Marejeo ya Historia: Mahatma Ghandi, Abraham Lincoln, Nelson Mandela na Mama Tereza waenziwe kwa utume kama Muhammad?


SANCTUS ANACLETUS

SANCTUS ANACLETUS

JF-Expert Member
Joined
Mar 5, 2016
Messages
3,001
Points
2,000
SANCTUS ANACLETUS

SANCTUS ANACLETUS

JF-Expert Member
Joined Mar 5, 2016
3,001 2,000
Wanahistoria, wanaharakati,wanateolojia na wanasiasa:

Ni ukweli usiopingika kwamba historia ya Mambo mengi yaliofanywa na watu waliotutangulia ama imetusaidia katika kujirekebisha kutofanya makosa kama watangulizi wetu au imetusaidia katika kufanya mambo vizuri zaidi kuliko walivyowahi watangulizi hao kuyafanya. Jamii yoyote ile inayofikia hatua ya kupuuzilia mbali historia au kukosa kuihifadhi historia vizuri ni wazi inajiweka katika mazingira ya kupoteza uelekeo wake.Na matokeo yake ni kuparaganyika kwa jamii husika kama si kila siku malumbano na mapigano yasiyokoma.

Ni kwa mantiki hii ya umuhimu wa historia,leo naomba tuangazie suala jingine linalohusiana na mambo ambayo wahenga wetu wamepata kufanya hapa duniani katika historia ya uwepo wa Ulimwengu,mintarafu Sayari yetu ya Dunia.Mada hii inahusu kuwachambua kwa ufupi watu kadhaa ambao wametokea kuwa maarufu sana katika historia ya Dunia na kishapo tuone kama namna watu hao wanavyochukuliwa ni sahihi ama sifa zao wanazopewa leo hii ni pungufu kulinganisha na waliyoyatenda au walizidishiwa tu kugawiwa sifa na hivi kuna haja ya kuwapatia hadhi nyingine kabisa leo au siku zijazo ili kusaidia vizazi vingine kuchepuka kutoka kuogelea katika sifa ambazo hazistaili.

Basi,bila kupoteza muda ninawaleteni kwenu watu hawa: Mtume Muhammad, Mahatma Ghandi, Martin Luther King, Nelson Mandela na Mama Tereza. Kati ya watu hawa watano, wawili (Mtume Muhammad na Mama Tereza) historia inawachora kushughulika na mambo ya Imani kwa Mungu na watatu(Mahtma Ghandi,Martin Luther King na Nelson Mandela) wanakumbukwa kwa majitoleo yao kwa maisha ya kijamii na kisiasa.

Naomba nianze uchambuzi wangu na sifa za wahusika kama ifuatavyo:


1. Mtume Muhammad.

Muhammad,alizaliwa mwaka 570 BK, katika Mji wa Makka ulioko katika Peninsula ya Kiarabu.Alizaliwa katika ukoo ujulikanao kama Banu Hashimu,tawi la ukoo ulioheshimika sana na maarufu kutoka kabila la Wakureshi(Quraysh).

Baba yake Muhammad, Abd al-Muttalib, alifariki dunia na kumuacha mke wake aliyeitwa Amina binti Wahb akiwa na ujauzito (mimba ya Muhammad). Mzee Abd al-Muttalib alifia karibu na Madina akiwa safarini kibiashara kutokea katika nchi ya Palestina na Al-sham (leo ikiitwa Siria).Inahadithiwa kwamba hata mama yake Muhammad alikuja kuaga dunia wakati Muhammad akiwa na umri wa miaka sita na hivi kutoa nafasi kwa Muhammad kulelewa na Baba yake mdogo.Baadaye Muhammad katika makuzi yake Muhammad alifanikiwa kuwa mfanya biashara jambo lililotoa nafasi kwake kuwa na heshima na sauti katika jamii yake ya Kikureshi.

