Kikwete: Lowassa ndiye mhusika wa Richmond

Status
Not open for further replies.
Ampeleke mahakamani ili awasukumie kesi makatibu aliowalazimisha kuunda kamati kisa? Ndiyo maana alipigwa chini. Huyo mtu ni mjanja mno alitumia kiti chake ku shift burden kwa makatibu wakuu hivyo si ajabu mahakamani akachomoka na akaendelea kuaminiwa kumbe ni town boy tu.

Hivi kwa nini yeye naye asimpeleke JK mahakamani au hao makatibu wake? Kwa nini hadi yeye tu ndiyo apelekwe huko mahakamani? Mahakama ya ccm ni kumvua tu uboss

Je, Lowasa ndio amebeba uozo wote wa CCM?
 
Amechelewa tulimsistiza sana atoe utetezi wake mapema mbele ya mahakama ya umma akagoma. Too late. Hakuna trafiki anaesimamisha gari katikati ya pori.
 
Yeye kasema hivo na hajasema hivo ili umpigie kura Makifuli, ilikuwa ni taarifa kwa wanachama wa ccm na ambao walikuwa hawajui-kwa wewe unayesema kuwa kachelewa pia ni mtazamo wako na uelewa wako.

Kachelewa ndio ukweli. Rais badala ya kuchukua hatua miaka nane iliyopita, anatoa porojo kwenye mkutano wa kampeni???
 
Dunia nzima inajua Lowasa ni FISADI wewe kwa Mahaba huko huwezi kubadilisha hiyo.

Tambua kwamba FISADI hawezi kua Rais wa nchi hii Watanzania ni Werevu hawawezi kucheza KAMARI ya SIASA kama alivyocheza Mbowe.

Mimi sio ukawa mimi ni ccm kindakindaki lakini penye ukweli lazima tuseme
 
mbona waliendelea kulipa hiyo kampuni kama walijua hivyo?
na kwanini hakupelekwa segerea Mara moja???

unafki
 
Dunia nzima inajua Lowasa ni FISADI wewe kwa Mahaba huko huwezi kubadilisha hiyo.

Tambua kwamba FISADI hawezi kua Rais wa nchi hii Watanzania ni Werevu hawawezi kucheza KAMARI ya SIASA kama alivyocheza Mbowe.

It was mis calculations tungepata taarifa hizo mapema zingesaidia kidogo.Ila ni vigumu kuhalalisha Richmond kuwa ni wizi bila kusema escrow ni nani.Jana ningefurahi sana kama mkuu wa nchi angetuambia escrow ni ya nani.maana wizi wa escrow ni mkubwa kuliko wa Richmond.
 
Ndo yale yalee..mwananchi analalamika,viongozi wanalalamika, hadi rais naye analalamika. Nani sasa achukue hatua?? Leo wananchi wanachukua hatua
 
Raisi akiri kulea ufisadi.
Si alisema kuwa hamjui mmiliki wa Dowans ambaye ni mtoto wa Richmond!? Wakati akisema hivyo hazina/tanesco ikiwa chini ya mamlaka yake kwa 100% iliendelea kuilipa kampuni 'isiyojulikana'.
Maneno mengine inabidi kuyafikiria sana kabla ya kuyaweka public maana mbali na wananchi pia kuna kizazi chako kinaweza kuja kujiuliza uwezo wa mababu!

 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom