Kikwete, Lowassa, Membe na wengineo na historia zao za utoto

The Boss

JF-Expert Member
Aug 18, 2009
49,110
115,886
Kumfahamu mtu yeyote ni lazima utazame historia yake ya utotoni aliosoma nao, aliocheza nao... walimu wake... walezi wake, majirani na kadhalika...

Sasa sisi Tanzania ni nadra sana kusikia historia za utotoni za viongozi wetu kiasi kwamba maambo meengi tunayoyalalamikia pengine majibu yake yapo kwenye historia zao za utotoni...

Mfano:
Utotoni mtu alikuwaje na wenzie? Mbinafsi? Mchoyo?
Mpira alicheza vipi na wenzie? Aliwahi kuwa refa? Kuwa nahodha? Au alikuwa 'anafuata mkumbo tu'?

Je, ndani ya familia wazazi waliwalea vipi?
Chakula kilitosha? Kama hakikutosha ilikuwaje? Alijipigania chakula chake?alikificha? Mama alimfichia chakula chake? Aliwaacha wadogo zake washibe kwanza? Au alikula yeye kwanza?

Na je kwa wenzake shuleni alikuwaje? A bully? A natural leader? The peacemaker? Au mchonganishi?
Alikubali kushindwa kihalali? Au ilikuwa lazima ashinde by any means necessary?..

Kuna meengi mno ya kujifunza kama tukijua historia za utotoni za hawa watu wanaojiona ni viongozi wetu na wote wale ambao wanataka kuongoza....

Sijui kwa nini hatuna waandishi wa kuchimbua historia za utotoni za hawa watu...
 
Waandishi wenyewe mpaka wapewe bahasha.

but baadhi yao wapo wanajitolea
hii ni idea tu
sio lazima waandishi hao
yeyote mwingine anaweza fanya hii homework....ikawa msaada
kwa wengi
 
but baadhi yao wapo wanajitolea
hii ni idea tu
sio lazima waandishi hao
yeyote mwingine anaweza fanya hii homework....ikawa msaada
kwa wengi
Tatizo hakuna recollection ya wakati wakiwa wadogo. Recollection itabidi itoke kwa walengwa wenyewe au watu waliokuwa karibu nao, which may not necessarily be true. Nilishaona interview moja ya Ngeleja YouTube akielezea enzi za ujana wake.
 
Tatizo hakuna recollection ya wakati wakiwa wadogo. Recollection itabidi itoke kwa walengwa wenyewe au watu waliokuwa karibu nao, which may not necessarily be true. Nilishaona interview moja ya Ngeleja YouTube akielezea enzi za ujana wake.

kuna mtu aliandika kitabu kuhusu 'mafisadi wa elimu'
nafikiri inawezekana mtu akiamua.....
 
Wapo na vitabu vipo hasa kwa JK. Marehemu Ben Mtobwa (RIP) 2005 na Prince Bagenda 2006.
 
kuna mtu aliandika kitabu kuhusu 'mafisadi wa elimu'
nafikiri inawezekana mtu akiamua.....

Hiyo rahisi kupata data kuliko kujua mtu wakati akiwa na miaka chini ya 10 alikuwa anacheza mchezo gani na akina na unless wahusika wakuambie wao wenyewe.

320820_10150304906766225_33236101224_8227470_830515022_n.jpg


306846_10150304906851225_33236101224_8227471_959808821_n.jpg
 
EMT mbona ni rahisi saana muhusika ukisoma historia yake utakuta kijiji au mtaa aliozaliwa na shule ya msingi aliyosomea unaanzia hapo
unatafuta wazee wa hapo unauliza maisha ya wazazi wake na kina nani alicheza nao halafu unawatafuta ambao wapo hai sasa.

Na usisahau hakuna anaependwa na wote huwezi kukosa watu ambao wako tayari kuongea ukweli 'off-record' unaanzia hapo.....
 
  • Thanks
Reactions: EMT
The Boss

Ina gharama zake pia. Unaenda Mtwara huko kwa Membe, unaambiwa rafiki yake wa karibu utotoni anaishi Kigoma siku hizi. Unaenda Kigoma anakuambia itabidi kwanza aongezee na mzee kama atakubali kushare hii maneno. Na pengine ukute hata Membe alishampiga chini long time. Inawezekana lakini nani yuko interested kujua tabia za Membe wakati akiwa mtoto? Nafikiri ni wachache japokuwa ni muhimu.
 
