokea zawadi maalum ambayo rais wa marekani tu ndiye aliyewahi kupewa

Source: CHADEMA DIASPORA : Breaking News: Dr. Slaa Ndani Ya NASA. Aionya CCM Kwa Kuuwa Elimu na Ubunifu !

Hata haya hamuoni kuzuwa?
 
mkuu pinda akitoka poland anakwenda oman si unajua sultan zawadi zake ni mwendo wa bata kwenda mbele


Tujiandae kusikia nayeye kahongwa Suti na Saa kama yule mwanariadha ambaye amezunguka dunia nzima!
 
Kikwete amepoteza utu wa mtanzania. Kuwa ombaomba siyo sifa, ni aibu, ni kukiri unyonge wa akili na moyo.

Kama Kikwete hawezi kufikiri atashindwa hata kutazamia? Wenzetu Kenye uchumi wao unazidi kuimarika kwa mipango thabiti ya Wakenya na Rais wao, sisi wa kwetu kila siku kiguu na njia, unadhani nyumbani kafukuzwa.

'Siku moja akapatikana kiongozi wa Taifa letu, akasema huko nje kuna pesa kuliko hapa nyumbani, mwambieni, wewe ni mpumbavu'. Rais wetu anaamini huko nje kuna pesa kuliko hapa nyumbani.
 
Nasikia NASA walimpa zawadi ya begi Dr.Slaa hiyo zawaidi wameishapewa watu wawili tu duniani, Dr.Slaa na Obama.

teh teh teh

Hata ile zawadi ya suti ilikuwa ya kipekee duniani kwa kiongozi wa nchi kupewa. Na zinampendeza kweli.
 
Ni aibu kubwa kutetea ufisadi rushwa elimu kuanguka dawa hakuna
Ufisadi gani kuchukuwa ruzuku na kwenda kununua nyumba Dubai na kukiuzia chama fuso chakavu kwa milioni 400.
 
Back
Top Bottom