Rais Samia awateua Lukuvi, Bulembo, Balozi Luhwavi na Omar Kheir kuwa Washauri wa Rais Siasa na Uhusiano wa Jamii

benzemah

JF-Expert Member
Nov 19, 2014
1,504
3,034
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi Washauri wa Rais wafuatao:-

(i) Amemteua Mhe. William Vangimembe Lukuvi (Mb.) kuwa Mshauri wa Rais (Siasa na Uhusiano wa Jami). Mhe. Lukuvi ni Mbunge wa Jimbo la Ismani, Iringa;

(ii) Amemteua Bw. Abdallah Bulembo kuwa Mshauri wa Rais (Siasa na Uhusiano wa Jamii). Bw. Bulembo ni Mbunge Mstaafu;

(in) Amemteua Balozi Rajab Omar Luhwavi kuwa Mshauri wa Rais (Siasa na Uhusiano wa Jami). Balozi Luhwavi alikuwa Balozi wa Tanzania nchini Msumbiji; na

(iv) Amemteua Bw. Haji Omar Kheir kuwa Mshauri wa Rais (Siasa na Uhusiano wa Jamii). Bw. Kheir ni Mjumbe wa Baraza la Wawakilishi na Waziri Mstaafu wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.

Fyhb_cVWIBwRNbp.jpeg
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi Washauri wa Rais wafuatao:-
(i) Amemteua Mhe. William Vangimembe Lukuvi (Mb.) kuwa Mshauri wa Rais (Siasa na Uhusiano wa Jami). Mhe. Lukuvi ni Mbunge wa Jimbo la Ismani, Iringa;

(ii) Amemteua Bw. Abdallah Bulembo kuwa Mshauri wa Rais (Siasa na Uhusiano wa Jamii). Bw. Bulembo ni Mbunge Mstaafu;

(in) Amemteua Balozi Rajab Omar Luhwavi kuwa Mshauri wa Rais (Siasa na Uhusiano wa Jami). Balozi Luhwavi alikuwa Balozi wa Tanzania nchini Msumbiji; na

(iv) Amemteua Bw. Haji Omar Kheir kuwa Mshauri wa Rais (Siasa na Uhusiano wa Jamii). Bw. Kheir ni Mjumbe wa Baraza la Wawakilishi na Waziri Mstaafu wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.

View attachment 2656461
Jamni mhe. Hivi kila siku tunakutetea hadi tunatukwanwa uoni hata kutupa ukatibu tarafa..
Jamani hii sio fear kabisa..
 
Sawa kamchomekea Mzee Lukuvi, ila tunajuaaaa kamchomekea Kwa makusudi na Wala hampendi.



Siku akijifunza Kusimama kwenye haki, Akaachana na Uswahili ,na Uislam, atafaa japo ameshachelewa.




Nimshauri tu, aondoe wazi la kugombea.



Hivi kweli BULEMBO naye, ni wa kua mshauri wa Rais?? Huyu BULEMBO huyu jambazi la Mali za CCM?? .


Alafu hapo Rais anajiona salama?.


Mnajua Pengine, Rais Wetu Kawa blackmailed ila sisi hatujui , hivi ni Akili yake kabisa???.
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi Washauri wa Rais wafuatao:-

(i) Amemteua Mhe. William Vangimembe Lukuvi (Mb.) kuwa Mshauri wa Rais (Siasa na Uhusiano wa Jami). Mhe. Lukuvi ni Mbunge wa Jimbo la Ismani, Iringa;

(ii) Amemteua Bw. Abdallah Bulembo kuwa Mshauri wa Rais (Siasa na Uhusiano wa Jamii). Bw. Bulembo ni Mbunge Mstaafu;

(in) Amemteua Balozi Rajab Omar Luhwavi kuwa Mshauri wa Rais (Siasa na Uhusiano wa Jami). Balozi Luhwavi alikuwa Balozi wa Tanzania nchini Msumbiji; na

(iv) Amemteua Bw. Haji Omar Kheir kuwa Mshauri wa Rais (Siasa na Uhusiano wa Jamii). Bw. Kheir ni Mjumbe wa Baraza la Wawakilishi na Waziri Mstaafu wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.

View attachment 2656461
Hee!! Kabudi kaachwa au katenguliwa? maana alipowapiga chini uwaziri, kabudi na Lukuvi alitangaza kuwa ni washauri wake.
Ndugu yangu Ambr.Dr.Bashiru Kakurwa vep..
 
𝗗𝗥. 𝗦𝗟𝗔𝗔; 𝗠𝗞𝗔𝗧𝗔𝗕𝗔 𝗪𝗔 𝗕𝗔𝗡𝗗𝗔𝗥𝗜 𝗡𝗔 𝗗𝗣𝗪 𝗬𝗔 𝗗𝗨𝗕𝗔𝗜 𝗡𝗜 𝗨𝗨𝗭𝗔𝗝𝗜 𝗪𝗔 𝗡𝗖𝗛𝗜.

