Kikwete, sasa umemwelewa Sumaye?

CCM imebakiza mwezi mmoja na siku kadhaa madarakani, watukabidhi nchi yetu kwa Amani. Hatutaki fujo, wala damu ya mtu imwagike! Watukabidhi kiroho safi kama waingereza walivyofanya kwa Nyerere mwaka 1961.


Sasa sijui wameelewa au bado wanajifunza....
 
ulutheri na UKANDA NDIYO ULIYOMPELEKA SUMAYE UKAWA NA SIYO HOJA SISI TUNALIJUA ILA TUTAONANA OCTOBR 25
 
Nakumbuka sana sasa sijui hiyo chandimu imeishia wapi!!!
Nadhani alijimaliza pale pale jangwani alipoishia kusema "miwani oyeee,Kifimbo oyeee,kofia oyeee..."
nadhani hapo ndo wakamuona kituko na si ajabu alikanywa ndo maana kasepa.
 
Ndugu wana JF,

Nimelazimika kumwandikia rafiki yangu kipenzi JK waraka huu wa swali kwamba sasa amemwelewa Sumaye? Ktk makundi ya wanafunzi tunazo aina tatu yaani gold...silver...stone.

Gold huweza kuelewa bila msaada wa mwalimu na kwa haraka sana... Silver huelewa mara moja akifundishwa na mwalimu na hahitaji nguvu ya ziada ... Stone yeye hata akifundisha ni ngumu kuelewa na huhitaji mbinu kali zaidi aelewe ikibidi kwa kurudia rudia somo lkn hawa hawafiki mbali kielimu.

Nimeanza na utangulizi huo nikiikumbuka kauli ya rafiki yangu JK pale jangwani kwenye ufunguzi wa kampeni za CCM aliposema amemsikiliza Sumaye hajamwelewa!! anasema mpaka siku hiyo anapokwenda uwanjani alikuwa hajamwelewa!!!!

Lakini ktk sokomoko hilo tumeshuhudia CCM ikibadili mbinu na sera... Bajeti ya kampeni ikiongezeka maradufu na hata kuwakumbatia wale JK aliowaita wanamiliki viwanda vya uongo ili tu kupunguza mvumo wa kauli na sumu za Sumaye majukwaani ndo nauliza sasa JK amemwelewa Sumaye?

Ndani ya vikao vya siri ajenda imekuwa Sumaye... ndugu yangu BM hana raha tangu Sumaye aondoke CCM...

Vilio na kutupiana lawama vimetawala ndani ya CCM juu ya kile Sumaye anafanya huko UKAWA!!!

Mafaili machafu dhidi yake yametafutwa yamekosekana!! hata hoja ya shamba halali la mvomero iliyoletwa na Makamba haijauza sasa wanaulizana ITAKUWAJE SUMAYE ANAYETUJUA SISI BINAFSI AKIAMUA KUFUNGUKA??

Siku anajitoa CCM Sumaye alisema huko CCM mmemuona ni sisimizi tu kiasi cha kuandika barua kutojibiwa hivyo wataona umuhimu wake akiwa Upinzani na ni dhahiri sasa anawatetemesha ndipo nauliza JK sasa umemwelewa Sumaye?

Nimeuliza kote walikopita wana UKAWA nimeambiwa watu wamekua na shauku kubwa mno yakumsikiliza bwana zero kuliko yeyote na amekuwa akitoa hamasa sana ....

Sumaye amejenga ujasiri sana kwa wapinzani na wapenda mabadiliko... ameondoa hofu na woga... amejenga kujiamini sasa vinaanza vitisho kuwa nchi haiendi upinzani!!!!

Nauliza tena JK uliyesema kwa dharau humwelewi Sumaye sasa umemwelewa au abadili mbinu za ufundishaji? umuulize na mdogo wako Makongoro ule mchezo wa CHANDIMU vipi mbona amechoka mapema??

Ahsante kwa kunisoma natumai umenielewa!!!

Ndimi LUSUNGO.

