Kikwete, humkomoi Mengi bali unaikomoa CCM

Kikwete, humkomoi Mengi bali unaikomoa CCM

Tunahitaji wengi nchi hii wanaojitambua kama Mengi!
 
Mtoa mada ameteleza kidogo tu ila wengi wetu tumemuelewa, cha kuelewa hapa ni: hasara ya mtu yeyote ni faida ya mwingine, Prof Muhongo amekosea na Mengi anatake advantage, likewise ccm inapokosea upinzani wanatake advantage. Sijui kwanini madudu ameyafanya Prof Muhongo then Mengi analaumiwa kila kukicha

Mengi analaumiwa kwa sababu anatumia vyombo vyake vya Habari kumchafua Mhongo pekee kisa Vitalu vya Gesi , Mengi hana Uchungu na Nchi hii yeye Yupo kwa Masilahi yake tu lakini huwatumia Wananchi kusaka Huruma kisha akifanikiwa hupotea ghafra, Amri ya kulipa ilitoka Mahakamani Gavana na Waziri wa fedha wakalipa baada ya kupata ushauri toka kwa mwanasheria mkuu hiyo Kampuni ilisajiliwa na Wizara ya viwanda na biashara kuna Mlolongo mrefu hadi hizo pesa zilipolipwa iweje Mengi akomae na Mhongo peke yake?
 
mwambie mengi aludishe pesa za nbc bank alizokopa kisha akala njama wakapotaza ushahidi,
tuanzie mbele kurudi nyuma 1.escrow 2.....3.......4.........5.......6......epa.........7.........8........
 
Nimrod Mkono alikuwa mwanasheria kwa sakata hili hawezi kuhukumiwa ukizangatia kesi alipewa mwanasheria mwingine.
Baba na muasisi wa sakata hili ni Nimrod Mkono baada ya ulaji wake uliokuwa unatokana na ugomvi wa IPTL na TANESCO kusitishwa na akina Muhongo/Maswe/Jaji Werema.

Mkono alilipeleka sakata hili kwa mara ya kwanza kwa Richard Mgamba( naye wa Mara huyu) wa The Citizen. Kisha akampatia Zitto naye akampasia kafulila ili penati ikipigwa Zitto awe golini pale PAC!
 
Labda kama nafasi ya urais inatolewa na wachaga, lakini kama itawajumuisha watanzania wengi ataendelea kulia lia kama anavyolilia gas na Kilimanjaro Hotel. Sijui ni kwa nini kila anachotaka Mengi akikosa lazima azue tafrani. Nani alimwaminisha kuwa Tanzania ni Mengi na Watanzania ni Mengi? Very selfish huyu mtu na ndiyo picha halisi ya wachaga wote.
N kwa taarifa Mengi akisema anagombea uraisi hata kupitia chama cha Ushirika Shitimbi anauchukua uraisi wa nchi hii kiulaini,Mengi kajiotesha mizizi ya uzalendo nchii hii na wengi wa watawala wetu wanamuhofia na kumuogopa Mzee Mengi .
 
Naona unahukumu bila uhakika.

Makosa ya kuhukumu bila kuwa na uhakika ndiyo ambayo Kikwete hayafanyi na kasema wazi juzi, bado anachunguza kuhusu Mhongo ili aweze kufanya maamuzi.

Ni nini usichokielewa?

Hivi kikwete ni nani hasa?
 
Profesa Kitila Mkumbo wa UDSM alisema: “Profesa Muhongo anatakiwa kuachia ngazi. Kauli ya Rais kwamba ‘anamweka kiporo’ maana yake anamtaka ajiuzulu bila aibu kama iliyomkuta Profesa Tibaijuka. Rais hakuyadharau maazimio ya Bunge kama viongozi wengine walivyoyadharau. Wote waliotajwa katika ripoti ile wanatakiwa kuachia ngazi na si kusubiri mpaka kutimuliwa.”Mwananchi 23/12/2014

Mkoroshokigoli kujiuzuru kwa viongozi wetu ni dhana ngeni kwani wengi wanasahau kuwa cheo ni dhamana. Kuwapata kina Kagasheki kwa sasa hivi ni nadra sana.
 
Tunahitaji wengi nchi hii wanaojitambua kama Mengi!

