Kikwete na semina elekezi kwa Mawaziri - Dodoma 2011

CCM lazima iwapige tena CDM 2015,natabiri CDM watapata asilimia 27 na wabunge 15!

tumekataza ulopokaji,sasa mwenzetu mbona akili yako ngumu kuelewa,jipange upya toa hoja zenye mashiko.we need facts,valid&vivid examples with clear,accurate,relevant,logic and precise information.
 
Lini hizi semina elekezi zitalipa?


e6faaa817268d28347d2eecce1d2e5dc

Na editor - Imechapwa 11 May 2011

Maoni ya Mhariri



RAIS Jakaya Kikwete juzi Jumatatu alizindua semina elekezi iliyoshirikisha mawaziri, naibu mawaziri, makatibu wakuu na manaibu wao, viongozi wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama kupata maelekezo juu ya utendaji kazi serikalini.

Maudhui ya semina hiyo iliyofanyika mjini Dodoma, mbali na kukumbusha majukumu yao kama viongozi wakuu wa serikali, pia kujifunza utendaji wa vyombo vingine vya serikali.

Mada za semina hiyo ni umuhimu wa kuisemea serikali, kuimarisha mapambano dhidi ya rushwa, dawa za kulevya na uhalifu mwingine.
Aidha, amewataka wateule wake katika ngazi zote za uongozi kufanya kazi kwa uadilifu mkubwa; wawe watu wa kupigiwa mfano, wasinyooshewe kidole kwa ulevi, uchelewaji kazini na kuwahi kuondoka, kwa uzembe, wizi, kutumia ofisi kujinufaisha, kwa uzinzi na ubabe.

Rais amefanya jambo muhimu sana kukumbusha watendaji kuzingatia uwajibikaji kwa wananchi kwani baadhi ya mawaziri walikuwa mzigo kipindi chake cha kwanza.

Mwaka 2006, Rais aliandaa semina elekezi kama hii mjini Arusha ili kuchochea ufanisi na kukuza uwajibikaji kazini. Lakini haikuchukua muda, baadhi yao walianza kulaumiwa kutowajibika ipasavyo.

Mathalani, baadhi ya mawaziri waliingia kwenye kashfa ya ufisadi kwa kuidhinisha zabuni ya kampuni feki ya kufua umeme ya Richmond, Juni 23, 2006.

Hiyo ikamgharimu waziri mkuu na mawaziri wawili waliolazimika kujiuzulu na hatimaye kusababisha serikali kuvunjika.
Waziri mwingine alijiuzulu kwa shinikizo baada ya kuhusishwa na ufisadi katika ununuzi wa rada ya taifa. Alituhumiwa kupokea mlungula hadi kuchunguzwa na shirika la ukachero la Uingereza, ingawa aliita fedha alizokutwa nazo kama “vijisenti.”

Mkuu mmoja wa wilaya akajisikia raha kuwacharaza viboko walimu eti kwa vile shule zao zimepata matokeo mabaya katika mtihani wa darasa la saba.

Ripoti ya kila mwaka ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) huonyesha wizi, ubadhirifu wa fedha za serikali katika idara za serikali na halmashauri. Ukiacha wakurugenzi waliosimamishwa katika wilaya ya Bagamoyo, wengine wanaendelea na kazi licha ya kuitia hasara serikali.

Ni dhahiri semina hizi hazijaleta matunda kwa mawaziri na watendaji wengi serikalini kwani matendo maovu ikiwemo uzembe na ufisadi yanaongezeka. Lini zitalipa?
Tunaamini sasa kilichobaki ni kwa rais mwenyewe pamoja na waziri mkuu kuonyesha mfano wa utendaji bora, na pale anapotokea kiongozi ameshindwa kuwajibika, ni kumtimua pasina kusita.
 
zinalipa kwa sababu wengi wa mawaziri hawajafanya kazi serikalini.na serikali yeyote inaoutaratibu wa kuendesha mambo yake.
 
zinalipa kwa sababu wengi wa mawaziri hawajafanya kazi serikalini.na serikali yeyote inaoutaratibu wa kuendesha mambo yake.

kwa hiyo unataka kutuambia walikua wanafundishwa jinsi ya kuendesha wizara zao? kama ni hivyo ni nani alikua anawafundisha?

kwani kama mwalimu ni yule yule na mtaala ni ule ule kila mwaka nadhani tunahitaji kuuangalia upya huo mtaala na waalimu pia..

semina zinafanyika kila mwaka na madudu ni yale yale... kwangu hizi semina ni upuuzi na ufujaji wa hela za walipa kodi
 
hazilipi na upuuzi mtupu
ivi anapotembelea wizara uwa anafanya nini?
kwanza, ni kutumia kodi zetu kwa ufujaji huu usio na tija
pili,wanaenda kuuza sura tu pale/kutalii basi
tatu,mbona uzembe ndo uko mwingi sana?semina ya kwanza ilifanya nini!
nne,waache uhuni tunakata matendo/utekelezaji na sio vikao vya ajabu
tano,nchi iko gizani na shilingi inazidi kushuka

i hate this semina toka ndani ya roho yangu.
 
