Mkapa na Kikwete Walidanganywa na Wakadanganyika!, Magufuli Anadanganywa!, Jee Atadanganyika?

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
52,653
119,267
Wanabodi,
Leo nimapata tena fursa ya kuendelea na zile makala zangu za "Kwa Maslahi ya Taifa, leo nikizungumzia jinsi rais Mkapa na rais Kikwete, walivyodanganywa kwenye rasilimali za taifa na matokeo yake Tanzania tukaibiwa rasilimali zetu kwa kufanywa sisi ni shamba la bibi. Lengo la hii makala ya leo ni kueleza jinsi rais Magufuli nae anavyodanganywa, sasa kwa vile muda upo, makala hii itamgutusha kuwa rais Magufuli anadanganywa wapi ili asikubali kudanganyika!.

Angalizo!.
Wanabodi, naomba kuanza na angalizo hili kuwa hii ni thread ya swali, maana watu humu, tunatofautiana sana uelewa, mtu unaweka alama ya kuuliza, msomaji haioni!, akaona thread imeandikwa fulani amedanganywa!. Hapa nimewataja marais watangulizi wa rais Magufuli waliodanganywa, kwa kueleza walidanganywa kwenye nini, walidanganyikaje na matokeo ya kudanganyika huko, ili kumzui rais Magufuli asikubali kudanganywa, na hata kama atadanganywa, asikubali kudanganyika, na kwa vile wadanganyaji bado wapo na wanaendelea kudanganya, swali ni kwa wanaodanganywa, jee nao wataendelea kukubali kuendelea kudanganywa na kudanganyika ili hali wameelezwa bayana kuwa wanadanganywa?!.

Ni Kwa Kutokujua, Mkapa na Kikwete na Sisi Kama Taifa, Tulidanganywa, Tukadanganyika!, Sasa Tunajua Kuwa Tulidanganywa, Jee Bado Tutadanganyika?.
Katika suala zima za kuibiwa kwa rasilimali zetu, kupitia mikataba mibovu ya kinyonyaji ambayo ni wizi mtupu wa mchana kweupe, vita vya kupambana na rushwa kubwa "the grand corruption na vita dhidi ya ufisadi na uhujumu uchumi, marais waliotangulia wamekuwa wakidanganywa na kudanganyika, hivyo tukapigwa sana. The only excuse ya marais waliopita kudanganywa na kudanganyika, ni kufuatia kutokujua, lakini sasa kupitia hili sakata la mchanga wa makinikia wa Acacia, kwanza tumeishajua kuwa tulikuwa tunadanganywa na tunaibiwa, tatizo letu bado kama liko pale pale kwasababu hata rais Magufuli naye, tayari kadanganywa, swali linabaki jee rais Magufuli naye atadanganyika na sisi tuendelee kuibiwa?.

Naomba nisizungumze kuhusu awamu ya Nyerere na Mwinyi, mimi bado nilikuwa mdogo, lakini awamu ya Mkapa, Kikwete na hii ya Magufuli, mimi ni mtu mzima ninayejielewa, hivyo nazungumza vitu ninavyovijua, vingine nilivyovishuhudia vikitokea na sio vitu vya kuambiwa au kuhadithiwa!.

Kwenye mikataba ya madini, na manunuzi makubwa, Mkapa alidanganywa sana tuu na akadanganyika, tukaibiwa sana kwa kupigwa kwenye madini yetu na tunaendelea kuibiwa mpaka kesho, kupitia sheria mbovu, Kikwete nae pia kwenye mikataba ya Umeme, gesi asili, na manunuzi makubwa, alidanganywa na akadanganyika, hivyo pia tukapigwa na tukaibiwa sana na tunaendelea kuibiwa kupitia mikataba hii mibovu ya kinyonyaji, huku rushwa kubwa kubwa, the grand corruption na ufisadi mkubwa vikishamiri. Yote haya yaliweza kufanyika na kufanikiwa kutokana na kutokujua kwetu!. Sasa ili haya yasiendelee kufanyika, lazima kwanza mambo matatu makubwa yafanyike.
1. Kwanza tuwe na uwezo wa kujua kuwa tunadanganywa.
2. Tuwe na uwezo wa kutokubali Kudanganywa, na
3. Tukidanganywa, Tuwe na Uwezo wa Kuzuia Tusidanganyike!.

Rais Magufuli tangu alipoingia, akatangaza kupambana na rushwa na ufisadi, na alipoanza, alianza kwa kasi kubwa, zile tumbua tumbua za mwanzo na ziara za kushtukiza za mwanzo, ziliamsha amsha, ilikuwa ni hakuna kulala!, kumbe ilikuwa ni nguvu ya soda tuu!, lakini kadri siku zinavyokwenda, spidi inazidi kupungua kidogo kidogo, zile shtukiza na amsha amsha za mwanzo, sasa zimetulia au hazipo tena!, kilichobaki sasa sio tena ziara za kushtukiza kweli kama mwanzo, bali sasa naona kama yanafanyika maigizo ya ziara za kushtukiza!, au labda ni mimi tuu ndio naona kama ni maigizo, lakini in reality ya ukweli wenyewe bado ni ziara za kushtukiza?.

Kikwete na Mkapa Walidanganywa, Wakadanganyika!. Sasa Magufuli Anadanganywa, Jee Atadanganyika?.
Kwa vile watangulizi wa rais Magufuli, yaani rais Mkapa na rais Kikwete, walidanganywa na wakadanganyika na kuzidi kulizamisha taifa letu kwenye lindi la umasikini huu uliotopea unaondelea hadi sasa, huku tukibebeshwa mzigo mkubwa wa madeni, sasa kuna kila dalili kuwa hata rais Magufuli naye ameanza kudanganywa mchana kweupe na mifano nitatoa!, ila pia sio tuu rais Magufuli ameanza kudanganywa tuu, bali naona kama ameanza kudanganyika, sasa ili asiendelee kudanganywa na kudanganyika, bandiko kama hili ni kumgutusha rais wetu kwa kumuonyesha anadangwa wapi na kutoa ushauri wa jinsi ya kuzuia asidanganywe na akidanganywa asidanganyike!.

Jee Magufuli Anadanyanywa Wapi?.
Kipimo kuwa rais Magufuli anadanganywa hakina mjadala, kwa sababu ya documentary evidence ya datas , wataalamu wanasema numbers don't lie, rais Magufuli ambaye yeye mwenyewe ni mzuri sana in numbers, lakini kadanganywa in numbers na kadanganyika kirahisi!.

