Kikwete, humkomoi Mengi bali unaikomoa CCM

Kikwete, humkomoi Mengi bali unaikomoa CCM

Bado unaendeleza tetesi ushahidi hujawekwa hapa

Weka Ushahidi wako juu ya pesa iliyotoka Stanbic bank na orodha ya waliopokea ndipo na mie nitakupa Ushahidi wa Madhambi ya baba yako Mengi.
 
Weka Ushahidi wako juu ya pesa iliyotoka Stanbic bank na orodha ya waliopokea ndipo na mie nitakupa Ushahidi wa Madhambi ya baba yako Mengi.

Stanbic wamekataa kutoa listi ya mihamala.na ndio maana report ya CAG haipo
 
"Kufanya kosa ni KOSA. Kurudia kosa ni KOSA KUBWA"
.
Kikwete should never have been a president in any civilized state (to begin with); so the fact he has served two terms PRESIDENCY only shows how pathetic Tanzania is.

But, the only glimmer consolation is that he and CCM are a special twins!
 
Mengi atabaki kuwa Mengi,ataendelea kuwepo na kusikika lakini Muhongo....??? JK....??? ni muda tu utasema
 
Mengi kacheza vizuri.. yule Muhongo nina wasiwasi na uprofesa wake

Muhongo pamoja na makosa aliyofanya kwenye ishu ya escrow bado ni msomi wa kujivunia na mafanikio aliyopata! Kwahiyo akubali kuachana na siasa akubali pale alipokosea na arudi kwenye fani take huko atafanya vema zaidi na atazidi kujijengea heshima kitaifa na kimataifa! Siasa na uongozi wa kisisa haviwezi amefeli kwenye hilo eneo
 
Tatizo kubwa ni Mengi kukomaa na Mhongo peke yake wakati hili sakata linawagusa watu kibao akiwemo hata huyo Mkono ambaye ndiye alinyetisha Umbea baada ya kunyang'anywa tonge, hili ngoma si ya Mhongo peke yake ndiyo maana watu wajanja wamemshitukia Mengi mapema baada ya kugundua ana Chuki binafsi baada ya kunyimwa Vitalu vya Gesi.
Mengi utakapomjua kwamba ni mnafiki linapokuja suala la kujifanya yeye ni mpambanaji dhidi ya ufisadi, mara zote huwa anakomalia ufisadi wa wale aliokorofishana nao pekee yake! Kumbukumbu zangu zinaonesha kwamba, kama kuna wafanyabiashara ambao Mengi amewahi kuwatuhumu hadharani kwamba ni mafisadi basi ni Yusuf Manji na Rostam Aziz... hawa wote alianza kugombana nao kwanza ndipo akaanza kutumia media zake na kuwaita mafisadi... Hakuna mwenye akili timamu asiyefahamu kwamba kila panapo fisadi mfanyabiashara basi upande wake wa kuume kuna fisadi mtendaji wa serikali. Hadi leo Mengi hajauambia umma kwamba ufisadi wa Yusuf Manji na Rostam Aziz unawahusisha viongozi gani serikalini... hajauambia umma na wala hatakaa aje kuuambia coz' lengo lake yeye sio kutaja mafisadi wa nchi hii bali kuwapiga stamp ya ufisadi wabaya wake... Back in mid-1990's alipoanza kugombana na Dewji hadi kudaganya ametishiwa kuuawa... wananchi wengi walimuamini! Na kama ilivyo kawaida yake ya kutafuta public sympath, wakati wa sakata lile ghafla from nowhere akaanza kujifanya eti kuifadhili Yanga ili mradi tu wawepo watu watakamsaidia ku-play innocence! Haifahamiki, mapenzi yake kwa Yanga cjui yameishia wapi!!!

Alipokuja kugombana na akina Rostam Aziz, akakimbia na ITV yake na kwenda kupiga picha na watoto wa madrasa Kibaha! Bila aibu, akaanza kuuliza vitoto: "watoto wazuri, eti wanasema mimi ni mdini....!" Tangu hapo, wasio tayari kushikiwa akili wakamshitukia kwamba huyu mzee sio!
 
mwenye uwezo wa kufikiri ccm alikuwa mmoja tu MWL JULIUS KAMBARAGE NYERERE kikwete ni mgoni tu

Nakubaliana na wewe kuwa Mwalimu Nyerere alikuwa na uwezo wa kufikiri LAKINI sio uwezo wa kufikiri VIZURI yaani matokeo ya kufikiri yanakuwa na matunda mazuri. Hivi kuchukua barmaids na kuwafanya waalimu wakati ule wa UPE ni kufikiri vizuri huko?
 
