Kikwete on Channel 10

MKJJ Mahojiano haya Rais alifanya na nani? Na inaonekana alifanya Mahojiano haya Hotelini New York!.Maelezo yake ni mazuri lakini si kweli kwamba Tanngazo la Utalii kuhusu Tanzania lipo kwenye Kipindi cha Larry King.Tangazo hilo lipo kwenye prime Time,Lakini hakuna Tangazo hilo kwenye Larry King.

Nimefurahi kuona kwamba Rais amekiri kwamba kuna Utata/na Migongano mingi ktk Sekta ya Madini,Lakini kitendo chake cha kumsifu Mzee Warioba nakitilia mashaka,amejaribu bila kuwa wazi kutetea mikataba ya madini.Kuna ukweli hapa kwamba JK alijua mambo yaliyotokea kule Hotelini London,na kwa maneno yake haya naona hawezi kumwajibisha Karamagi!! kwa sababu anamtetea.
 
naona hajauona mkataba wa Buzwagi.. kinachopigiwa kelele siyo suala la asimilia 15 peke yake..
 
....anaongelea kujenga reli mpya kwenda rwanda...na kulink reli ya tazara na ya TRC..you know what inaonekana jk anajua mambo mengi na ana will tatizo sijui liko wapi mambo hayaendi,,,..yaani mambo mengi wenye mawazo mapya tunayoyataka anayajua,..tatizo mambo hayaendi...why..why..


anaongelea MILLENIUM CHALLANGE GOAL...aliongea na bush...
 
alikutanba na rais wa benki ya dunia ,rais wa nigeria na rais wa rwanda....

rais wa benki ya dunia anataka jk awe kwenye timu ya kuongea na G8..About AIDA 15...
 
ALIKUTANA NA rais wa baraza kuu la umoja wa mataifa na kumuaidi ushirikiano kwani ndio huyo rais anaaza kazi..na pia kuhusu utekelezaji wa malengo ya millenium..alikutana na katibu mkuu wa umoja wa mataifa ...waliongelea burundi,darfur na nia ya tanzania kupeleka majeshi.somalia...kuhusu kurudisha wakimbizi mpakani kwetu kurudishwa makwao....kulikua na hisia kuwa tanzania inawarudisha kwa nguvu..

amekutana na condy rice akamwambia hana maongezi marefu kwa kuwa anaona tanzania tunaendelea vema..pia condy alimuahidi msaada kwa jeshi letu linaloenda darfur........
 
madai kwamba tatizo ni wasaidizi inawezekana hayana ukweli, naona Rais anajua zaidi kuliko tunavyofikiri...
 
kapewa tuzo ..kuhusiana na mafanikio ya elimu hasa ..elimu ya msingi..enrolment..

hafla ya sullivan..ameahidi kutakuwa na mount kilimanjaro sullivan mount climbing....

alihudhuria kikao clinton initiative..kuhusu michango ya mataifa tajiri kwa michango ya kuzuia vifo vya kina mama kwenye uzazi...

anaamalizia kwa kusisitiza kuwa ziara yake imefanikiwa...
 
Huyu Jk mbona anakuwa kama chamelion? leo anasema tunarudia mikataba wapumbavu wake wanakimbia kusaini mikataba hiyo hiyo bado anawatetea nakutoa stupid smiles, alitwambia tutaje wanaohujumu uchumi na majambazi mpaka akatupa namba za simu, lakini leo hii anatugeuka nakutwambia eti tusiwe wapelelezi, mahakimu etc. kweli this is the worst Prezida ever to rule wadanganyika
 
Nimekuwa nasema hapa for a while now kuwa everything kinachoendelea TZ Kikwete anakijua na he is part of it.

Hakuna chochote kitakachofanyika na walokuwa wanasubiria maisha bora wajiandae tu na inflation ya double digits kwa vitu vyote muhimu!
 
mwafrika wakike inflation imepaa si mchezo ..ndio maana nashangaa kwa nini rais anatokota hivi...nafikiri watu aliowaweka pia ni tatizo..can you imagine bei ya cement hapo jijini..leo imefikia tzs 16,000..last week bei ilikuwa tzs 13,500...just a one week difference tofauti ya tzs 1,500.......
 
hilo changa la macho kama Dr Slaa naye anasababisha inflation then thas too much to think of. kama rais anadiriki kushika cheque feki sijui hao viongozi wenzake kazi wanayofanya
 
MH Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Jakaya Mrisho Kikwete.
Mbwa akikukenulia meno kamwe hatabasamu, Tabasamu la mbwa ni kuchezesha mkia.
MH Rais Umesoma Alama za Nyakati Vibaya sis akina MADELA WA- MADILU tunatakiwa kukupa vipande vyako.