Kipimo cha taifa letu kujua kuwa rais wetu kadanganywa wapi na kwenye nini na kudanganyika vipi, tutakipima kwa matokeo ya mwisho, yaani results oriented outcomes za baadhi ya mipango mkakati yetu ya mendeleo ya muda mfupi, muda wa kati na muda mrefu katika sekta muhimu za uchumi wetu, ikiwemo sekta nyeti ya madini, mimi nikijikita kwenye specific hili la makinikia ya Acacia, ununuzi wa ndege bila kuwepo kwa mpango kazi, kwa kulipa cash badala ya hire purchase, na ujenzi wa miundo mbinu mikubwa kama SGR kwa mtindo wa zimamoto huku tukiambiwa ni fedha za ndani lakini muda sii mrefu tutashuhudia hata yeye atatuingiza Tanzania kama taifa kwenye mzigo mkubwa madeni kwa taifa letu kutokana na makosa fulani fulani ya kiutendaji, kama ilivyotokea kwa watangulizi wake na zaidi!, ila hili la taifa kubebeshwa mzigo wa madeni, linaweza lisizungumzwe sana sasa kutokana na kutokuwepo transparency ya ni lini serikali yetu huwa inakopa fedha, inakopa wapi, kiasi gani, kwa riba gani, na fedha hizo zinazokopwa ni fedha zinakopwa kufanyia nini?. Haya yote hatutayajua kwa sasa kwa sababu huwa serikali zetu hazina utamaduni wa transparency kwenye deni la taifa lakini kitakacho kuja kuonekana na kujulikana baadaye ni kutuna tuu kwa deni la taifa kwenye Ripoti ya CAG, watu watashangaa tunaelezwa tunatekeleza miradi mikubwa kwa fedha zetu za ndani, ila watu mtashangaa kwa deni la taifa linazidi kukua na kutuna!. Sasa kama tunatekeleza miradi hii kwa fedha za ndani, mbona bado tunakopa?, jee tunakopa fedha za kufanyia nini?, mbona huwa hatuambiwi, Bunge letu sio tuu haliambiwi!, bali hata kuombwa kuidhinisha hayo matumizi, haliombwi!, itakuja tuu taarifa ya kuongezeka kwa deni la taifa ndani ya taarifa ya GAC. Bunge ambalo moja ya majukumu yake ni kuisimamia Serikali ikiwemo kuhakikisha matumizi yote ya fedha za umma, lazima yafuate sheria, taratibu na kanuni, ikiwemo kuidhinishwa na Bunge, lakini katika ripoti ya CAG, kila mwaka tunashuhudia Serikali yetu ikifanya matumizi makubwa yasiyo ya dharura bila kuidhinishwa na Bunge,
sasa unajiuliza, huu usimamizi wa Bunge kuisimamia serikali ndio usimamizi gani?, ukisema Bunge ni dhaifu katika kuisimamia serikali, utakuwa umelikosea, au tukisema Bunge halitimizi wajibu wake kikamilifu tutakuwa tunalionea au kulidhalilisha?.

Mfano Hai ya Rais Kunadanganywa ni Kiwango cha Dhahabu Kwenye Makinikia ya Acacia Mining
Swali ni jee baada ya rais Magufuli kushtukia kuwa tunadanganywa kwenye makinikia, akazuia usafirishaji wa mchanga nje ya nchi, swali sasa ni jee naye yeye rais Magufuli hata baada ya kushtuka tunaibiwa, akadanganywa kiwango cha dhahabu iliyopo kwenye makinikia hayo, jee ataendelea kudanganyika kama watangulizi wake?, au yeye atabadilisha sheria ili tusiendelee kudanganywa?. Na jee Watanzania wazalendo wa taifa hili, wenye insight, mnapoona rais wetu anadanganywa, wazi wazi mchana kweupe tena mbele ya kadamnasi ya watu na mnajua kabisa kuwa hapa rais wetu anapigwa kamba, anadanganywa, jee mtanyamaza tuu na kumuachia rais wetu aendelee tuu kudanganywa na watu waliomzunguka, kwa sababu yeye ndiye mkuu wa nchi anayepaswa kujua kila kitu kama malaika?, au baadhi ya wazalendo, tutapaza sauti zetu kumgutusha rais wetu kuwa kwenye hili, hapa Mhe. rais wetu unadanganywa?. Hiki ndicho ninachokifanya kwenye bandiko hili.
Raia wema wa taifa lolote na wazalendo wakweli wa taifa lao, wana wajibu, as a duty of care, kama ilivyo fiduciary relationships nyingine zote, (uhusiano wenye wajibu) as duty to a good citizenship, kuisaidia nchi yako na watu wake, ikiwemo kumsaidia rais wako na kulisaidia taifa lako lisiendelee kudanganywa na kufanywa kuwa ni shamba la bibi kwa kila mwenye mkono mrefu kujichumia tuu na kujivunia tuu rasilimali zetu kwa urefu wa mkono wake kama ameokota na kujilia tuu kama mbuzi kwa urefu wa kamba yake!

Nashauri yoyote anayeona rais wetu anadanganywa wazi wazi, mchana kweupe, ajitokeze wazi wazi kama nifanyavyo mimi kupitia bandiko hili, na kusema kwa ukweli na uwazi kuwa hapa Mhe.Rais unadanganywa!, kwa kueleza anadanganywaje na kuweka documentary evidence ya udanganyifu, na ikiwezekana kutoa ushauri wa ukweli ni upi na nini cha kufanywa ili kumzuia rais wetu asiendelee kudanganywa, na sisi kama taifa tusiendelee kudanganywa na kufanywa ni shamba la bibi kila mjanja kuja kujichumia.
Rais Akidanganywa, Akagutushwa Kuwa Anadangaywa, Akidanganyika Baada ya Kugutushwa ni Kukubali Kudanganywa na Kudanganyika!.
Lakini ikitokea rais akadanganywa, na akaelezwa kabla kuwa hapa mhe. rais unadanywa!, lakini yeye asisikie kelele hizi za kumgutusha kuwa anadanganywa ili kumsaidia asidanganyike, rais akiendelea kudanganyika, then lazima tukubali kuwa ni Mhe rais wetu, atakuwa amekubali mwenyewe kwa ridhaa yake kudanganywa na kudanganyika, kwa sababu angalau aliambiwa kabla kuwa anadanganywa, ili kukija kutokea mabadiliko sheria na mabadiliko ya utawala, sisi Watanzania tuwe na nguvu za kuwawajibisha viongozi wetu hawa wanaokubali wenyewe kudanganywa kuhusu rasilimali za taifa letu na kukubali kudanganyika kirahisi rahisi mchana kweupe, hivyo kulitia hasara taifa letu, japo wale wa mwanzo waliomtangulia na waliodanganywa na kudanganyika, wanaweza kuwa excused na kusamehewa kwa hoja kuwa, wakati walipo danganywa, walidanganyika kwa kutokujua kuwa wanadanganywa, na hakuna yoyote aliyawashtua ua kuwagutusha kuwa wanadanganywa!, lakini hawa viongozi wetu waliopo sasa, kwenye huu ulimwengu wa uwazi na utandawazi, wanapodanganywa sasa, huku watu wenye insight, wanaona wazi kabisa kuwa hapa rais wetu anadanganywa, kisha wanamshtua na kumgutusha kuwa mhe. rais, hapa unadanganywa, ili asidanganyike, ikitokea amekubali kudanganyika ili hali aliambiwa kabla kuwa anadanganywa, then tutaamini kuwa amedanganyika kwa sababu amekubali mwenyewe kudanganyika!.

Jee Watanzania wenzangu, katika mazingira kama haya, jee tuendelee kukubali tuu viongozi wetu wadanganywe na wadanganyike kirahisi rahisi?. Jee tuendelee kui entertains ile sheria ya kinga ya rais wetu kutokushitakiwa?. Nasema No, kamwe tusikubali rais wetu au viongozi wetu wadanganywe mchana kweupe na kudanganyika!, tupaze sauti zetu, tupige kelele kuwa hapa rais unadanganywa!, kama akiendelea kudanganyika baada ya kumpigia kelele, Watanzania tumfanye nini kiongozi kama huyu?. Japo Bunge lina uwezo wa kuisimami serikali, lakini Bunge letu hili la vyama vingi /kimoja, kweli linaweza kumwajibisha rais anayekubali kudanganyika katika masuasa ya rasilimali za taifa?.

Nakiri kupandisha bandiko hili kutokana na inspiration kutoka kwa mwana jf huyu Mkuu Chakii
Kwanza naunga mkono hoja, linapokuja suala la kutanguliza mbele maslahi ya taifa, Watanzania wazalendo wa kweli, have a duty of care kwa nchi yao na watu wake, ikiwemo kumsaidia rais wao, asidanganywe kirahisi rahisi, haswa pale ambapo wanaona wazi kabisa kuwa hapa rais wetu anadanganywa!, wanapaswa wasikae kimya!.

