Nyerere, Mwinyi, Mkapa and Kikwete: Leadership Styles and A Lesson to Learn! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nyerere, Mwinyi, Mkapa and Kikwete: Leadership Styles and A Lesson to Learn!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Gosbertgoodluck, Jan 3, 2011.

 1. Gosbertgoodluck

  Gosbertgoodluck JF-Expert Member

  #1
  Jan 3, 2011
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 2,866
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  WanaJF,

  Mnaionaje hoja hiyo kwamba Nyerere alijitahidi kujenga nchi lakini alipokuja Mzee Mwinyi akaibomoa. Mkapa alipoingia madarakani ilibidi aanze upya kuijenga nchi. By the time anamaliza ngwe yake ya uongozi nchi ilikuwa tayari imerudi kwenye mstari kiuchumi.

  Lakini akaja mzee wa sifa JK na sifa zake, nchi imeporomoka kwa kasi ya ajabu kwa kiwango ambacho hata wana CCM wenzake inawatia shaka sana.

  Nyerere Alijenga Mwinyi Akabomoa, Mkapa Alianza Tena Ujenzi, JK Akabomoa Mpaka Msingi


  Wachambuzi karibuni kwa mawazo yenu.

  >>>>>>>>
  Baadhi ya majibu:

   
 2. P

  Popompo JF-Expert Member

  #2
  Jan 3, 2011
  Joined: Nov 9, 2010
  Messages: 411
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 33
  umenena mkuu!
   
 3. Z

  ZenaTulivu Senior Member

  #3
  Jan 3, 2011
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 137
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Sasa tuwemacho tuangalie hayo mawe ya msingi nayo yasije yakauzwa kwani rais ajaye atapata shida sana pa kuanzia.
   
 4. K

  KERENG'ENDE JF-Expert Member

  #4
  Jan 3, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 398
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Miaka 50 ya ccm ya tosha kuwa kimezeeka wala haina haja ya kubebesha mzigo huu kwa mtu yeyote.........kifaacho sasa ni kukaa pembeni watawale vijana
   
 5. G

  Gad ONEYA JF-Expert Member

  #5
  Jan 3, 2011
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 2,641
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Mkapa and Co. kujigawia mgodi? Kujiuzia nyumba za serikali? Uh, huwezi kumshawishi mtu mwenye akili rational! All amounts to misuse of public office and public coffers! Hapa wote wako kwenye line moja except JKN na AHM kidoogo!
   
 6. Z

  ZenaTulivu Senior Member

  #6
  Jan 3, 2011
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 137
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Nashangaa huyu mtoa hoja kuona tu kwamba marais waislamu ndiyo wafujaji wasioweza kitu. Uongozi tumpe raisi wetu mpya Prof Lipumba muone utaalam uko wapi ndio mtapenda.
   
 7. C

  ChiefmTz JF-Expert Member

  #7
  Jan 3, 2011
  Joined: Apr 15, 2008
  Messages: 2,519
  Likes Received: 292
  Trophy Points: 180
  Kwani yeye ndo analima mashamba. Toa mfano wa alichoharibu na kubomoa
   
 8. N

  Nonda JF-Expert Member

  #8
  Jan 3, 2011
  Joined: Nov 30, 2010
  Messages: 13,223
  Likes Received: 1,958
  Trophy Points: 280
  Mkuu,

  Hao uliowataja wote ni CCM. Nyerere nchi ilimshinda alituachia foleni za kila kitu na ufukara na umasikini wa ajabu. sifa kubwa aliyotuachia ni "masikini jeuri". Hatukuchagukiwa marafiki.Ile vita ya Uganda iliifilisi nchi.

  Ali mwinyi"mzee ruksa". Wanasema ukifungua dirisha sio hewa nzuri inaingia lakini inzi na mbu pia. Huyu watanzania watamkumbuka sana kwa unafuu wa upatikanaji wa bidhaa madukani na kuruhusu watu kusema na hata kutukana.uhuru wa kuzungumza.tatizo kila kitu kiliagizwa nje, hela nje nje!

