Kikwete, Lowassa, Membe na wengineo na historia zao za utoto

Gharama yake itahitaji Uwekezaji hasa, kwa mtu anayefikiria faida tusahau kufanyika hicho kitu...

Inahitaji mwandishi mwenye uwezo binafsi wa kifedha na uelewa mpana wa hichi kitu (sio shabiki), tena awe anaelewa kuwa anaandikkia umma wa namna gani kwamba hautajali sana kuhusu kazi yake japo kwa mda huo hivyo awe na matumaini ya mbele sana kwamba miaka ijayo....

Nayo kupata jembe la namna hiyo kwenye mazingira ya saivi hajonekana Mtu wa hivyo...
Nimesoma ya Jk iliyoandikwa na Ben Mtobwa (rip) mule umejaa ushabiki tu wala hamna kile unachokilenga TB...

Kwa kifupi kwa mazingira na asili ya jamii yetu, hii kazi inataka moyo sana na pesa mingi (rejea gharama alizoziainisha Pasco)
 
Kumfahamu mtu yeyote ni lazima utazame historia yake ya utotoni aliosoma nao, aliocheza nao... walimu wake... walezi wake, majirani na kadhalika...

Sasa sisi Tanzania ni nadra sana kusikia historia za utotoni za viongozi wetu kiasi kwamba maambo meengi tunayoyalalamikia pengine majibu yake yapo kwenye historia zao za utotoni...

Mfano:
Utotoni mtu alikuwaje na wenzie? Mbinafsi? Mchoyo?
Mpira alicheza vipi na wenzie? Aliwahi kuwa refa? Kuwa nahodha? Au alikuwa 'anafuata mkumbo tu'?

Je, ndani ya familia wazazi waliwalea vipi?
Chakula kilitosha? Kama hakikutosha ilikuwaje? Alijipigania chakula chake?alikificha? Mama alimfichia chakula chake? Aliwaacha wadogo zake washibe kwanza? Au alikula yeye kwanza?

Na je kwa wenzake shuleni alikuwaje? A bully? A natural leader? The peacemaker? Au mchonganishi?
Alikubali kushindwa kihalali? Au ilikuwa lazima ashinde by any means necessary?..

Kuna meengi mno ya kujifunza kama tukijua historia za utotoni za hawa watu wanaojiona ni viongozi wetu na wote wale ambao wanataka kuongoza....

Sijui kwa nini hatuna waandishi wa kuchimbua historia za utotoni za hawa watu...

Nafikiri historia za utoto siyo muhimu kama za ujanani yaani kuanzia high school mpaka chuo..hapa unapata picha kamili ya mtu kwani kunakua na outside influences nyingi zaidi na maamuzi makubwa yanakuja kumsuka mtu mbeleni na kumweka kwenye tabia aliyonayo sasa. utotoni primary school na early secondary hautapata info zenye nguvu ya ushawishi wa maisha wa baadae ya mhusika
 
Ukifika high schoo na vyuoni tayari unakuwa una values zako ambazo zinaku-define wewe as a person.
Kwa hiyo zinaumuhimu mkubwa, hayo anayoyafanya mtu ni mwendelezo wa alivyoishi.

Nafikiri historia za utoto siyo muhimu kama za ujanani yaani kuanzia high school mpaka chuo..hapa unapata picha kamili ya mtu kwani kunakua na outside influences nyingi zaidi na maamuzi makubwa yanakuja kumsuka mtu mbeleni na kumweka kwenye tabia aliyonayo sasa. utotoni primary school na early secondary hautapata info zenye nguvu ya ushawishi wa maisha wa baadae ya mhusika
 
Kama ungefuatilia wafuatao basi na kadi zao za chama mngezichukua:
LEMA,SUGU na ...... Hawa historia zao ziko wazi na mkizitaka nitazimwaga hapa jamvini..................
 
Mwaka 1994, Jarida la Africa Now lilichapisha makala ndefu ya "The private and public Nyerere: special interview" iliyoandikwa na mwandishi David Martin.
Makala hiyo ilihifadhiwa home library yetu siku ya siku nitatafuta nafasi niitafute for future use. (nimei search makala hiyo imehifadhiwa kwenye ma library ya wenzetu ulaya!)

Ila kiukweli Tanzania tuna tatizo la waandishi wa biography na bibliography.
Hata kazi rasmi ya kuandika historia ya CCM alipewa Kanyama Chiume (rip) na alifariki kabla ya kuikamilisha!.