Katika muktadha wa kulinda rasilimali za taifa, na ili kuzuia viongozi wetu wasidanganywe, tena na kudanganyika kwa kuingia mikataba yoyote mibovu na ya kinyonyaji, ya rasilimali zetu nashauri tutunge sheria au kanuni kuwa kuanzia sasa, mikataba yote ya rasilimali zetu za taifa ikiwemo maliasili zetu, yenye maslahi kwa taifa, iwekwe wazi, na ipitishiwe bungeni, ijadiliwe kwa uwazi kabisa (on open government initiatives and maximum transparency) kwa maslahi ya taifa na maslahi ya wote ili kujua kinachoendelea, na pia iwe na kipengele cha 'clausula rebus sic stantibus' ili iweze kufumuliwa, na kufanyiwa mapitio tuweze kufaidika wote na sio kama hali ilivyo sasa, anayefaidika ni mwekezaji tuu. Hii itasaidia sana ili kama kuna kudanganywa, wenye insight waone na waseme wazi, tunadanganywa!, sio watu wanakwenda kujifungia chumbani hotelini kule London na kusaini mikataba inayohusu rasilimali za taifa letu!, mijitu inakuja nchini, inajivunia tuu rasilimali hizo kwa kujichotea kwa kujiokotea kama hazina wenyewe kwa sababu tuu wao wamejipatia chochote kitu, lakini the rest of Watanzania are left with nothing!.

Kiukweli kwenye hili la mikataba, nakiri wazi kuwa Tanzania ni nchi ya ajabu sana!. Mikataba ya kimataifa ndio inaletwa bungeni na kuridhiwa na Bunge, lakini mikataba muhimu ya kitaifa inayohusu rasilimali za taifa, rasilimali za nchi, rasilimali zetu na vizazi vyetu, hii ni siri!, siri gani kwenye maslahi ya taifa?!, tunafanya siri kwa maslahi ya nani?!. Hata wabunge wetu ambao ndio wawakilishi wa hao wananchi wenye rasilimali hizo, wanafichwa!, wanafichwa nini?!. Hapa linakuja swali muhimu sana, hivi hii nchi ya Tanzania ni nchi ya nani?. Ni nchi ya viongozi au ni nchi ya wananchi wakiwemo viongozi wetu?. Rasilimali za nchi hii ni mali ya nani?. Kwa maoni yangu, Tanzania ni nchi ya Watanzania na rasilimali zetu ni rasilimali za nchi, za taifa, za wananchi!.

Rais wetu sio malaika ni binadamu tuu kama sisi, japo ana mamlaka kuu, lakini kama binadamu, hawezi kujua kila kitu, ndio maana tumemuwekea wasaidizi wa kumsaidia katika kutimiza wajibu na majukumu yake ikiwamo kumshauri ushauri sahihi na sio kumdanganya, na Watanzania wazalendo, wakiona rais wao anadanganywa, tena mchana kweupe, wana jukumu la kumsaidia kwa kumwambia hapa Mhe. Rais, wetu, unadanganywa ili asidanganyike!.

Hivyo watu wa kwanza wanaomdanganya rais ni wale wasaidizi wake ambao ni washauri wake wenye jukumu la kuhakikisha rais anakuwa well informed, hadanganyi, hadanganywi na wala hadanganyiki!. Kwenye mikataba mikubwa ya rasilimali zetu, kunaundwa timu kabisa ya government negotiating team yenye wabobezi wa fani tofauti tofauti wakiwemo wanasheria wanaopitia mikataba hiyo na kushauri!, lakini kama mkataba ulisainiwa hotelini London, sijui ni kina nani waliipitia na kushauri kabla haijasainiwa?!.

Kwenye hili la washauri wa rais, na rais wetu kushauriwa na kusaidiwa, tumelizungumza sana humu.
Wasaidizi wa Rais, Please Msaidieni Rais Wetu Kwenye Public ...
Tusimlaumu Rais Magufuli Kwa Kila Kosa, Rais Yeye Hana Kosa Bali ...
Naamini Rais Magufuli ana washauri wazuri na anashauriwa vizuri ...

Rais Mkapa Alidanganywa Vipi, Wapi na Akakubali Kudanyanyika Tukapigwa!.

Licha ya Tanzania kuibiwa kupitia mikataba mibovu, pia Tanzania tunaibiwa sana kwa kupigwa changa la macho!. Nikutolee mifano michache kuanzia awamu ya Mkapa. Watu walichonga deal wakamshauri rais Mkapa tununue ndege mpya ya rais, tunahitaji radar na vifaa muhimu vya kijeshi. (Hili la vifaa vya jeshi naomba msiliulizie).

Ununuzi ulifanywa kupitia restricted tendering kupitia kwa a single source. Wasaidizi wa rais wakamshauri rais Mkapa kwa kumdanganya kuwa Tanzania kama taifa, tunahitaji sana hiyo radar ya kisasa, ndege na hizo zana!. Kumbe ulikuwa ni uongo mtupu!. Watanzania wazalendo hadi wazungu wakapinga sana na kupiga kelele, na haswa bei tunayopigwa!. Nakumbuka Mzee, John Cheyo enzi hizo akiwa ni mpinzani kweli, hadi akamuonyesha rais Mkapa bei halisi ya Gulf Stream toka kwenye website yao, lakini rais Mkapa alitia pamba masikioni na tukanunua ndege, radar na zana za kijeshi mtumba kwa kupigwa!. Manunuzi yote hayo yalifanywa na ajenti huyo huyo mmoja!.

Kilichofuata sote tunakijua, japo watu walilipwa mlungula, kwa mtindo wa kickbacks mimi siamini kabisa kuwa Mkapa hakujua kilichokuwa kinafanyika na kilichoendelea, kwasababu aliambiwa kabla, hivyo kwenye ununuzi wa Radar na ndege ya rais, Rais Mkapa alidanganywa na akadanganyika!, tena thank God, BAE walikubali kulipa chenji ya radar ili kuwalinda mafisadi hao waliolamba cha juu!, kama BAE wasingekubali, ma majina ya viongozi wetu waliokula mlungula yangetatwa!, watu mngeshangaa!.

Likaja suala la EPA, CCM ikataka fedha za kampeni, kwa kuzichota kutoka ndani ya Strong Room ya Benki Kuu yetu, kumejaa minoti. Wajanja wakapiga dili, wakaunda vikampuni, na wajanja wengine wengi nao wakautumia mwanya huo huo wakachomekea vikampuni vyao, wakapiga pesa ndefu. Waziri Fedha wa wakati huo, Mama Meghji aliletewa vimemo akaambiwa Mzee anajua. Akaruhusu pesa zikachotwa. Tukapigwa!.

Siamini kama rais Mkapa hakujua kuwa kuna fedha za umma zinaibiwa BOT ili kukinufaisha chama tawala, wala siamini rais Kikwete hakujua kuwa ameingia ikulu yetu kupitia fedha chafu za wizi za kampuni ya Kagoda!. Jee unajua hii maana yake ni nini? . Thanks God marais wetu wana kinga ya kutokushitakiwa!. Hii kinga mimi ni mmoja wa watu wanaoipinga.
Ushauri wa bure kwa CCM: Hope for the best but get prepared for ...
Serikali ya CCM, Yapewa Onyo la "Mwanagutu"-" Siku Yake Ipo ...

