Kikwete hajajifunza kwa Mkapa? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kikwete hajajifunza kwa Mkapa?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by BAK, Aug 6, 2009.

 1. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #1
  Aug 6, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,814
  Likes Received: 83,213
  Trophy Points: 280
  Kikwete hajajifunza kwa Mkapa?

  [​IMG]
  Lula wa Ndali-Mwananzela
  Raia Mwema~Muungwana ni Vitendo
  Agosti 5, 2009

  [​IMG]NINA hakika kuwa kama tungembana aliyekuwa Rais wetu Bw. Benjamin Mkapa enzi za utawala wake, baadhi ya mambo yasingefika hapa yalipofika. Kama tungewabana mawaziri wake enzi zile na kuwanyooshea vidole bila kupepesa macho kama tunavyofanya leo, nina hakika nchi yetu ingekuwa na mjadala tofauti leo hii.
  Hofu yangu ni kuwa, yawezekana tumejenga katabia kabaya kakusubiri hadi watoke madarakani ndiyo tuanze kuwanyooshea vidole na kusema kuwa "walifanya hivi na hawakufanya vile; hivyo ni mafisadi". Tabia hii ni mbaya kwani inawalea viongozi wabovu, inachochea kutowajibika, na kwa hakika inatuonyesha ni jinsi gani wanaharakati ni watu wa kutegea.
  Ni kweli kuwa kwa kiasi kubwa hilo limebadilika wakati huu. Tumeweza kupiga kelele na kuinyooshea mkono serikali; japo mara ya kwanza tulikabiliwa na mikwara toka kwa wale wanufaika.

  Tumeweza kuwapigia kelele kina Lowassa, Chenge, Karamagi, Msabaha, Mwanyika, na wengine wengi. Japo kelele hizo nyingi hazikusikika lakini kwa kiasi fulani zilifika kunakotakiwa japo kama kwa kulazimisha kama mtu anayesukuma kufungua mlango uliogoma.

  Hata hivyo, naanza kuona dalili mbaya inayoendelea hususan juu ya Rais wetu wa sasa Mh. Jakaya Kikwete. Inaonekana bado hajajifunza yale yaliyotokea kwa Mkapa na sasa tunapoingia "ndani ya 18" kabla ya uchaguzi mkuu, kuna dalili kuwa hawezi kujifunza tena na hivyo tukubali tu ngwe yake iishe tufikirie kuanza upya 2010.

  Mambo matatu yananifanya niamini kuwa Kikwete hajajifunza kutokana na yale ambayo yanamkabili Mkapa leo hii.
  Kwanza ni suala la Richmond. Sijui ni nani mshauri wa hawa watawala, lakini ilichofanya serikali kutotekeleza maelekezo ya Bunge ni dalili ya kiburi, kutokuelewa, dharau na kejeli dhidi ya Bunge.

  Bunge limefanya uchunguzi kupitia Kamati yake Teule iliyoongozwa na Dr. Harrison Mwakyembe; uchunguzi ukaletwa bungeni na ukatangazwa, ukajadiliwa na matokeo yake aliyekuwa Waziri Mkuu akajiuzulu pamoja na mawaziri wengine wawili husika katika sakata hilo. Na matokeo yake Baraza zima likavunjika na kulazimisha serikali kuundwa upya.

  Kilichotakiwa kufuatia baada ya hapo ni kujiuzulu kwa Edward Hosea, Johnson Mwanyika, na wale viongozi wote wa wizara na idara waliotajwa kwenye ripoti hiyo kuwa wawajibishwe. Hilo lilitakiwa kufanyika siku ya pili baada ya Baraza la Mawaziri kuvunjika. Hicho hakikufanyika.

  Alipoingia Waziri Mkuu mpya, Mizengo Pinda, ambaye sasa tunajua ana tatizo kubwa la kuitii Katiba na kufuata sheria (sitorudia mifano nilishaandika huko nyuma), akaamua kuanzisha uchunguzi wake nje ya ule wa Bunge. Akaamua kutotii maelekezo ya Bunge na kujaribu "kutafuta ukweli" juu ya Richmond na hawa wahusika waliotajwa.