Kama Chuo chetu kikuu kimetoa wahitimu wa fasihi andishi tangu miaka ya 70 lakini mpaka leo literature zote za shule za sekondari ni wale wale kina Chinua Achebe, James Ngungi wa Thiong'o na kina Atek B'itek, etc etc, unategemea nini kwenye kuandika bio datas?!.

Waandishi wa habari ndio msitutegemee kabisa!, kuandika tuu balanced news ni shughuli!.

Ila pia sisi Watanzania hatupendi kujisomea mambo makubwa, tunapenda mambo laini laini ndio maana magazeti ya udaku ndio yanayoongoza kwa circulation!.

That is a maturity statement. Now you know where you are and the problems, mtabadilikaje sasa kusaidia sisi wapiga kura halali kuwajua hawa wanasiasa?
 
Ni kitu kizuri sana,ila viongzoi wengi wa mwaka 1947 wengi waliwalisisha tabia za usiri vijana wa miaka ya 1980 ambao walio wengi leo ndio viongozi wetu.Hakika wengi wameficha sana taarifa zao nyingi

Ila upatikanaji wa taarifa zapo za utotoni na ujanani sio shida,shida ni nani atagharimia upatikaji wa taarifa hizo ukizingatia upatikanaji hiuo hautapitia mfumo wa kibongo bali kutumia shortcut wa kumanipulate source ya information ili iweze kutoa data na information pasipo kuitaji mlolongo mlefu wa kumuona katibu kata na barua ya mkuu wa mkao kwamba ni dta fulani na fulani tu ndio zitoke na si vinginevyo.Wakati taarifa za kiongozi ikibidi hata za kitabu cha Black book zama za sekondari zipatikane.

Watwala walio wengi wa sasa,hawapedni kuonyesha upande wa maisha yao ya utotoni na wengi kuishia kuficha mambo muhimu ambayo yatatoa indication ya kiongozi aliyeko madarakani amepitia kwenye maisha ya aina gani ambayo yameinflunce mienendo mizima ya jinsi anavyo amua maamzuzi yake kwa mujibu wa jinsi alivyolelewa.Waswahili hawakukosea kusma mtoto umleavyo ndivyo akuavyo.

Swala kwa zama hizi tulizo nazo tunaitaji investigation Journalism, ambao media zao zitawalipa vizuri kwenda kutafuta habari kwenye vyanzo kuhusu viongozi walengwa.Naona tatizo letu ni vyumba vya habari kutokuwa na maono ya kuunda news na kuwa creative wa kuunda habari.

Bali JF tunanafasi kubwa sana ya kuchangia kupata taarifa za viongozi wetu hawa haswa huko mitaani [Ni vyema kama umeikuta inaitwa ni hears say au rumous ilete na andika kuwa ni hears say au rumous basi wenye kujua watatoa recommendation kwenye thread kisha wenye ufahamu watapigia mstari>

Mfano kuna Kuna Kiongozi mmoja maalufu kanda ya magharibi,rumous zinasema yeye wakati ule wa shule ya msingi enzi zake walikuwa ni wale watoto ambao kila anakopita uacha ALAMA YA UTAMBULISHO WAKE.Unaweza kupita kwenye daraja au kuta za majengo ya umma kama Community Centre ukakuta maandishi [Kizazi cha leo tunsema Charter] yakimtambulisha yeye kuwa "................AMEPITA HAPA".Hivyo basi unaweza kujua ni namna gani maisha ya utotoni yanavyoweza kuonyesha ni jinsi gani unaweza kuwa mtoto mdogo lakini ukaonyesha your true colour.

Kwa technology ya sasa Viongozi wategemee taarifa nyingi sana ama za kweli au za uongo kuwahusu kipimo kitakuwa ni umma kuamua nani yuko sahihi kwa kuwa ulimwengu umekuwa kiganjani.Leo hii watu walidiliki kuonyesha picha za binti ambae inatuhumika kuwa alikuwa ni mama ya kiongozi mkubwa wa Taifa kubwa ulimwenguni zikiwa na muonekanao usiopendeza.Hivyo Taarifa nyingi kwa mujibu wa technolojia zitakuwepo kwenye vioo vya computer,simu kwa muda mfupi popote pale.

Wazo zuri mwenye taarifa zozote, zimwageni!!
 
320820_10150304906766225_33236101224_8227470_830515022_n.jpg

Ridhwan mtupu!! duh! no wonder

Amefanana sana na Miraj..kwa sura na Kimo..au urefu........hata kwa namna wanavyochanganyikana na watu....in short ujana ukimpita Miraj Ana future Nzuri kisiasa kuliko Rizwan Mfupi ambaye ..in short hapendwi au hata hapendeki..............Miraj anaweza kukaa na mtu yeyote.....
 
  • Thanks
Reactions: DSN
Mfumo wa bahasha umeua tasinia ya habari nchini mwandishi akipewa bahasha ya kaki anampamba mwanasiasa kuliko maelezo.
 
Amefanana sana na Miraj..kwa sura na Kimo..au urefu........hata kwa namna wanavyochanganyikana na watu....in short ujana ukimpita Miraj Ana future Nzuri kisiasa kuliko Rizwan Mfupi ambaye ..in short hapendwi au hata hapendeki..............Miraj anaweza kukaa na mtu yeyote.....

Wabongo bwana huwa hamueleweki kama kinyonga
 
Hapa Marekani, watu wanahusudu sana humble beginning. Hivyo watu wanataka ulianza wapi mpaka kuwa rais au kufikia sehemu ya juu. Na hawaoni aibu kutoa historia zao.

Bios za Kwame na Mandela zimeeleza kwa kiasi fulani. Nivutiwa na Kwame alivyodandia meli kuja Marekani kusoma na jinsi alivyosota.

sisi tunasema haiwezekani
lakini Wamarekani na wengineo pengine wanazo historia kamili za viongozi wetu weengi
sisi tumekazana kuambiana haiwezekani
soma historia sa Saddam na Osama na hata Iddi Amin
utakuta waandishi ni wazungu lakini wanachimba hadi siku aliozaliwa mtu....
 
Keil,

Baada ya Lowassa kuteuliwa kuwa waziri mkuu, kuna mwandishi alim-sanitize jamaa. Akaeleza sifa zake na jinsi alivyosaidia Mtanzania nchini Romania.

Hata mimi nisiyemjua Lowassa, nikaona timu kweli imepatikana. Najaribu ku-google kipande hicho lakini sikioni.

mimi nikimtazama Lowassa napata hisia za utotoni alivyokuwa ni kuwa
alizaliwa katika familia ya watoto weengi
na pengine baba alikuwa na wake wengi pia
so alijifunza 'ku fight' na labda mama yake alimfundisha 'kuji take care always'
na katika familia hiyo baba hakuwa anapendwa na kuheshimiwa saana na watoto
pengine alikuwa mzee hivi.....but hiyo ni hisia zangu tu
sijui ukweli ukoje...
 
Watu hubadilika. Unaweza kukuta utotoni walikuwa bize kwenye nyumba za ibada hadi wazazi wakajua watakuwa imam au wachungaji now ni fisadiz.
 
Ni kitu kizuri sana,ila viongzoi wengi wa mwaka 1947 wengi waliwalisisha tabia za usiri vijana wa miaka ya 1980 ambao walio wengi leo ndio viongozi wetu.Hakika wengi wameficha sana taarifa zao nyingi

Ila upatikanaji wa taarifa zapo za utotoni na ujanani sio shida,shida ni nani atagharimia upatikaji wa taarifa hizo ukizingatia upatikanaji hiuo hautapitia mfumo wa kibongo bali kutumia shortcut wa kumanipulate source ya information ili iweze kutoa data na information pasipo kuitaji mlolongo mlefu wa kumuona katibu kata na barua ya mkuu wa mkao kwamba ni dta fulani na fulani tu ndio zitoke na si vinginevyo.Wakati taarifa za kiongozi ikibidi hata za kitabu cha Black book zama za sekondari zipatikane.

Watwala walio wengi wa sasa,hawapedni kuonyesha upande wa maisha yao ya utotoni na wengi kuishia kuficha mambo muhimu ambayo yatatoa indication ya kiongozi aliyeko madarakani amepitia kwenye maisha ya aina gani ambayo yameinflunce mienendo mizima ya jinsi anavyo amua maamzuzi yake kwa mujibu wa jinsi alivyolelewa.Waswahili hawakukosea kusma mtoto umleavyo ndivyo akuavyo.

Swala kwa zama hizi tulizo nazo tunaitaji investigation Journalism, ambao media zao zitawalipa vizuri kwenda kutafuta habari kwenye vyanzo kuhusu viongozi walengwa.Naona tatizo letu ni vyumba vya habari kutokuwa na maono ya kuunda news na kuwa creative wa kuunda habari.