Rais Kikwete pia alidanganywa na akadanganyika. Kwenye kashfa ya EPA Rais Kikwete alidanganywa hadi kuvunja katiba kwa kuiachia mijizi ya EPA kurudisha ilichokwiba. Kwenye Escrow pia alidanganywa. Pamoja na mazuri yake yote, rais Kikwete aliiacha nchi yetu in a mess!. Kazi ya kwanza ya rais Magufuli alipoingia tuu madarakani, was clearing up Kikwete's mess!.

Kagoda: Kamwe haitafikishwa Mahakamani! | JamiiForums | The Home ...
Kagoda Haina Kesi, hawafikishwi Mahakamani Ng'o! | JamiiForums ...
Kwanini Mijizi ya EPA Ilisamehewa?!. Jee Unaunga Mkono au Unapinga ...

Kama rushwa na ufisadi vilishamiri na kusadifu Mkapa's era na Kikwete's era, this means both of them could possibly, they have always been a part and parcel, of this mess, they might be were all corrupts!.

Rais Magufuli Ameonyesha Nia Kwa Maneno na Matendo Kuwa ni Mkweli, Anachukia Rushwa ila Anadanganywa!.

Sasa kwenye awamu hii ya 5 ya Magufuli, Rais Magufuli ameonyesha kwa maneno na matendo, nia ya dhati toka moyoni mwake, kuwa anachukia rushwa, unachukia ufisadi, anachukia uzembe, na anachukia sana kudanganywa, hili tunalishuhudia kupitia tumbua tumbua. Ila pia on the other side he is only human anaweza kudanganywa na akadanganyika, ila pia naamini akiambiwa ukweli kuwa "Mzee hapa inabidi tudanganye" katika baadhi ya mambo " kweli Kuna udanganyifu ila umefanywa kwa nia njema" rais Magufuli ni muelewa hivyo anaelewa kuwa huu ni uongo ila unafanywa kwa nia njema!. Nikitolea mfano mzuri ni issue ya Bashite, mimi naamini baada tuu ya issue ile kuibuliwa itakuwa Bashite mwenyewe alimwendea na kuconfess kila kitu kuwa yote ni kweli, rais Magufuli ni mwelewe ndio maana mpaka leo, mpaka kesho, anamlinda. Waongo wa uongo huu wa nia njema wapo wengi na rais Magufuli amewakubali na anafanya nao kazi wakiwemo Kigwangala na Mwigulu Nchemba
Mwanzo nilikuwa sina uhakika kwanza kama hata rais Magufuli anadanganyika, au kama atakubali kudanganywa kwenye mikataba, kama Mkapa na Kikwete. Ila kama nilivyosema mwanzo na yeye ni binadamu na sio malaika, hivyo anaweza akadanganywa na akadanganyika, lakini Watanzania wazalendo wenye uoni mkubwa, wenye uwezo wa kuona kuwa hapa rais wetu anadanganywa!, tusikubali rais wetu adanganywe huku tumekaa kimya!, na akidanganywa, tusikubali adanganyike, kwa kumweleza wazi kuwa hapa mhe. rais unadanganywa!, ili ikitokea, rais akadanganywa na akadanganyika iwe ni yeye tuu kwa ubinaadamu wake, amekubali kudanganywa na kudanganyika, lakini sisi Watanzania wengine wazalendo, kamwe tusikubali rais wetu kudanganywa na kudanganyika!.

Rais Magufuli Amedanganywa Kiwango cha Dhahabu Kwenye Makinikia
Kwenye hili la mchanga wa makinikia ya dhahabu, wajameni kiukweli kabisa, rais wetu amedanganywa mchana kweupe, na masikini rais wetu tayari ameishadanganyika kupitia ripoti ya makinikia, imemdanganya rais wetu kuwa Tanzania ndio nchi inayoongoza kwa kuzalisha dhahabu nyingi duniani kuliko nchi nyingine yoyote lakini dhahabu hiyo imekuwa ikiibiwa kupitia mchanga wa dhahabu!, uongo huu ni kupitia taarifa ya viwango vya dhahabu vilivyokokotolewa na tume yake kwenye makinikia yaliyomo ndani ya makontena 277 ya mchanga wa dhahabu wa migodi miwili tuu ya ya Acacia, nashauri tusilinyamazie hili, tuungane na rais wetu katika kutafuta ukweli hakika na bayana kwa maslahi mapana zaidi ya taifa letu.

Hapa nimesema rais amedanywa na akadanganyika kwa sababu sii kweli kuwa Tanzania ndie mzalishaji mkubwa kabisa wa dhahabu duniani, hata tungekuwa tunaibiwa vipi, tungeibiwa viwango vya ndani lakini hiyo dhahabu inayoingia kwenye soko la dunia, ingeonyesha wazi kabisa kuwa inatoka Tanzania!. Ni kama ilivyo kwa Tanzanite, japo Tanzania ndio mzalishaji pekee wa Tanzanite duniani, anayeongoza kuuza Tanzanite ni India, Afrika Kusini halafu ndio Tanzania. Unless wathibitishe kwa ushahidi usiotia Shaka kuwa kuwa Tanzania ndio inaongoza kuzalisha dhahabu duniani, lakini dhahabu hiyo hairekodiwi kuonyesha inatoka Tanzania, hivyo dhahabu hiyo inaibiwa kupitia makinikia, na kuingizwa kwenye soko la dunia ikiandamana na certificates of origin za kutokea nchi nyingine!, hivyo hairekodiwa na WB na haionyeshi kuwa inatoka Tanzania, hivyo kwenye records Tanzania ndio ilipaswa kuwa ndio inaongoza kwa uzalishaji wa dhahabu duniani kitu ambacho sii kweli. Kitu cha kwanza kwenye international business ya bidhaa ni certificates of origin, unless wathibishe kuwa ni kweli Tanzania ndio ya kwanza ila tumekuwa tukiigwa na kuwa biwa dhahabu yetu!.

Hii maana yake ni kuwa kwenye ripoti za tume ya makinikia, rais wetu amedanganywa kiasi cha dhahabu kilichomo, na kupitia uongo huo, TRA ikatoa deni la ajabu la dola bilioni 191 kwa Acacia ambalo kiukweli kabisa, halilipiki!, ukweli wa uongo huu utajulikana pale tuu, tutakapouchenjua wenyewe Mchanga unaoshikiliwa katika makontena 277 tunayoyashikilia na kuuthibitisha sio ukweli wa tunachoibiwa bali uongo wa tume ya rais ya makinikia!.

Baada ya Rais Magufuli Kudanganywa, Tutapataje Ukweli?
Ukweli huu kuwa rais wetu amedanganywa kiwango cha dhahabu kilichopo ndani ya makinikia, utabainika only if kama sisi wenyewe kama nchi na ndio wenye mchanga, tutauchenjua wenyewe mchanga huo na kuthibitisha kilichomo kwa kuzianika mbichi na mbivu!, lakini kwa vile waliomdanganya rais, pia wanajua kuwa wamemdanganya, ili kumpa rais ripoti ya kile anachopenda kusikia kuwa tunaibiwa, watahakikisha, hakuna juhudi zozote za kuuchenjua mchanga huo, ili kilichomo kisijulikane!, na kwa mahesabu ya Acacia, hana the capacity kulipia kiasi hicho tunachowadai ambacho hadi sasa sio cha kweli na sio cha uongo hadi verification ifanyike na kiukweli sijasikia juhudi zozote kuutafuta ukweli kupitia verification!,

Tunachosikia na ndicho kitakachotokea ni mazungumzo ya kitu kinachoitwa amicable settlement ya a win win situation, kwa sisi kulambishwa asali kidogo, Acacia wapewe Mchanga wao, tuendelee kuibiwa!. Time will tell!.
Mungu Ibariki Tanzania.
Paskali
 
Wanabodi,
Katika suala zima za kuibiwa kwa rasilimali zetu, kupitia mikataba mibovu ya kinyonyaji ambayo ni wizi mtupu, vita vya kupambana na rushwa kubwa "the grand corruption na vita dhidi ya ufisadi na uhujumu uchumi, naomba nisizungumze kuhusu awamu ya Nyerere na Mwinyi, nilikuwa mtoto, lakini awamu ya Mkapa, Kikwete na hii ya Magufuli, mimi ni mtu mzima ninayejielewa, hivyo nazungumza vitu nilivyovishuhudia vikitokea.