Kodi ipi wewe? kodi Ruge kauza kapata pesa kalipa kodi.

Kodi ya capital gains Tax, Habinder haimuhusu.

Pesa za escrow hazina kodi.

Kama itatokea katika mahesabu kuwa IPTL anadaiwa, iwe kodi au chochote kingine kile PAP katowa guarantee ya kimahakama kuwa atalipa yeye.

Hiyo kodi uisemayo kodi ipi?


kwahiyo unampinga hata mwenyekiti wako aliyesema TRA wanafatilia kodi inayokadiriwa kufika bilion 21 kwanini mnapenda kupingana waziwazi? kwaiyo kikwete ni mwongo?
 
Sio Wachagga tu, ni madalali wote kisiasa na kibiashara nchi hii ambao wamenufaiki sana kupitia wizara ya Nishati na Madini kabla ya ujio wa Prof Muhongo na Katibu Mkuu Maswe.

Utajiri mkubwa wa sasa wa Mzee Mengi upo kwenye wizara hii. Utajiri wa Nimrod Mkono kwa sehemu kubwa umechangiwa na TANESCO iliyo chini ya wizara hii. WanaSIASA walioko kwenye payroll za hawa jamaa wawili mnawajua angalau kwa kauli na matendo yao!

ivi mkisema uongo mnapata faida gani? tueleze huo utajiri wa mengi uliotokana na wizara hii??????????????????
 
Kwahiyo unaunga mkono wizi wa mengi kwa mali zetu kisa anabebwa na ccm huu ujinga hali ya juu yani mengi apewe vitaru vya gesi bure,vitaru vya madini bure hii nchi tunaipeleka wapi haiwezekani kabisa muhongo komaa kama unafukuzwa uwaziri poa lakini msimamo palepale tumechoko kuibiwa na mengi.
Jeuri ya Muhongo ipo Mtwara ambako kwa kushirikiana na makampuni ya kigeni, kuna meli zime-anchor pale mtwara na zinaondoka na mafuta crude kupeleka anakokujua Muhongo. Mwizi mkubwa wa mafuta yetu kwa hoja kwamba wannafanya utafiti. Hii siri anajua Muhongo na Kikwete halafu unatufanya hatujui kinachoendelea.
 
Mengi atabaki kuwa Mengi,ataendelea kuwepo na kusikika lakini Muhongo....??? JK....??? ni muda tu utasema

Atabakia kuoa wajukuu na kazaa na mapacha kwa kutumia wanaume wengine wenye sura kama yake, Masilingi,Malima,Masha,Maswi,Manji , Mhongo na Rostam ni mojawapo ambao wamepata kushiriki Ligi za Mengi japo Rostam Azizi sasa wapo pamoja baada ya kumugawia zile dola milion 300 alizouza hisa za voda kisha akatokomea pasipo kulipa Kodi lakini mengi kauchuna kwa kuwa amefaidika na mgao.
 
Mengi utakapomjua kwamba ni mnafiki linapokuja suala la kujifanya yeye ni mpambanaji dhidi ya ufisadi, mara zote huwa anakomalia ufisadi wa wale aliokorofishana nao pekee yake! Kumbukumbu zangu zinaonesha kwamba, kama kuna wafanyabiashara ambao Mengi amewahi kuwatuhumu hadharani kwamba ni mafisadi basi ni Yusuf Manji na Rostam Aziz... hawa wote alianza kugombana nao kwanza ndipo akaanza kutumia media zake na kuwaita mafisadi... Hakuna mwenye akili timamu asiyefahamu kwamba kila panapo fisadi mfanyabiashara basi upande wake wa kuume kuna fisadi mtendaji wa serikali. Hadi leo Mengi hajauambia umma kwamba ufisadi wa Yusuf Manji na Rostam Aziz unawahusisha viongozi gani serikalini... hajauambia umma na wala hatakaa aje kuuambia coz' lengo lake yeye sio kutaja mafisadi wa nchi hii bali kuwapiga stamp ya ufisadi wabaya wake... Back in mid-1990's alipoanza kugombana na Dewji hadi kudaganya ametishiwa kuuawa... wananchi wengi walimuamini! Na kama ilivyo kawaida yake ya kutafuta public sympath, wakati wa sakata lile ghafla from nowhere akaanza kujifanya eti kuifadhili Yanga ili mradi tu wawepo watu watakamsaidia ku-play innocence! Haifahamiki, mapenzi yake kwa Yanga cjui yameishia wapi!!!

