Kikwete, Lowassa, Membe na wengineo na historia zao za utoto

Nadhani ni busara na wajibu wetu wanachi kutafuta ukweli wa mtu anayetaka kwa hamu sana kuongoza nchi yetu bila kujua lengo lake ni nini.

Au wewe una maoni tofauti?
Hili swali unalipenda sana. Naona kiu yako bado haijapata majibu. Labda tusubiri Hutaki unaacha na Mtoahabari warudi. Wakichelewa tuwatumie nauli!
 
Amefanana sana na Miraj..kwa sura na Kimo..au urefu........hata kwa namna wanavyochanganyikana na watu....in short ujana ukimpita Miraj Ana future Nzuri kisiasa kuliko Rizwan Mfupi ambaye ..in short hapendwi au hata hapendeki..............Miraj anaweza kukaa na mtu yeyote.....

Yaah naona kama baba kama mtoto!!akijifunza mapungufu ya msure wake kisha akajaza character zinazompa baba yake veto basi anauwezekano wa kuja kuingia kwenye mbine za kisiasa japo anajionyesha wazi kuwa hapendi siasa.Sometimes genetically wanasema kazi aliyoifanya baba kabla ajazaa mtoto husika ikawa ndani ya damu yake kwa maana ya kuipenda na kuhifurahi basi atakapo kuja kuzaa mwana basi genetically mtoto anaweza kuja kuifanya kazi ambayo mzazi aliifanya kwa ufanisi mzuri sana.
 
mkuu umenikumbusha kuhusu hear say na rumours
nimewahi kukutana na watu wanaosema wanamjua Kikwete na niliyosikia
kwa kweli nilitamani mtu wa kuyathibisha upi ukweli na upi sio ukweli...

baadhi niliyoambiwa ni haya....jina Jakaya kwa kikwere maana ya ke ni mtoto wa nyumbani
ja-kaya.....wa-nyumbani.....jina hili linapewa kwa watoto waliofiwa na baba zao na kubaki kulelewa na mama zao tu

sasa yasemekana mama JK alilelewa na baba mwingine aliemuoa mama yake...ndo maana anaitwa Jakaya...

sasa jiulize maswali kibao hapo....na kuna madai kuwa ana dada ambae ndie mtoto hasa wa baba aliemlea
ambae ameolewa na IGP MWEMA.....ilimradi kuna story nyiingi zinazohitaki Clarifications..
...but unapa picha ya personality yake ilivyo....'ya kuthamini waliomsaidia' no matter what...
he doesn't forget a favor.....

hayo ni machache tu lakini Mtikila aliwahi kusema kitu kama 'magonjwa ya kurithi' siku Kikwete alipochaguliwa
sijui alikuwa anajaribu kusema nini......

Hakika ndio maana nikasema hata kama ni hear say au rumours sisi tulio nje ndio tunaweza kupima kupitia hayo.Na kwa upnde fulani kama kuna misemo hiyo napigia mstari kisha naweka dot ya kwa maana ya dot kusubilia story nyingine nipigie mstari kuweza kujenga picha.

Hakika malezi ya utotoni yana maana sana kama ulivyosema.Lakini ni kitu kizuri sana kuludisha favour kibinadamu na inaonyesha kuwa unathamini waliokusaidia.Kama ndio hivyo basi mfumo ulipaswa kujiandaa na kujua kumsaidia jinsi gani anaweza kuendesha office huku mapungufu yake hayo binafsi yenye nia njema basi hayana madhara kwenye usimamizi wa Taifa tuliomkabidhi.

Napata shida sana hivi uwa hakuna think tank ambayo iko nyuma ya Rais ambayo kazi yake ni kuingineer maswala yote yanayohusu ofisi ya Rais ikiwemo kumsaidia kwa kujua sehemu ambazo wanajua kuwa ni weakness ya kibinadamu wanajenga mfumo sahihi wa kucover up mapungufu hayo.Anajambo jema la kukumbuka waliomsaidia lakini ikizidi kwenye utendaji hasa kwenye sehemu hiyo ya ofisi kuu basi mambo mengine yana athilika kwa sura hii yake ya mazao ya malezi ya utotoni.