  Katika uchunguzi wao wakafikia mahali wakaona WOTE hawakufanya makosa ya kulazimisha kujiuzulu. Hivyo, wakapeana "makaripio" wakitegemea yaishe.
  Walichotengeneza kimsingi ni mazingira ya kumsafisha Lowassa. Yaani, kama hawa wengine wote hawakuwa na makosa ya kujiuzulu, na kuwa ripoti haikuwatendea haki; iweje Lowassa awe na hatia? Tunajua tuliambiwa kujiuzulu kulikuwa kwa kisiasa; je yawezekana kuwa hata kujiuzulu huko kulikuwa ni adhabu kubwa mno kuliko kosa lenyewe? Jibu la kina Pinda ni lenye mkazo - Ndiyo!
  Hivyo, serikali ikaamua kulindana na kusafishana kiaina. Wakaamua kulionyesha Bunge kuwa ni la uonevu, lisilofuata haki, ni butu, na lisilo na uwezo wa kuisimamia serikali. Cha kuudhi hapa ni kuwa Kikwete aliridhia serikali kutolitii Bunge. Hilo ni kosa la kiutendaji na kiutawala, na kikatiba.

  Kikwete alitakiwa kuwaandikia wale ambao wako kwa ridhaa yake na kuwataka waandike barua za kujiuzulu na wale walio chini ya mawaziri au makatibu kufanyiwa hivyo hivyo na suala la Richmond lingekuwa limefungwa mwezi wa pili au wa tatu mwaka jana. Tungebakia na la Dowans tu!

  Suala la pili ni suala la madini. Kama vile Mkapa alivyoshindwa kuleta mabadiliko katika sekta ya madini na kuendelea kuuza urithi wetu kwa wageni kama njugu mtaani, ndivyo Kikwete naye ameshindwa kuleta mabadiliko katika sekta ya madini kwa sababu yeye kama Mkapa wanaogopa kuwakwaza na kuwatisha wawekezaji.
  Sheria mbovu ya madini ya 1998 ambayo ilipitishwa baada ya Meremeta (kuna uhusiano) imeendelea kufanya kazi na Kikwete, na CCM wameshindwa kuleta mabadiliko muafaka ya sheria hiyo.