Wakati ambao Muhammad alikuwa “amenawiri” kibiashara na kihadhi ni wakati ambao pia jamii yake ilikuwa katika matatizo na migogoro mikubwa ya hali ya njaa kali tokana na miundombinu ya chakula kuharibiwa na vita,watu kukosa kazi za kuwawezesha kumudu mahitaji ya kila siku, hali ya vuruguvurugu,hali ya kubaguana(hususani wanawake), mapigano baina ya makabila na uongozi mbaya wa viongozi wa kikabila,mmomonyoko wa maadili wa hata watu wake,hasa toka kabila lake.

Mambo yote haya,inasemekana yalimfanya Muhammad awe anahitaji kukaa peke yake kutafakari.Basi,ni katika mkondo huo, inasemekana alijikuta akiwa amejenga utamaduni wa anahudhuria huko kwenye pangoni, Hira,lililoko Jabal an-Nour, karibu na Makka, umbali wa maili tatu hivi kusini mwa Makka ili kuwa anafanya taamali(meditation). Kufanya taamali ilikuwa ni desturi ya watu wa jamii ya Muhammad.

Ni kutokana na mazoea hayo ya kuwa anaenda huko pangoni, inasemekana siku moja usiku akiwa hapo pangoni,nyota zikiwaka kwa namna ambayo miale yake ilikuwa inapenya macho yake na anga zikiwa linawaka utafikiria ni mchana,mara alimuona Malaika Gabrieli mbele yake na kisha Malaika kumuamrisha hivi: “Soma”.Naye akamjibu malaika, “Sijui kusoma”.

Malaika akiisha kujibiwa hivyo na Muhammad, akamshika na kumkaba kwa nguvu. Inasemekana Malaika alifanya hivyo mara mbili na kisha akamuamuru Muhammad kukariri tena au kurudia maneno (aya) yafuatayo baada ya kuwa yametamkwa na malaika:

“Soma kwa jina la Mola wako Mlezi aliyeumba; amemuumba binadamu kwa tone la damu. Soma! Na Mola wako Mlezi ni mkarimu kushinda wote! Ambaye amefundisha kwa kalamu. Kamfundisha mtu aliyokuwa hayajui.”


Inasimuliwa katika hadithi za Kiislamu kwamba malaika alirudia mara safari nne kumuamuru Muhamnad kukariri ujumbe ambao Malaika alikuwa ameandikiwa na Mungu na hivi kutakiwa kuufikisha kwa Muhammad na mara zote alipomtaka Muhammad kukariri maneno aliyokuwa akipewa naye, mara zote Muhammad alishindwa kuyakariri na hivi kujikuta akipigwa au akikabwa na Malaika huyo.(Rejea The Religion of Islam).


Baada ya majaribio manne yote ya kumtaka Muhammad kukariri ujumbe ambao malaika Gabrieli alikuwa ametoka nao kwa Mungu, inasemekena kwamba malaika aliondoka, na kumuacha Muhammad akiwa katika hali ya mfadhaiko na hivi akaamua kuondoka kurudi nyumbani kwake ambapo alipofika huko alimusimulia mke wake Khadija yaliyomkuta huko pangoni.

Uthibitisho wa utume wa Muhammad

Mkewe Muhammad, Mama Khadija baada ya kuwa amepewa mkanda mzima wa mkasa huo huko pangoni, akampa moyo Muhammad na akamshauri wakamuone binamu yake aliyeitwa Waraqah bin Nawafal (ambaye alikuwa ni mtawa/kasisi wa Wa-nestorian) ili kupata mausia yake juu ya jambo hilo.Wanestorian walikuwa ni kundi(wazushi) ambao walikuwa wametengwa na Kanisa Katoliki kutokana na kiongozi wao aliyeitwa Mar Nestorius kutengwa na Kanisa kufuatia Mtaguso wa Efeso(Ephesius) uliofanyika mwaka 431BK.

Nestorius, alikuwa ni Mtawa na Askofu wa Constantinople(leo ikiitwa Instabul).Nestorius alitengwa kutokana na fundisho lake lililojulikana kama Theotokos(Mother of God).Kimsingi kupitia fundisjho hilo,ni kwamba Nestorius hakuwa akiamini kwamba Yesu alikuwa Mungu kweli.


