MH Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Jakaya Mrisho Kikwete.
Mbwa akikukenulia meno kamwe hatabasamu, Tabasamu la mbwa ni kuchezesha mkia.
MH Rais Umesoma Alama za Nyakati Vibaya sis akina MADELA WA- MADILU tunatakiwa kukupa vipande vyako.
Namkumbusha Rais Kikwete juu ya Siasa ya nje ya Marekani.
Namkumbusha Rais Kikwete juu ya hila za mabepari Duniani.
Serikali ya Marekani haina nchi rafiki hata siku moja, hiyo ndo sera yao ya nje.
Ni ajabu sana kwa mtawala wa wetu Tanzania Rais JM Kikwete kudhani wamarekani wako tayari kutusaidia sisi Watanzania.
Yeye Binafsi kama rais wa nchi si muoni akitembeza Sera ya kuikomboa nchi zaidi ya kukata stori Muflisi kama bado anahudhuria Disco la TAZARA na kupepesa macho huku akiwa na kigugumizi kama kaona msululu wa mademu wakali wa vimini wakikatiza kwa madaha.
Mtu hapa ajitokeze aniambie nchi moja tu iliyosaidiwa na marekani na kuendelea!
Wajapana walishaendelea mbali kabisa hata kabla ya Vita kuu ya 2 ya Dunia ndiyo maana ilichukua miaka 3 kwa nchi kubwa kama Mareakani kupigana na Japan na bado ilibidi watumie Bomu la Atomic ili kumaliza Kilanga heavy cha Wajapan.
Wajapana walikuwa wakitengeneza ndage kwa kutumia injini za Mitsubishi kipindi Kirefu kabla hata Dime moja ya Mmarekani haijatua Japan kama msaada.
Japan,Singapore,SouthKorea na sasa China hazijasaidiwa na Marekani kuendelea ila zinapambana kiuchumi na marekani kwa mikakati mikali ilo jengwa kiuthabiti ndani ya nchi zao na viongozi wao wenyewe.
Marekani inabidi itoe ushirikiano kwa nchi hizi kwa vile haina cha kufanya, Sasa hivi Marekani inajitahidi kukuza uchumi wa nchi za Amerika ya Kusini ili baadaye ku counter check maendeleo ya Asia, lakini inaonekana Timing yao ni mbaya kwani wako akina Chavez wanao wavurugia Dili zao nyingi.
India ndiye supplier mkubwa wa Maengineer na Madaktari nchini marekani, Marekani inabidi atoe ushirikiano kwa India kwa sababu hana watu wake mwenyewe wa kuwafundisha udaktari. Watu wengi ndani ya Marekani wanataka kusomea michezo na management ya biashara.Au kuwa macelebrity kwa kufanya jambo lolote lile hata liwe la aibu kiasi gani; kama Kupost Video yako ukijamiaana na mwenzi wako kama Paris Hilton, kupiga picha za uchi nenda YOU TUBE,kukaa vibaya na kuonyesha uchi kwa wapiga picha kana kwamba ni bahati mbaya kama livyofanya Britney.
Waswahili wanasema ukishikwa shikamana.
Marekani akikupa mtaji katika hali yeyote ile nia yake kubwa ni kukunyonya tu.
Ili kukwepa kunyonywa ni lazima akili yako kama Rais ifanye kazi mara mbili na uwe ni kiongozi wa Machale kweli kweli si kama Rais Kikwete amabye ziara yake anafuatana na Makuwadi washika tunguri na watoto wa rafiki zake akina Makamba kama wapambe uchwara.
Ukipewa mshiko na marekani, ni mipango yako ya ndani ndiyo itadetermine maendeleo yako siyo misaada upewayo.
Kama nchi, Tanzania tunepewa mabillioni ya $$$$$ kwa kipindi kirefu sana hata kabla; Kingunge hajawa Mkuu wa mkoa wa Tanga na Class mate wake Kleruu ajachapwa risasi na Mzee Mwamwindi,lakini bado tuko nyuma kwa kila kitu.
Sasa hivi, MH Rais Kikwete unatuonyesha wazi Kama kiongozi wa nchi na Serikali ya SISIEMU kwamba hata kwa mawazo na sera tuko nyuma kabisa.
Huwezi kuwa na Sera za kiilma kama za SISIEMU ukategemea kukwamua nchi na wananchi kiuchumi.