Ili la Mtikila hakika sina cha msingi nachoweza kusema WAAFRIKA wana MILA na DESTURI zao ambazo kumuelimisha mtu ambae ajakulia mazingira hayo ni ngumu sana.Ndio maana Mwalimu alikuwa na kwao anaasema USIMUULIZE kabila yake kwani UNATAKA KUTAMBIKA, na kwao walikuwa na sehemu yao ambyo wanaita MWITONGO ambako ndiko walikuwa wanamalizia mambo yanayohusu kabila yao huko.Hivyo ilo la Mtikila kama ni UAFRIKA binafsi sina hoja nalo kwa kuwa hayo ni ya nyumbani kwa muhusika na ukoo wake na kabila yake kwa kuwa MUACHA ASILI SI JASILI NA JASILI AACHI ASILI.
 
Historia inatusaidia kumjua mtu alikuwaje ingawa kuna nafasi kubwa ya improvement as the time rolls on.
 
Historia inatusaidia kumjua mtu alikuwaje ingawa kuna nafasi kubwa ya improvement as the time rolls on.
Sasa unakuta kuna mtu anasema hiyo ni personal life
Kwamba hata kama alishindwa kuihudumia familia yake
Akiwa mtu mzima kabisa, wala sio vya utotoni,
Bado ni personal life, haihusiani na maisha ya watanzania
Familia yake mwenyewe kashindwa, ndio ataweza taifa nzima?

Mfano: tunamchaguaje mtu akatuwakilishe EAC huku tukijua kua
mtu huyo hana time na mke wake, mtu huyo hana time na mtoto wake?
Na akiulizwa swali hilo anapiga kimyaaaaa.
 
Sasa unakuta kuna mtu anasema hiyo ni personal life
Kwamba hata kama alishindwa kuihudumia familia yake
Akiwa mtu mzima kabisa, wala sio vya utotoni,
Bado ni personal life, haihusiani na maisha ya watanzania
Familia yake mwenyewe kashindwa, ndio ataweza taifa nzima?

Mfano: tunamchaguaje mtu akatuwakilishe EAC huku tukijua kua
mtu huyo hana time na mke wake, mtu huyo hana time na mtoto wake?
Na akiulizwa swali hilo anapiga kimyaaaaa.

Umbea wa sijui William kakimbia child support Marekani hauhusu!
 
Kwa jinsi bongo ilivyo, saa hizi ukamuulize mtu aliyesoma ama kuwa jirani na JK ama EL kuwa alikuwaje akiwa mtoto, atampamba hadi nyuki wawashambulie! Kujipendekeza kumeshika hatamu. We ar not honest kabisa! Sijui tuna shida gani!
Niliwahi kumuuliza mama wa mtu kiutani 'mwanao alikuwa mtundu sana...', alisisitiza mwanae alikuwa mtaratibu asiyegombana na mtu. Ilhali mwanae aliniambia mwenyewe kuwa alikuwa mtundu, mchokozi na alikuwa anapiga dada zake na kuchoma midoli moto! Imagine historia unachukua kwa mama huyu! Anayesubiria ruzuku ya mwanae! Ama kwangu mie ambae ninategemea kuna siku mshkaji ataniona anipe walau ka-ukatibu mkuu?!
 
Historia inatusaidia kumjua mtu alikuwaje ingawa kuna nafasi kubwa ya improvement as the time rolls on.

Kuna wakati nikiwa mtoto mwenye binafsi nilikuwa mtundu,lakini siku zinavyokwenda ndio utundu wa utoto unapotea lakini ufahamu wa mahusiano ki utu uzia unashape kunipeleka kwenye maisha ya utu uzima mpaka hapa ni myu mzima kati ya nafasi ya ujana na utu uzima.

Kwa siku hizi uwa naweza kuwaona watoto wadogo wanacheza mi binafsi naanza kuona hawa watoto wanaocheza mbele ya macho yangu kila mmoja unaweza kuona future yake imesimama wapi kwa jinsi wanavyojisimamia kila mmoja kwa mujibu wa anavyojitabaisha,kama ni ubabe,upole,utundu,usemaji, uongozi nk.

Nilichojifunza nimeogopa sana kuona mtoto mdogo akiwa mpole sana,kwa kuwa anafasi kubwa sana ya kusimama kwenye uovu,na akipona hapo basi mtoto huyo ni genius kuliko mtoto aliye mtunda sana wakati wa utoto.Na daima watoto waliochangamka sana yani ukifika nyumbani ukosi kusikia story zinazo muhusu au umekaa kasogea na yeye kaanza maswali ya udadisi mara nyingi watoto hawa wamefanikisha sana kwenye maisha ya kawaida tunayoishi.

Hivyo historia ya maisha ya mtu ya utotoni inaweza kukupa ni aina gani ya mtu alipaswa kuwa kabla hajatuvalia kava [mask] kupata anachotaka iwe ni uongozi au madaraka katika ofisi.
 
Back
Top Bottom