Kwa hiyo, kwa wadhifa ule bila shaka kasisi Waraqah alikuwa na ufahamu wa kiasi fulani juu ya maandiko ya kiyahudi na Kikristu na hivi Khadija na Muhammad walichukulia kwamba kwa nafasi yake angaliweza kueleza ni nini hasa hicho kilichokuwa kimemtokea Muhammad. Kwa hiyo, wakishakumuona Kasisi Waraqah,inasemekana, kwa maelezo ya vyanzo vya kiislamu,Waraqah alimuthibitishia Muhammad kuwa hicho kilichokuwa kimemtokea pangoni ulikuwa ni unabii,

Kasisi Waraqah alienda mbali kudai kisa cha kule pangoni ulikuwa ni ufunuo kutoka kwa Mungu.Nanukuu: “Oh,binamu! Unasema, uliona nini?”


Basi, Muhammad akarudia kumueleza kilichomtokea.Waraqah akiishakusikia hivyo akahitimisha kwa kumwambia Muhammad hivi:

“Huyo alikuwa ni Namus(akimaanisha Gabriel) ambaye Mungu alimtuma pia kwa Musa.Natamani ningalikuwa nina umri mdogo niishi muda mrefu nione jinsi ambavyo watu wangalikufurusha”. ( “I wish I could live up to the time when your people would turn you out.”).(Tafsiri ni yangu).

Basi, Muhammad, akishakusikia hivyo, akumuuliza Waraqah: “Ni kweli watu watanipinga?”(“Will they drive me out?”). (Tafsiri niyangu).Bila kusita, Waraqah akamwambia: ”Mtu yeyote aliyepata kuja mbele ya jamii na jambo kama hili lako, aliashia kuwa adui mkubwa; na laiti kama ningalikuwa na siku nyingi za kuishi hadi nyakati hizo basi, ningalipambana upande wako.( “Anyone who came with something similar to what you have brought was treated with hostility; and if I should be alive until that day, then I would support you strongly.”).(Tafsiri ni yangu).

Muhammad alivyoridhishwa na Tafsiri ya Kasisi Waraqah na kuanza utume

Maelezo hayo ya kasisi Waraqah yalimkolea Muhammad na mkewe Khadija na hivi kuamini kwamba kweli maono yale yalikuwa ni mwito wa yeye kufuata nyayo za Mitume wengine waliokuwa wakiamini juu ya Mungu mmoja-yaani, Mitume kama Musa,Abrahamu na wengineo na hivi Muhammad tokea wakati huo akaanza kujichukulia kwamba alikuwa ametumwa kupeleleka ujumbe kwa watu wa kabila lake waliokuwa wanaamini katika miungu wengi na waliokuwa wakiongea Kiarabu.

Katika muktadha huo, inasemekana, Muhammad aliendelea kutokewa na hali hiyo ya kuwa Malaika Gabriel anamtokea na kumshushia ujumbe spesheli toka kwa Mungu, kwa muda wa miaka 22 hadi mauti yalipomfika na kabla ya mauti yake, alianza kuwa anakukusanya vikundi vidogo vya watu na kuwafanya wafuasi wake na hasa wale ambao walikuwa na muelekeo wa kupenda kusikia imani kwamba kuna Mungu mmoja tu.

Wafuasi wa Mwanzo wa Muhammad

Kwa kiasi kikubwa,wafuasi wa mwanzo mwanzo wa Muhammad, walikuwa ni wale waliokuwa wakiamini juu ya miungu wa kiarabu, vimiungu vidogo vidogo na wale miungu wa kike.Kwa hiyo, ukichukulia kwamba Muhammad alikuwa akiwathibitishia kuwa hata binamu yake, kasisi Waraqah alikuwa ameridhika na maono yale kuwa yanatoka kwa malaika Gabriel na ile kuona kuwa malaika alikuwa ameongea kwa lugha yao ya kiarabu, basi haikuwa kazi ngumu sana kwa baadhi ya watu kusadiki kwamba kweli Muhammad alikuwa amechaguliwa kuwa mtume wa mwenyezimungu na tena kwa ajili ya ardhi ya Arabia na watu wake. Basi, huku wafuasi wa Muhammad, wakisalia kuwa kundi dogo, lakini lililokuwa likiongezeka polepole,huku Muhammad akiwavutia waarabu waliokuwa wakiabudu dini za kijadi katika imani yake mpya.