  Mkapa, ambaye utawala wake tumeutangaza rasmi kuwa ulikuwa ni wa kifisadi, alishindwa kulinda urithi wetu. Ni yeye aliyewamegea wageni na kisha kujimegea mwenyewe na washirika wake.
  Ndiye aliyekuwa mnufaika wa sheria hiyo. Kwa maneno mengine, sheria hiyo ilikuwa ni kwa ajili ya kuwanufaisha wageni na siyo kulinufaisha taifa. Wabunge wa CCM waliikubali kama wanavyoikubali leo hii.
  Kikwete naye "ndani ya hizi 18" ameshindwa kuwaongoza wabunge wa Chama chake kusimama kidete kutetea utajiri wetu, na matokeo yake watu wetu wanakunywa maji ya sumu, tunaachiwa mashimo ya zebaki; huku dhahabu yetu ikiendelea kupeperushwa nje ya nchi huku wana CCM wakiendelea kuimba "CCM nambari wani ee, nambari wani CCM"!
  Kikwete amebakia kuburuzwa na wawekezaji kwani hataki, na hawezi kuchukua hatua kali za kutetea urithi wetu kwa mujibu wa Katiba. Ibara ya 27 ya Katiba yetu inasema hivi:
  (1) Kila mtu ana wajibu wa kulinda mali asilia ya Jamhuri ya Muungano, mali ya Mamlaka ya Nchi na mali yote inayomilikiwa kwa pamoja na wananchi, na pia kuiheshimu mali ya mtu mwingine.
  (2) Watu wote watatakiwa na sheria kutunza vizuri mali ya mamlaka ya nchi na ya pamoja, kupiga vita aina zote za uharibifu na ubadhilifu, na kuendesha uchumi wa taifa kwa makini kama watu ambao ndio waamuzi wa hali ya baadaye ya taifa lao.
  Kwamba Watanzania wote tuna haki ya kulinda maliasilia ya nchi yetu; dhahabu, tanzanite, almasi, nickel, mafuta, mbuga, wanyama, n.k; hili ni jukumu la kila Mtanzania. Na zaidi ya yote, tunatakiwa kupiga vita uharibifu na ubadhilifu wa aina zote.
  Na katika haya, wa kwanza katika kutuongoza katika mapambano haya ni Rais wetu. Kwani yeye ndiye ambaye mali yote ya asili ya nchi yetu iliyoko kwenye ardhi yetu anaishikilia kwa dhamana (in trust).
  Sasa Kikwete anapobabaika na kupata kigugumizi mbele ya wawekezaji tunachoweza kusema ni kuwa anaonyesha udhaifu ambao siku moja utakuja kumgeuka; kwani tutamnyoshea kidole kama Mkapa na tutaka kujua ni kwa kiasi gani yeye na familia yake wamenufaika na mfumo wa sasa.
  Kikwete anatakiwa kuwaambiwa wawekezaji "tunafanya mabadiliko ya sheria ya madini ili kuwanufaisha watu wetu kama hamtaki kwaherini".
  Lakini kwa vile hilo hawezi kulifanya kwa sababu ambazo wengi tunazijua, basi, Bunge lilitakiwa kufanya hivyo. Wabunge wa CCM na wa upinzani wangeweza kukaa pamoja na kuandika sheria mpya ya madini na kumpatia Rais ili aikubali, na kama hataki, basi, kama walivyosema wengine twende kwenye uchaguzi mkuu mapema mwakani!
  Kushindwa kwa Kikwete na CCM kuleta mabadiliko yatakiwayo kwenye sekta ya madini yamethibitisha ni jinsi gani CCM inahusiana moja kwa moja na kile tunachokiona kama umaskini katika taifa letu. Ni wao ndio wenye kubeba lawama yote kuhusu uporaji wa madini yetu na raslimali zetu; kuanzia Loliondo hadi Kagoda ni wao ndio wamechangia wageni kutukwangua vichwa vyetu kwa visu huku wakitutaka tutulie kimya ati "tunanyolewa".
  Jambo la tatu ambalao limenifanya nione kuwa Kikwete hajajifunza toka kwa Mkapa, ni kuchukulia viapo vyao vya kazi kwa uzito unaostahili. Kuna kamtindo ka kuapa bila kumaanisha unachoapa. Karibu watu wote ambao wanashika madaraka ya umma wanakula viapo vya utii kwa katiba na kile cha kazi zao na wengine wanakula kiapo cha usiri vile vile.
  Viapo hivyo vinatakiwa kuwa kama yamini ambayo mtu akiivunja anatakiwa yamkute. Lakini watawala wetu inaonekana wameshafikiria kuwa wanaweza kuvunja viapo vyao na kusiwe na matokeo yoyote. Mkapa alifanya hivyo na hakuna kilichomtokea; sasa kwa nini Pinda na Kikwete wasifanye hivyo hivyo?
  Hawavipi uzito viapo vyao kama inavyostahili, matokeo yake wanaongoza kwa kufuata jinsi wanavyojisikia na kufikiria.
  Ndio maana Bunge linapojaribu kusimamia majukumu yake kwa mujibu wa viapo vyao vya Kikatiba, linaonekana ni adui. Leo hii wapo watu wanaojaribu kulidhoofisha Bunge na wabunge kwa kueneza tuhuma mbalimbali za ufisadi dhidi ya viongozi wa Bunge.
  Nina ushauri mmoja kwao; kama wanaamini kuna kiongozi wa Bunge amevunja kiapo chake, basi, wawashawishi wabunge kwa uzito wa ushahidi ili viongozi hao waondolewe.
  Wakati huo huo, Bunge lisikubali kudharauliwa hata mara moja. Wabunge wanaporuhusu serikali ilidharau Bunge kama ilivyofanya kwenye suala la Richmond wanathibitisha udhaifu wao na kuwa na wao hawachukulii kwa umakini viapo vya wabunge.

  Ndio maana naungana na wale ambao wanataka suala hili la Richmond lifikie kikomo Novemba. Hatuwezi kama taifa kuendelea kucheza na mdoli wa Richmond wakati hata ya kina Kagoda hayajaanza na kina Dowans wanaendelea kutukalia shingoni!