Watz kwakudhalauliana hatujambo anayemwita rais wake jiwe yeye hata uwenyekiti wa ukoo hana.!
 
Atamwelewa tuu!! Sisi wapenda mabadiliko tunamwelewa, yeye amwelewe asimwelewe atupishe!! gari limeshika mwendoooo!!
 
ulutheri na UKANDA NDIYO ULIYOMPELEKA SUMAYE UKAWA NA SIYO HOJA SISI TUNALIJUA ILA TUTAONANA OCTOBR 25


Wakati anamponda Lowassa ulutheri na ukanda hakuwa nao?

Wakati EL na Sumaye wakiwa paka na panya hawakuwa wote walutheri? sasa ilikuwaje?

Mbona Mwigulu Mlutheri lakini anaendesha mashambulizi kwa EL?

Mbona Mangula Mlutheri lakini anaendesha mapambano dhidi ya EL?

Sitta... Mwakyembe je?

Hivi kwanini CCM mnapenda kukimbilia ajenda za kipuuzi zinazoweza wamaliza wenyewe?

Kuna walutheri wangapi wenye nguvu huko CCM ambao ndo mnawatumia kumpiga EL?

Unafikiri wote ni manyani kama wewe mnaokimbilia abracadabra za udini?
 
Nikumbushe Watanzania walimwita Sumaye nani?


JK amemwelewa Sumaye?

Habari ya watanzania walimwitaje haina nafasi hapa hoja ni vipi mnatumia nguvu kubwa sana kupambana na mtu ambaye hamjamwelewa?"

Nawe upo kwenye kundi la jiwe?
 
Watz kwakudhalauliana hatujambo anayemwita rais wake jiwe yeye hata uwenyekiti wa ukoo hana.!


Nani kasema rais ni jiwe?

Au ndio hizi akili za IT centre Masaki na Lumumba mlioshindwa vibaya ktk propaganda?

Umejuaje kama hata uongozi wa ukoo sina?
 
Sumaye anasuburi dakika za majeruhi atupie kambani bao la ushindi. Nina mashaka sana hapa kama hatuja juzwa ya KIWALA COAL MINE na ANBEN CO. LTD.
 
Nani kasema rais ni jiwe?

Au ndio hizi akili za IT centre Masaki na Lumumba mlioshindwa vibaya ktk propaganda?

Umejuaje kama hata uongozi wa ukoo sina?
Huyo nae yupo kwenye kundi la mawe, hawezi elewa unacho maanisha.
 
JK amemwelewa Sumaye?

Habari ya watanzania walimwitaje haina nafasi hapa hoja ni vipi mnatumia nguvu kubwa sana kupambana na mtu ambaye hamjamwelewa?"

Nawe upo kwenye kundi la jiwe?

Huwezi kumuelewa mtu ambaye kichwani hana kitu kama ambavyo mimi nashindwa kukuelewa wewe!
 
Sumaye anasuburi dakika za majeruhi atupie kambani bao la ushindi. Nina mashaka sana hapa kama hatuja juzwa ya KIWALA COAL MINE na ANBEN CO. LTD.


Hofu kuu iliyopo CCM ni kwamba mpaka sasa Sumaye hajafunguka chochote in details kuhusu uchafu wa CCM na viongozi wake...

Siku ile aliongea kiujumla tu... mtu aliyekaa kileleni for 10 years anafahamu mengi ya wale waliokua chini yake ..

mbaya zaidi CCM wamemaliza silaha zote ilhali Sumaye hajatumia bado...
 
Huwezi kumuelewa mtu ambaye kichwani hana kitu kama ambavyo mimi nashindwa kukuelewa wewe!


Nijuavyo huwezi kuhangaika na mtu ambaye humwelewi...

kama ndivyo kwanini CCM haimwachi Sumaye midomoni mwake?

Kwanini kutwa ni kupanga mbinu za kumnyamazisha?

Kwanini mnawaangukia wale mliowapuuza ili wapambane na Sumaye?

Kama hujamwelewa mtu unahangaika naye wanini??
 
Back
Top Bottom