Maisha ya Muhammad baada ya kupokea utume

Kutokana kwamba Muhammad wafuasi wa Muhammad walikuwa wakiongezeka,hali hiyo,hali hiyo iliwaogopesha wachuuzi(wafanya biashara) waliokuwa wakijipatia pesa kutokana na wahujaji waliokuwa wamezoea kufika Makka kila mwaka kwa ajili ya kuiabudu ile miungu yao ya kijadi. Hofu ya wachuuzi hawa ilikuwa ni kwamba ikiwa hiyo hali ya kuongezeka kwa watu wanaoamini juu ya uwepo wa Mungu mmoja ingeliendelea,basi bila shaka ingefikia kipindi wahujaji wakome kwenda tena hapo kwa suala la kuhiji kwenye maeneo ya miungu wao.Mazingira haya ya wasiwasi na hofu juu ya hatima ya biashara ya watu waliokuwa wakiishi na kujipatia ridhiki kutokana na maisha ya Uhujaji, yaliibua baadaye mapigano baina ya Muhammad akisaidiwa na wafuasi wake kwa upande mmoja na makabila mengine ambayo kwa upande mmoja yaliona maslahi yao yamehatarishwa.

Na hali hii ilidumu muda wote wa utume wa Muhammad hadi kufikia kugharimu maisha yake kwa sababu inasemekana kifo chake kilitokana na kulishwa sumu.2.Mama Thereza (1910-1997).


Mama Tereza alikuwa mtawa wa wa Kikatoliki mwenye asili ya Albania,ambaye mnamo mwaka 1950, aliweza kuanzisha Shirika la Wamisionari wa Upendo(Missionaries of Charity), huko Calcuta,India,shirika ambalo hadi leo hii liko katika nchi zaidi ya 130. Mama Tereza wakati wa uhai wake, aliwahangaikia sana watu maskini,wagonjwa,watoto na Yatima.Shirika la mama Tereza,kwa kufuata nyayo zake, hadi mwaka 2012, lilikuwa na masista wapatao 4,500 walioko katika nchi 133, duniani kote, wakiendesha vituo vya kuwahudumia watu wenye UKIMWI, Ukoma, Kifua Kikuu,Hospitali kwa ajili ya wagonjwa mahututi,vituo vya kuwalisha chakula wasiojiweza, chakula bila malipo(Soup Kitchen), program zinazotoa huduma kwa watoto na huduma za ushauri Nasaha,watoto yatima na mashule. Kwa yale aliyopata kufanya Mama Tereza, mwaka 1976, aliweza kutunukiwa Tuzo ya Amani ya Nobel,wakati huo akiwa na miaka 87 na sasa toka mwaka 2003 ni Mtakatifu,akitangazwa hivyo na Papa Yohane wa II kwa jina la Mbarikiwa Tereza wa Calcuta(Blessed Teresa of Calcuta.3. Mahatma Gandhi (1869-1948)

Kiongozi wa pili katika orodha ya watu ambao wamewahi kuiacha dunia ikistaajabia uongozi wao, alikuwa ni Mahtama Ghandi (Mohandas Karamchand Gandhi).Huyu ndiye aliyeendesha mapambano yaliyoliletea uhuru Taifa la India dhidi ya Mkoloni Mwingereza mnamo mwaka 1920.Staili yake, Ghandi, ya kutotumia njia za vita na fujo,hasa hasa kwa kutumia migomo isiyohusisha machafuko, iliweza kuwa chachu ya kuibuka kwa wapigania uhuru na haki wa mkondo kama huo wa Ghandi, sehemu mbalimbali duniani. Hadi leo Ghandi anapewa heshima kubwa sana nchini India kiasi kwamba tarehe yake ya kuzaliwa kila mwaka inapofika, tarehe 2 Oktoba, huadhimishwa kama ni siku ya kuzaliwa kwa Taifa la India (national holiday in India) na Kimataifa siku hiyo hiyo husherehekewa kama siku ya Kimataifa ya Amani (International Day of Nonviolence).