  Ushauri wangu kwa serikali ni kuwa msilichezee taifa. Waliotajwa na Bunge kuhusika na Richmond wawajibishwe. Ni hilo tu linalotakiwa kufanyika. Kitu cha kwanza kinachotakiwa kufanyika ni utii kwanza malalamiko baadaye.
  Watajwa kama watapewa majukumu mengine na iwe hivyo ili wajionyeshe kuwa wako safi, lakini hawawezi kuendelea kukalia nafasi zao zile zile wakati Watanzania wamewataka wawajibishwe.

  Kama Mh. Mizengo Kayanza Peter Pinda anaona ni vigumu kufuata sheria na taratibu na kuwa anaona hawa watu wameonewa na kuwa kwa kweli atakuwa anawaonea akitaka wawajibishwe, basi, yeye mwenyewe awe wa kwanza kujiuzulu ili kumpisha Waziri Mkuu mpya ambaye atafuata Katiba na Sheria na siyo hisia zake au fikra zake.
  Na kama Kikwete anashindwa kumsimamia waziri wake mkuu na kumuacha afanye mambo ya dharau kwa Bunge (contempt of parliament), basi, yeye mwenyewe vile vile ajiuzulu na Dk. Shein ashike madaraka ya urais hadi uchaguzi mkuu.
  Tumetaka utawala wa demokrasia na sheria sivyo? Basi tuwe tayari kulipa gharama yake. Na gharama ya kwanza ya utawala wa demokrasia ni mgawanyo wa madaraka, na zaidi ya yote utii kwa wawakilishi wa Watanzania.
  Siku kiongozi yeyote wa serikali anaposhindwa kuwatii Watanzania (kupitia wawakilishi wao) kiongozi huyo anajisimamisha kinyume na maslahi ya Watanzania, na anatakiwa kujiuzulu.
  Hamjajifunza toka kwa Mkapa?
   
 2. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #2
  Aug 6, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  hili swali zito. Lakini kuna kitu chochote ambacho JK anapaswa kujifunza kwa Pinda au na yeye anasubiri atoke aone tutakavyomshukia kama mwewe?
   
 3. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #3
  Aug 8, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,585
  Likes Received: 5,771
  Trophy Points: 280
  NINA hakika kuwa kama tungembana aliyekuwa Rais wetu Bw. Benjamin Mkapa enzi za utawala wake, baadhi ya mambo yasingefika hapa yalipofika. Kama tungewabana mawaziri wake enzi zile na kuwanyooshea vidole bila kupepesa macho kama tunavyofanya leo, nina hakika nchi yetu ingekuwa na mjadala tofauti leo hii.

 4. Josh Michael

  Josh Michael JF-Expert Member

  #4
  Aug 9, 2009
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 2,525
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Hakuna ndani ya CCM wa kufanya kweli na huku ushetani wao ndio uliochangia watu kuingia madarakani na hat kushinda uongozi
   
 5. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #5
  Aug 9, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280

  Kwa hiyo kimsingi tuko ndani ya 18 ladies and gentlemen!
   
 6. N

  Nakwetu Member

  #6
  Aug 10, 2009
  Joined: Apr 27, 2009
  Messages: 73
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hivi wewe Bubu ni bubu kweli. Je unajua mgawanyiko wa mihimili MITATU. Sasa unataka Bunge wafanye uchunguzi na Uchunguzi wao ndio uwe kama kitabu kitakatifu yaani wasielezwe chochote ila Serikali ni kutekeleza to the last comma. Sheria na taratibu ambazo wao Bunge walitunga zitatumika saa ngapi? Kanuni na taratibu za utumishi wa Umma ufutike kwa kuwa Bunge wamesema! Sikiliza kila uapande ndio na wewe utoe msimamo wako siyo kung'ang'ania kitu kile kile kama wewe huna Brain za Ufafanuzi. Toa na wewe maoni baada ya kupata maelezo mengi, yaani na wewe utakuwa umeshiriki kwa Mtazamo wako. Bunge limesema ndio wimbo wako BUBU, wake UP
   
Loading...