Kikwete awateua Prof. Sospeter Muhongo, Janet Mbene na James Mbatia kuwa wabunge

Kweli JF ni kiboko,

Hizi tetesi za Mbatia kulipwa fadhila ya ubunge zimefika humu zaidi ya mwaka. Huyu mbatia ni sumu kwa upinzani zaidi ya mrema watch out kambi ya upinzani 2015 haipo mbali. It's a strategic move
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amefanya uteuzi wa wabunge watatu wapya kwa mujibu wa mamlaka ya uteuzi aliyo nayo chini ya Ibara ya 66(i) (e) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Wabunge hao wapya ni Profesa Sospeter Muhongo, Bi. Janet Mbene na Bwana James Mbatia.

Uteuzi huo unaanza mara moja.

Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
Dar es Salaam.

3 Mei, 2012

Thanks invisible. Lakini mkuu naomba nisaidie kufuta ujinga, Rais anaweza kumteua mbunge wa kuteuliwa kuwa waziri? Ni kwanini amemchagua James Mbatia au hao wengine kuwa wabunge? Au ndio plan ya ku-hit back baada ya watu kijaribu kuitisha kura ya kutokuwa na imani? Hiki kipengele cha katiba kinachompa rais madaraka ya kuteua wabunge kidogo kinanitia kizunguzungu.
 
Ni kweli Mkuu cheki hii
Sospeter Muhongo

Full Professor of Geology, University of Dar Es Salaam
Editor-in-Chief, Journal of African Earth Sciences, Elsevier
Vice President, Commission for the Geological Map of the World
Honorary Fellow, Geological Society of London
Honorary Research Fellow, Chinese Academy of Geological Sciences

Prof Dr Sospeter M. Muhongo

FGSAf, FAAS, FASSAf, FGIGE, FASI, FTWAS, HonFCAGS, HonFGS, CGeol, EurGeol.
(Officier,Ordre des Palmes Académiques)

Yaani tayari mmeshashoboka na hiyo resume?

Uwezo wake wa kuongoza je?
 
hapo keshafunga ndoa na NCCR as well, CDM watabaki wenyewe aisee

tactic ya ccm nzuri sana, kwenye serikali zao wana cuf, sasa wanachukua na nccr hivi huoni hapo kua ccm inaunganisha vyama ili viweze kushindana na chadema? yani hapa naona kama vile ccm ni upinzani na chadema ndio wenye power

Majority yote ya wabunge wa ccm watajisikiaje wakiona kua bwana mkubwa kachukua mtu upinzani na wao wapo...ina maana ana wadharau na kuona wao hawana ujuzi wa kuongoza wizara?? kaaaziiii ipoooo hapoooo
 
Invicible tell me you are kidding of all the wabunge we have kaona hakuna anayefaa mpaka kucreate hawa ili awachomeke kwenye baraza jipya!
Je inaruhusiwa mbunge mteule kuwa waziri si mpaka aapishwe jamani
Khaaaaaaaaaaaa JK ana washauri kweli
 
Sasa hao wanachukua nafasi za wabunge gani?
wamachukua nafasi za wabunge wa kuteuliwa na rais ambao huwa 10. Na katika teuzi zake huko nyuma sidhani hata kama tano zilifika, hivyo bado ana nafasi zake za kistratejia. Ukiona hivyo Mbatia atakuwa amekubali kuwa waziri. Nadhdni CDM wamemgomea kaamua kwenda kwa jamaa ili 2015 wapate fine line kuwa hata wapinzani wakishinda hakuna jipya maana tayari walikuwa sehemu ya serikali, kuanzia Zanzibar mpaka bara. Ila Ubunge wa kuteuliwa maana yake upo responsible kwa mteuzi.

Hongereni sana mlioteuliwa na rais. Rais kaonesha imani kwenu msimuangushe, mfanye anayoyataka.
 
Tatizo ubunge ni FUNCTION na sio Profession, mtu aweza kuwa na elimu lakini asilisaidie Taifa!!
 
Ndoa ya NCCR-MAGEUZI na CCM~~~~kuna lengo la kudhoofisha CHADEMA nini?
 