Mengi analitambua kwa lipi ? Mbona hawalipi mishahara mizuri wafanyakazi wake? Kuwapa mapesa akina Sendeka wamung'oe Mhongo kisa Vitalu vya Gesi ni kujitambua? Mbona hajatambua kuwa Rostam aliuza hisa za Vida kwa dola milion 300 hakulipa Kodi na akamugawia pande wakamaliza Ugonvi wao, Mengi anajitambua kwa mbinu za kimafya labda kama alivyofanya NBC bank akakopa kisha akala njama kumbukumbu zote zikapitezwa huku ndiko kujitambua? Mzee kwenda kuoa mjuu ni kujitambua?
 
Membi kisa Vitalu vya Gesi kaamua kukomaa na Mhongo pekee katumia Mabilioni kumpa Sendeka ili amung'oe Mhongo tu, hapa ndipo Mengi watu wanapomshangaa kwani Masilahi binafsi yake ndiyo kayapenyeza kwa Wananchi ili Apate Huruma zao kisha akifanikiwa anakula peke yake huku akiuza Vitalu kurejesha pesa zake aliyotumia kwenye Ligi yake na Mhongo. Mengi mwenyewe si Mtu Saafi hafai kuwanyooshea watu Vidole kwani amejaa Dhambi Nyingi hakuna Mfano, Mojawapo ni Hii ya kugawana Pesa na Rostam baada ya kuuza hisa zake Voda kwa dola milion 300 kisha akahamia Dubai Nchi pasipo kulipa Kodi huku Mengi akimsadia baada ya kumaliza Ugonvi wao,ingine Mengi aliwahi kukopa Mabilioni NBC bank kisha akachoma nyaraka na kupoteza Ushahidi, Bank inayumba hadi ikaja kuokolewa na Uwekezaji, Mengi huwa si mlipaji Kodi mzuri hata akilipa huwa halipi Kodi Stahiki ni mjanja Mjanja fulani hivi.wafanyakazi wake huwa Anawaibia kwa kuwalipa mishahara Mibovu huku akitumia Mabilioni kwenye Ligi zake binafsi, Nchi Hii hakuna aliye msaafi kiasi cha kumnyooshea mwenzake kidole.

Dah. mengi amefisadi sana nchi
 
Baba na muasisi wa sakata hili ni Nimrod Mkono baada ya ulaji wake uliokuwa unatokana na ugomvi wa IPTL na TANESCO kusitishwa na akina Muhongo/Maswe/Jaji Werema.

Mkono alilipeleka sakata hili kwa mara ya kwanza kwa Richard Mgamba( naye wa Mara huyu) wa The Citizen. Kisha akampatia Zitto naye akampasia kafulila ili penati ikipigwa Zitto awe golini pale PAC!
Bila kumsahau Sendeka na Filoponjombe na wenzao
 
Ni kweli Mengi na Muhongo inaonekana wana ugomvi wao binafsi ila pamoja na ugomvi huo, alichofanya Mengi ni ku-take advantage tu ya makosa ya Muhongo kummaliza.Hii maana yake ni kwamba,Muhongo bado ana makosa yake mwenyewe na Mengi hahusiki na makosa hayo hivyo wa kulaumiwa hapa ni Muhongo mwenyewe na wala si Mengi.

Alichofanya Mengi ni sawa na kinachofanywa na vyama vya upinzani nchini ku-take advantage ya makosa ya CCM kuimaliza kisiasa kama jinsi UKAWA walivyo-take advantage ya sakata la Escrow kuimaliza CCM katika uchaguzi wa serikali za mitaa hivi karibuni.

Kwa maana hiyo,kama ambavyo CCM hawawezi kuilaumu UKAWA kwa makosa yao wenyewe,vivyo hivyo,Muhongo hawezi kumlaumu Mengi kwa makosa yake mwenyewe.

Swali la msingi hapa;je Muhongo hakutena makosa hayo au alitenda na kama alitenda, Mengi anaingiaje hapo?

Na kama Mengi anashabikia makosa ya Muhongo; je ana tofauti gani na sisi wengine tunaofanya hivyo?

Kwahiyo kwa Kikwete kuendelea kumlinda Muhongo, maana yake ni kuihujumu CCM na wala si kumkomoa Mengi kama inavyofikirika na wengi.

Tatizo kubwa ni Mengi kukomaa na Mhongo peke yake wakati hili sakata linawagusa watu kibao akiwemo hata huyo Mkono ambaye ndiye alinyetisha Umbea baada ya kunyang'anywa tonge, hili ngoma si ya Mhongo peke yake ndiyo maana watu wajanja wamemshitukia Mengi mapema baada ya kugundua ana Chuki binafsi baada ya kunyimwa Vitalu vya Gesi.
 