Bali JF tunanafasi kubwa sana ya kuchangia kupata taarifa za viongozi wetu hawa haswa huko mitaani [Ni vyema kama umeikuta inaitwa ni hears say au rumous ilete na andika kuwa ni hears say au rumous basi wenye kujua watatoa recommendation kwenye thread kisha wenye ufahamu watapigia mstari>

Mfano kuna Kuna Kiongozi mmoja maalufu kanda ya magharibi,rumous zinasema yeye wakati ule wa shule ya msingi enzi zake walikuwa ni wale watoto ambao kila anakopita uacha ALAMA YA UTAMBULISHO WAKE.Unaweza kupita kwenye daraja au kuta za majengo ya umma kama Community Centre ukakuta maandishi [Kizazi cha leo tunsema Charter] yakimtambulisha yeye kuwa "................AMEPITA HAPA".Hivyo basi unaweza kujua ni namna gani maisha ya utotoni yanavyoweza kuonyesha ni jinsi gani unaweza kuwa mtoto mdogo lakini ukaonyesha your true colour.

Kwa technology ya sasa Viongozi wategemee taarifa nyingi sana ama za kweli au za uongo kuwahusu kipimo kitakuwa ni umma kuamua nani yuko sahihi kwa kuwa ulimwengu umekuwa kiganjani.Leo hii watu walidiliki kuonyesha picha za binti ambae inatuhumika kuwa alikuwa ni mama ya kiongozi mkubwa wa Taifa kubwa ulimwenguni zikiwa na muonekanao usiopendeza.Hivyo Taarifa nyingi kwa mujibu wa technolojia zitakuwepo kwenye vioo vya computer,simu kwa muda mfupi popote pale.

Wazo zuri mwenye taarifa zozote, zimwageni!!

mkuu umenikumbusha kuhusu hear say na rumours
nimewahi kukutana na watu wanaosema wanamjua Kikwete na niliyosikia
kwa kweli nilitamani mtu wa kuyathibisha upi ukweli na upi sio ukweli...

baadhi niliyoambiwa ni haya....jina Jakaya kwa kikwere maana ya ke ni mtoto wa nyumbani
ja-kaya.....wa-nyumbani.....jina hili linapewa kwa watoto waliofiwa na baba zao na kubaki kulelewa na mama zao tu

sasa yasemekana mama JK alilelewa na baba mwingine aliemuoa mama yake...ndo maana anaitwa Jakaya...

sasa jiulize maswali kibao hapo....na kuna madai kuwa ana dada ambae ndie mtoto hasa wa baba aliemlea
ambae ameolewa na IGP MWEMA.....ilimradi kuna story nyiingi zinazohitaki Clarifications..
...but unapa picha ya personality yake ilivyo....'ya kuthamini waliomsaidia' no matter what...
he doesn't forget a favor.....

hayo ni machache tu lakini Mtikila aliwahi kusema kitu kama 'magonjwa ya kurithi' siku Kikwete alipochaguliwa
sijui alikuwa anajaribu kusema nini......
 
The Boss. Siyo historia yao ya nyuma tu,hata wakistaafu hawaandiki juu ya maisha yao. Najua Mwl. Nyerere wakati anafariki alikua ameanza maandalizi. Mzee Mtei ameandika kitabu. Jiulize watu kama mzee Mwinyi, Malecela, Warioba,Salim,Mkapa, Msuya, nk hawaandiki historia ya maisha yao kama watumishi umma?

inashangaza mno
mimi nilikuwa sijui Lowasa na Sumari ni wakwe
na sasa sijui watoto wengine wa Lowassa wameoa au kuolewa na kina nani?
wa Kikwete?
nasikia tu Lubuva ni shemeji wa Lowassa but sijui kivipi....sasa kama haya yanayotokea now
hatu pay attention....jiulize historia za utotoni?????
 
Watu wanafika kutaka tuwape kura za urais-nafasi ya juu zaidi ya uongozi Tanzania-bila ya kujua hata historia zao za miaka 30 tu nyuma

Dr.Slaa, Mbowe na Lipumba nao ni giza nene

Gaijin umegusa penyewe
Lipumba inasemekana hana mke wala hajawahi kuwa na mke
wala watoto
hakuna anaejua why.....
Dr Slaa alikuwa padri lakini ana watoto wakubwa wapo vyuoni go figure...

Mbowe kuna tetesi za 'biashara haramu; huko nyuma sijui linazungumzwaje hili....
 
Mzee thread hii umeianzisha na kuijadili mwenyewe. Au imekuchachia, wana jamvi hawajaikubali?
 
Hizi issue huwa zina utata sana,Obama mwenyewe wamelia naye kweli.Wameenda hadi Asia alipoishi utotoni, kutafuta marafiki zake wa utotoni na hata kudai hati yake ya kuzaliwa!

Mara nyingi wakati wanagombea huwa wanajipanga sana, mtakuja juwa baadhi ya mambo wakati mtu yuko state house tayari, tena mtu kama JK aliyesema alijiandaa kwa zaidi ya miaka 10?

Na ni mtu aliyeishi kwa priveledges za kiuongozi, kichama tawala na kichifu toka akiwa mdogo.

Ndo maana ni vyema kumpata rais ambaye amefuatwa kuombwa agombee kuliko anayejitayarisha kwa kiasi kikubwa.

Kwasababu kuna watu ambao itabidi "washughulikiwe" kwenye matayarisho hayo kama ikiwa wataonekana kuwa tishio ama kikwazo towards accomplishing nia yake hiyo, kama kuna ndugu, jamaa, marafiki wenye kuongea, basi kama alivyosema mchangiaji mmoja, kuna woga pia ikiwa ni mojawapo ya sababu nyinginezo zinazochangia kutokupatikana kwa taarifa kama hizo za viongozi wetu.

Mwishoni, muda wa kampeni nao ni mfupi, so wao mara nyingi wanakuwa na muda wanaouita wa "kutangaza sera" na mgombeaji kutambulishwa.However mengi yanayoongelewa ni kuhusu the so called achievements, ambazo mara nyingi ndo hizo za kisiasa, na mafanikio ndani ya vyama vyao vya kisiasa.

Je tatizo linaweza kupungua, na kutuwezesha kuwafahamu viongozi wetu vyema zaidi endapo wagombea watatakiwa kujitambulisha mapema?

Na wakati wa kujitambulisha, ni mambo gani hayo ya utotoni ambayo tutasema sasa haya yatapelekea kuwa mtu wa aina ama kiongozi wa aina gani?

Je habari za utotoni zinaweza kutujulisha traits za kiuongozi alizonazo a certain individual/leader?
 
sisi tunasema haiwezekani
lakini Wamarekani na wengineo pengine wanazo historia kamili za viongozi wetu weengi
sisi tumekazana kuambiana haiwezekani
soma historia sa Saddam na Osama na hata Iddi Amin
utakuta waandishi ni wazungu lakini wanachimba hadi siku aliozaliwa mtu....
Sisi tunawategemea waandishi wa bahasha, hatutoweza kupata habari sahihi na media ni za wanasiasa na zisizo za wanasiasa zina wanasiasa zinaowasapoti.

Some of their dirties huwa zinatoka kwenye magazeti ya udaku, ambayo watanzania wanayachukulia kama kiburudisho tu, sijui kama hayo wanayakumbuka wakati wa kupiga kura, or maybe mengi hatuyaoni kuwa ni ya ajabu kwasababu ndo jamii yetu ilivyo.

Kwa mfano hilo la Slaa kuwa na watoto wakubwa, kama aliwahi kuwa padri, basi kwenye jamii yetu hilo si la ajabu, rushwa ndogo ndogo si kitu cha ajabu etc etc.
 
The Boss,
Unakumbuka hili swali lako?

Je, unaonaje kwa uzi huuhapa https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/207455-jk-huu-mtandao-ni-hatari-be-careful-otherwise-waweza-kuwa-historia-part-1-a-46.html#post3090094 unapata majibu?

huwa natamani mtu mwenye kujua historia sahihi ya EL ailete hapa hasa historia ya kabla ya kufika chuo

Hili swali unalipenda sana. Naona kiu yako bado haijapata majibu. Labda tusubiri Hutaki unaacha na Mtoahabari warudi. Wakichelewa tuwatumie nauli!
 
Umegusa pale pale,

Mi nadhani hii kitu kuwaachia waandishi wa habari tu, itakuwa na utata.
Kwanza waandishi wako katika kundi lenye kipato cha kati kwa hiyo kushawishiwa ili watoe taarifa kwa maslahi ya mlengwa ni rahisi sana.

Sasa kama wasomi wataona umuhimu wa jambo hili na wao kujaribu kufanya itatusaidia sana.

Hata kama habari ya mtu mmoja ikiandikwa kwa mitazamo miwili kwa yule anayemsifia na yule anamponda.
Ukisoma zote vitabu vyote lazima utachuja point ziko wapi.

Back
Top Bottom