Ni kweli Mkuu cheki hii
Sospeter Muhongo

Full Professor of Geology, University of Dar Es Salaam
Editor-in-Chief, Journal of African Earth Sciences, Elsevier
Vice President, Commission for the Geological Map of the World
Honorary Fellow, Geological Society of London
Honorary Research Fellow, Chinese Academy of Geological Sciences

Prof Dr Sospeter M. Muhongo

FGSAf, FAAS, FASSAf, FGIGE, FASI, FTWAS, HonFCAGS, HonFGS, CGeol, EurGeol.

(Officier,Ordre des Palmes Académiques)
Hakuna chochote hapo! ukishajiunga na serikali ya ccm akili zako zote unaziacha kabatini na kuazima akili za Lusinde au
konda wa daladala.
 
Prof. Mulongo ataukwaa uwaziri wakati Bi. Janet ataukwaa unaibu waziri . Mbatia ni gamba tu lililoongezwa bungeni.
 
sasa nimejua kuwa NCCR, NA CUF NI KAKA NA DADA HATA WAKIGOMBANA KUNA SIKU WANAKUTA KWA BABA YAO CCM. HII NDO SABABU ILIYOWAFANYA CHADEMA KUKATAA KUUNGANA NA VYAMA VINGINE KWENYE KAMBI RASMI MBUNGENI.SASA CHAMA CHA UPINZANIA TANZANIA NI NI CHADEMA . PEOPLEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEE.....POWER
 
Katika kumteua Mbatia, sina shaka yoyote kwamba JK anawajenga Watanzania na wanasiasa kisaikolojia! Nina mashaka kama ana shida sana na Mbatia lakini ninaamini anamtamani Zitto Kabwe na Lipumba!! Hawa jamaa, (Zitto na Lipumba) wanaweza kuweka ukaidi kukubali uteuzi wa Rais kwa sasa...ama uikaidi wa kweli au ukaidi wa kuona soo kwamba wanausaliti upinzani au wapo kimaslahi zaidi!

Katika kumteua Mbatia, ni katika kuwaandaa wale anaowataka waone ni jambo la kawaida tu....mbona Mbatia alimteua, watu wakasema sana lakini maisha yakaendelea!! Hivyo, sitashangaa sooner or later nikiwaona Lipumba na Zitto kundini!

In short, James Mbatia ni chambo tu!!
 
Muhongo na Mbene wako vizuri sana, Mbatia ni nadharia zaidi

Shida yangu ni "system" na uwezo wa hao akina muhongo kuongoza.... LEADING AND MANAGING NI ZAIDI YA CREDITS ZA MWALIMU KWENYE MTIHANI

Inaweza kuwanyima nafasi ya kufanya kazi.... labda yule mpare "katibu kiongozi" aamue kuwa mkali na kuwapa ruhusa watu wawe wakali.... which i am yet to see so far
 
wamachukua nafasi za wabunge wa kuteuliwa na rais ambao huwa 10. Na katika teuzi zake huko nyuma sidhani hata kama tano zilifika, hivyo bado ana nafasi zake za kistratejia. Ukiona hivyo Mbatia atakuwa amekubali kuwa waziri. Nadhdni CDM wamemgomea kaamua kwenda kwa jamaa ili 2015 wapate fine line kuwa hata wapinzani wakishinda hakuna jipya maana tayari walikuwa sehemu ya serikali, kuanzia Zanzibar mpaka bara. Ila Ubunge wa kuteuliwa maana yake upo responsible kwa mteuzi.

Hongereni sana mlioteuliwa na rais. Rais kaonesha imani kwenu msimuangushe, mfanye anayoyataka.

Duh!

Mimi ningependa kujua kabla ya hawa watatu raisi alikuwa keshateua wangapi kwenye bunge la sasa.
 
Yaani tayari mmeshashoboka na hiyo resume?

Uwezo wake wa kuongoza je?

Ndio maana nikasema huko juu kwamba uongozi ni Function na sio Profession, mtu aweza kuwa na elimu lakini asilisaidie Taifa....

BTW, namfahamu sana! Sidhani kama ni kiongozi mzuri!
 
Back
Top Bottom