𝗡𝗔 𝗠𝗱𝘂𝗱𝗲 𝗡𝘆𝗮𝗴𝗮𝗹𝗶.

Akiongea na waandishi wa habari kuhusu sakata la bandari leo 13th June 2023 Dr. Slaa amesema kuwa mkataba huo ni uuzaji wa nchi kwenye kipindi ambacho serikali iliyopo madarakani ina uhalali wa wasiwasi kutokana na uchaguzi mkuu kuvurugwa mwaka 2019 na mwaka 2020.

Dkt. Slaa anaendelea kusema kwamba kabla ya bunge kufikia hatua ya kuridhia azimio hilo la kubinafsisha bandari, makubaliano ya awali yalifanyika tarehe 28 February 2023. Kwamba kampuni ya DP World kutoka Dubai na mamlaka ya bandari TPA waliingia kwenye makubaliano yalitokana na shughuli iliyofanyika Dubai expo 2022. Lakini hatujaambiwa ni tathmini gani au utafiti gani ulifanyika mpaka makubaliano hayo yanafanyika.

Anaendelea kusema kwamba, kwenye expo, kwenye maonesho kama yale ya sabasaba Dar es Salaam watu wanaingia kwenye mkataba mkubwa wa kulifunga Taifa, huku akisisitiza kwamba watanzania wanaelewa maana ya kufunga taifa.

Dr.Slaa anadai kwamba hadi wakati huu Taifa na watanzania walikuwa hawajapewa taarifa yoyote ile inayohusu mkataba mkubwa unaohusu bandari zao. "Kwamba ziara ya maonesho Dubai 2022 Serikali ya Tanzania iliwakilishwa na Rais mwenyewe kulisainiwa mikataba 17, nani kati yenu hadi leo hii anaifahamu mikataba 17 inahusu nini? Aliuza Dr. Slaa na kuongezea kwamba mikataba hiyo ni usiri mtupu, ni nchi inaingizwa kwenye giza, Rais wa Nchi amehudhuria lakini mambo hayo yote yako ndani ya giza.

Dr. Slaa anaendelea kwa kusema waliohudhuria maonesho huko Dubai ni viongozi wa Serikali, wamesafiri, wamelala hoteli, wamekula chakula kwa kodi ya watanzania na bado yakafanyika mambo ya ajabu ya kulijuhumu taifa. Kwamba ni Tanzania pekee ambako Serikali haiwajibiki kwa wananchi wake, jambo ambalo katika hatua hii tunapaswa kupata katiba mpya na bora kabla ya uchaguzi ujao.

Kwamba hata hii taarifa tunayozungumzia hatukuipata Serikalini, bali tumepata taarifa iliyovujishwa na msamalia mwema huko serikali. Ni nchi gani duniani tunasubiri taarifa ivuje tuanze kuizungumzia na kuichambua? Anauliza Dr. Slaa. Anadai kwamba siku siku 30 zilizotajwa kwenye mkataba na Bunge, kwa maneno mengine umeridhiwa ndani ya siku 30 lakini umekuja kuridhiwa baada ya miezi takribani 8. Kwa hali hiyo tuna uhakika gani Tanzania ina uwezo wa kutimiza mkataba huu kama mwanzo tayari ni mbaya na hakuna anayeeleza uchelewashaji huo unatokana na nini? Anauliza Dr. Slaa.

Katika mkutano huo na waandishi wa habari Dr. Slaa ameweka hoja 10 zinazoweza kupelekea mapungufu ya mkataba huo.

1. - Dkt. Slaa anadai nchi inayojulikana kisheria ni United Arab Emirates, Je Dubai ni Serikali? Dubai ni mji unaojiongoza, sisi ni nchi ya Jamhuri ambayo maamuzi yetu yanafanyika kwa kutumia Bunge. Bunge lilitangaza wanataka maoni ya wananchi tarehe 5 Juni wanaotoka maeneo mbalimbali wawe wamefika bungeni tarehe 6. Kwa saa 24 mtanzania gani anafika Dodoma na kutoa maoni yake. Ni dhahiri kuliwa na hila na Serikali haikuwa na nia ya kushirikisha wananchi wake. Hatukushirikishwa na imepelekwa bungeni na mjadala ulivyokuwa bungeni ulikuwa ni mjadala wa kimagumashi.

2. Dr. Slaa anasema ikumbukwe Serikali iliyopo ina legitimacy ya wasiwasi kutokana na uchaguzi wa 2019 na 2020. Anadai kwenye hilo hamung'unyi maneno, uchaguzi wa 2019 na 2020 inaweza kuwa na legitimacy lakini sina hakika kama uchaguzi huo ulikuwa sahihi, najua ulivurugwa kwa makusudi na chama cha mapinduzi na vyombo vyake. Mwenye macho haitaji kuambiwa kuhusu hilo na wananchi wote ni mashahidi. Hivyo kuingia mkataba wa namna hii kunaongeza wasiwasi kwa wananchi ambao ndio wenye nchi.