Kwenye mikataba ya madini, Mkapa alidanganywa sana tuu na akadanyika, tukaibiwa sana, Kikwete nae pia kwenye mikataba ya gesi asili, alidanganywa na akadanganyika, hivyo pia tukaibiwa sana na tunaendelea kuibiwa kupitia mikataba mibovu ya kinyonyaji, huku rushwa kubwa kubwa na ufisadi vikishamiri.

Magufuli tangu alipoingia, akatangaza kupambana na rushwa na ufisadi, na alipoanza, alianza kwa kasi kubwa, zile tumbua tumbua na ziara za kushtukiza za mwanzo, ziliamsha amsha, ilikuwa ni hakuna kulala, lakini kadri siku zinavyokwenda, spidi inazidi kupungua, zile shukiza sio shtukiza tena bali maigizo ya shtukiza, ila kwa vile watangulizi wake walidanganya na wakadanganyika na kuzidi kulizamisha taifa letu, kuna kila dalili sasa Magufuli naye ameanza kudanyanywa. Sawa ni jee Magufuli naye atadanganyika kama watangulizi wake, au huyu hadanganyiki?. Na jee Watanzania wazalendo wa taifa hili, wenye insight, mnapoona rais wetu anadanganywa, na mnajua kabisa anadanganywa, jee tutamuacha tuu adanganyike kwa sababu yeye ndiye mkuu, au tutapaza sauti zetu kumgutushakuwa anadanganywa, as a fiduciary duty to a good citizenship, ili hata ikitokea na yeye adanganyike, adanganyike kwa ridhaa yake kwa sababu aliambiwa, ili kukija kutokea mabadiliko ya utawala, tuwe na nguvu za kuwawajibisha hawa viongozi wa taifa hili wanaodanganywa na kudanganyika, japo wale wa mwanzo waliodanganywa na kudanganyika, tunaweza kuwasamehe kwa kusema walidanganyika kwa kutokujua, lakini hawa wanaodanganywa, kisha tunawaambia wanadanganywa, ikitokea wamedanganyika ili hali tuliwaambia, tutaamini wamekubali kudanganyika!. Jee Watanzania tukubali viongozi wetu wadanganywe na wadanganyike?.

Nakiri kupandisha bandiko hili kutokana na inspiration kutoka kwa mwana jf huyu Mkuu
Kwanzanaunga mkono hoja, linapokuja suala la maslahi ya taifa, Watanzania wazalendo, wana a duty of care kwa nchi yao kumsaidia rais, asidanganywe, pale ambapo wanaona wazi kabisa rais wetu anadanganywa!.

Rais wetu sio malaika ni binadamu tuu kama sisi, japo ana mamlaka kuu, lakini kama binadamu, hawezi kujua kila kitu, ndio maana tumemuwekea wasaidizi wa kumsaidia katika kutimiza majukumu yake ikiwamo kumshauri ushauri sahihi na sio kumdanganya, na wakuiona anadanganywa, wana jukumu la kumsaidia kwa kumwambia hapa anadanganywa ili asidanganyike!.

Hivyo watu wa kwanza wanaomdanganya rais ni wale wasaidizi wake ambao ni washauri wake wenye jukumu la kuhakikisha rais anakuwa well informed, hadanganyi, hadanganywi na wala hadanganyiki!.

Nikutolee mifano michache kuanzia awamu ya Mkapa. Watu walichonga deal wakamshauri Mkapa tununue ndege mpya ya rais, tunahitaji radar na vifaa muhimu vya kijeshi. (Hili la vifaa vya jeshi naomba msiliulizie).

Ununuzi ulifanywa kupitia restricted tendering kupitia kwa a single source. Wasaidizi wa rais wakamshauri tunahitaji sana hiyo radar, ndege na hizo zana!. Kumbe ulikuwa ni uongo mtupu. Watanzania wazalendo hadi wazungu wakapinga sana, na haswa bei tunayopigwa. John Cheyo hadi akamuonyesha bei ya Gulf Stream toka kwenye website yao, lakini Mkapa alitia pamba masikio na tukanunua ndege, radar na zana za kijeshi kwa kupigwa!. Manunuzi yote hayo yalifanywa na ajenti huyo huyo mmoja!.

Kilichofuata sote tunakijua, japo watu walilipwa mlungula, mimi siamini kabisa kuwa Mkapa hakujua kilichokuwa kinafanyika!.

Likaja suala la EPA, CCM ikataka fedha za kampeni, ndani ya Benki Kuu yetu, kumejaa minoti. Wajanja wakaunda vikampuni, na wajanja wengine wengi nao wakautumia mwanya huo huo wakachomekea yao wakapiga pesa ndefu. Waziri Meghji aliletewa barua akaambiwa Mzee anajua. Akaruhusu pesa zikachotwa. Tukapigwa!.

Siamini kama Mkapa hakujua wala Kikwete hakujua kuwa ameingia ikulu yetu kupitia fedha za wizi za kampuni ya Kagoda!. Jee unajua hii maana yake ni nini? . Thanks God marais wetu wana kinga ya kutokushitakiwa!

Kagoda: Kamwe haitafikishwa Mahakamani! | JamiiForums | The Home ...
Kagoda Haina Kesi, hawafikishwi Mahakamani Ng'o! | JamiiForums ...
Kwanini Mijizi ya EPA Ilisamehewa?!. Jee Unaunga Mkono au Unapinga ...

Rais Kikwete pia alidanganywa na akadanganyika. Kwenye kashfa ya EPA Rais Kikwete alidanganywa hadi kuvunja katiba kwa kuiachia mijizi ya EPA kurudisha ilichokwiba. Kwenye Escrow pia alidanganywa. Pamoja na mazuri yake yote, pia aliiacha nchi yetu in a mess!. Kazi ya kwanza ya Magufuli was clearing up Kikwete's mess!.

Kama rushwa na ufisadi vilishamiri na kusadifu Mkapa's era na Kikwete's era, this means both of them were possibly corruptible!.

Kwa utendaji huu wa Magufuli ameisha onyesha nia ya dhati toka moyoni mwake, kwa maneno na matendo kuwa anachukia rushwa, unachukia ufisadi, anachukia uzembe, na anachukia sana kudanganywa. Ila pia on the other side he is very human akiambiwa ukweli na mfano mzuri ni issue ya Bashite, baada tuu ya kuibuliwa Bashite alimwendea na kurudisha confess kila kitu kuwa ni kweli. Akamlinda.

Hivyo sina uhakika kwanza kama Magufuli anadanganyika, au kama atakubali kudanganywa kwenye mikataba, kama Mkapa na Kikwete. Ila kama nilivyosema mwanzo na yeye ni binadamu na sio malaika, Hivyo anaweza akadanganywa na akadanganyika, lakini Watanzania wazalendo wenye uoni mkubwa, wenye uwezo wa kuona kuwa hapa rais wetu anadanganywa!, tusikubali rais wetu adanganywe, na akidanganywa asidanganyike, ila ikitokea, akadanganywa na akidanganyika iwe ni yeye tuu kwa ubinaadamu wake, lakini sisi Watanzania wengine wazalendo, kamwe tusikubali rais wetu kudanganywa na kudanganywa!.

