Kikwete anasubiri nini kumfukuza kazi Ngeleja?

Kujiudhuru wadhifa kwa serikali hii sio kitu cha kutarajia, tutarajie maumivu tu kwa kipindi chote cha Kikwete na mtu atakaye mpokea
 
Labda ataambiwa 'ajipime mwenyewe' kwa sababu masuala ya kufukuzana/kuwajibishana katika utawala wetu ni ndoto.
 
Hivi mnataka kusema kwamba ngeleja ndiye sababu ya tatizo la umeme tanzania? Katu siwezi kuamini kitu hicho. Tatizo la umeme Tanzania ni la kimfumo zaidi wa serikali yetu kama serikali na siyo mtu binafsi kama ngeleja, kwa mfumo uliopo kule hata akipelekwa magufuli, au akipelekwa huyo makamba jnr hawawezi kutatua tatizo la umeme tz kama mfumo haujabadilishwa.

Mfumo uliopo serikalini kwetu ni kwamba hakijulikani kipi na kipi ni kipaumbele cha taifa, kwamba hatuwezi kupanga kitu chetu na tukakitekeleza bila msaada wa wafadhili, kwamba tunapanga na kutekeleza miradi ambayo ina faida binafsi ie 10%.

Tunasubiri nchi itufanyie kitu badala ya kufikiri kipi cha kuifanyia nchi, akili zetu kuwazia uchaguzi zaidi badala ya maendeleo ya taifa, wanasiasa kupewa kipaumbele zaidi kuliko wataalam nk.

Sasa katika mfumo huu , ngeleja kama ngeleja atafanya nini kuondoa tatizo la umeme kama serikali kwa ujumla wake haijaona kwamba hicho ni kipaumbele ikatoa fedha za kutosha kutekeleza mipango mizuri ya umeme iliyopo?

Ngeleja anaewza akawa na mipango mizuri tu, lakini fedha atapata wapi kama hakuna kipaumbele kama taifa?
 
Rais awatimue viongozi ambao wamekuwa mzigo
Monday, 30 May 2011 20:34
Mwananchi

jk%20muundo.jpg

Rais Jakaya Mrisho Kikwete

KWA mara nyingine, wito umetolewa kwa Rais Jakaya Kikwete kuwaondoa katika nyadhifa zao, wateule wake wote ambao wamedhihirisha kushindwa kuhimili kasi ya serikali yake katika safari ya kuipeleka nchi yetu katika sayari ya maendeleo. Kwa muda mrefu sasa, taasisi mbalimbali na wananchi kwa jumla wamekuwa wakimwomba Rais awatimue viongozi ambao wamekuwa mzigo kwa nchi yetu kwa kushindwa kutimiza majukumu waliyopewa.

Juzi, Mwenyekiti wa Baraza la Maaskofu wa Kanisa la Mennonite nchini, Askofu Stephen Mang'ana, naye aliongeza sauti yake na kumtaka Rais Kikwete achukue hatua haraka kwa kuwafuta kazi wasaidizi wake ambao wanang'ang'ania madaraka wakati hawana uwezo wa kuongoza, huku mzigo wa lawama akibebeshwa yeye.

Akizungumza jijini Mwanza wakati wa sherehe za kusimikwa Askofu Mteule, Albert Jella Randa kuwa Askofu Mkuu wa Dayosisi ya Mwanza ambazo pia zilihudhuriwa na Rais Kikwete, Askofu Mang'ana alisema kuwa umefika wakati sasa kuwawajibisha viongozi walioteuliwa na Rais katika nafasi nyeti serikalini, lakini utendaji wao umekuwa siyo wa kuridhisha na akamtaka Rais achukue hatua mara moja.

Aliwataka viongozi hao wamwendee Rais na kumwambia kuwa wanajiuzulu kwa sababu madaraka waliyopewa hawayawezi, na kusisitiza kuwa nchi yetu inahitaji viongozi wawajibikaji na walio na uchungu na nchi, sio viongozi wababaishaji wanaomwacha Rais alazimike kushughulikia matatizo madogo madogo.

Kauli hiyo ya Askofu Mang'ana kwa Rais Kikwete ni ya kupongezwa na sisi hatuna jipya la kuongeza isipokuwa kusisitiza kwamba nchi yetu inakwenda mrama kwa sababu ya kutokuwapo viongozi wenye dhamira na uwezo wa kutafuta suluhu ya matatizo lukuki yanayowakabili wananchi.

Kama tulivyosema awali, Askofu Mang'ana siyo kiongozi wa kwanza kuzungumzia suala hilo la viongozi kushindwa kazi na kuendelea kung'ang'ania madarakani. Viongozi wengi, hasa wa kidini, wamekuwa wakipiga kelele na kumtaka Rais Kikwete awaondoe. Hata hivyo, Askofu huyo anastahili pongezi za pekee kwa sababu, kama walivyofanya baadhi ya viongozi wenzake, akiwamo Kardinali Polycarp Pengo, ameonyesha ujasiri kwa kutoa kauli hiyo mbele ya kiongozi huyo wa nchi badala ya kulalamikia uvunguni mwa kitanda.

Tafsiri ya maudhui yaliyobebwa na kauli hiyo ya Askofu Mang'ana na viongozi wenzake waliomtangulia ni kwamba, ingekuwa vyema iwapo Rais Kikwete angetambua kuwa viongozi wengi aliowapa mamlaka mbalimbali hawamsaidii kutekeleza sera za Serikali na ilani ya chama chake katika kuipeleka nchi kule inakopaswa kwenda, hivyo kuona umuhimu wa kuwaondoa na kuteua wenye uwezo na uadilifu wa kufanya kazi kwa ufanisi.

Kwa maneno mengine, ujumbe unaoelekezwa kwa Rais ni kuwa, viongozi wengi aliowateua kushika nafasi nyeti serikalini na katika sekta ya umma hawana uwezo wala moyo wa kutatua matatizo ya wananchi na wanafanya kazi kwa mazoea tu. Pengine ndio maana viongozi hao hawapati ufanisi katika kazi zao, pamoja na Rais kuwapa semina nyingi elekezi tangu aingie madarakani yapata miaka sita iliyopita.

Matokeo yake tunashuhudia kila kukicha ubadhirifu na ufisadi katika halmashauri zetu, kufirisika kwa mashirika na makampuni makubwa ya umma ambayo wakati fulani yalikuwa ndiyo fahari yetu, yakiwamo ATCL, Shirika la Reli, Tanesco, Kampuni ya Posta, UDA na mengine mengi. Lazima tukiri kuwa balaa lote hilo kwa nchi yetu limetokana na viongozi wenye mawazo mufilisi wasiojali uadilifu, isipokuwa kuchumia matumbo yao na familia zao.

Ni imani yetu kuwa ujumbe wa Askofu Mang'ana na viongozi waliomtangulia umemfikia Rais. Sote tunajua jinsi alivyo msikivu na mnyenyekevu na pengine ndiyo maana baadhi ya wateule wake wanatumia mwanya huo kumsaliti. Sisi tunachukua nafasi hii kumshauri azisafishe sasa safu za uongozi ndani ya serikali na sekta ya umma pasipo woga wala upendeleo. Tunamuhakikishia kuwa tutamuunga mkono muda wote pasipo kutetereka.
 
Kikwete alikwenda nje ya nchi kwenye mkutano akiongozana na Ngeleja na ndani ya ule mkutano Ngeleja alipigwa picha amelala fofo ; hakumchukulia hatua zozote na mpaka leo anadunda, kwani wanamfichia siri zake nyingi za kifisadi na haikuwa bahati mbaya kumteua kuwadi wake Jairo kuwa katibu mkuu wa wizara ya nishati!! Wote hawa ni wezi!!

Aaaa!! ya kweli hayo? tunge iona hiyo picha ingefaa zaidi.
 
Aggreko, Glasgow-based temporary power firm said it had signed a deal with the Tanzania Electric Supply Company to provide 100MW of power for 12 months.