3. Kwa mujibu wa kifunge cha nne cha IGA kinatamka wazi rasilimali zote zilizotajwa zinakabidhiwa kwa Serikali ya kigeni. Rasilimali hizo ni bandari zote za nchi nzima(bahari, maziwa, mito, zitakazokuwepo hata kwenye mabwawa) yale yote yaliyokuwepo leo na hata yatakayokuja. Huu ni uuzaji wa nchi, hakuna mwenye Tanzania mwenye akili atakaekubali jambo hilo la kuuza rasilimali za nchi.

4. Dr. Slaa anadai wakati wa Serikali ya awamu ya nne walivujishiwa taarifa kwamba serikali inataka kutaifisha mashirika muhimu ikiwemo bandari. Kwamba aliyetoa taarifa hiyo alifukuzwa kazi lakini pamoja na kufukuzwa kazi alisisitiza tusimamie na kutokubali kuyataifisha kutokana umuhimu wake kwa usalama wa Taifa. Dr. Slaa ameongelea mfano wa mbia katika kampuni ya mafuta wakati wa vita ya Uganda ambapo Tanzania ilikuwa inamiliki 51% katika kampuni hiyo huku mbia akiwa na 49% lakini mbia aliweka ngumu kwasababu alidai mtu tunayepigana nae ni mbia wake pia kitu kilichopelekea kwa siku 5 vifaa havikuweza kuondoka kwenda kwenye uwanja wa vita kwasababu ya mafuta huku nchi inaendelea kupigwa na adui.

5. Dr. Slaa pia ametoa mfano wa 'Entebbe Raid' ambapo amesema ndege ya Air France ilitekwa nyara na wapiganaji wa Palastine wakishinikiza mambo yao ya kisiasa. Ndani ya ndege hiyo kulikuwa na waisraiel na ilitua uwanja wa Entebbe Uganda. Dr. Slaa amedai iliwezekana Waisrael kuchukua chini ya dakika 90 kuwakomboa watu wao kwa sababu wao ndio waliojenga uwanja huo wa Intebbe na ramani zote walikuwa nazo ikiwepo sehemu ya kuingilia na kutokea. Kwamba hali ya usalama wa nchi yetu itakuwaje iwapo watu wa nchi nyingine waendeshe bandari zetu? Anauliza Dr. Slaa.

6. Dr. Slaa ameendelea kusema sababu hapo juu pia ilisababisha Serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Magufuli itumie wajenzi wa ndani kujenga Ikulu ya Chamwino lakini sasa bandari zote zinakabidhiwa kwa mgeni sasa usalama wa nchi unakuwaje? Anaendelea kuhoji Dr. Slaa.

7. Dr. Slaa anadai mkataba unaotoa 'exclusive rights' daima uogope sana, inatoa pia kifungu baadae yatakayojadiliwa kwenye mikataba midogo midogo, unatoa kwanza mali yako. "Unajuaje wakifika kwenye hiyo mikataba midogo midogo wakikutalia! Una nguvu gani? ulishasain 'exclusive rights" anahoji dr. Slaa.

8. Dr. Slaa anaendelea kusema utekelezaji wa DP World sio kwamba unaanza Tanzania, bali katika Afrika peke yake tuna migogoro mingi. Nenda nchi za Ulaya, Brussels ni ya Ulaya kesi iko wako mahakaman. Anadai kwamba karibu kote kunakogombaniwa na DP World ni rushwa. Dr. Slaa anadai kwamba kuna wabungwe walipelekwa Dubai, wakalishwa, wakapewa posho ya dola 20000 yote hiyo ni rushwa. Kama ingekuwa nchi nyingine, hizo zinatosha kufuta mkataba huu na kapeleka hata hiyo kampuni mahakamani.

9. Dr. Slaa anadai hajawahi kuona mkataba(IGA) Marekani na Ulaya amabo una lugha kama hii ya kwetu. Kwamba waathirika tumewaandaaje mfano ujenzi wa reli bandarini mpaka airport. Tumeona barabara ya Kibaha watu walivyolia Kimara. Mikataba hii lazima iwe ya tahadhari sana. Amesema Dr. Slaa.

10. Dr. Slaa amemalizia kwa kusema kwamba, Tunayasema haya kwa nia njema lakini tunashangazwa na kutishwa na propaganda ambayo Serikali inafanya. Dr.Slaa anadai kwamba Jambo jema huwa haliendeshwi kwa propaganda, ukiona mtu anafanya propaganda ikiwa ni pamoja na kwenda kwenye madhehebu ya dini anza kuweka mashaka, kuna maslahi gani nyuma ya makubaliano hayo.

Mwisho mpeni maua yake mzee.
 
3:1

Aisee!. Lukuvi kawekwa kama Geresha tu. Ndiyo maana nafasi yake na Bulembo zinafanana.

Ukweli ni kuwa Uislamu umetamalaki. Tunatunza hizi posts, 2030 akiingia Mgalatia tusisikie midomo ya Wavaa Makobazi.
 
Back
Top Bottom