Kwenye hili la mchanga wa makinikia ya dhahabu, japo tayari rais wetu ameishanganywa kuwa Tanzania ndio inchi inayoongoza kwa kuzalisha dhahabu nyingi duniani kuliko nchi
nyingine yoyote kupitia taarifa ya viwango vya dhahabu kwenye makinikia yaliyomo ndani ya makontena 277 ya mchanga wa dhahabu wa migodi miwili tuu ya ya Acacia, nashauri tusilinyamazie hili, tuungane na rais wetu katika kutafuta ukweli hakika na bayana kwa maslahi mapana zaidi ya taifa letu.

Mungu Ibariki Tanzania.
Paskali
ni mwenda wazimu tu ndie anayetengemea ccm kufanya jambo la maslahi kwa watanzania. CCM hawapo kwa ajili ya Tanzania wapo kwa ajili ya kutawala maisha na kujaza matumbo yao FULL STOP
 
tunataka uwajibikaji wa mfumo, tumbuatumbua ya msimu haitoshi! magufuli aweke mfumo unaowajibika ikiwezekana kubadili na baadhi ya sheria na katiba! vipi aking'atuka, si tutarudi ktk mfumo uleule
 
Kudanganywa kupo japo sio jambo zuri kwa rais kudanganywa.

Ukakasi unakuja pale wanaosema walidanganywa na wakadanganyika wanapogoma kukubali na ikiwezekana kusaidia tusiendelee kudanganyika kwa kukaa kimya.
Inaleta walakini kwamba walidanganyika kweli au waliamua kwa makusudi kudanganywa kwa maslahi yao binafsi?
 
Hadanganyiki.

Na hizo za kushtukiza usiseme spidi imepungua bali sema hajamua, ana uwezo wa kuzifanya dakika yoyote anapoamua. Ila zimesaidia sana kwa asilimia kubwa. Mabadiliko ya watendaji wa kazi yanaonekana, na bado watazidi kunyooshwa.

Hapa kazi tu

Magudfuli 2020
 
Wanabodi,
Katika suala zima za kuibiwa kwa rasilimali zetu, kupitia mikataba mibovu ya kinyonyaji ambayo ni wizi mtupu, vita vya kupambana na rushwa kubwa "the grand corruption na vita dhidi ya ufisadi na uhujumu uchumi, naomba nisizungumze kuhusu awamu ya Nyerere na Mwinyi, nilikuwa mtoto, lakini awamu ya Mkapa, Kikwete na hii ya Magufuli, mimi ni mtu mzima ninayejielewa, hivyo nazungumza vitu nilivyovishuhudia vikitokea.

Kwenye mikataba ya madini, Mkapa alidanganywa sana tuu na akadanyika, tukaibiwa sana, Kikwete nae pia kwenye mikataba ya gesi asili, alidanganywa na akadanganyika, hivyo pia tukaibiwa sana na tunaendelea kuibiwa kupitia mikataba mibovu ya kinyonyaji, huku rushwa kubwa kubwa na ufisadi vikishamiri.

Magufuli tangu alipoingia, akatangaza kupambana na rushwa na ufisadi, na alipoanza, alianza kwa kasi kubwa, zile tumbua tumbua na ziara za kushtukiza za mwanzo, ziliamsha amsha, ilikuwa ni hakuna kulala, lakini kadri siku zinavyokwenda, spidi inazidi kupungua, zile shukiza sio shtukiza tena bali maigizo ya shtukiza, ila kwa vile watangulizi wake walidanganya na wakadanganyika na kuzidi kulizamisha taifa letu, kuna kila dalili sasa Magufuli naye ameanza kudanyanywa. Sawa ni jee Magufuli naye atadanganyika kama watangulizi wake, au huyu hadanganyiki?. Na jee Watanzania wazalendo wa taifa hili, wenye insight, mnapoona rais wetu anadanganywa, na mnajua kabisa anadanganywa, jee tutamuacha tuu adanganyike kwa sababu yeye ndiye mkuu, au tutapaza sauti zetu kumgutushakuwa anadanganywa, as a fiduciary duty to a good citizenship, ili hata ikitokea na yeye adanganyike, adanganyike kwa ridhaa yake kwa sababu aliambiwa, ili kukija kutokea mabadiliko ya utawala, tuwe na nguvu za kuwawajibisha hawa viongozi wa taifa hili wanaodanganywa na kudanganyika, japo wale wa mwanzo waliodanganywa na kudanganyika, tunaweza kuwasamehe kwa kusema walidanganyika kwa kutokujua, lakini hawa wanaodanganywa, kisha tunawaambia wanadanganywa, ikitokea wamedanganyika ili hali tuliwaambia, tutaamini wamekubali kudanganyika!. Jee Watanzania tukubali viongozi wetu wadanganywe na wadanganyike?.

Nakiri kupandisha bandiko hili kutokana na inspiration kutoka kwa mwana jf huyu Mkuu
Kwanzanaunga mkono hoja, linapokuja suala la maslahi ya taifa, Watanzania wazalendo, wana a duty of care kwa nchi yao kumsaidia rais, asidanganywe, pale ambapo wanaona wazi kabisa rais wetu anadanganywa!.

Rais wetu sio malaika ni binadamu tuu kama sisi, japo ana mamlaka kuu, lakini kama binadamu, hawezi kujua kila kitu, ndio maana tumemuwekea wasaidizi wa kumsaidia katika kutimiza majukumu yake ikiwamo kumshauri ushauri sahihi na sio kumdanganya, na wakuiona anadanganywa, wana jukumu la kumsaidia kwa kumwambia hapa anadanganywa ili asidanganyike!.

Hivyo watu wa kwanza wanaomdanganya rais ni wale wasaidizi wake ambao ni washauri wake wenye jukumu la kuhakikisha rais anakuwa well informed, hadanganyi, hadanganywi na wala hadanganyiki!.

Nikutolee mifano michache kuanzia awamu ya Mkapa. Watu walichonga deal wakamshauri Mkapa tununue ndege mpya ya rais, tunahitaji radar na vifaa muhimu vya kijeshi. (Hili la vifaa vya jeshi naomba msiliulizie).

Ununuzi ulifanywa kupitia restricted tendering kupitia kwa a single source. Wasaidizi wa rais wakamshauri tunahitaji sana hiyo radar, ndege na hizo zana!. Kumbe ulikuwa ni uongo mtupu. Watanzania wazalendo hadi wazungu wakapinga sana, na haswa bei tunayopigwa. John Cheyo hadi akamuonyesha bei ya Gulf Stream toka kwenye website yao, lakini Mkapa alitia pamba masikio na tukanunua ndege, radar na zana za kijeshi kwa kupigwa!. Manunuzi yote hayo yalifanywa na ajenti huyo huyo mmoja!.

Kilichofuata sote tunakijua, japo watu walilipwa mlungula, mimi siamini kabisa kuwa Mkapa hakujua kilichokuwa kinafanyika!.

Likaja suala la EPA, CCM ikataka fedha za kampeni, ndani ya Benki Kuu yetu, kumejaa minoti. Wajanja wakaunda vikampuni, na wajanja wengine wengi nao wakautumia mwanya huo huo wakachomekea yao wakapiga pesa ndefu. Waziri Meghji aliletewa barua akaambiwa Mzee anajua. Akaruhusu pesa zikachotwa. Tukapigwa!.

Siamini kama Mkapa hakujua wala Kikwete hakujua kuwa ameingia ikulu yetu kupitia fedha za wizi za kampuni ya Kagoda!. Jee unajua hii maana yake ni nini? . Thanks God marais wetu wana kinga ya kutokushitakiwa!