Aggreko will supply two 50MW diesel-powered plants at Ubungo and Tegeta, as well as manage fuel supply.

Aggreko said the exact value of the contract would depend on the monthly price of diesel and the amount of power generated. The firm will charge "a small fee" for managing the fuel supply.

The Scottish firm said the addition of 100MW of power would help stabilise the country's power supply and support continued economic growth while the Tanzania Electric Supply Company worked to implement long-term solutions to improve power generation and distribution.

Aggreko chief executive, Rupert Soames, said: "Having successfully delivered 40MW of emergency power between 2006 and 2008, we are delighted that - following a competitive tender process - we have once again been selected to be of service to Tanzania." This latest contract will take Aggreko's order intake in the first six months of 2011 to at least 630MW.



kama mnakumbuka,walizima umeme wakasaini mkataba na symbion power,sasa tena zima umeme wamesaini mkataba na hao jamaa,hiyo ndiyo tabia mpya ya kuingia mikataba
 
Thank you........... halafu tukisema tunaambiwa hatuna uzalendo, poor me!!
 
Thank you........... halafu tukisema tunaambiwa hatuna uzalendo, poor me!!

Hii mbinu wanayokuja nayo sasa ni kali,haingii akilini kwa Tanesco kutangaza Mgawo wa umeme eti kisa Bwawa la mtela maji yamepunguwa,na hiki ni kipindi cha kumalizia masika,Je ifikapo kiangazi si ndio mgawo utakuwa wa kila baada ya mwezi mmoja?

lakini tumegundua kuwa ni janja yao,lengo ni kuwaonyesha watanzania kuwa kunatatizo la umeme na hii iwape wao uwezo ama uhalali wa kusaini mikataba

kazi japani

tutafika kweli?
 
Wakuu hii nchi kwakweli sielewi tunakoelekea kuna mgao wa umeme unaoendelea kwa saa 24 kila siku huku mikoani ambao hauko katika ratiba iliyotolewa magazetini wiki hii umeme unakatwa saa 12 jioni na haurudi hadi kesho yake saa 12 jioni na hapo kesho yake asubuhi unakatwa tena huku tunaelekea wapi jamani naona maisha sasa ni magumu ajabu.

Nilipita mtaani kazi zote zimesimama vijana wamekaa wanatazamana hali ikiendelea hivi vijana hawa ambao kazi zao zimechukuliwa na mgao wa umeme wataamua kufanya kazi usiku ya kutukaba na kuvunja vijumba vyetu amani itatoweka kabisa muda si mrefu hakuna tena usalama na ukizingatia usiku mzima giza mgao huu utaongeza pia mimba zisizotarajiwa na kuongeza idadi ya watu katika familia ambao ni mzigo na kuzidisha umasikini kwakuwa sasa usiku klwakuwa hakuna umeme itakuwa full mchezo wa baba na mama!! Serikali mpoo kuna janga kubwa mbele yetu!
 
Yah, vicious cycle eeh? lakini Magamba a.k.a stone agers kiza kwao si kipaumbele I guess, tutapiga kelele tu hapa mpaka tukaukiwe makoo.
 
  • Thanks
Reactions: LAT
Washenzi hawa, mie naona masaa 48, huku kwetu Mbagala leo siku ya pili tuko gizani!
 
Utasikia bajeti ya ngeleje yapita kwa KISHINDO

yeah,tena kwa kupiga meza huku wamelala,wakati wananchi wanaumia

kwanini Tz hatuna vyanzo vya umeme wa kudumu? tunakazi ya kutegemea mvua tu,mvua isipo nyesha basi tena

lakini pia hivi vyanzo aliviacha Mwl Nyerere,ina maana hawa maraisi wa sasa hakuna hata mmoja aliyeweza kuanzisha chanzo chake

kweli hii ni bongo

haya sasa wameingia mkataba wa kutumia majenereta,gharama juu ya gharama,hizo pesa tulipazo tungeweza kuanzisha chanzo kingine
 
Back
Top Bottom