Jakaya Kikwete na Mkewe wawasili Msibani kwa Lowassa

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
119,326
222,444
Kikwete_Lowassa_Salma.jpg
Taarifa ikufikie popote ulipo kwamba Mh Jakaya Kikwete, leo Jumatatu ni miongoni mwa wadau waliofika nyumbani kwa Lowassa kuhani Msiba na kushiriki Maombolezo , ameambatana na Mkewe Mama Salma Kikwete.

Itakumbukwa kwamba Lowassa ndiye aliyekuwa Waziri Mkuu wa Kwanza kuteuliwa kwenye awamu ya Kikwete na baadaye kujiuzulu kwa kilichoitwa Kashfa ya RICHMOND.

Hapo awali 1995 wawili hao waliwahi kuunda Kolabo kabambe iliyopachikwa jina la "BOYS II MEN"

Kikwete_Lowassa.png
 
Kila kona taifa limeoza kwa ufisadi, leo hakuna uhakika wa umeme, shirika linapata hasara kwa kulipa madeni kutokana na mikataba ya hovyo ukiwemo wa RICHMOND sijui DOWANS ambao ulipelekea Lowassa kujiuzulu kwa kashfa ya ufisadi.

Kila mahali kunanuka ufisadi, watoto vyuo wanaishi maisha magumu kisa watu wanatafuta pesa, watu wanakufa hospitalin kisa huduma mbovu ama hakuna kabisa. Vijana hawana mitaji ili kuinua maisha yao.

Yote hii ni kutokana na ufisadi, na wote wanaoukumbatia hawapaswi kupewa heshima ya kuzikwa kishujaa na taifa wakati wao ndio wameliangamiza taifa, familia zao zinaishi vizuri, utajiri wa taifa wamerithisha familia zao na koo zao.
 
Hakuna mzalendo yoyote wa hili taifa atakayeumizwa na misiba ya watu ambao wameangamiza uchumi wa taifa na kujenga uchumi wa familia.

Marehemu, JK, Ruge n.k hawa wote ni wezi na sihani kama wakifa wanapaswa eti kupewa heshima ambayo wanapewa, bendera ya taifa inapepea nusu mlingoti.

sasa hivi tunauza bandari, kule kwao zanzibar hajauza bandari yoyote ile, naye akifa tutanifanya kuumizwaaaa na kumpa heshima yake.

Hovyo kabisa.
 
hivi unawezaje kwenda kwenya msiba huku unacheka? binafsi naona tanzagiza tuna exaggerate sana misiba ilipaswa iwe kwa watu walioguswa tu kama wewe haukuhusu na haujaguswa usiende, siyo lazima.

Kikristo msiba ni sehemu ya huzuni na ndiyo maana hata nyimbo za maziko zinasikitisha sana …
 
Kila kona taifa limeoza kwa ufisadi, leo hakuna uhakika wa umeme, shirika linapata hasara kwa kulipa madeni kutokana na mikataba ya hovyo ukiwemo wa RICHMOND sijui DOWANS ambao ulipelekea Lowassa kujiuzulu kwa kashfa ya ufisadi.

Kila mahali kunanuka ufisadi, watoto vyuo wanaishi maisha magumu kisa watu wanatafuta pesa, watu wanakufa hospitalin kisa huduma mbovu ama hakuna kabisa. Vijana hawana mitaji ili kuinua maisha yao.

Yote hii ni kutokana na ufisadi, na wote wanaoukumbatia hawapaswi kupewa heshima ya kuzikwa kishujaa na taifa wakati wao ndio wameliangamiza taifa, familia zao zinaishi vizuri, utajiri wa taifa wamerithisha familia zao na koo zao.
Ww inaonekana haujui chochote kuhusu ilo Santa. Lowassa hakuhusika na huo ufisadi. Huyo mzee wa MSOGA ndio muharibifu. Sio Lowassa.
 
Taarifa ikufikie popote ulipo kwamba Mh Jakaya Kikwete, leo Jumatatu ni miongoni mwa wadau waliofika nyumbani kwa Lowassa kuhani Msiba na kushiriki Maombolezo , ameambatana na Mkewe Mama Salma Kikwete.

Itakumbukwa kwamba Lowassa ndiye aliyekuwa Waziri Mkuu wa Kwanza kuteuliwa kwenye awamu ya Kikwete na baadaye kujiuzulu kwa kilichoitwa Kashfa ya RICHMOND.

Hapo awali 1995 wawili hao waliwahi kuunda Kolabo kabambe iliyopachikwa jina la "BOYS II MEN"

REST IN PEACE MZEE LOWASA.
FB_IMG_1707735205387.jpg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Inawezekana si kinywa changu ila vidole vyangu. Najaribu kuangalia wingi wa comment hapa zinaonyesha zimebebwa na yaliyopita si ndwele!
 
Lowassa alianza kuugua na kunyong'onyea kidogokidogo baada ya maumivu ya moyo yaliyosababishwa na kusalitiwa na rafiki yake wa karibu mno aliyetoka naye mbali mno na alimsaidia mno kufanikiwa. ila sijamtaja mtu. poleni wafiwa. unajua kuna wakati unaweza kuumia moyo hadi magonjwa rundo yakakuandama.
 
Back
Top Bottom