Alipokuja kugombana na akina Rostam Aziz, akakimbia na ITV yake na kwenda kupiga picha na watoto wa madrasa Kibaha! Bila aibu, akaanza kuuliza vitoto: "watoto wazuri, eti wanasema mimi ni mdini....!" Tangu hapo, wasio tayari kushikiwa akili wakamshitukia kwamba huyu mzee sio!
Huyo Kibabu kwanza si mwaminifu kwenye ndoa yake bado anaendekeza Michepuko sana japo Umri umeenda sana, Tabia njema huanzia kwenye familia, sasa mshauri wake ni Klyn akisema chochote lazima Mengi afuate babu anapokea Amri za mjukuu bila kuhoji, Mengi pamoja na kujifanya ni Mtemi fulani mbele ya jamii lakini akiwa mbele ya Mjukuu wake Kylin huwa hafurukuti hata nukta.
 
Mkoroshokigoli kujiuzuru kwa viongozi wetu ni dhana ngeni kwani wengi wanasahau kuwa cheo ni dhamana. Kuwapata kina Kagasheki kwa sasa hivi ni nadra sana.
Balozi Kagasheki amejijengea heshima sana,ila sasa kama kuna danadana zitapigwa hapa watu miongoni mwao(Watawala) watakua na vinyongo sana
 
Huyo Kibabu kwanza si mwaminifu kwenye ndoa yake bado anaendekeza Michepuko sana japo Umri umeenda sana, Tabia njema huanzia kwenye familia, sasa mshauri wake ni Klyn akisema chochote lazima Mengi afuate babu anapokea Amri za mjukuu bila kuhoji, Mengi pamoja na kujifanya ni Mtemi fulani mbele ya jamii lakini akiwa mbele ya Mjukuu wake Kylin huwa hafurukuti hata nukta.
Hayo ni mambo binafsi ya mtu na wala hayatuhusu unless angekuwa kiongozi wa umma.

Mkikosa hoja; msilete majungu!

Isitoshe,kwa mwanaume kuwa mbeya ni aibu sana!
 
Huyu muhogo ache kujiamini watamfanya atakuwa kiazi kwani mengi huwa hawezi kutoa liliongia moyoni wewe angalia kakomaa viwanja mjini kati kumbe alipewa kawauzia wahindi vitalu anavyo mpaka huku mwakitolyo shinyanga kawapa wachina kali lia na Manji kakuta kajamaa hakana cheo selikalini so kaja kwa rostom mpaka kachia ngazi sasa we muhogo mchungu katu hatokuacha mengi labda mpe visima vya gesi
 
Hivi makosa ya Muhongo ni yepi? Tumetajiwa ya Tibaijuka ila ya Muhongo hatujaambiwa

Kuna vitu havijawekwa wazi,Pammoja na kutowekwa wazi ,Tumeambiwa waliochota pesa za Escrow toka Mkombozi benki majina yao na kiasi kilichochotwa.Lakini pesa za Escrow zilizochotwa kutoka Stabic bank ambazo ni nyingi kuliko zilizochotwa Ukombozi benki majina yao hayakutolewa na benki hiyo.Kwa lugha nyepesi wapo watu wengine na wenye nguvu kuliko akina Vijisenti,Tibaijuka,Kilaini n.k.Yawezekana ndio kigugumizi au sintojua inayotafuna serikali.Lakini Raisi JK alisema tunayo Financial Intelligence,kama ipo hai tunashindwa nini kujua watu waliochota pesa Stabic?benki ilio kilomita chache tu tokea Ikulu,Benki kuu,Usalama wa Taifa naTakukuru ?
 
Hivi CCM watatuibis mpaka lini
TAKUKURU>ESCROW HELA ZA UMMA
TRA>ESCROW HELA ZA UMMA
CAG>ESCROW KUNA HELA ZA UMMA.
Hebu tujikumbushe sakata kwa ufupi.Rugemalila aliwaambia Tanesco wanaibiwa tozo nikubwa hailingani na umeme unaodhalishwa.Tanesco ikafungua kesi mahakama za london kupinga toza .kesi haijaisha hela zimechotwa .halafu CCM-MAFISADI WANADAI SIO HELA ZA UMMAA.
 
Back
Top Bottom