Sera zisizo weza kuhusianisha Umasikini wa wananchi na maamuzi ya NEKI ndani ya SISIEMU na ya viongozi wazembe kama Karamagi ndani ya serikali.
Sera Imla kama hii ya SISIEMU ni sera itakayo wafanya watu wachache ndani ya Tanzania kuendesha nchi kama Estate ya baba yao na hivyo kutoa maamuzi kwa namna Roho na utashi wao upendavyo na si kwa kuzingatia Masklahi ya Wananchi wa Tanzania na Taifa kwa ujumla.
Misifa wanayommwagia Kikwete inatokana na ukweli kwamba mauzo yetu ya dhahabu huko ughaibubni yameongekezeka 100 folds sasa kila Bepari kupitia kila chombo anajitahidi kumpaka Rais wetu mafuta kwa Mgongo wa chupa na kumvisha kilemba cha manyasi ili naye kama nchi kampuni zake zipenyeze mirija nchini Tanzania.
Wamarekani wameona mwenzao Canada kapenyeza mlija wake hadi kwenye Figo na Maini ya nchi ya Tanzania wanamwonea Gele kweli kweli.
Nia na madhumuni yao ya kumsifia Kikwete ni kutaka alegee ili wapenyeze mirija yao hadi kwenye akili zetu na kutulamba kila kitu na uikiwezekana watufukuzie Mikumi na Lake Manyara tukaishi na hayawani ili kuonyesha vizazi vyao jamii ya Watanganyika waliosawa na Tumbiri.
Rais Kikwete ameshindwa kubaini kwamba Wazungu hawajali nani anafaidika na Utajiri wa Tanzania.Sifa wampazo Rais Kikwete ni kumlegeza ili waje na mashirika yao na kuingia mikataba duni na kufyonza kila rasili mali na pengine kugeuza nchi yetu kuwa Paradise yao na kutugeuza sisi Watwana katika nchi yetu wa kuwatumikia milele.
Ili mradi sasa kuna access ya kuutwaa utajiri wa Tanzania wazungu wanaamini kwamba kama watanzania watabakia masikini huku utajiri wao ukiwatajirisha wao ni makosa ya watanzania wenyewe kushindwa kutajirika na mali yao Rjea Movie au Documntary ya Sauper Darwin's Nightmare mwenye nguvu anashiba na kuishi munyonge munyongeni.
Pia kwao si jambo la kuwakosesha usingizi endapo watui weusi sisi dhahabu yetu itashindwa kujenga uchumi wetu,kwani watu weusi Duniani kote wana mawazo duni na wako nyuma kimaendeleo kwa kujali cha wengine na kudharau chao hat akama chao ni dhahabu ya kweli.
MH Kikwete amekuwa akirukia majibu yaliyotolewa kujibu hoja ya Dr Slaa bila kuisasambua hoja yenyewe.
Hii inadhihirisha kwamba anaiogopa hoja ya Dr Slaa na hayuko tayari kukabiriana na ukweli hasa ukweli huo utokeapo upande wa upinzani.
Kumpa misifa tele Warioba ni sawa na jamii ya Paka kujipanga kumsifia Panya muasi kwa ushujaa wake wa kuasi mapambano ya jamii ya Panya.
Kwa kuongezea tu MH rais kwa nini usimpe ulaji kabisa MH Warioba, kama ukurugenzi kwenye mashirika kadhaa ili tujue moja kwamba wote mlikuwa timu moja mkicheza mchezo wa kuigiza ulioandikwa na Gwiji la michezo ya kuigiza na Bingwa na msomi katika fani hiyo MH Edward Lowassa?!
Mwisho nakushukuru sana MH Rais kwa kuonyesha Udhaifu wako wazi wazi ili mwaka 2010 tukikuchagua tena tujue moja kwamba ni Sura yako nzuri tu na mvuto wako kwa dada na shangazi zetu ndivyo vyenye uwezo wa kukupa kura kuliko akili na uwezo wako wa kupembua majambo.
Pia ukweli kwamba Mafisadi wenzi wako hawakulala wakati wa msimu mzima wa kura kwa kugawa sehemu ya ufisadi wao na kuhakikisha unachaguliwa kulinda himaya yao ya kunywa damu za ndugu zao Watanzania bila huruma.
MAPAMBANO NDO KWANZA YANAANZA NA USHINDI NI LAZIMA