Namkumbusha Rais Kikwete juu ya Siasa ya nje ya Marekani.
Namkumbusha Rais Kikwete juu ya hila za mabepari Duniani.

Serikali ya Marekani haina nchi rafiki hata siku moja, hiyo ndo sera yao ya nje.

Ni ajabu sana kwa mtawala wa wetu Tanzania Rais JM Kikwete kudhani wamarekani wako tayari kutusaidia sisi Watanzania.

Yeye Binafsi kama rais wa nchi si muoni akitembeza Sera ya kuikomboa nchi zaidi ya kukata stori Muflisi kama bado anahudhuria Disco la TAZARA na kupepesa macho huku akiwa na kigugumizi kama kaona msululu wa mademu wakali wa vimini wakikatiza kwa madaha.

Mtu hapa ajitokeze aniambie nchi moja tu iliyosaidiwa na marekani na kuendelea!

Wajapana walishaendelea mbali kabisa hata kabla ya Vita kuu ya 2 ya Dunia ndiyo maana ilichukua miaka 3 kwa nchi kubwa kama Mareakani kupigana na Japan na bado ilibidi watumie Bomu la Atomic ili kumaliza Kilanga heavy cha Wajapan.

Wajapana walikuwa wakitengeneza ndage kwa kutumia injini za Mitsubishi kipindi Kirefu kabla hata Dime moja ya Mmarekani haijatua Japan kama msaada.
Japan,Singapore,SouthKorea na sasa China hazijasaidiwa na Marekani kuendelea ila zinapambana kiuchumi na marekani kwa mikakati mikali ilo jengwa kiuthabiti ndani ya nchi zao na viongozi wao wenyewe.

Marekani inabidi itoe ushirikiano kwa nchi hizi kwa vile haina cha kufanya, Sasa hivi Marekani inajitahidi kukuza uchumi wa nchi za Amerika ya Kusini ili baadaye ku counter check maendeleo ya Asia, lakini inaonekana Timing yao ni mbaya kwani wako akina Chavez wanao wavurugia Dili zao nyingi.

India ndiye supplier mkubwa wa Maengineer na Madaktari nchini marekani, Marekani inabidi atoe ushirikiano kwa India kwa sababu hana watu wake mwenyewe wa kuwafundisha udaktari. Watu wengi ndani ya Marekani wanataka kusomea michezo na management ya biashara.Au kuwa macelebrity kwa kufanya jambo lolote lile hata liwe la aibu kiasi gani; kama Kupost Video yako ukijamiaana na mwenzi wako kama Paris Hilton, kupiga picha za uchi nenda YOU TUBE,kukaa vibaya na kuonyesha uchi kwa wapiga picha kana kwamba ni bahati mbaya kama livyofanya Britney.

Waswahili wanasema ukishikwa shikamana.

Marekani akikupa mtaji katika hali yeyote ile nia yake kubwa ni kukunyonya tu.

Ili kukwepa kunyonywa ni lazima akili yako kama Rais ifanye kazi mara mbili na uwe ni kiongozi wa Machale kweli kweli si kama Rais Kikwete amabye ziara yake anafuatana na Makuwadi washika tunguri na watoto wa rafiki zake akina Makamba kama wapambe uchwara.

Ukipewa mshiko na marekani, ni mipango yako ya ndani ndiyo itadetermine maendeleo yako siyo misaada upewayo.

Kama nchi, Tanzania tunepewa mabillioni ya $$$$$ kwa kipindi kirefu sana hata kabla; Kingunge hajawa Mkuu wa mkoa wa Tanga na Class mate wake Kleruu ajachapwa risasi na Mzee Mwamwindi,lakini bado tuko nyuma kwa kila kitu.
Sasa hivi, MH Rais Kikwete unatuonyesha wazi Kama kiongozi wa nchi na Serikali ya SISIEMU kwamba hata kwa mawazo na sera tuko nyuma kabisa.

Huwezi kuwa na Sera za kiilma kama za SISIEMU ukategemea kukwamua nchi na wananchi kiuchumi.
Sera zisizo weza kuhusianisha Umasikini wa wananchi na maamuzi ya NEKI ndani ya SISIEMU na ya viongozi wazembe kama Karamagi ndani ya serikali.
Sera Imla kama hii ya SISIEMU ni sera itakayo wafanya watu wachache ndani ya Tanzania kuendesha nchi kama Estate ya baba yao na hivyo kutoa maamuzi kwa namna Roho na utashi wao upendavyo na si kwa kuzingatia Masklahi ya Wananchi wa Tanzania na Taifa kwa ujumla.

Misifa wanayommwagia Kikwete inatokana na ukweli kwamba mauzo yetu ya dhahabu huko ughaibubni yameongekezeka 100 folds sasa kila Bepari kupitia kila chombo anajitahidi kumpaka Rais wetu mafuta kwa Mgongo wa chupa na kumvisha kilemba cha manyasi ili naye kama nchi kampuni zake zipenyeze mirija nchini Tanzania.

Wamarekani wameona mwenzao Canada kapenyeza mlija wake hadi kwenye Figo na Maini ya nchi ya Tanzania wanamwonea Gele kweli kweli.
Nia na madhumuni yao ya kumsifia Kikwete ni kutaka alegee ili wapenyeze mirija yao hadi kwenye akili zetu na kutulamba kila kitu na uikiwezekana watufukuzie Mikumi na Lake Manyara tukaishi na hayawani ili kuonyesha vizazi vyao jamii ya Watanganyika waliosawa na Tumbiri.

Rais Kikwete ameshindwa kubaini kwamba Wazungu hawajali nani anafaidika na Utajiri wa Tanzania.Sifa wampazo Rais Kikwete ni kumlegeza ili waje na mashirika yao na kuingia mikataba duni na kufyonza kila rasili mali na pengine kugeuza nchi yetu kuwa Paradise yao na kutugeuza sisi Watwana katika nchi yetu wa kuwatumikia milele.

Ili mradi sasa kuna access ya kuutwaa utajiri wa Tanzania wazungu wanaamini kwamba kama watanzania watabakia masikini huku utajiri wao ukiwatajirisha wao ni makosa ya watanzania wenyewe kushindwa kutajirika na mali yao Rjea Movie au Documntary ya Sauper Darwin's Nightmare mwenye nguvu anashiba na kuishi munyonge munyongeni.
Pia kwao si jambo la kuwakosesha usingizi endapo watui weusi sisi dhahabu yetu itashindwa kujenga uchumi wetu,kwani watu weusi Duniani kote wana mawazo duni na wako nyuma kimaendeleo kwa kujali cha wengine na kudharau chao hat akama chao ni dhahabu ya kweli.

MH Kikwete amekuwa akirukia majibu yaliyotolewa kujibu hoja ya Dr Slaa bila kuisasambua hoja yenyewe.
Hii inadhihirisha kwamba anaiogopa hoja ya Dr Slaa na hayuko tayari kukabiriana na ukweli hasa ukweli huo utokeapo upande wa upinzani.
Kumpa misifa tele Warioba ni sawa na jamii ya Paka kujipanga kumsifia Panya muasi kwa ushujaa wake wa kuasi mapambano ya jamii ya Panya.

Kwa kuongezea tu MH rais kwa nini usimpe ulaji kabisa MH Warioba, kama ukurugenzi kwenye mashirika kadhaa ili tujue moja kwamba wote mlikuwa timu moja mkicheza mchezo wa kuigiza ulioandikwa na Gwiji la michezo ya kuigiza na Bingwa na msomi katika fani hiyo MH Edward Lowassa?!

Mwisho nakushukuru sana MH Rais kwa kuonyesha Udhaifu wako wazi wazi ili mwaka 2010 tukikuchagua tena tujue moja kwamba ni Sura yako nzuri tu na mvuto wako kwa dada na shangazi zetu ndivyo vyenye uwezo wa kukupa kura kuliko akili na uwezo wako wa kupembua majambo.
Pia ukweli kwamba Mafisadi wenzi wako hawakulala wakati wa msimu mzima wa kura kwa kugawa sehemu ya ufisadi wao na kuhakikisha unachaguliwa kulinda himaya yao ya kunywa damu za ndugu zao Watanzania bila huruma.

MAPAMBANO NDO KWANZA YANAANZA NA USHINDI NI LAZIMA
 
Mimi nadhani kwamba Mungwana anapenda kusema vitu ambavyo anafikiri vinasikika vizuri (they sound good), lakini he does not mean it.
 
MADELA WA- MADILU,
Mkuu naomba Mungu na Ramadhan hii huyu JK apate kusoma maelezo yako, pia salamu hizi ziwafikie Wadanganyika wengine wengi wasiolewa siasa za Marekani. Wapo wengi sana wanaofikiria kwamba Marekani wana huruma sana na wanaweza kuitajirisha nchi ikiwa nao karibu... mimi huita kufanya Umalaya!

Siku zote Marekani husaidia nchi kulinda maslahi yao, maslahi ambayo huwanufaisha wao na sio kinyume. Leo hii kama Tanzania ikiamua kushirikiana na China ama nchi za Nordic kiuchumi badala ya Marekani urafiki wetu utakufa!..Marekani wapo tayari kutetea shetan ikiwa maslahi yao yanalindwa ( Pakistan). Tazama basi wakati JK akiongoza ukuhadi (pimping) kati yetu na UK na Marekani, hao Wachina na nchi za Nordic bado ni marafiki zetu na wanatusaidia kwa kiasi kikubwa sana.
 
Back
Top Bottom