MwanaFalsafa1
JF-Expert Member
- Feb 26, 2008
- 5,564
- 849
- Mkuu Jasusi dataz ziko sawa, anakuja na delegation ya watu 40, kwa hesabu niliyopata jana toka pale kwenye kuchukua viza ya US, na wote hao wanalipiwa hii safari na kodi yetu.
- Halafu mind you kwamba, akifika LA lazima balozi wetu US asafiri kutoka DC na maofisa kama watano toka ubalozini kwenda kumpokea na kusaifi naye ndani ya US, ti is incredible yaani ajabu na kweli!
- Halafu September, atarudi tena huko US, yaani UN kwenye General Assembly! na watu zaidi ya 40.
Mungu Aibariki Tanzania.
FMES
Rais Kikwete pamoja na Ujumbe wake wanategemea kukutana na Watanzania huko Los Angeles (CA),Kutakuwa na utambulisho na baadaye Rais ataongea na kujibu baadhi ya maswali ya Watanzania waishio huko,Ili kujua utaratibu na venue wasiliana na mratibu wa shughuli hiyo Ms.Assenga au Uongozi wa Watanzania Los Angeles.
Rais Kikwete pamoja na Ujumbe wake wanategemea kukutana na Watanzania huko Los Angeles (CA),Kutakuwa na utambulisho na baadaye Rais ataongea na kujibu baadhi ya maswali ya Watanzania waishio huko,Ili kujua utaratibu na venue wasiliana na mratibu wa shughuli hiyo Ms.Assenga au Uongozi wa Watanzania Los Angeles.
Rais atakutana na Jumuiya ya Wafanyabiashara weusi (African American) waishio huko Los Angeles na miji ya karibu na siku ya Jumatano Jioni atahudhuria hafla ya chakula cha jioni iliyoandaliwa na USDFA,Kutokana na Mchango wake Binafsi wa kupambana na maradhi na kuboresha Ustawi wa Afya ya Jamii Tanzania na Afrika kwa ujumla...Sifa na maneno hayo yapo kwenye kadi ya mualiko wa shughuli hiyo iliyoandaliwa na CEO wa USDFA, Bw.Ted Alemayehu.
Katika ratiba ya awali ilielezwa kuwa Rais alikuwa na safari ya kwenda Houston (TX) kuzindua DICOTA "Diaspora Council Of Tanzanians in US" uzinduzi uliopangwa kufanyika tarehe 20/may...Uzinduzi wa organization hiyo umeaahirishwa mpaka Septemba,Rais atakapokuja tena kwenye General Assembly.Kamati ya Uandaaji wa shughuli hiyo inayoongozwa na Dr.Lennard Tenende imethibitisha kutokuwepo kwa shughuli hiyo.
Siku ya Alhamis Rais atakwenda Washington DC,ambako pamoja na mambo mengine atakutana na Uongozi wa World Bank na Uongozi wa State Department.Pia imeleezwa kuwa Rais atakutana na Rais Mstaafu Benjamin Mkapa ambaye yupo Washington DC kwenye mkutano wa GLCA "Global Leadership For Climate" Rais Mstaafu Mkapa anatarajia kurudi nyumbani Ijumaa.
Rais Kikwete atamaliza Ziara yake Ijumaa baada ya Mkutano na Naibu katibu Mkuu wa UN ,Dr Asha Rose Migiro.Hii ni mra ya pili kwenye mwezi huu Rais kukutana na Naibu Katibu Mkuu,mara ya kwanza ilikuwa mwanzoni mwa mwezi walipokutana Copenhagen,Denmark.Vyanzo vya habari vinaeleza kuwa Dr.Migiro amekuwa karibu na siasa za Tanzania katika siku za karibuni.Rais na Ujumbe wake wanamaliza Ziara yao Ijumaa jioni!
mbinu nyingine.. are you kidding me? Have you ever heard CCM ikisema curbing government spending? kufunga mianya ya extravagances kama iliyoko kwenye ripoti ya CAG au mfumo mzuri wa kodi?
Kwa kadiri misaada inaendelea kutawala hawaoni haja ya kutafuta mbinu mbadala!
On the other hand.. unajua wizi mkubwa wa fedha za umma unafanywa katika trip hizi.? Wakati akiwa anapitia UAE miezi michache iliyopita baadhi ya wapambe walinunua injini za magari yao kuziweka kwenye ndege kwa hela ya walipa kodi wa Bongo.. na JK hajui hilo!
Kwa wale mlioko Los Angeles mheshimiwa rais Kikwete anawasili huko Tuesday. Atakutana na Watanzania pia. Atawasili Washington D.C jumatano lakini hana mpango wa kukutana na Watanzania kwa kisingizio kuwa Jumuiya ya Watanzania Washington bado ina mzozano wa uongozi. Atakutana na Hillary Clinton jumatano hiyo na Ijumaa anaingia NY.
Mwanakijiji na wengineo mimi bado napata tabu sana kwa kweli na sielewi kwa kweli hivi hawa jamaa walipogombea urais walikujuwa ni nini wataenda kufanya huko ikulu kuiendeleza hii nchi na wananchi au waliutaka tu urais then basi? Katika karne hii kuwa na rais ambaye anaamini katika maendeleo ya nchi kwa kutegemea misaada peke yake huko ni kuliwa ndugu zangu.
Mwanakijiji umetaja mfumo wa kodi. Naomba niongeze kidogo, last week kulikuwa na thread hapa ya kodi. Kuna watu kariakoo wanapata 100ml mpaka 1b lakini wanalipa kodi laki 7 mpaka 1m si kwa kuevade no na kwa mfumo mbovu wa kodi tulionao, tax net yetu iko na shida kubwa kupita maelezo. Na kuna dollars kibao tunazipoteza kwenye income tax ya rent income. Wanaomiliki apartments na nyumba nyingine za kupangisha hawalipi income zaidi ya land rent simply kwa sababu kitilya na wenzie wa TRA wamelala usingizi wa pono. Naambiwa kuna survey ilifanywa kuhusu hilo na report ilikuwa submitted miaka imepita sasa hakuna kilichofanyika kama ile kamati ya madini ya kikwete. Na uzembe wa bandarini ndio usiseme. Hivi ccm na kikwete hawayaoni yote haya? So kazi yao nini basi kusafiri tu nje na bakuli la misaada? POLE SANA TANZANIA.
Huyu JMK sasa ni kituko.
Kikwete bila shaka anashauriwa vibaya ama anadanganywa... na watu ambao hawamtakii mema ama wanafaidika na safari hizo za Kikwete......................
Rais
Rais Kikwete atamaliza Ziara yake Ijumaa baada ya Mkutano na Naibu katibu Mkuu wa UN ,Dr Asha Rose Migiro.Hii ni mra ya pili kwenye mwezi huu Rais kukutana na Naibu Katibu Mkuu,mara ya kwanza ilikuwa mwanzoni mwa mwezi walipokutana Copenhagen,Denmark.Vyanzo vya habari vinaeleza kuwa Dr.Migiro amekuwa karibu na siasa za Tanzania katika siku za karibuni.Rais na Ujumbe wake wanamaliza Ziara yao Ijumaa jioni!