Kikwete anasubiri nini kumfukuza kazi Ngeleja?

Sinza yetu wameifanya Shamba la Bibi... umeme unawaka masaa 5 hadi 8 tu... Ahadi ya Kikwete kuhusu mgao imeota MBAWA...
 
wakuu mbona sipaelewi hapa? kwani siku ina masaa mangapi mpaka mgao uwe wa msaa 24 kwa siku?? huo mgao ukoje vile? mie natumia solar siku nyingi.
 
Wakuu hii nchi kwakweli sielewi tunakoelekea kuna mgao wa umeme unaoendelea kwa saa 24 kila siku huku mikoani ambao hauko katika ratiba iliyotolewa magazetini wiki hii umeme unakatwa saa 12 jioni na haurudi hadi kesho yake saa 12 jioni na hapo kesho yake asubuhi unakatwa tena huku tunaelekea wapi jamani naona maisha sasa ni magumu ajabu nilipita mtaani kazi zote zimesimama vijana wamekaa wanatazamana hali ikiendelea hivi vijana hawa ambao kazi zao zimechukuliwa na mgao wa umeme wataamua kufanya kazi usiku ya kutukaba na kuvunja vijumba vyetu amani itatoweka kabisa muda si mrefu hakuna tena usalama na ukizingatia usiku mzima giza mgao huu utaongeza pia mimba zisizotarajiwa na kuongeza idadi ya watu katika familia ambao ni mzigo na kuzidisha umasikini kwakuwa sasa usiku klwakuwa hakuna umeme itakuwa full mchezo wa baba na mama!!serikali mpoo kuna janga kubwa mbele yetu!
Angalau mtafanya kweli kwenye sanduku la kura!
 
Huooooooooo!!!! Ndio makelele nimeyasikia mtaani kwetu just now baada ya Tanesco kuturudishia umeme waliotukatia toka juzi!!
 
na majuzi nasikia Ngeleja katinga Club saa 9 alfajiri akiwa na Aunt Ezekiel na walivyokuwa ni kama vile wametoka kutoomba na katika hali hii unafikiri waziri anaumiza kichwa kuhusu mgao?
 
yaani mimi nimeamka asubuhi umeme upo nina kikazi cha mtu nafungua laptop kuweka charger ya laptop haiwaki nikaanza kuhangaika kuhamisha hamisha kwenye socket zingine hola! Kumbe mimi sijui wameshalamba umeme wao muda mwingi!

Kama hatutaandamana kwa hili basi hakuna maandamano tena nchi hii yatakayokuwa na tija!

Mimi nashauri CDM waachane na vikao vya bunge watuambie tufanye nini katika hili... It is too much na kinachoudhi zaidi Tanesco na serikali yake wanadhubutu kutudanganya sisi kama watoto wao! Kwanini hawakusema ukweli toka mwanzo? Hawa watu ni wabaya sana wanaweza kutumaliza maana wanaajenda zao za siri ambazo sisi wananchi tunafichwa. Mpka leo hakuna statement ya maana iliyotolewa zaidi ya ubabaishaji wa mhando tena baada ya kutafutwa na chombo cha habari!

CDM tafadhari nyinyi ndo serikali ya wananchi hebu toeni maelekezo nini wananchi tufanye. Sioni hata faida ya kuwa bungeni wakati huu. Matatizo haya hayatapa majibu hapo bungeni hata siku moja. Jawabu liko kwa wananchi!
 
Jaman mgao wa sasa n mkal kuliko hata ule ulioisha mwez ulopita, mfano mwanza mgao n karibu kila siku asubuh mpaka jion na usiku.
 
Halafu chakushangaza leo asubuhi kwenye kipindi cha nipashe redio 1 Tanesco wametangaza kua kufuatia mgao wa umeme nchi nzima kuna kijiji kimoja kule Tanga eti watafungiwa umeme wa kudumu na waondokane na kukaaa kwenye giza! Kweli hapa mimi sipati picha.
 
Zenj umeme ukikatika umechelewa sana ni masaa2.......kulinda muungano!!!
 
Bora tukae gizani mwaka mzima mpaka Magogoni ndo tutapata akili wa kutafuta umeme wa maana. hivihivi yataendelea haya haya ya leo!!
 
haya magamba mbona sasa hata hawatuambii tena tatizo la mgawo ni nini?? kwa nini pia wasitoe ratiba?? hivi kweli ngeleja na muhando wanaamka kila siku na wanasema wako kazini? jamani nchi hii lini viongozi watawajibika? magamga oneni aibu hii mtuondolee
 
Hivi Tanzania haturuhusiwi kutumia umeme wa Nyukilia? Au kwetu sie hatuna wataalamu wa kutosha kwenye suala hilo? Na ile Idara ya Fizikia na Kemia pale UDSM kwa miaka 50 wanayojivunia huwa hawafikirii hata siku moja kuhusu Maendeleo ya nchi yetu? Au wanapenda kuandika kwenye mavitabu na kisha kuyaweka Library baadaye wanaitwa Maprofesa wa Fizikia au Kemia.

Nadhani iwepo dhana nzima ya kubadilisha nishati yetu ya sasa hasa, wewe Waziri uliepewa dhamana ya suala la Umeme. Unatakiwa uibadilishe Tanzania.
 
Walisema mgao utakuwa historia, ndiyo historia yenyewe, mgao 48 hours? Nakumbuka miaka ya 96 kule Songea watu walikuwa wanakaa mpaka mwezi mzima bila umeme.
 
Back
Top Bottom