Tutafakari pia kama semina lukuki nyinginezo zinazofanyika kila kukicha kwa majina tofautitofauti zinalipa then tuangalie na hizi za watendaji wakuu wa serikali kama zinalipa pia.
 
hazilipi na upuuzi mtupu
ivi anapotembelea wizara uwa anafanya nini?
kwanza, ni kutumia kodi zetu kwa ufujaji huu usio na tija
pili,wanaenda kuuza sura tu pale/kutalii basi
tatu,mbona uzembe ndo uko mwingi sana?semina ya kwanza ilifanya nini!
nne,waache uhuni tunakata matendo/utekelezaji na sio vikao vya ajabu
tano,nchi iko gizani na shilingi inazidi kushuka

i hate this semina toka ndani ya roho yangu.

Trust me Aza, you are not alone. Ati semina elekezi............wanaelekezwa nini hawa wasichokijua kuhusu kazi zao? Yaani mi nasikia kichefuchefu na hii sirikali yenu..........
 
Zinalipa sana yaani hapo Perdiem za kutosha,
watu wamepata nafasi ya kusupply refreshments na msosi. mlo mmoja kwa mtu mmoja ni 35,000
mkuu alipokuja kufungua hiyo semina amelamba perdiem na hela ya kufungulia semina
Acha bana imelipa sana hii semina
 
a: hivi uliposema "Semina ya Ngurdoto hatukufanya vizuri sana" ulimaanisha nini mkuu?

b: naomba unifahamishe kati ya semina ya ngurdoto na hii ya dodoma, ni ipi ilitafuna kodi zetu na **** za watu sana?

unajua bwana kikwete inabidi uwe unafikiria kidogo kabla ya kutoa kauli zako zenye kuacha maswali. hivi unajua ni Watanzania wangapi wanakusonya na kujiapiza unapotoa matamshi na kauli zenye utata? ni heri mara mia uwe unasoma uliyoandikiwa kwenye hotuba zako kuliko kujifanya unafafanua mambo kwa mdomo, maana inavyoelekea wewe ni mropokaji na huwezi kutoa hotuba kwa kushusha pointi kutoka kichwani kama wenzako kina Sarkozi, Obama, Bush na wengineo maarufu.

Iga mtindo wa mtangulizi wako BWM ambaye alikuwa anaanza hotuba kwa kusoma na namaliza kwa kusoma kila kitu mpaka "Mungu Ibariki Afrika, Mungu Ibariki Tanzania".

ni ushauri tu mkuu.
 
Huwa anahudhuria humu jamvini?
Je hao ambao wanachunguliaga humu jamvini kwa niaba yake wanaweza kumfikishia ujumbe huo?
Kama wakimfikishia atautekeleza?
 
Kutoka Nipashe:

----------------
Aliwataka vingozi na watendaji wakuu hao, kupigana na kuonekana kama wanapigana na rushwa ili kero hiyo waimalize au kuipunguza.

Alisema wananchi wangependa kuona baada ya semina hiyo kasi na ufanisi wa utekelezaji wa majukumu yao inaongezeka.

" Kwa ajili hiyo tuhakikishe kuwa mipango inapangwa vizuri na kunakuwa na umakini mkubwa katika kutekeleza miradi ya kutekeleza mipango mbalimbali," alisema.

Aidha, Kikwete alisema wananchi pia wangependa kuona wanazingatia misingi ya utawala bora, kuheshimu katiba, utawala wa sheria na nidhamu ya kazi na uwajibikaji.

Rais Kikwete aliwataka viongozi hao wanaporejea ofisini kwako kuchemka zaidi katika kutimiza wajibu wao.

HATUNA MUDA, CHEMKENI
“Lazima tukumbuke tumemaliza miezi yetu saba kati ya miezi yetu 60, muda uliobaki miezi hiyo 53 unaweza kuonekana ni mrefu lakini ni mfupi sana nirudie tena na kusisitiza tokeni, tembeeni msikae ofisini,”alisema.

Hata hivyo, alisema haimaanishi mambo ya ofisini hayana umuhimu, lakini wajipangie muda wa kutoka na kwenda katika halmashauri, vijijini taasisi zao ili wafanye kazi ya kusukuma mbele gurudumu la maendeleo.

Alisema kila tatizo linalowasumbua wananchi au linalozikabili taasisi zao lipo katika mamlaka yao katika kulipatia ufumbuzi.

"Msipokwenda nyinyi na kuyatafutia majawabu nani afanye kazi hiyo, wananchi watabaki wananung’unika kama vile serikali haipo, viongozi hawapo, kumbe mna majawabu ya matatizo yao,"alisema.

TOENI HABARI
Aliwataka pia kutoa taarifa ya shughuli wanazozifanya, shughuli za wizara na taasisi zao kupitia vyombo vya habari ili wananchi wajue kinachotendeka.

Alisema kwa kufanya hivyo sio tu kwamba watakuwa wametimiza wajibu wao, bali pia watakijengea Chama Cha Mapinduzi (CCM), uhalali wa kuendelea kungoza katika kipindi kijacho.