  Mkapa akazichukua hela zote kutoka mfukoni kwa mlalahoi.Maarufu mzee ukapa.watu waliishiwa hela, alizitumia kulipa madeni ya nje. kwa sura ya nje alionekana mzuri lakini siri zilizofichuka baada ya kuondoka nae tuone tu mlolongo wa CCM na ufisadi.

  Huyu aliyepo, sina cha kuchangia kwani threads nyingi zishamchambua....hata wikileaks...

  Wasiwasi wangu na thread yako ni kuwa unawapigia kampeni CCM. Ukitaka tuamini kuwa Rais atakayefuata pia atatoka CCM. kwa hiyo kama haikuwa nia yako kutu-tune akili zetu huko, hivi ulivyoileta inaathari hiyo.

  Unataka tusalimu amri na tukubali tu kuwa next rais atatoka CCM na pengine katika hiyo order uliyoiweka...mkilisto-muichilamu..paulo..ali...

  Au una maana gani mkuu? Toa ufafanuzi zaidi.

  Au kampeni zimeshaanza mapema...
   
 9. Gosbertgoodluck

  Gosbertgoodluck JF-Expert Member

  #9
  Jan 4, 2011
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 2,866
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  Mwambie aoe kwanza na apate angalau mtoto mmoja, ndipo tutampatia urais. Hatutaki rais asiye na mke.
   
 10. Gosbertgoodluck

  Gosbertgoodluck JF-Expert Member

  #10
  Jan 4, 2011
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 2,866
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  Nashukuru kwa maoni mazuri. Ukweli ni kwamba naichukia ccm tena sana. ningekuwa na uwezo ningeiuwa na kuitupilia mbali. Hoja yangu ilikuwa ni kuonyesha trend mbaya kwamba wananchi wakiendelea kuichagua ccm nchi itakuwa stagnant kwamba term hii mnajenga, term inayofuata mnabomoa, and the trend goes that way.
   
 11. N

  Nonda JF-Expert Member

  #11
  Jan 4, 2011
  Joined: Nov 30, 2010
  Messages: 13,223
  Likes Received: 1,958
  Trophy Points: 280
  Mkuu,
  Nimekusoma!
   
 12. kabila01

  kabila01 JF-Expert Member

  #12
  Jan 4, 2011
  Joined: Apr 21, 2009
  Messages: 3,014
  Likes Received: 1,823
  Trophy Points: 280
  Soma alama za nyakati Lipumba saizi aende tu kwenye ubunge kama Mrema. Uwezekano wa Lipumba kua Rais wa JMT haupo kabisa na wala hakuna dalili yeyote ya Lipumba kuja kua Raisi
   
 13. Nanren

  Nanren JF-Expert Member

  #13
  Jan 4, 2011
  Joined: May 11, 2009
  Messages: 1,739
  Likes Received: 184
  Trophy Points: 160
  Thread hii haina tija!
  Hakuna kiongozi anayefanya mabaya tu, au anafanya mazuri tu...
  Hata Bush na Saddam walikuwa na mazuri na mabaya kwa watu wao.

  Kila mtu ana strength na weakness zake.
  Nyerere alichemsha kwenye uchumi, akajenga utaifa
  Mwinyi aka-liberalize uchumi, na ndipo hata watu wakaacha kuvaa matairi
  Mkapa akaendeleza nguvu alipoachiwa na mwinyi, akakuza uchumi, wakati huo huo akawaachia wajanja wajitajirishe,
  Kikwete, si vizuri kumjaji sasa hivi, to be fair, ngoja tuangalie akimaliza miaka 10 kwenye utawala

  Muhimu ni kuwa Viongozi wote hata kama walikuwa wana mapungufu, walipokuw madarakani, walikuwa na NIA NZURI KWA TAIFA LAO.
   
 14. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #14
  Jan 4, 2011
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Gosbertgoodluck

  Nyerere "alipong'atuka" Tanzania haina pesa, foleni za hata mafuta ya taa wacha petroli na dizeli, bank kuu oimechomwa moto, wizara ya mambo ya ndani imechomwa moto, yote kuficha madudu yake aliokuwa akiyafanya.