4. Nelson Mandela

Hayati Nelson Mandela,maarufu kwa jina la Madiba, alikuwa ni mpigania uhuru wa Taifa la Afrika Kusini,hasa kwa kupinga utawala wa ubaguzi wa rangi na ambaye baada ya kukaa kifungoni kwa zaidi ya miaka 27, alifanikiwa kuliongoza Taifa hilo kama Raisi, kuanzia mwaka 1994 hadi mwaka 1999. Mandela,historia inamkumbuka kama mtu aliyepigania haki za watu weusi walio wengi katika Taifa la Afrika Kusini.Na jambo la ajabu sana ambalo liliwashangaza walimwengu ni kwamba hakupata kuingiza siasa za kulipiza kisasi katika uongozi wake. Mandela alipata kupokea tuzo za heshima zaidi ya 250, ikiwemo Tuzo yenye heshima kubwa kabisa duniani iitwayo “Nobel Peace Prize(Tuzo ya Amani ya Nobel).

5. Abraham Lincoln (1809-1865)

Naomba nihitimishe uchambuzi wangu kwa Abaraham Lincoln,rais wa 16 wa Taifa la Marekani, ambaye aliliongoza taifa hilo wakati wa ghasia na machafuko ya Vita vya wenyewe kwa wenyewe (American Civil War), ambayo ilipiganwa toka mwaka 1861 hadi mwaka 1965.

Lincoln, atakumbukwa kwa hotuba yake ya Gettysburg(Gettysburg Address) ambayo hadi leo ni moja ya hotuba nzuri kabisa katika historia ya Taifa la Marekani, iliyopaza sauti juu ya masuala ya Usawa (principles of Human equality), kama yalivyoelezwa katika Tangazo la Uhuru wa taifa la Marekani, na kubashiri kwamba kumalizika kwa Vita ile ya kiraia pamoja na kuwepo kwa udumishaji wa Muungano,ni mambo ambayo yangalileta usawa wa kweli miongoni mwa raia wote wa Marekani. Juhudi za Raisi Lincoln kukomesha masuala ya utumwa ziliishia kwa kutolewa kwa tangazo la Ukombozi (Emancipation Declaration) mnamo tarehe I Januari 1863, tamko ambalo lilipelekea Bunge la Seneti kuifanyia mabadiliko ya 13, Katiba ya Marekani, kuharamisha mambo ya utumwa katika Taifa hilo.Lincoln aliauwa mnamo tarehe 14 April 1865, mjini, Washington, Dc, akiwa na umri wa miaka 56.

Kwa hapa nyumbani, tunaye Marehemu, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, ambaye alisaidia sana kupigania uhuru mataifa mengi, kusini mwa Afrika, ambayo yalikuwa bado yakitawaliwa na wakoloni katika kujipatia uhuru wao.Sote tunafahamu wapigania uhuru wengi walilelewa hapa Tanzania kwa kupewa mafunzo ya Kijeshi,mikakati ya hali na mali.Sote tunafahamu jinsi Mwalimu Nyerere alivyopinga Ubeberu wa Mataifa ya Magharibi kuendelea kuzitawala nchi za Afrika kiuchumi huku wakijidai kutoa uhuru wa bendera.

Mambo ya kutafakari

Baada ya kukuchambulia kwa ufupi wasifu wa wahenga tajwa katika uzi huu,sasa naomba nikudondolee maswali kadha ambayo yanaibuka kwa kusoma historia ya watu hao:1. Kwa kuzingatia historia ya Manabii wote tokea Agano la Kale na Mitume wote wanaotambuliwa na Agano Jipya, ni kwa namna gani Muhammad anakosa kupewa sifa ya uanaharakati na badala yake historia inamchora kama Mtume wa Mungu na tena kwamba mbele yake hakuna Mtume mwingine?

