Kikwete, Lowassa, Membe na wengineo na historia zao za utoto

Keil, waandishi wepi hao unawazungumzia, kama wangekuwa na nia ya kupata ukweli bila chenga?!.

Waandishi sisi sisi ambao ukituita kwenye press conference yako, utalazimika kutupatia na "bahasha" ya kausafiri ili tuweze kuchukua taxi tuwahi newsroom ndipo story yako itoke!, hiyo nauli ya kwenda Kibaha sekondari atatoa nani?!. Na hapo sio tuu nauli kufika Kibaha sec, itakubidi umpooze Headmaster kukubali registry ifungunguliwe, umpooze attendant kusaka mafaili ya zamani hizo, tena sio kazi ya siku moja kuseme usubirie, kuna nenda rudi nenda rudi, kalete barua ya ofisa elimu kanda, ofisa elimu wilaya, ofisa elimu mkoa, barua toka wizarani kukuruhusu wewe kufanya hayo etc, nani atalipia hizo gharama?. Kama una "bahasha" you cut the long story short kumtake care attendant anakunyofolea faili lote zima zima unamaliza kila kitu!, its all about "bahasha"!.
 
Last edited by a moderator:
The Boss

mkuu kwa kuwa wewe una idea jinsi gani mtu anaweza kuanza kupata taarifa ya kuweza kuandika kitabu ni bora hiyo kazi ukaifanya wewe mwenyewe na utakuwa umesaidia watanzania wengi, ubarikiwe
 
Last edited by a moderator:
Kwenye modern life, tutake tusitake, tukubali, tukatae, "bahasha" ndio kila kitu only it can't buy love or happyness but can only influence!.
Nilidhania ni sisi tu tuliokimbia umande tunafanya haya makosa "happyness"
 
Nilidhania ni sisi tu tuliokimbia umande tunafanya haya makosa "happyness"
Elimu yetu karibu yote ni sawa tuu na waliokimbia umande!. Hivi wewe una taarifa Tanzania hatutengenezi hata toothpick!, hata pini tuu au sindano ya kushonea nguo hatuwahi kuweza kutengezeza!, ndio unazungumzia hili lugha za watu?, tena sometimes afadhali hata waliokimbia umande, are better off!.
 
320820_10150304906766225_33236101224_8227470_830515022_n.jpg

Ridhwan mtupu!! duh! no wonder
 
Watu wanafika kutaka tuwape kura za urais-nafasi ya juu zaidi ya uongozi Tanzania-bila ya kujua hata historia zao za miaka 30 tu nyuma

Dr.Slaa, Mbowe na Lipumba nao ni giza nene
 
niliwahi kuona ka biography cha Kikwete na moja ya sifa zake za utotoni ni kuwa alikuwa anapenda sana Ngoma,
 
Tusiende mbali, mbona Kikwete alikua kiongozi tangu shule ya msingi - je tanaona ajabu gani anapokuwa RAISI wa nchi, kwani kote kule alipopita alikuwa anapata upendeleo? We sema kila mtu ana kalama yake ya kuongoza, utafiti mwingine hauwezi kutuletea tija kwa sababu binadamu ubadirika tabia zao kutegemea UMRI, mazingira na experience aliyopitia katika maisha yake baada ya kuachana na wazazi/walezi wake. Mambo mengine ya kisaikolojia ni very complicated kiasi kwamba huwezi kuya-quantify kwenye facts na figures kama Uhandisi/Engineering. Unaweza kujikuta unawahuku watu ndiyo sivyo.
 
ungeanza na kumwaga hapa hitoria yako kama mfano wa kuigwa ingependeza zaidi kwani hata wewe unaweza kuwa kiongozi siku moja tukikujua mapema inapendeza.

