mafutamingi
JF-Expert Member
- Feb 14, 2011
- 2,772
- 2,171
Ni kweli kabisa hizi semina hazina tija. Jana saa 3 usiku TBC walirusha ufunguzi wa semina hiyo na nikashangaa kuona kwamba mambo ambayo viongozi hao wanafundwa niyale ambayo kila mtu anayeteuliwa kuwa Waziri au Katibu Mkuu anatakiwa awe anayafahamu. Vinginevyo hakuna haja ya mtu asiyefahamu mabo ya kawaida kuteuliwa kushika wadhifa huo. Kwa mfano kweli Waziri au Katibu Mkuu anahitaji kufanyiwa semina ili aelewe hali ya uchumi wa dunia au athari ya madawa ya kulevya? Hii ni kupoteza fedha zetu bure.