2. Ni mambo gani ya kipekee ambayo Muhammad kabla ya kifo chake alipata kuifanyia ardhi ya Arabia ambayo leo yanamfanya aikwae hadhi ya Kinabii sawa na Yesu Kristu?

3. Je, pamoja na Muhammad kuwa na huruma na kuchoshwa na matatizo yaliyokuwa yakizikabili koo na kabila mbalimbali katika ardhi ya Arabia, hayo tu ndio yaliyotosha yeye kujibatiza jina la utume na unabii?

4. Je,katika maisha ya Mwl.Nyerere, kuna mahali alisikika kujiita Mtume au Nabii? Je, kwa yale aliyoifanyia Afrika tunaweza leo kumchora Nyerere kihistoria kama Mtume?

5. Lakini pia ukiachana na hao viongozi niliokutajia hapo juu, nadhanipia utakuwa umewahi kuwasikia wapigania hazi za Binadamu maarufu duniani kama akina: Fredrick Douglass, Octavius Catto,Pankhursts, Sophia Duleep Sigh.Je,umewahi kuwasikia au kuwasoma akina Sedick Issacs,Rosa Parks au Claudette Colvin wakiitwa Mitume na manabii?

6. Mungu wetu ni Mungu mwenye kufanya hata yale yanayopita ufahamu na uwezo wa akili zetu.Na ndio kisa katika historia pale walipozuka manabii wa uongo, aliwaumbua kwa kufanya miujiza kama ule tuliuona katika mfano wa Elisha na manabii wa mungu wa Baali.Au pale nabii Yona alipogoma kwenda nchi ya Ninawi alimezwa na samaki na kisha kutapikwa ufukweni mwa Bahari akiwa mzima.Au kwa kurejea mamia ya miujiza aliyopata kuifanya Yesu Kristu, ikiwemo kutembea juu ya maji,kulisha maelfu ya watu kwa samaki wawili na mikate mitano tu,kuponya wagonjwa na vipofu,kufufua wafu kama vile akina Lazaro na wengineo,kusoma na kutambua mawazo na mioyo ya watu,kufahamu yaliyopita,yaliyokuwapo muda huo na hata yaliyokuwa yakija baada yake na hata yatakayokuja baada yetu.

7. Je,kwa historia hiyo ya mambo na matukio ya kutisha na kustaajabisha yaliyofanywa na Mungu kupitia manabii mbalimbali na hatimaye kwa njia ya Yesu kristu,mwanae na Mitume kama akina Paulo na Sira(waliotoka Gerezani huku milango ya gereza ikiwa imepigwa makufuli),kuna lolote linalofanana na hayo,aliyopata kuyafanya Muhammad hadi astahili kujinyakulia utume au unabii?

8. Kama Mungu aliona haja ya kutenda miujiza kupitia kwa manabii wote waliomtangulia Yesu kristu na hata kwa mitume wa Yesu walioishi kabla ya Muhammad na hata leo,ilikuwaje kweli kama Muhammad ni mtume wake, ashindwe kumudhihirisha kwa watu wake hata kwa muujiza hata mmoja tu?

9. Muhammad anakuwa mtume wa mwisho wa sifa zipi,zinazomstahilisha kuwa hivyo? Muhammad anakuwaje mtume wa mwisho kwa kumpinga Mungu kwamba sio nafsi tatu zisizotenganishwa na kwamba Yesu sio mwanae?

10. Muhammad, kwa kufanywa mtume wa mwisho, ina maana ilitegemewa yeye akamilishe mambo yote ambayo hayakuwa sawa na au hayakuwa yanaeleweka sawa sawa kwa wanadamu, ikiwemo mafundisho ya wazushi kwamba kwa kuwa Mungu hana mke, basi hawezi kuwa na mwana.Je,Muhammad aliweza kutoa fundisho lolote la kusahihisha upotoshaji kama huo au ndio kwanza alinakili mambo hayo kutoka kwa Wayahudi na wapagani wengine na kisha kuyapa nguvu tena kwa kuyaandika katika Kurani?