Kagoda: Kamwe haitafikishwa Mahakamani! | JamiiForums | The Home ...
Kagoda Haina Kesi, hawafikishwi Mahakamani Ng'o! | JamiiForums ...
Kwanini Mijizi ya EPA Ilisamehewa?!. Jee Unaunga Mkono au Unapinga ...

Rais Kikwete pia alidanganywa na akadanganyika. Kwenye kashfa ya EPA Rais Kikwete alidanganywa hadi kuvunja katiba kwa kuiachia mijizi ya EPA kurudisha ilichokwiba. Kwenye Escrow pia alidanganywa. Pamoja na mazuri yake yote, pia aliiacha nchi yetu in a mess!. Kazi ya kwanza ya Magufuli was clearing up Kikwete's mess!.

Kama rushwa na ufisadi vilishamiri na kusadifu Mkapa's era na Kikwete's era, this means both of them were possibly corruptible!.

Kwa utendaji huu wa Magufuli ameisha onyesha nia ya dhati toka moyoni mwake, kwa maneno na matendo kuwa anachukia rushwa, unachukia ufisadi, anachukia uzembe, na anachukia sana kudanganywa. Ila pia on the other side he is very human akiambiwa ukweli na mfano mzuri ni issue ya Bashite, baada tuu ya kuibuliwa Bashite alimwendea na kurudisha confess kila kitu kuwa ni kweli. Akamlinda.

Hivyo sina uhakika kwanza kama Magufuli anadanganyika, au kama atakubali kudanganywa kwenye mikataba, kama Mkapa na Kikwete. Ila kama nilivyosema mwanzo na yeye ni binadamu na sio malaika, Hivyo anaweza akadanganywa na akadanganyika, lakini Watanzania wazalendo wenye uoni mkubwa, wenye uwezo wa kuona kuwa hapa rais wetu anadanganywa!, tusikubali rais wetu adanganywe, na akidanganywa asidanganyike, ila ikitokea, akadanganywa na akidanganyika iwe ni yeye tuu kwa ubinaadamu wake, lakini sisi Watanzania wengine wazalendo, kamwe tusikubali rais wetu kudanganywa na kudanganywa!.

Kwenye hili la mchanga wa makinikia ya dhahabu, japo tayari rais wetu ameishanganywa kuwa Tanzania ndio inchi inayoongoza kwa kuzalisha dhahabu nyingi duniani kuliko nchi
nyingine yoyote kupitia taarifa ya viwango vya dhahabu kwenye makinikia yaliyomo ndani ya makontena 277 ya mchanga wa dhahabu wa migodi miwili tuu ya ya Acacia, nashauri tusilinyamazie hili, tuungane na rais wetu katika kutafuta ukweli hakika na bayana kwa maslahi mapana zaidi ya taifa letu.

Mungu Ibariki Tanzania.
Paskali
Paskali, wewe ni mweledi ila unajitiaga kutufool, nimeanza kukuelewa sasa. Soma hili andiko kutoka humu JF... nimekopi link for easy of reference lakini nimeweka contents za like usome bila kusumbuka:....... AMEDANGANYWA AKADANGANYIKA,
Kesi ya ACACIA
NIMEIOKOTA SEHEMU: Kuna sababu za msingi hapa serikali ishaurike!Huyu ameshauri hivi:
Huenda uchunguzi wa madini ndani ya mchanga ukaishia kuwa swala la JPM kutafuta sifa tu na usiwe na manufaa kwa umma kwa sababu zifuatazo:

1. Acacia kama ilivyo migodi mingine Tanzania ni mali ya wawekezaji na siyo mali ya serikali maana stahili ya serikali ni asilimia 4 tu ya thamani ya madini yanayochimbwa. Serikali kufungua container za acacia na kuchukua sampuli bila kuwashirikisha acacia ni kosa.

2. Sampuli za mchanga zilizochukuliwa na kaati ya rais zimepimwa kwenye maabara bila uwakilishi wa acacia na ni kosa maana tayari acacia wamesema hawatambui huo uchunguzi na kwa hivyo serikali haiwezi kutumia matokeo ya ripoti hiyo kudai fidia mahali po pote.

3. Mikataba kama huo wa acacia inapotokea kutoelewana mahali pa kutafuta suluhu ni mahakama ya kimataifa ya usuluhishi na mahakama hiyo pia haitatambua matokeo kwenye ripoti ya kamati ya rais. Mahakama utatumia ripoti ya SGS maana inatambulika kimataifa au serikali ikikataa ripoti ya SGS mahakama itateua chombo kingine huru cha kimataifa kurudia uchunguzi wa mchanga kwenye container. Kama vipimo vya kiasi cha madini kwenye mchanga kitafanana na zile za SGS basi serikali ya Tanzania itabwagwa chini na acacia na kutakiwa kulipa gharama za kufidia kwa acacia.

4. Kuna uwezekano pia acacia wakasema mchanga kwenye container siyo wa kwao maana serikali imefungua container bila wao kuwepo na kupelekea uwezekano wa mchanga wao kutolewa na serikali kuweka mchanga mwingine.

5. Kwenye sakata hili uwezekano mkubwa ni serikali kupoteza na siyo kupata. Mikataba ya kimataifa inahitaji weledi na wala siyo mihemko ya kisiasa na ubabe wa serikali.

Mkinga mkinga
 
Sisi tunataka mfumuko wa bei ushuke. Umeme ushuke . Gesi ishuke watoto wetu wapewe mikopo wote.hatuna shida michanga sie.
 
Wanabodi,
Katika suala zima za kuibiwa kwa rasilimali zetu, kupitia mikataba mibovu ya kinyonyaji ambayo ni wizi mtupu, vita vya kupambana na rushwa kubwa "the grand corruption na vita dhidi ya ufisadi na uhujumu uchumi, naomba nisizungumze kuhusu awamu ya Nyerere na Mwinyi, nilikuwa mtoto, lakini awamu ya Mkapa, Kikwete na hii ya Magufuli, mimi ni mtu mzima ninayejielewa, hivyo nazungumza vitu nilivyovishuhudia vikitokea.

Kwenye mikataba ya madini, Mkapa alidanganywa sana tuu na akadanyika, tukaibiwa sana, Kikwete nae pia kwenye mikataba ya gesi asili, alidanganywa na akadanganyika, hivyo pia tukaibiwa sana na tunaendelea kuibiwa kupitia mikataba mibovu ya kinyonyaji, huku rushwa kubwa kubwa na ufisadi vikishamiri.

Magufuli tangu alipoingia, akatangaza kupambana na rushwa na ufisadi, na alipoanza, alianza kwa kasi kubwa, zile tumbua tumbua na ziara za kushtukiza za mwanzo, ziliamsha amsha, ilikuwa ni hakuna kulala, lakini kadri siku zinavyokwenda, spidi inazidi kupungua, zile shukiza sio shtukiza tena bali maigizo ya shtukiza, ila kwa vile watangulizi wake walidanganya na wakadanganyika na kuzidi kulizamisha taifa letu, kuna kila dalili sasa Magufuli naye ameanza kudanyanywa. Sawa ni jee Magufuli naye atadanganyika kama watangulizi wake, au huyu hadanganyiki?. Na jee Watanzania wazalendo wa taifa hili, wenye insight, mnapoona rais wetu anadanganywa, na mnajua kabisa anadanganywa, jee tutamuacha tuu adanganyike kwa sababu yeye ndiye mkuu, au tutapaza sauti zetu kumgutushakuwa anadanganywa, as a fiduciary duty to a good citizenship, ili hata ikitokea na yeye adanganyike, adanganyike kwa ridhaa yake kwa sababu aliambiwa, ili kukija kutokea mabadiliko ya utawala, tuwe na nguvu za kuwawajibisha hawa viongozi wa taifa hili wanaodanganywa na kudanganyika, japo wale wa mwanzo waliodanganywa na kudanganyika, tunaweza kuwasamehe kwa kusema walidanganyika kwa kutokujua, lakini hawa wanaodanganywa, kisha tunawaambia wanadanganywa, ikitokea wamedanganyika ili hali tuliwaambia, tutaamini wamekubali kudanganyika!. Jee Watanzania tukubali viongozi wetu wadanganywe na wadanganyike?.

