Wajue wanyama hawa na sifa zao za kipekee

Kichangiri

JF-Expert Member
Feb 16, 2017
331
670
1. Nyangumi.
Huyu ndio mnyama mkubwa kuliko wanyama wote, ukimuweka katika kiwanja cha mpira mpira, hubakiza mita chache ili kufikia nusu ya kiwanja hicho, mbali na ukubwa huo lakini ni mnyama mwenye macho madogo sana, ila sehemu za siri noma sana dume huwa na uume wenye futi 12.View attachment 819544

2. Twiga.
Huyu ndiye mnyama mrefu kwenda juu kuliko wanyama wote unaowafahamu, anapenda amani, ni mpole lakini hapendi mizaha, miguu yake ndio silaha pindi anapovamiwa na hilo teke usiombe.View attachment 819543

3. Kozi
Huyu ndiye kiumbe mwenye uwezo wa kukimbia kuliko mnyama yoyote, ni ndege mwenye ufanano sana na tai, ukimshitua akakimbia kama upo Dar es salaam usiendelee kumtafuta dar, wapigie ndugu zako moro kuuliza kama ametua huko au lah.View attachment 819542

4. Nyegere.
Ndio anavunja rekodi kwa wivu alishawashangaza watalii hapo Serengeti baada ya jike wake kujikwaa, alichimba shimo refu kidogo kuhakiki kama ile ilikuwa ni ajali kweli, au kuna faulo alitaka kuchezewa kwa bae wake.View attachment 819541

5. Kobe
Ndiye mnyama anayeishi miaka mingi duniani, pengine kuliko wanyama wengine wote hufikia miaka hadi 350, kwa Tanzania tunao wenye miaka 200+, kama nakuona raha za dunia zinavyokufanya utamani kuwa Kobe.View attachment 819540

6. Kicheche.
Ndiye mnyama anayependa ngono kuliko kiumbe yoyote, wanapokutana jinsia tofauti kabla ya salamu huanza kusasambua kwanza, yaani hawa katika jamii zao hata msibani hukutana kwa mapenzi pia, inakadiriwa kwa siku ili walale usingizini mwororo auheni wapitiane mara 60 na zaidi ! Na ndio sababu hata mtu akiwa kiwembe huitwa kicheche.View attachment 819539

7. Konokono.
Ndio kiumbe anayesafiri taratibu sana na hii ni kwa sababu hujitengenezea njia ya kupita kwanza ndipo apite.View attachment 819538

8. Tai
Ndio kiumbe mkorofi kupita kiasi ni kawaida kunyang'anya watalii chakula, ni kawaida kusumbua ndege wenzie wanapoatamia, kupigana nk ili mradi fujo.View attachment 819537

9. Nyati
Mnyama mwenye hasira na kisasi kuliko wanyama wengine wote, simba wanamwelewa vyema sana huyu kiumbe, wakithubutu kuua mtoto wake na wao huenda kukanyaga watoto wake vile vile au vipi bwana jicho kwa jicho, jino kwa jino tuone sasa.View attachment 819536

10. Kipepeo.
Ndiye kiumbe mpenda amani pasina mfano, ukipita msituni umenuna usitegemee watakusogelea, ila mkipita na mwenza wako, mnacheka mna furaha, ahaa utashangaa wanawapamba !View attachment 819535

11. Simba.
Pengine sababu ya kuitwa Mfalme ni ubabe, Dume la simba ndio mnyama pekee anayejijua kwamba anaogopwa na hata majike wake wanapopata dhahama, akipata taarifa hujitokeza mara moja na ukiona madume yameongozana mawili basi jua huo mziki mwamuzi ni Mungu.View attachment 819534

12. Mbu
Ndio kiumbe aliyeweza kuua binadamu wengi sana kuliko mnyama yoyote yule unayemfahamu wewe, utapokaona tafadhari Katie kitasa.View attachment 819532

13. Komba
Ndiye mnyama mlevi kuliko wanyama wote na akilewa hulia pasina sababu ya msingi, hata ukibahatika kumuona sura yake imekaa kilevi levi, hupendelea pombe za kienyeji kuliko bia, we watege kwa mnazi au ulanzi sio misosi hapo utawapata.View attachment 819531

14. Popo
Pamoja kwamba mchoro wake hupendeza sana katika michoro, ila ni miongoni mwa viumbe wenye sura mbaya sana kuliko wengine wote.View attachment 819530

15. Tembo
Ndiye mnyama mwenye uwezo wa kuhifadhi sana kumbukumbu katika kichwa chake, kama ulipojenga walihawi kupita tegemea kuna siku watakuwa wageni wako, wakati tunakazana kusema tembo wamevamia sehemu fulani tukae tukijua maeneo hayo wana historia nayo, sasa siku mpige jiwe mkutane baada ya miaka kumi ndio utajua ule mkonga ni bakora au pua.View attachment 819529

16. Pomboo
Ndiye mnyama mwenye huruma sana kiasi kwamba akikuona una tatizo, huacha mambo yake na kutaka kukusaidia.View attachment 819528

17. Ngekewa
Huyu ndiye mnyama anayependwa na wanyama wengine wengi. Ana uwezo wa kukaa kitako na simba, chui cobra na wengine wengi wakali bila kudhuriwa.
 
Last edited:
Umemsahau Ngekewa asee anapendwa na wanyama Wengi sana, Ila Pomboo ni Shidaa ana huruma sana
 
Ngekewa
tapatalk_1532608324328.jpeg
tapatalk_1532608328418.jpeg
tapatalk_1532608335178.jpeg
 
Back
Top Bottom