11. Je,ni lipi, jambo la pekee ambalo bado halikuwa katika akili za wanadamu, ambalo Mungu aliona kuna haja ya kumleta Muhammad ili alikamilishe kama Muhammad alishindwa kusahihisha uzushi uliokuwapo kabla yake,kama vile kwamba Mungu hana nafsi tatu au kwamba Yesu Kristu alikuwa sawa na wanadamu wengine tu?

Maswali mengine YANAYOHITAJI MAJIBU

12. Hivi,ni kweli kwamba Muhammad alistahili kuwa nabii kwa sababu tu, alidai alizaliwa kutokana na Ukoo wa Abrahamu na Ishmaeli? Ni jambo la ukweli, kwamba kabila lake Muhammad la Kikureshi, lina unasaba na Uzao wa Abrahamu? Na kama ni kweli, hoja hiyo tu, ilitosha kumfanya Muhammad awe nabii hata kama hakuna ushuhuda wa kutotiliwa shaka au pale ambapo umekosekana kabisa ushuhuda, hata ule tu wa kuungaunga?

13. Je,unafikiria Kwa Yesu kristu,kuzaliwa katika ukoo wa Daudi kungalitosha yeye kuwa nabii,kuhani na mfalme, ikiwa kungalikosekana sifa mahiri za Kimasiha?

14. Je,kwa Muhammad kutokana na uzao wa Ishmaeli, ndio ilitosha kumfanya Muhammad kumsingizia malaika Gabriel kuwa alimkaba na kumlazimisha kukariri maneno ya Mungu kama njia ya kuukwaa utume?

15. Je,ikiwa historia nzima ya unabii hakuna mtu aliyewahi kukabwa,kusukwa sukwa au hata kudundwa ngumi na Malaika, kama njia ya kulazimisha ujumbe kufika kwa walengwa, tukio la Muhammad, lilikuwa na upekee gani hata malaika Gabrieli aamue kutumia nguvu katika kumuelimisha?

16. Hebu tuulizane, Mungu ni mwanadamu hata tuseme kwamba siku hiyo alikuwa hajala au alikuwa amelewa au kwamba alikuwa amepandwana hasira kiasi kwamba ashindwe kumuelekeza malaika Gabrieli njia muafaka ya kuchukua katika kumfanya Muhammad aelewe ujumbe aliokuwa anateremshiwa na badala yake ionekane kwamba njia pekee ya kutumia, ilikuwa mabavu

TUENDELEE KUULIZANA

17. Je, ni kwa nini sasa historia isimchoree Muhammad heshima kama mwanaharakati wa jamii ya Waarabu kwa wakati ule na au mtetezi wa haki za wajane au mtu aliyefanikiwa kusuluhisha migogoro na mizozo katika jamii yake na wala sio mtume au nabii?

18. Je. Ni kwa nino Dunia isimpe mkono wa pongezi Muhammad, kwa mambo ya kijamii aliyoweza kuyaweka sawa katika jamii yake.Kwa nini tusimpe mkono wa kihistoria kwa kuguswa na masuala ya wanawake wajane katika jamii yake?

20. Je,ni kwa nini , Abraham Lincoln hadi mauti yanamfika hakuwahi kuujiita Mtume au Nabii kama alivyofanya Muhammad na wala hata leo Dunia haimpi heshima hiyo?Je, historia imemtendea haki?

MASWALI HAYA PIA NI MUHIMU


21. Pamoja na yote aliyofanya, Mt.Tereza(mama Tereza), ambayo yaliacha na yanaendelea kuacha alama katika mioyo ya makundi yote ya kijamii niliyoyataja, bado ni kwa nini mama Tereza hakuwahi kujiita Mtume au Nabii kama ambavyo alifanya Muhammad?