Last edited by a moderator:
EMT

nchi za wenzetu kama kitu ni topical publisher anagharamia research yote na kumcomission mwandishi mahiri. vinginevyo mwandishi pekee hstamudu gharama.
 
Last edited by a moderator:
Tatizo za waandishi wao Bios za watanzania ni kuandika kiongozi akiwa na madaraka yake. Lakini kuandika maisha private toka utoto wao inakuwa vigumu. Ningependa kusoma Bio ya private citizen Nyerere.
 
Tatizo za waandishi wao Bios za watanzania ni kuandika kiongozi akiwa na madaraka yake. Lakini kuandika maisha private toka utoto wao inakuwa vigumu. Ningependa kusoma Bio ya private citizen Nyerere.
Exactly. Ni mpaka wakiwa viongozi ndio unasikia kidogo historia yao tena on the positive side tuu. Labda tatizo lingine hatuwaandai watu tokea utotoni kuwa watu wa aina fulani ili kuweza kuhiafadhi data zao. Unashangaa mtu anaibukia from nowhere ukubwani anataka kuwa Rais. Ukidodosa background yake wala huipati.
 
Hiyo rahisi kupata data kuliko kujua mtu wakati akiwa na miaka chini ya 10 alikuwa anacheza mchezo gani na akina na unless wahusika wakuambie wao wenyewe.
Sasa kama hizi si zipo kwenye Facebook page ya Jakaya Kikwete......... tabu kupata zile picha ambazo alikuwa anatembezwa mtaani kindumbwe chaaliya, kikojozi na nguo tuzitie moto ndani na kuna viroboto. (kama alikuwa anakojoa kitandani)
 
  • Thanks
Reactions: EMT
Sasa kama hizi si zipo kwenye Facebook page ya Jakaya Kikwete......... tabu kupata zile picha ambazo alikuwa anatembezwa mtaani kindumbwe chaaliya, kikojozi na nguo tuzitie moto ndani na kuna viroboto. (kama alikuwa anakojoa kitandani)

Hizo hutazipata. Inawezekana hata yeye hana.
 
Exactly. Ni mpaka wakiwa viongozi ndio unasikia kidogo historia yao tena on the positive side tuu. Labda tatizo lingine hatuwaandai watu tokea utotoni kuwa watu wa aina fulani ili kuweza kuhiafadhi data zao. Unashangaa mtu anaibukia from nowhere ukubwani anataka kuwa Rais. Ukidodosa background yake wala huipati.

Hapa Marekani, watu wanahusudu sana humble beginning. Hivyo watu wanataka ulianza wapi mpaka kuwa rais au kufikia sehemu ya juu. Na hawaoni aibu kutoa historia zao.

Bios za Kwame na Mandela zimeeleza kwa kiasi fulani. Nivutiwa na Kwame alivyodandia meli kuja Marekani kusoma na jinsi alivyosota.
 
Tatizo za waandishi wao Bios za watanzania ni kuandika kiongozi akiwa na madaraka yake. Lakini kuandika maisha private toka utoto wao inakuwa vigumu. Ningependa kusoma Bio ya private citizen Nyerere.
Mwaka 1994, Jarida la Africa Now lilichapisha makala ndefu ya "The private and public Nyerere: special interview" iliyoandikwa na mwandishi David Martin.
Makala hiyo ilihifadhiwa home library yetu siku ya siku nitatafuta nafasi niitafute for future use. (nimei search makala hiyo imehifadhiwa kwenye ma library ya wenzetu ulaya!)

Ila kiukweli Tanzania tuna tatizo la waandishi wa biography na bibliography.
Hata kazi rasmi ya kuandika historia ya CCM alipewa Kanyama Chiume (rip) na alifariki kabla ya kuikamilisha!.

Kama Chuo chetu kikuu kimetoa wahitimu wa fasihi andishi tangu miaka ya 70 lakini mpaka leo literature zote za shule za sekondari ni wale wale kina Chinua Achebe, James Ngungi wa Thiong'o na kina Atek B'itek, etc etc, unategemea nini kwenye kuandika bio datas?!.

Waandishi wa habari ndio msitutegemee kabisa!, kuandika tuu balanced news ni shughuli!.

