Kikwete awateua Prof. Sospeter Muhongo, Janet Mbene na James Mbatia kuwa wabunge

Mara baada ya kukiua kile chama kilichokua maarufu sana kule visiwani Zanzibar, CUF, sasa Mhe Kikwete kaonelea hata Bara CCM hakifi peke yake hivihivi. NCCR Mageuzi kwishney!!!

Chama hiki cha NCCR Mageuzi sasa kimerudi RASMI nyumbani kwa baba yake CCM kwenda kugawana mabua dam dam.

Sasa tunasubiri kuona udhati wa kile alichokua akikiping David Kafulila je ataendelea kushiriki na Mhe Mbatia kula vya UKIBARAKA KWA CCM au sasa ataachia ngazi kulinda heshima na msimamo wake hapo nyuma kidogo?
What? Mbatia?....kweli nimeamini Mbatia na NCCR yake ni kibaraka wa ccm
Na sasa naamini CDM ndicho chama cha upinzani wa kweli Tanzania. Kazi ipo!
 
ndugu invisible mbona nimepitia kule ikulu mawasiliano sijaona hii kitu?
 
Dah!nimesikia sasahivi breaking newz kupitia clouds fm.mbatia ndani ya mjengo COMFIRMED.
 
Thanks invisible. Lakini mkuu naomba nisaidie kufuta ujinga, Rais anaweza kumteua mbunge wa kuteuliwa kuwa waziri? Ni kwanini amemchagua James Mbatia au hao wengine kuwa wabunge? Au ndio plan ya ku-hit back baada ya watu kijaribu kuitisha kura ya kutokuwa na imani? Hiki kipengele cha katiba kinachompa rais madaraka ya kuteua wabunge kidogo kinanitia kizunguzungu.
Shamsi Vuai Nahodha ni mbunge wa kuteuliwa na ni Waziri wa Mambo ya Ndani.
Labda swali lije kua mambo ya kusema "uteuzi unaanza Mara moja" inamaanisha hakutakua na kusubiri kuapishana mwezi juni???
Ina maana wanaweza kua mawaziri now??
 
Ilishasemwa kwamba Mbatia anatumiwa na CCM akabisha. Hata Halima Mdee alipoiweka hii kitu wazi kwenye kampeni Kawe akaenda mahakamani. Leo hii, kweli Mungu hamfichi mnafiki.
 
Yaani tayari mmeshashoboka na hiyo resume?

Uwezo wake wa kuongoza je?
Hapo sasa....mi nawaanagalia tu watu wanavyoshoboka na huu uteuzi wa hawa majamaa.
Huwezi kuwa ndani ya serikali ya ccm alafu utegemee utakuwa na meno au sauti! BIG NOOO!
 
Hivi huyu jk mbona ni waajabu sana yaani muda umeisha ndo anawateua alikuwa wapi, nadhani ni kama alivyofanya kwa jusa kumteua akakaa bungeni mwaka 1 tu!. Hii siyo sawa.
 
baada ya kuvunja baraza la mawaziri ana zidi kuongeza idadi ya wachukua posho,jamani tuo neeni huruma sisi maskini
Hao ndio wako baraza jipya la mawaziri.
 
Sasa hawa wana chukuwa nafasi za kina nani ? Mnajaza wa bunge tu . Mmh haya bna tz.dot.com hi kila kitu shaghalabagala.
 
Wanaweza kuwa mawaziri kabla ya kuapishwa kuwa wabunge?

Hivi kuapa ni lazima uape Bungeni au kwa Spika?

Na je, wakiteuliwa lazima waanze kuwajibika hapo hapo?

Je Bunge la Zito la Dharura litakuwepo?
 
Ni ujuha kuamini kuwa Kikwete kumteua mpinzani kwenye serikali yake. But kama ni hovo basi tukubali kuwa CCM sasa ni tambara ambalo kikwete anajaribu kuliziba viraka kws kitambaa cha dukani. Hatari sana kwa wapenda nguo za kijani.
 
JK ameamua ku-balance dini baada ya kupigiwa sana kelele kutokana na uteuzi wake wa mara ya kwanza ambapo aliteua Waislam tupu ktk wale wabunge wa kuteuliwa na rais. Taratibu tutafika tu!
 
Why siku zinavyokwenda wasomi wengi ( Ma dr na maprof) wanakimbilia au wanachomekwa kwenye Politics?

Nyani Ngabu said:
Duh!

Mimi ningependa kujua kabla ya hawa watatu raisi alikuwa keshateua wangapi kwenye bunge la sasa.

SIna uhakika sana lakini nadhani katika viti maalum vya ubunge 10 vya rais alishateua 7. Hao watatu ndio kamalizia
 
Back
Top Bottom