- Accept critiques and let the same be your best friend and consequently your fault will be easily determined
 
Keil, waandishi wepi hao unawazungumzia, kama wangekuwa na nia ya kupata ukweli bila chenga?!. Waandishi sisi sisi ambao ukituita kwenye press conference yako, utalazimika kutupatia na "bahasha" ya kausafiri ili tuweze kuchukua taxi tuwahi newsroom ndipo story yako itoke!, hiyo nauli ya kwenda Kibaha sekondari atatoa nani?!. Na hapo sio tuu nauli kufika Kibaha sec, itakubidi umpooze Headmaster kukubali registry ifungunguliwe, umpooze attendant kusaka mafaili ya zamani hizo, tena sio kazi ya siku moja kuseme usubirie, kuna nenda rudi nenda rudi, kalete barua ya ofisa elimu kanda, ofisa elimu wilaya, ofisa elimu mkoa, barua toka wizarani kukuruhusu wewe kufanya hayo etc, nani atalipia hizo gharama?. Kama una "bahasha" you cut the long story short kumtake care attendant anakunyofolea faili lote zima zima unamaliza kila kitu!, its all about "bahasha"!.

Mkuu Pasco,

Mimi ninapingana na swala la bahasha pale linapotumika kwa malengo ya kudanganya jamii au kusema sifa za mhusika ambazo hana.

Hata ukisema umpe mwandishi bahasha ya fungu nono na uende kulipia airtime ya kurusha kipindi maalum cha madudu ya wana siasa kwenye vituo vya ITV, Channel 10, Mlimani TV, Star TV na nyinginezo, chances za kukubaliwa kurusha kipindi ni ndogo sana. Kama hiyo documentary yako ina negatives haiwezi kurushwa mpaka kwanza wai-scan [edit] ili kutoa virus na wabakize mazuri tu.

Lakini ninakuhakikishia kwamba chukua same documentary ya mwanasiasa machachari ambaye hayuko kwenye corridors za power halafu uweke negatives na positives za maisha yake, inaweza kugombewa kama njugu na nina uhakika kuna wana siasa walio madarakani au wanaowaniwa kuingia Ikulu wanaweza kukulipa hela ya ziada na kipindi kitarushwa bila ku-scan virus.

Wamiliki wa vyombo vya habari [hasa TV] wako pro-watawala au wanawaogopa prospective candidates wa kutoka chama tawala. Sasa hivi tunajua madudu mengi ya Mkapa kwa kuwa hayuko tena madarakani, lakini huwezi kupata madudu/negative info za akina EL, Membe, Mwandosya na wengineo wanaowania nafasi ya kuingia Ikulu kupitia chama tawala kwa kuwa wanajitahidi sana kuziba mianya ya madudu/uchafu wao kujulikana nje. Hata kama ukiupata, unaweza kukosa TV ya kurusha hayo madudu kwa kuwa walimiliki wa TV wengi ni waoga. Angalau kuna baadhi ya magazeti yanaweza kuandika lakini kwa woga mkubwa na kuweka majina kapuni as if tunasoma magazeti ya Shigongo.

Kuna baadhi ya wana siasa wameweka mtu kwenye kila media house, na kazi ya hao watu ni kunusa habari ambazo zitatoka kwenye kila toleo la gazeti. Ndio kuna siku Gazeti la Raia Mwema lilichelewa kutoka kwa kuwa lilikuwa na habari za kuwagusa vigogo ambazo zilikuwa negative. Sasa ukijiuliza, hao vigogo walijuaje kwamba gazeti la Raia Mwema litakuwa na habari hiyo kabla halijachapwa?

Ukweli halisi ni kwamba Uhuru wa Habari Tanzania ni mdogo sana. Waandishi nao wanachangia kufanya mambo yawe mabaya zaidi na hasa wanapopokea bahasha ili kuandika habari kwa ushabiki na kuficha ukweli. Wamiliki wa vyombo vya habari nao ni waoga ndio maana kila siku tunalishwa kasa!
 
Hiyo rahisi kupata data kuliko kujua mtu wakati akiwa na miaka chini ya 10 alikuwa anacheza mchezo gani na akina na unless wahusika wakuambie wao wenyewe.


306846_10150304906851225_33236101224_8227471_959808821_n.jpg

Kikwete na Prof Mark Mwandosya walikuwa wapi hapo?
 