Ila pia sisi Watanzania hatupendi kujisomea mambo makubwa, tunapenda mambo laini laini ndio maana magazeti ya udaku ndio yanayoongoza kwa circulation!.
 
Tuna tatizo la viongozi wetu kutotaka kuweka wazi maisha yao huku wakisema mazuri na mabaya na hata mambo ya aibu ambayo walishawahi kuyafanya, wanataka watu tujue tu mambo mazuri wakihisi kwamba tukijua mambo mabaya tunaweza tusiwachague.

Mfano, nilisoma kitabu cha Mzee Mandela, "A Long Walk to Freedom", kwenye kitabu kile anaelezea maisha yake kwa uwazi mpaka na totoz ambazo aliwahi kuzifia, lakini hakuwaambia kwa kuwa alikuwa domo zege. Haoni aibu kusema kwamba aliwahi kuiba mahindi kwenye shamba.

Sasa ukija kwa viongozi wetu, hakuna ambaye anajua Mkapa ana watoto wangapi, wakati mwingine hata watoto wa Mramba tunaambiwa nao ni wa kwake. Ukienda kwa Kikwete utaambiwa ana mke mmoja na watoto kadhaa [hakuna idadi], maana ukianza kuhoji idadi itabidi uulize je wote ni wa Salma? Publisher ambaye anataka kuchapisha kitabu ambacho kina credible stori anaweza kusita baada kukipitia na kuona mapengo au flow ya masimulizi ina utata.

Kwa upande mwingine, mtu akishakuwa prospects za kuwa mkubwa huwa wanajitahidi kuzuwia info mbaya za maisha yao zisije zikavuja kwa watu wengine. Watu waliokuwa ma-best wa mtarajiwa, wanakuwa na woga wa kutoa details ama kwa kuhofia kwamba wakija kujulikana jamaa anaweza kuwafanyizia.

Kikwete alipoteuliwa kuwa mgombea wa CCM, coverage ya maisha yake ya utotoni kwa kiasi kikubwa ilikuwa ime-focus kwenye familia pale Msoga. Ndugu wa karibu hawezi kufunguka kwa uwazi kuhusu tabia na mwenendo wa mtu. Kama waandishi wangekuwa na nia ya kutupatia ukweli bila chenga wangeenda Kibaha Sekondari na kupita kwenye shule zote ambazo JK alisoma na kuwahoji walimu na wanafunzi wenzake na JK. Tuliishia kuonyeshwa picha za JK akiwa sekondari bila details za maelezo kwamba alikuwa mwanafunzi wa aina gani.
 
Waandishi wenyewe mpaka wapewe bahasha.
Kwenye modern life, tutake tusitake, tukubali, tukatae, "bahasha" ndio kila kitu only it can't buy love or happyness but can only influence!.

Ili kuandika historia ya JK, unaanzia hapo msoga, alipozaliwa, majirani wapo, waliocheza nae wapo, waliokuwa nae wapo, aliosoma nao primary wapo, shule aliosoma ipo, data zake za shule zipo, walimu waliomfundisha wapo etc. Unahitati "bahasha' kukuwezesha kufanya hayo!.

Sekondari aliyosoma ipo, data zake za shule zipo, hata grades zake zipo, waliomfundisha wapo, waliosoma nae wapo, vivyo hivyo mpaka chuo kikuu!.

Alipoanzia kazi papo, alipoiishi papo, wamama aliozaa nao hao watoto wake 8 wapo, sehemu alizofanyia kazi zipo, mlolongo wa aliowapitia upo, kila alichofanya, kila alipopita mpaka hapo magogoni alipo, aliacha traces zipo na datas zipo, ila zinahitaji "bahasha" nene kuzi compile!.

Mimi nilishajipambanua kusupport "bahasha" za uwezeshaji kwa asilimia 100%!, hatu huu mgomo wa juzi wa madaktari wetu, issue ilikuwa ni "bahasha" tuu!. Kumbuka "penye uzia.....".
 
Keil,

Baada ya Lowassa kuteuliwa kuwa waziri mkuu, kuna mwandishi alim-sanitize jamaa. Akaeleza sifa zake na jinsi alivyosaidia Mtanzania nchini Romania.

Hata mimi nisiyemjua Lowassa, nikaona timu kweli imepatikana. Najaribu ku-google kipande hicho lakini sikioni.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom