Kimilidzo
JF-Expert Member
- Jan 3, 2011
- 1,346
- 628
Zitto naye vp hagombei kweli?
Atagombea Chama gani? CHADEMA amefukuzwa huku ACT imekufa kabla hata haijaanza kutambaa
Zitto naye vp hagombei kweli?
nitajie mmoja mkuu
Bahati nzuri ni kwamba ndani ya CDM kuna mtu Spesho wa kugombea uraisi na vijana wa CDM kamwe hamruhusiwi tofauti na mawazo ya wateule yaani hata wewe katibu wa Bavicha hutaki vijana wenzako waukwae uraisi?? wewe unawakirisha vijana wa aina gani? ina maana kina Mnyika, Lissu, Lema, Msigwa hawafai kuwa maraisi kweli?? hadi mteule mmoja tu?
1. Awe kijana
2. Awe ni rais atakayeliunganisha taifa
3. Awe anaijua historia ya nchi yake vizuri kwa maana ya ilikotoka, iliko na inakokwenda
4. Awe na uwezo wa kufanya uamuzi mgumu kwa ajili nchi yake.
5.Awe tayari kuondoa matabaka yaliyoko nchini(ukabila, udini n.k
Akifafanua sifa ya ujana ZITTO alitolea mfano viongozi wa Tanzania waliopewa nafasi za uongozi wakiwa vijana na kufanya vizuri kuwa ni pamoja na JULIUS NYERERE, Jaji Mstaafu Joseph Waryoba na Salim Ahamed Salim.
ZITTO KABWE anaungana na Jaji Joseph Waryoba na Salim Ahamed Salim Katika mtazamo wa Rais ajae kuwa Kijana.
source: jambo leo
Kama wewe ni chadema unawafahamu, kama wewe ni ccm niambie tuanze majina na comparizon kiuwezo kwa kila chama.
ccm
.1. SAMWEL SITA
2. DR. MAKYEMBE
3. STEVEN WASIRA
4.MAGUFULI
5. LOWASA
6. MEMBE
7.JANUAR
8. MALIZIA.........
Ikumbukwe kuwa Zitto ni representative ya vijana WASILITI,WAOGA na WABINAFSI!Aidha kijana mwingine anayepigiwa chapua J.Makamba alikuwa akitoza dola 500 mpaka 1500 kama kiingilio cha kuonana na rais IKULU.Vilevile ana kashfa ya kuiba paper pale Galanos Sec(Galax).Nawaonjesha tu wale fata upepo.sioni kijana mwenye credibility.Chama changu nakitakia malezi mema kwa J.Mnyika na Tundu Lisu hawa ni wazalendo
Sijui unaongelea ubora upi! Reagan amechukua uongozi wa taifa lake akiwa na miaka 69, lakini ni mmoja wa marais wa nchi hiyo walioheshimiwa sana. Na huko majeshini vipi, kwa nini tusiwape ujenerali vijana? Maana naona wote ni wazee.Edward Sokoine ...pia alipata uwaziri Mkuu akiwa 38.
All in all ujana..sio sifa pekee ...ila Rais asizidi miaka 60 .....akiwa angalau na miaka 45 hadi 50 no bora Zaidi
1. Awe kijana
2. Awe ni rais atakayeliunganisha taifa
3. Awe anaijua historia ya nchi yake vizuri kwa maana ya ilikotoka, iliko na inakokwenda
4. Awe na uwezo wa kufanya uamuzi mgumu kwa ajili nchi yake.
5.Awe tayari kuondoa matabaka yaliyoko nchini(ukabila, udini n.k
Akifafanua sifa ya ujana ZITTO alitolea mfano viongozi wa Tanzania waliopewa nafasi za uongozi wakiwa vijana na kufanya vizuri kuwa ni pamoja na JULIUS NYERERE, Jaji Mstaafu Joseph Waryoba na Salim Ahamed Salim.
ZITTO KABWE anaungana na Jaji Joseph Waryoba na Salim Ahamed Salim Katika mtazamo wa Rais ajae kuwa Kijana.
source: jambo leo
Uwe mzee uwe kijana kwangu mimi hakuna tija.
Kama huna uadilifu usiotiwa mashaka, huna rekodi ya uwajibikaji uliotukuka, huna dira sahihi ya kuliongoza taifa hili na huna uzalendo usio na mawaa kwa taifa letu, hustaili kuwa kiongozi wa tifa hili kwa vyovyote vile iwavyo uwe mzee uwe kijana.
Kuongoza vijana sio turufu ya kutetea ujinga.
Makene ni kweli kwamba kila alisemalo ZITTO kwenu ni usaliti, Ubaguzi na kuwa na kitu nyuma ya pazia, lakini haya WARYOBA , SALIM AHAMED SALIM nao ni wasaliti? Lakini swali la msingi sifa ya kijana ikiwa na mashiko mnachohofu nini? CHADEMA hamna vijana wa kushndana na vijana wa vyama vingine?
Kampeni hii ya Sifa ya ujana, mbali ya kwamba inabeba dhana ya ubaguzi lakini pia inabeba dhana ya uoga na hofu!
Hiyo ni mbali na mkakati mwingine ulioko nyuma ya mapazia.
Wanaoipigia chapuo kama ndiyo sifa kubwa ya wao kufanikisha tamaa, uchu wa kuwa blockers wa kisiasa, (naamini akina Warioba na Salim hawamo katika hila hizo) wanasumbuliwa na mambo hayo!
Naona hiki kikampeni kimefufuliwa tena. Kilikufa kifo cha mende wakati fulani hasa baada ya Mzee Butiku kuwalipua pale Ukumbi wa Nkrumah, UDSM!
Ilikuwa baada ya wanazuoni makini na mahiri vijana kama Sabatho Nyamsenda, Bashiru Ally et all kuandika kwa details na kuonesha ubaguzi huo wa kukimbilia ujana eti sifa ya kupambana na watu wengine wenye umri mkubwa wenye sifa za uongozi lakini wanawatia kiwewe vijana.
Ilikuwa ni baada ya wananchi kuendelea kuonesha imani kubwa na watu wengine badala ya watu wanaojigamba kwa sifa ya ujana pekee huku wakiwa wameharibikiwa kweli kweli kwenye sifa za msingi za uongozi.
Nao wanajua kuwa jambo pekee wanaweza kujivunia nalo ni umri, mbali ya hapo ni questionable tu!
Waambieni wafanye Kazi, wafuate ushauri wa Butiku. Ujanja ujanja huu hautasaidia.
Hakuna mahali panasema Mwalimu Nyerere, Warioba na Salim walifanya vizuri kwa sababu walikuwa vijana unless mnataka kusema walipoongezeka umri waliboronga katika nafasi zao! Jambo ambalo si kweli kwa sababu hao hao tumewaona wakifanya mambo makubwa zaidi ya uongozi uliokomaa wakiwa umri mkubwa wa kutosha kuitwa wazee!
1. Awe kijana
2. Awe ni rais atakayeliunganisha taifa
3. Awe anaijua historia ya nchi yake vizuri kwa maana ya ilikotoka, iliko na inakokwenda
4. Awe na uwezo wa kufanya uamuzi mgumu kwa ajili nchi yake.
5.Awe tayari kuondoa matabaka yaliyoko nchini(ukabila, udini n.k
Akifafanua sifa ya ujana ZITTO alitolea mfano viongozi wa Tanzania waliopewa nafasi za uongozi wakiwa vijana na kufanya vizuri kuwa ni pamoja na JULIUS NYERERE, Jaji Mstaafu Joseph Waryoba na Salim Ahamed Salim.
ZITTO KABWE anaungana na Jaji Joseph Waryoba na Salim Ahamed Salim Katika mtazamo wa Rais ajae kuwa Kijana.
source: jambo leo
Hayo ni Mawazo yao hayawezi kuwa Sheria, Zitto Kabwe hawezi kuwa Rais kwakuwa hajatimiza miaka 40 mwakani, January Makamba haamininiki wala hachaguliki.
Chapuo liko kwa wakongwe, Stephen Wassira,Samwel Sitta na Edward Lowassa.
Kijana John Pombe Magufuli for Presidency 2015