Kikwete Vs. Mkapa

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,667
40,546
"Kikuu kinanukia aaa.. yeke yekee komoa yeke yeke"

Kuna kila dalili kuwa kuna mtu yuko karibu kumtolea uvivu mwingine. Kwa kadiri mambo yalivyo bila ya shaka Rais Kikwete anajikuta yuko njia panda, hajui afanye nini na Mkapa. Bila ya shaka mojawapo wa majeruhi wa sakata la Balali atakuwa ni Mkapa. Lakini Kikwete ataweza kumnyoshea kidole Mkapa bila yeye mwenyewe kujinyoshea kidole hicho hicho? Je wakati utapofika ataweza kumtosa Mkapa?

Beti wamezipoteza
Wakidhani wameweza,
Moyoni wakajikuza,
Waliko wakajikweza!

Fikira ni kama wingu
Kamwe hazifungwi pingu
Wajizanio miungu,
Rohoni wana machungu!

Zinazimwa kompyuta,
Na seva wakazifuta,
Wakidhani wamepata,
Jambo yetu itajuta!

Mbona bado twasimama,
Na hoja tunazitema,
Kamwe haturudi nyuma!
Mafisadi mmekwama!

Fisadi numero uno,
Mkapa mwenye maneno,
Aliyejaa unono,
Na kiburi kama pono!

Na anayemfuata,
Mramba mwenye kunata,
Benki yetu wamechota,
Tetemeko kuwapata!

Jambo hii itadumu,
Kwa chungwa hata kwa ndimu,
Mbakie kulaumu,
Mafisadi wadhalimu!

Mtajiju!!!!
 
Kijiji sijui kuandika mashahiri lakini nitakuwa balali na kuchapia hivi

Michuzi tumekula, mkapa,mramba na mwaimuna
wabongo tumewala, hata kama wananuna
Pesa ndiyo tawala,maneno maneno ni kama pumba
Wabaya mtaandika nakala, sisi tunapesa hamtatufuma.

Nilianza masikini, Nimetoka milionea
Nilifanya kwa makini,Hata darubini haikuonea
Wizi ni kama uhaini, Domo kubwa sikuongea
Sasa natanua mitini, wabongo wote mnaongea

Nilioa na mke wa pili, kwa wali na kachumbali ulaya
Kila mtu alinitii, daktari na pesa ilembaya
nilikua kama nabii, kujua uchumi mzuri na mbaya
Sijui kama nilistahili,lakini nilitesa ilembaya

Kakaja haka kaswahili, maneno mengi vitendo hafifu
Kamekaa kibahili, mawaziri wake wala kikamilifu
Anza na namba mbili, wala rushwa wakubwa si waadilifu
Eti na bilioni mbili, mikataba nyie ndiyo waalifu

Wobongo wivu mwingi, Hata nikifungwa nimetesa
madongo kelele mingi, Ha Ha daktari sasa anapesa
Maneno hayajengi msingi, ni jitihada na pesa
Si muhindi wala mangi, samahani daktari anapesa
 
Naona mnanisema , kila kunapokucha
Eti mimi fisadi, nilificha makucha
Michuzi kuwaibia,nakuwaacha mmechacha
Naishi kwa wasiwasi, lupango kunanukia.
 
Bismillahi naanza, wa Rehema Rahamani,
Wakili ulo muweza, Subihana Maanani,
Maliki mwenye kujaza, ya dunia na mbinguni,
Wabarakatau walid, mtetezi wa Kuduri!

Mtoto nipe kalamu, nikae chini nitunge,
Niyasema yalojimu, kwa tungo chache nipange,
Lile niloazimu, la mafisadi nilonge,
Mkapa atiwe pingu, asimamishwe Kisutu?

Kikwete ataliweza, la kumfunga kengele,
Paka mwenye kujikuza, ajaye bila kelele,
Ili watu kuwajuza, hatari iliyo mbele,
Mkapa atiwe pingu, asimamishwe Kisutu?

Au ndiyo imetoka, kama mabasi ya Keko!
Balali kishatimka, katuacha na mbeleko,
Mgonja akichopoka, kama kinyaa na toko,
Mkapa atiwe pingu, asimamishwe Kisutu?

Mapesa wameyachota, Kikwete yu njia panda,
Ni sime atajikita, Jitu Pateli adunda,
Mwenye kupata kapata, walokonda wamekonda,
Mkapa atiwe pingu, asimamishwe Kisutu?

Mramba mtapata, akaishie Maweni,
Au twacheza kalata, magelesha ni yanini,
Na wengine watanata, au ndiyo magirini,
Mkapa atiwe pingu, asimamishwe Kisutu?

Beti zangu zinakoma, usingizi wanibana,
Nyani huyu twamkoma, si Ngabu hilo bayana,
Fisadi tutawazima, kama kupe kuwakana,
Mkapa atiwe pingu, asimamishwe Kisutu?
 
  • Thanks
Reactions: SMU
Ni ishara ya mambo
Si bishara za tambo
toka hapo kitambo
twalisema hili jambo

wenye mpini wa mambo
wasema hatuna nyimbo
haki inachapwa fimbo

likilia la mgambo
jua hapo pana jambo
Mali inavushwa ng'ambo
tunaachiwa makombo.
 
Naona mnanisema , kila kunapokucha
Eti mimi fisadi, nilificha makucha
Michuzi kuwaibia,nakuwaacha mmechacha
Naishi kwa wasiwasi, lupango kunanukia.

'Bubu anapotaka kusema,
Jua mambo yamemzidia" (kwa wazee wenzangu nadhani mnakumbuka DDC mlimani , kila nikiliona hili jina nakumbuka huo wimbo)
 
Mkapa katuibia huku tukiwa tunamsifu na kumwona Mr Clean. Amelitumia 'vyema' joho alilovishwa na Nyerere: "Mchagueni Mkapa ni safi". Naikumbuka hiyo sentensi kwa uchungu. Afadhali hata tungemchagua mzee wa kiraracha.

JK yuko njia panda. Hana ubavu wa kuruhusu uchunguzi dhidi ya Mkapa. Hata akiruhusu, Takukuru itamsafisha kama ilivyofanya kwa Richmond.

Lakini bado naamini kuna njia ya kumtia hatiani huyu Chinga. Think deep.
 
Mlituangusha kwa kumuacha mzee wa kiraracha. Radhi zake mnaziona.
 
Mkapa katuibia huku tukiwa tunamsifu na kumwona Mr Clean. Amelitumia 'vyema' joho alilovishwa na Nyerere: "Mchagueni Mkapa ni safi". Naikumbuka hiyo sentensi kwa uchungu. Afadhali hata tungemchagua mzee wa kiraracha.

JK yuko njia panda. Hana ubavu wa kuruhusu uchunguzi dhidi ya Mkapa. Hata akiruhusu, Takukuru itamsafisha kama ilivyofanya kwa Richmond.

Lakini bado naamini kuna njia ya kumtia hatiani huyu Chinga. Think deep.

Madaraka matamu asikwambie mtu si unamwona kibaka i mean kibaki anavyong'ang'ana huko kenya..Nathubutu kusema hata huyo mzee wa kiraracha nae ange-adapt tabia za kifisadi...fedha sabuni ya roho!Bado tanzania hatujawa na committed leaders ambao wataweka maslahi ya taifa mbele na ubinafsi nyuma..
 
Back
Top Bottom