Nakiri kupandisha bandiko hili kutokana na inspiration kutoka kwa mwana jf huyu Mkuu
Kwanzanaunga mkono hoja, linapokuja suala la maslahi ya taifa, Watanzania wazalendo, wana a duty of care kwa nchi yao kumsaidia rais, asidanganywe, pale ambapo wanaona wazi kabisa rais wetu anadanganywa!.

Rais wetu sio malaika ni binadamu tuu kama sisi, japo ana mamlaka kuu, lakini kama binadamu, hawezi kujua kila kitu, ndio maana tumemuwekea wasaidizi wa kumsaidia katika kutimiza majukumu yake ikiwamo kumshauri ushauri sahihi na sio kumdanganya, na wakuiona anadanganywa, wana jukumu la kumsaidia kwa kumwambia hapa anadanganywa ili asidanganyike!.

Hivyo watu wa kwanza wanaomdanganya rais ni wale wasaidizi wake ambao ni washauri wake wenye jukumu la kuhakikisha rais anakuwa well informed, hadanganyi, hadanganywi na wala hadanganyiki!.

Nikutolee mifano michache kuanzia awamu ya Mkapa. Watu walichonga deal wakamshauri Mkapa tununue ndege mpya ya rais, tunahitaji radar na vifaa muhimu vya kijeshi. (Hili la vifaa vya jeshi naomba msiliulizie).

Ununuzi ulifanywa kupitia restricted tendering kupitia kwa a single source. Wasaidizi wa rais wakamshauri tunahitaji sana hiyo radar, ndege na hizo zana!. Kumbe ulikuwa ni uongo mtupu. Watanzania wazalendo hadi wazungu wakapinga sana, na haswa bei tunayopigwa. John Cheyo hadi akamuonyesha bei ya Gulf Stream toka kwenye website yao, lakini Mkapa alitia pamba masikio na tukanunua ndege, radar na zana za kijeshi kwa kupigwa!. Manunuzi yote hayo yalifanywa na ajenti huyo huyo mmoja!.

Kilichofuata sote tunakijua, japo watu walilipwa mlungula, mimi siamini kabisa kuwa Mkapa hakujua kilichokuwa kinafanyika!.

Likaja suala la EPA, CCM ikataka fedha za kampeni, ndani ya Benki Kuu yetu, kumejaa minoti. Wajanja wakaunda vikampuni, na wajanja wengine wengi nao wakautumia mwanya huo huo wakachomekea yao wakapiga pesa ndefu. Waziri Meghji aliletewa barua akaambiwa Mzee anajua. Akaruhusu pesa zikachotwa. Tukapigwa!.

Siamini kama Mkapa hakujua wala Kikwete hakujua kuwa ameingia ikulu yetu kupitia fedha za wizi za kampuni ya Kagoda!. Jee unajua hii maana yake ni nini? . Thanks God marais wetu wana kinga ya kutokushitakiwa!

Kagoda: Kamwe haitafikishwa Mahakamani! | JamiiForums | The Home ...
Kagoda Haina Kesi, hawafikishwi Mahakamani Ng'o! | JamiiForums ...
Kwanini Mijizi ya EPA Ilisamehewa?!. Jee Unaunga Mkono au Unapinga ...

Rais Kikwete pia alidanganywa na akadanganyika. Kwenye kashfa ya EPA Rais Kikwete alidanganywa hadi kuvunja katiba kwa kuiachia mijizi ya EPA kurudisha ilichokwiba. Kwenye Escrow pia alidanganywa. Pamoja na mazuri yake yote, pia aliiacha nchi yetu in a mess!. Kazi ya kwanza ya Magufuli was clearing up Kikwete's mess!.

Kama rushwa na ufisadi vilishamiri na kusadifu Mkapa's era na Kikwete's era, this means both of them were possibly corruptible!.

Kwa utendaji huu wa Magufuli ameisha onyesha nia ya dhati toka moyoni mwake, kwa maneno na matendo kuwa anachukia rushwa, unachukia ufisadi, anachukia uzembe, na anachukia sana kudanganywa. Ila pia on the other side he is very human akiambiwa ukweli na mfano mzuri ni issue ya Bashite, baada tuu ya kuibuliwa Bashite alimwendea na kurudisha confess kila kitu kuwa ni kweli. Akamlinda.

Hivyo sina uhakika kwanza kama Magufuli anadanganyika, au kama atakubali kudanganywa kwenye mikataba, kama Mkapa na Kikwete. Ila kama nilivyosema mwanzo na yeye ni binadamu na sio malaika, Hivyo anaweza akadanganywa na akadanganyika, lakini Watanzania wazalendo wenye uoni mkubwa, wenye uwezo wa kuona kuwa hapa rais wetu anadanganywa!, tusikubali rais wetu adanganywe, na akidanganywa asidanganyike, ila ikitokea, akadanganywa na akidanganyika iwe ni yeye tuu kwa ubinaadamu wake, lakini sisi Watanzania wengine wazalendo, kamwe tusikubali rais wetu kudanganywa na kudanganywa!.

Kwenye hili la mchanga wa makinikia ya dhahabu, japo tayari rais wetu ameishanganywa kuwa Tanzania ndio inchi inayoongoza kwa kuzalisha dhahabu nyingi duniani kuliko nchi
nyingine yoyote kupitia taarifa ya viwango vya dhahabu kwenye makinikia yaliyomo ndani ya makontena 277 ya mchanga wa dhahabu wa migodi miwili tuu ya ya Acacia, nashauri tusilinyamazie hili, tuungane na rais wetu katika kutafuta ukweli hakika na bayana kwa maslahi mapana zaidi ya taifa letu.

Mungu Ibariki Tanzania.
Paskali

Naona hata kwenye kile kivuko kibovu cha mwaka 1928 Waziri wa Ujenzi alidanganywa ?Uzuri unamjua hulka ya Rais wako hata akielezwa hata kubali,pili yake wote ni wale wale,hatuguzi Makaburi,na hilo linaloguswa ni kaburi la miaka 20 iliyopita unadhani litaendelea kuchimbwa??Au ndiyo limeisha baada ya kutenguliwa kwa Muhongo?
 
Magufuli hadanganyiki, mfano mzuri ni alipowanyima Wachina tender ya SGR akawapa wazungu yeye anaponzwa na mikataba ya waliomtangulia
 
Kwa mfano vyeti feki vya Bashite utasema raisi kadanganyika? Jibu ni hapana ila amehalalisha kudanganywa na kuwaita wapenda udaku waliomkumbusha na kumjulisha kwamba alidanganywa. Kwa kifupi ni kwamba kiongozi kiongozi mkuu haitaji kukumbushwa wala kushauriwa cha kufanya kwakua fomu alichukua mwenyewe na yeyote atakaye mshauri au kumkumbusha kitu ambacho ni tofauti na anachowaza yeye basi huyo ni mpiga dili na sio mzalendo au muuza madawa ya kulevya.
 
Back
Top Bottom