"Mwaka 2015 mimi sipo tena mimi nataka mfanye vizuri ili chama chetu hata tukisema mmoja wetu abebe bendera yetu tuwe na uhakika anashinda, lakini nguvu yetu iko kwa kufanikisha haya," alisisitiza.

DAWA ZA KULEVYA
Kuhusu suala la dawa za kulevya nchini, Kikwete, alisema aliwaona baadhi ya washiriki katika semina hiyo wakiogopa wakati muwasilisha mada alipoonyesha picha za vijana wakijichoma sindano za dawa za kulevya katika maeneo mbalimbali.

Bila kufafanua, alisema mahali pengine aliposhiriki aliona wanavyoonyesha picha za Watanzania wanavyouana katika biashara ya dawa za kulevya.

Alisema serikali inajiandaa kuanzisha kikosi maalum cha kupambana na dawa za kulevya ambacho wakilala wakiamka kazi yao itakuwa ni kupambana na dawa za kulevya ili kuongeza nguvu ya kuzitokomeza.

Alisema kikosi hicho kitachanganya maafisa waliopo na wengine kutoka polisi na kuunda umoja mkubwa ili kupambana na tatizo hilo kwa ababu linazidi kukua.

DODOMA SI NGURDOTO
Rais, alisema semina hiyo iliyomalizika jana ilikuwa na ufanisi mkubwa kuliko ile iliyofanyika Ngurdoto mkoani Arusha mwaka 2006, kwa sababu wakati huo hawakuwa na maarifa kama waliyokuwa nayo wakati huu.

Alisema katika semina hiyo washiriki walipata nafasi ya kujigawa katika makundi na kujadili na hivyo kutoa mapendekezo ya kina na yenye ubora zaidi.

Kikwete aliwataka kutumia elimu waliyoipata katika kutekeleza na majukumu yao.

MAAZIMIO 14 YAFIKIWA
Naye Katibu Mkuu Kiongozi, Philimon Luhanjo, alisema waliazimia mazimio 14 ambayo viongozi hao wanatakiwa kuyatekeleza na kuyawasilisha katika ofisi yake kila baada ya miezi mitatu.

Miongoni mwa maazimio hayo ni serikali imeamua kuchukua hatua madhubuti za kuongeza mapato ya ndani na kudhibiti matumizi ili ifikapo mwaka 2015 kiwango cha utegemezi wa misaada ya wadau wa maendeleo kwenye bajeti kuu ya serikali isizidi asilimia 10.

Aidha, alisema wameamua kuchukua hatua madhubuti za kuhakikisha kuwa usimamazi, nidhamu, weledi, uadilifu na uwajibikaji na mapambano dhidi ya rushwa vinaimarishwa katika ngazi zote za utendaji kazi serikalini ili kuongeza fanisi katika utoaji huduma kwa umma na kuvutia wawekezaji.

Pia alisema Taasisi ya Uongozi inatengeneza programu za mafunzo na uelekezi kwa viongozi ili wawe chachu ya maendeleo endelevu.

"Ili kutimiza azma hiyo kuanzia sasa viongozi wote hususan vijana watalazimika kupata mafunzo maalum kama itakavyopangwa na baada ya hapo kupimwa utendaji
 
sasa kama wewe jk ndo umeshindwa nani ataweza? Mawaziri wako woote wamevurunda lakini bado unaongea tuuu ,tumechoka kusikiriza maongezi yako tunaomba sasa kaa kimya tu haina maana.....kuongea bila action........kikwete ni bora usimamie watu kwa kuwaangalia tu kuliko kubwabwaja yaaani wanakudharau hao unao waongoza ndo maana hawatekelezi mambo mengi uliyo waagiza...........
 
baba yangu alikuwa akikasirika alipenda kusema HOVYO! na mimi sasa nimekasirika vibaya mno kuona rais asiye na meno na serikali ya wasanii naiita serikali ya HOVYO KABISAAAA!!
 
Mwenzenu sasa hivi anawaza kuanza maisha mapya baada ya kumaliza kipindi chake, hakuna atakachofanya sasa hivi!
Wanaotegemea kutekelezewa zile ahadi za Trilioni 900 imekula kwao!
Sisi tunachongoja sasa hivi ni kukabidhi nchi kwa Dr Slaa...basi.
 
hadi leo anavunja katiba kwa kuendelea kuwatumikisha wakuu wa wilaya na mikoa term mpya kabla ya kula kiapo cha utii na kuilinda katiba....rais akishaapishwa ni lazima atangaze mawaziri,wakuu wa mikoa na wilaya na watakula kiapo..kwa kifupi kwa saasa wakuu wa mikoa na wilaya wanafanya kazi kinyume cha katiba......na mwanasheria mkuu wa serikali yupo..anaangalia!
Unamzungumzia Welema Yule Aliyekuwa Mwanasheria!!! na asiyejijua yupo kwenye cheo hicho cha ukuu, Alishaacha Sheria ni Mwanasiasa Sikuhizi... Nchi Inajiongoza Yenyewe hii... Tumeachwa wakiwa na Baba wa Taifa
 
Back
Top Bottom