  Maviwanda na mashamba "alio taifisha" yote dead. Hakuna chema alicho kiacha, ukisafiri nje ukija na colgate airport unang'ang'aniwa kama kama umeleta johari za ughaibuni.

  Ukipita na kikapu tu, hao mgambo wamesha kusimamisha wanataka kujuwa kuna nini? Foleni za hata vitu basic kama sukari na unga wa ugali vilikuwa vitu vya kawaida wakati wa Nyerere.

  Na mengi sana mabaya hayasemeki yote.

  Leo unasema Nyerere kajenga? Ni nini alicho kijenga? To the contrary, kaharibu na kabomowa kila kitu.

  Mwinyi, hakuna malumbano, tunajuwa aliposhika madaraka nyoyo za wa Tanzani zikaanza kupowa, umaarufu wa RUKSA ulitokana na kila kitu basic kuwa luxury kwa wa Tanzania wakati wa Nyerere. Hata sabuni ya Lux ilikuwa ni kioja kuogea wakati wa Nyerere.

  Mkapa, duhhh, ndio hayo madudu tunayaona Kikwete akiyafukuwa na kuyashughulikia taratibu na scientifically kabisa. Madudu yote ya ubadhirifu, ya wizi ya epa, yalikuwa wakati wa nani? MKAPA.

  Kikwete, tunaona mema anayoyafanya, wala hatuna shaka nae. Mashule, leo kama kuna mtoto wa kiTanzania hafiki japo sekondari, ni kosa la jinai hilo. Maji, visima na upatikanaji wa maji safi Tanzania kwa kipindi kifupi cha Kikwete ni kushinda awamu zote za kabla yake. Ma-barabara, juzi tu wakati wa Mkapa ukitaka kwenda Mwanza inabidi uzungukie Kenya! Au nalo hulijui? Licha ya hiyo, nenda katazame Singida-Katesh-Babati-Minjingu. Nenda katazame Tanga-Horohoro. Nenda katazame Mbeya-Chunya- Tabora. Nenda Mkata-Handeni-Korogwe. Nenda Dodoma-Babati. Nenda, nenda, nenda.

  Sijaongelea bado ya zahanati, sijaongelea vitengo vipya vya moyo na meno Muhimbili, sijaongele kutokomeza Malaria, sijaongelea madawa ya kupunguza makali ya Ukimwi, sijaongelea vyuo vikuu. Sijaongelea mengi tu.

  Huoni? Au Husikii?
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 15. kabila01

  kabila01 JF-Expert Member

  #15
  Jan 4, 2011
  Joined: Apr 21, 2009
  Messages: 3,014
  Likes Received: 1,823
  Trophy Points: 280
  Naona hapo umeandika kisiasa zaid na hasa kwenye red. Tabora kuna nini cha ajabu. mkoa hadi leo haujaunganishwa kwa barabara ya Lami. kama ni mashule hata mkapa aliyaboresha sana pale alipoleta mpango wa MMEM tuliona shule zetu za msingi zikibadilika kutoka kwenye mapagale waliyokua wakisomea watoto wetu enzi za mwinyi. Kwa kifupi wote ni pumba hakuna cha maana walichofanya ni sawa na mtu anakuja kukugongea mkeo then anakupa zawadi ya sharti, unendelea kushangilia shat zuri ulilopewa unasahau maumivu ya kugongewa mkeo.

  Huyu wa sasa hayo ma Richmond, DOWANS, EPA, hamyaoni badala yake mnashangilia kuwepo kwa majengo ya zahanati yasiyokua na wafanyakazi pamoja na vifaa. Tabora wilaya ya URAMBO ina Zahanati 16 zimefungwa hazina wataalam wa kufanya kazi.
   
 16. spencer

  spencer JF-Expert Member

  #16
  Jan 4, 2011
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 2,792
  Likes Received: 1,337
  Trophy Points: 280
  We zomba,

  Mbona umesahau kutaja na Kilwa Road pia Mandela Road ambazo inabidi zirudiwe maana hakuna kitu kilichofanyika.