Akiwa mtoto mchanga JK alipachikwa kifuu cha nazi kichwani kwa ajili ya kuzaliwa bila kichwa...
 
Ila pia sisi Watanzania hatupendi kujisomea mambo makubwa, tunapenda mambo laini laini ndio maana magazeti ya udaku ndio yanayoongoza kwa circulation!.
Sio watanzania tuu, binadamu kwa ujumla wanapenda udaku. Hivi wewe unajua kuwa national enquirer inaongoza kwa kuwa na idadi kubwa ya wasomaji nchini Marekani?
 
Akiwa mtoto mchanga JK alipachikwa kifuu cha nazi kichwani kwa ajili ya kuzaliwa bila kichwa...
Source JF JUKWAA LA UTANI
 
Akiwa mtoto mchanga JK alipachikwa kifuu cha nazi kichwani kwa ajili ya kuzaliwa bila kichwa...
Source JF JUKWAA LA UTANI
Mkuu lugha umetumia ina ukakasi, JK ni Rais wetu. Kuna mamilioni ya Watanzania wamempigia kura,ina maana wote hawa wana vichwa vya nazi? Hizi lugha chafu tuwaachie akina Lusinde, Mwigullu na Wasira!
 
The Boss. Siyo historia yao ya nyuma tu,hata wakistaafu hawaandiki juu ya maisha yao. Najua Mwl. Nyerere wakati anafariki alikua ameanza maandalizi. Mzee Mtei ameandika kitabu. Jiulize watu kama mzee Mwinyi, Malecela, Warioba,Salim,Mkapa, Msuya, nk hawaandiki historia ya maisha yao kama watumishi umma?
 
Kumfahamu mtu yeyote ni lazima utazame historia yake ya utotoni aliosoma nao, aliocheza nao... walimu wake... walezi wake, majirani na kadhalika...

Sasa sisi Tanzania ni nadra sana kusikia historia za utotoni za viongozi wetu kiasi kwamba maambo meengi tunayoyalalamikia pengine majibu yake yapo kwenye historia zao za utotoni...

Mfano:
Utotoni mtu alikuwaje na wenzie? Mbinafsi? Mchoyo?
Mpira alicheza vipi na wenzie? Aliwahi kuwa refa? Kuwa nahodha? Au alikuwa 'anafuata mkumbo tu'?

Je, ndani ya familia wazazi waliwalea vipi?
Chakula kilitosha? Kama hakikutosha ilikuwaje? Alijipigania chakula chake?alikificha? Mama alimfichia chakula chake? Aliwaacha wadogo zake washibe kwanza? Au alikula yeye kwanza?

Na je kwa wenzake shuleni alikuwaje? A bully? A natural leader? The peacemaker? Au mchonganishi?
Alikubali kushindwa kihalali? Au ilikuwa lazima ashinde by any means necessary?..

Kuna meengi mno ya kujifunza kama tukijua historia za utotoni za hawa watu wanaojiona ni viongozi wetu na wote wale ambao wanataka kuongoza....

Sijui kwa nini hatuna waandishi wa kuchimbua historia za utotoni za hawa watu...

Umesema kitu kikubwa sana The Boss...tuna overlook some facts kuhusu historia zetu na za wanaotuongoza. Kuna sababu ya kufahamu kwa undani ili tusije anza kumfahamu mtu tayari akiwa anauza sura
 
Kweli kuna umuhimu wa kutafuta historia zao.

Baadhi ya viongozi wengi walioshindwa kiungozi au madikteta historia zao zinaonesha walikua katika mazingira aidha magumu au ya kunyanyaswa kifamilia.

Wapo waliotoka kwenye familia maskini sana, hali ya kujitenga.

Tukipata historia za hawa watu itasaidia kujua ni watu wa aina gani kwani mazingira ya mtu aliyoishi yanasaidia kujua tabia zake.
Mfani ukiweza pitia hata historia ya Aldolf Hitleri, Iddi Amin hata Pablo Escobar zinaonesha maisha yao ya awali.
 
Back
Top Bottom