Naona unahukumu bila uhakika.

Makosa ya kuhukumu bila kuwa na uhakika ndiyo ambayo Kikwete hayafanyi na kasema wazi juzi, bado anachunguza kuhusu Mhongo ili aweze kufanya maamuzi.

Ni nini usichokielewa?
Nikuwekee picha kama zilivyonaswa cctv za kazini za wale waliobeba pesa kwenye viroba na sandarusi?Kikwete hata kuomba hii hapa bank hawezi?ccm mna moyo
 
Hivi kila mtu anadai Mengi kamwaga mamilioni kwa wabunge ili ammalize muhongo.lakini hakuna hata mchangiaji mmoja aliyetoa ushahidi wowote mpaka sasa.naendelea kuamini ni porojo tu za kisiasa.
JAMANI TUNATAKA USHAHIDI WA MENGI KUMWAGA HELA
 
Nikuwekee picha kama zilivyonaswa cctv za kazini za wale waliobeba pesa kwenye viroba na sandarusi?Kikwete hata kuomba hii hapa bank hawezi?ccm mna moyo

Mkuu hizo picha si uzitupie tu kieleweke.
 
Baba na muasisi wa sakata hili ni Nimrod Mkono baada ya ulaji wake uliokuwa unatokana na ugomvi wa IPTL na TANESCO kusitishwa na akina Muhongo/Maswe/Jaji Werema.

Mkono alilipeleka sakata hili kwa mara ya kwanza kwa Richard Mgamba( naye wa Mara huyu) wa The Citizen. Kisha akampatia Zitto naye akampasia kafulila ili penati ikipigwa Zitto awe golini pale PAC!
Hasira ya Mkono imetusaidia kujua huu oavu na huenda ulikuwa ni mpango wa mungu ili umma ujue uhuni wa hii serikali ya CCM.
 
Hivi kila mtu anadai Mengi kamwaga mamilioni kwa wabunge ili ammalize muhongo.lakini hakuna hata mchangiaji mmoja aliyetoa ushahidi wowote mpaka sasa.naendelea kuamini ni porojo tu za kisiasa.
JAMANI TUNATAKA USHAHIDI WA MENGI KUMWAGA HELA

Mengi ana kamati za Ufundi lufufu nani ataweza kwenda kutoa Ushahidi live? Kumbuka Mengi anapenda ligi hana kazi ya kufanya zaidi ya ligi kwani pesa alizopewa na Rostam ni nyingi sana, watu wana majukuumu yao hawana mda wa kupeleka Ushahidi kwa Mengi kwani wanamjua ni Mzee wa fitna wanaweza kupotezwa, Lakini kama Mengi anaingia JF nina imani sasa amepata Somo kubwa sana.
 
Bado unaendeleza tetesi ushahidi hujawekwa hapa
 
Hii nchi hatuwezi kuendelea ku-entertain watu wanaojiliza liza kila siku wakitaka waonekane innocent wakati ni madalali ya kimataifa yaliyokubuhu katika nyanja za kidalali! Hivi wewe ni mtu gani unayegombana na watu kadhaa... wanasiasa na wafanyabiashara wenzako halafu kila siku unajificha kwenye kiota cha uzalendo na kwamba wengine wote unaogombana nao ndio mafisadi.

Ikiwa Muhongo ni dalali basi hakuna shaka yoyote kwamba Mengi ni dalali la kimataifa lililokubuhu huku kila siku likiendelea kutumia akili za mazuzu!! Kwa unafiki, anaongoza... juzi juzi tu hapa wakati TCRA wanazima mitambo ya analogy Mengi akasimama kidete eti akijifanya kutetea wananchi kwamba watanyimwa uhuru wao wa kupata habari kumbe uongo mtupu... alikuwa anataka zoezi licheleweshwe hadi ving'amuzi vya Digitek viingie sokoni!

Big up Professor Mkoma kwa kutoyumbishwa na hawa wabinafsi wanaojificha kwenye kivuli cha uzalendo.
Mengi kama lilivyo jina lake ana Madhambi Mengi hakuna Mfano,!Mengi ni Shiiiiiiiiiiiiiii...da
 
Back
Top Bottom