22. Ikiwa suala lililompatia Muhammad utume ni kutokana na heshima ya Unabii ni yeye kuhangaika na mambo ya kiroho,Je,Mt. Thereza yeye hakushughulika na mambo ya kiroho? Kama ndivyo,ni kwa nini historia hadi sasa haimpi Mtakatifu Tereza, hadhi ya unabii na utume?

23. Je, pamoja na heshima yote hiyo aliyo nayo Mahatma Ghandi,ni kwa nini hadi leo haitwi Mtume au Nabii wa India na walimwengu?

24. Pamoja na tuzo nyingi alizowahi kutunukiwa Nelson Mandela, ni kwa nini hakuna hata tuzo moja,ambayo inamtambua Mandela kama Nabii au Mtume wa Waafrika au Nabii wa watu wa Afrika Kusini.Ni kwa nini pamoja na Muhammad historia inamchora kama mtu alieneza dini kwa vita na wakati mwingine kwa kuwa anavamia misafara ya wafanyabiashara wenzie na kuwapora mali zao na pesa, bado anatazamwa au alifikia hatua ya kujiita au kuitwa Mtume au Mtukufu?

BASI,ninawaalikeni sasa tuidadavue historia kwa kieweledi, tukiambatanisha na mifano ya watu wengine ambao wamepata kuifanyia dunia hii makuu lakini wakapewa sifa wasizostahili au hawakufanya mambo ya kutisha sana na au yaliyoacha alama kiduchu lakini wakazawadiwa sifa kuuubwa kuliko ilivyostahili.
 
N

NAKWEDE

JF-Expert Member
Joined
Aug 1, 2007
Messages
23,904
Points
2,000
N

NAKWEDE

JF-Expert Member
Joined Aug 1, 2007
23,904 2,000
Sawa katekista SANCTUS ANACLETUS
 
SANCTUS ANACLETUS

SANCTUS ANACLETUS

JF-Expert Member
Joined
Mar 5, 2016
Messages
3,001
Points
2,000
SANCTUS ANACLETUS

SANCTUS ANACLETUS

JF-Expert Member
Joined Mar 5, 2016
3,001 2,000
Mahatma Ghandi hajawahi kuwa rafiki WA mtu mweusi na alimuona mtu mweusi kama kiumbe kisicho na thamani,soma mkuu
Sijasema alikuwa rafiki Wa mtu mweusi Bali nimeangazia majitoleo yake katika Taifa la India.
 
Astronomer The Great

Astronomer The Great

JF-Expert Member
Joined
May 2, 2018
Messages
823
Points
500
Astronomer The Great

Astronomer The Great

JF-Expert Member
Joined May 2, 2018
823 500
Umemsahau mmoja JESUS CHRIST THE MAGICIAN
 
T

Truth Matters

JF-Expert Member
Joined
Apr 12, 2013
Messages
1,054
Points
2,000
Age
33
T

Truth Matters

JF-Expert Member
Joined Apr 12, 2013
1,054 2,000
Kwa hawa jamaa wakina KOMANDO, MZEE WA UPAKO, MWINGIRA wote ni mitume! Tafsiri ya wakristo UTUME inaweza ikawa rahisi kuupata kuliko UASKOFU!

Hata tasfiri ya 'mungu' haiko serious sana kwa hawa ndugu!
 
SANCTUS ANACLETUS

SANCTUS ANACLETUS

JF-Expert Member
Joined
Mar 5, 2016
Messages
3,001
Points
2,000
SANCTUS ANACLETUS

SANCTUS ANACLETUS

JF-Expert Member
Joined Mar 5, 2016
3,001 2,000
Kichwa cha habari kingesomeka:-

Marejeo ya Historia: Mahatma Ghandi, Abraham Lincoln, Nelson Mandela na Mama Tereza waenziwe kwa utume kama Muhammad au Yesu?
Karibu sasa kwa mjadala.
 

Forum statistics

Threads 1,283,469
Members 493,707
Posts 30,790,701
Top