  Mbona hutaji wakuu wa mikoa na wilaya waliopewa kazi na JK wakati wananchi waliwazomea ktk kura za maoni

  Ongezea na biashara kuongezeka za kuuza scrapers na chupa za maji uhai huoni kama ni ajira, anazitambua JK.

  Mbona husemi?
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 17. Mvaa Tai

  Mvaa Tai JF-Expert Member

  #17
  Jan 4, 2011
  Joined: Aug 11, 2009
  Messages: 6,174
  Likes Received: 2,175
  Trophy Points: 280
  Unamchokoza Maralia sugu sasa. Maana jinsi ilivyokaa inadhalilisha dini fulani hapo:bump:
   
 18. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #18
  Jan 4, 2011
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Nenda Mbeya-Chunya-Tabora, hiyo route ya barabara ambayo imeshaanza kujengwa na kampuni ya kichina iitwayo CCCC kama una jamaa zako Chunya waulize.

  Hiyo Katesh ni barabara mpya inayopita hapo kutokea Singida kwenda Dareda-Babati.

  EPA ni madudu ya Nkapa.

  Dowans ni wafanya biashara halali walioleta mitambo ya kufuwa umeme ambayo wanataka kudhulumiwa lakini ICC wamesha amuwa walipwe.

  Kutokuwa na waTaalamu wa zahanati na waalimu wa kutosha ni madudu yaliofanywa toka wakati wa Nyerere. Leo Kikwete unajuwa toka kaingia madarakani anasomesha waalimu wangapi kwa mwaka? Sasa tazama hiyo idadi halafu uniambie kabla ya awamu yake ni nani alisomesha walimu kwa wingi namna hii. Pia kwa wa Taalamu wa tiba na zahanati, tazama wakati huu wa Kikwete ni wangapi idadi yao (wanaosomeshwa) na kabla ya hapo. Hapo ndio utajuwa Kikwete si mchezo.

  Hizo awamu zingine walikuwa wapi? Matunda ya hawa walimu na wahudumu wa tiba wanaosomeshwa leo tutaziona baada ya muda si mrefu. Laiti na kabla ya Kikwete wangefanya hivyo, leo hii Kikwete angekuwa na kazi ya kuboresha tu.
   
 19. kabila01

  kabila01 JF-Expert Member

  #19
  Jan 4, 2011
  Joined: Apr 21, 2009
  Messages: 3,014
  Likes Received: 1,823
  Trophy Points: 280
  zomba'

  Siasa mbaya sana. Jana nimepita kutoka nzega kwenda Tabora sijaona hata watu wakiwa na majembe wakitengeneza barabara achana na mkandarasi unaemsema. Kutoka Dodoma kwenda Babati ni safari ya hiyo lami imepitia mbinguni au ndo ile barabara tunayohangaika nayo ya kupitia Kondoa. siasa ni noma tunataka vitendo
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 20. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #20
  Jan 4, 2011
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  spencer

  Hizo barabara ni ma-engineer wabovu waliowachwa hapo na Nkapa au na hilo hutolipenda.

  Kuhusu hilo la scraper na chupa za maji na kufanyiwa recycling, nadhani huna upeo wa kuelewa kuwa hiyo biashara ni kubwa sana duniani na Jinsi Tanzania leo inavyozidi kuwekwa wazi kimawasiliano, ndio kwanza watu wanaishtukia biashara hiyo, ambayo wewe bado huijuwi kwani unaona ni muujiza mpaka ukaiweka hapa. Wenzetu wameianza miaka kadhaa nyuma. Kwa hilo, huna hoja.

  Kuhusu wakuu wa Mikoa na Wilaya uwasemao, mimi siwajui. Na for your information, kwa mtazamo wangu, sioni faida ya wakuu wa mikoa na wilaya kuteuliwa, mimi ningependa wawe wa kuchaguliwa na wananchi au wasiwepo kabisa na ingekuwa vyema tungekuwa na ma-gavana wa province wa kuchaguliwa na nadhani hilo litafikiriwa katika tume inayoundwa na Kikwete. Una jingine?
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
Loading...